Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Uhakika wa kupata lishe kwa kumuumiza mkulima? Yani mkulima masikini wa mwisho kijijini auze mahindi kwa hasara ili wewe upate milo mitatu?
halafu 80% ya tz population ni wakulima unamaanisha hao wote (80%) wazidi kukandamizwa kwenye umasikini ili ww ununue unga 200tsh?
Kilimo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine na kama ishu ni kumnufaisha mlaji bila kujali maslahi ya mzalishaji basi na mfuko wa cement uuzwe 5000, soda100, mafuta Lt 500tsh au ikiwezekana watuwekee bure kwenye magari,
Kama hayo hayawezekani why mkulima?? yeye pia anatumia rasilimali muda,mbolea,nguvu, madawa, usafiri nk kwenye uzalishaji.


Huu ni ubinafsi wa hali ya juu sana!!
Ukitaka kujua kwamba bichwa lako umejaza minyoo kichwani jiulize hili swali; "Je, ni asilimia ngapi kati ya hiyo asilimia 80 wanalima mahindi?", si kila mahali panafaa kulima mahindi, ndio maana wengine hulima ndizi, kahawa na mchele, na wote tunategemeana kama taifa kiujumla. Tena kuna sehemu zingine ni kame na hazitoi mazao yabkutosha, mfano ni mikoa ya Dodoma na Singida, kwahiyo tunategemeana kama taifa, Dodoma wakilima zabibu haimaanishi kwamba hawataki mahindi, bali ni mazingira ndio yanafavour zaidi zabibu, na ni lazima wauze zabibu na wanunue mahindi, tunategemeana kama taifa. Leo serikali ikikusanya kodi itokanayo na vileo vya zabibu kisha ikatumia hizo pesa kutoa ruzuku za pembejeo kwa mfumo wa vocha it means nao wamehusika kwenye uzalishaji wa hayo mahindi, na wote tunahaki yabkuyafaidi, kila mtu na kila kitu kiko intertwined, tuache ubinafsi wa kiboya huo. Masuala ya cement nk. kupungua bei hutegemea na demand na supply, viwanda vikizalisha cement nyingi kuliko demand kama mnavyofanya nyinyi wakulima wa mahindi bei itashuka tu, maana kwa sasa TZ hai-export cement kwenda nje, sana sana ndio tunazidi kuagiza cement toka pakistan lakini bado bei iko juu, means demand ni kubwa, sasa imagine tungeanza kuagiza mahindi toka marekani, bei si itakuwa 5,000/= kwa gunia? Kilimo ni biashara, hivyo tengenezeni feasibility study ya kujua zao gani litakuwa na demand kiasi gani wapi na lini, pia muangalie sera ya serikali juu ya zao husika, ndio mtu unalima, sio mnalima tu blindly wakati mnajua kabisa before hand sera ya serikali juu yabku-export chakula, maana kama Kenya bei ni kubwa kwanini msiende mkanunue ardhi Kenya mlime? Serikali ya TZ imehakikisha ardhi za wazawa zinalindwa ndio maana mazao ni mengi, bali Kenya kumiliki ardhi kwa mkulima ni ndoto, wengi ni vibarua kwenye mashamba ya akina uhuru Kenyatta, huku mtu unajikatia lishamba unalima tu, acheni kelele na fanyeni kilimo kinacholipa kama mahindi hayalipi!
 
Ukiachilia mbali bei kuwa ya hasara namna hiyo bado kuna waliohifadhi ili angalau wauze msimu huu wa mvua mahindi yao yameharibiwa na mafuriko.
Ile wizara imepewa muhuni amejaza ndugu zake kwenye sector nyeti kama ya mfumo wa akiba ya chakula waziri anaweka binamu yake hiyo inakuwa wizara au mradi wa familia?

Kujaza chakula nchini haikatazwi ila huyu mkulima alilima kwa ajili ya kuuza kwa hasara?

Upuuzi wa awamu hii unatia kinyaa. Mkuu anatangaza kwenda kufanya kazi mbinguni ndio maana anaua kilimo kwa kuweka makanjanja yasiyojielewa kwa sababu tu akishapaa kwenda zake mbinguni kule hatosikia njaa wala kiu. Malaika hawali wala hawanywi au sio[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

mkulima analia machozi yake hayatokwenda bure.
 
Hapa inayotusumbua ni Exposure, watanzania wengi hatuna Exposure na tunaishi kwa Itikadi Kali sema tumekosa mabomu tu.... katika Nchi yeyote suala la chakula halitakiwi kuwa na Gharama hata kidogo ili kila mtu aweze kupata hitaji hili la Muhimu... Mimi nimewahi Kaa Uswisi yaani bei za vyakula siyo kubwa kabisa na watu wanaishi kwa furaha. Sasa mnataka mahindi yaende nje halafu mwezi WA saba watu waanze kulia Njaa.... Wewe kama umelima na unaona umepata hasara acha kulima lakini mwenye Busara hawezi. Na yanatakiwa yashuke zaidi, bado Mchele.... Mazao ambayo wanatakiwa kusafirisha ni ya Biashara siyo chakula.... Acheni mambo ya Ajabu ajabu hapa sasa hivi hata mlala hoi anayelipwa Elfu tano kutwa ataweza kuishi
 
Mazao yote yanatakiwa kushuka bei zaidi ili watu waweze kuishi, Usiongee kwa sababu una Mshahara ambao hata kijijini kwenu huwatumii huo Mshashara ongea ukitafakari maisha ya Watanzania waliowengi. Mungu aendelee kusaidia Yashuke zaidi na zaidi, haitakiwi kufika sehemu mtu awaze anakula nini kula ni hitaji la Muhimu eboooo
 
Mna kumbuka mwaka Jana lile balaa au kwa sababu Nyingi mko dar hamuelewi watu wanaishi huku mikoani pumbafu.... Kilo moja ya Unga si ilifika 2,000 shenzi zenu na mabadiliko ya kweli hayawezi kuja kwa kuona kila kitu in a negative way
 
Hapa inayotusumbua ni Exposure, watanzania wengi hatuna Exposure na tunaishi kwa Itikadi Kali sema tumekosa mabomu tu.... katika Nchi yeyote suala la chakula halitakiwi kuwa na Gharama hata kidogo ili kila mtu aweze kupata hitaji hili la Muhimu... Mimi nimewahi Kaa Uswisi yaani bei za vyakula siyo kubwa kabisa na watu wanaishi kwa furaha. Sasa mnataka mahindi yaende nje halafu mwezi WA saba watu waanze kulia Njaa.... Wewe kama umelima na unaona umepata hasara acha kulima lakini mwenye Busara hawezi. Na yanatakiwa yashuke zaidi, bado Mchele.... Mazao ambayo wanatakiwa kusafirisha ni ya Biashara siyo chakula.... Acheni mambo ya Ajabu ajabu hapa sasa hivi hata mlala hoi anayelipwa Elfu tano kutwa ataweza kuishi

Umeangalia kijuu juu sana hili suala la bei ya nafaka iitwayo mahindi mkuu. Ila sio kosa lako kwa sababu hujui hata kidogo wakulima wanatumia gharama kiasi gani ili kuja kuuza kwa wewe mlaji sh 20,000 kwa gunia. Nakushuri tu pitia nyuzi mbalimbali humu ili kujiongezea upeo wa gharama za kilimo utaweza kuelewa kwa nini kilio kinasikika zaidi badala ya furaha. Wewe utapata chakula leo ila msimu unaofuata hutakuwa na uhakika wa kula kama ulavyo leo.

Usiifananishe Tanzania na Uswisi ni sawa na kulinganisha speed ya bicycle na train ya umeme mkuu.

Ndio kwanza tuko kwenye kilimo cha jembe chakavu la mkono.
 
Bei ilipokuwa juu mlilalamika sasahivi imeshuka ili kuwapunguzia ugumu wa maisha watu wa kipato cha chini tena mnalalamika! Watanzania mnataka nini? Kwani bei ya gunia la mahindi kuuzwa sh. 20,000/= ndio mara ya kwanza katika historia ya Tanzania toka ipate uhuru?
 
Mahusiano mabaya na jirani yana laana siku zote!

Elfu ishirini?!!
Ndio, it means hadi omba omba watakula walau milo miwili kwa siku, tumpongeze rais kwa kuwatetea masikini, au mlitaka unga upande bei kama sukari ili mpate cha kuongea?
 
sasa nausubiria mchele tu sasa ushuke sukari ndo wameigomea kushusha sijui kwavile ma papa ndo wana share kwenye hizo industry
 
Ila huoni kwamba masikini sasa wana uhakika wa kupata walau milo miwili kwa siku? Bei ya unga ingepanda pia ungelaumu serikali kwamba mnakufa njaa, bei ya mahindi na unga inashuka pia mnalia, mnataka nini nyinyi kasuku?
Hii akili hata kuku hana. Na yeye mkulima atakula mahindi, kuvaa mahindi, kutibiwa na mahindi nk??????? Kuna watu mnafanya propaganda hadi mnakuwa wehu.
 
Sasa serikali inatumia pesa za wakulima kutekeleza malengo yake kiujanjaujanja.Kwanini wasiweke ruzuku kwenye pembejeo ili mkulima azalishe kwa gharama nafuu kuendana na soko?
Kwani unaposikia serikali inatoa vocha za ruzuku huwa unaelewa nini? Au serikali inapojenga miundombinu za barabara kwenda vijiji vyabwakulima ili kurahisisha usafiri wa mazao huwa uanelewa nini? Au serikali inapoweka vituo vya hali ya hewa ili kwashauri wakulima muda muafaka wa kulima huwa unaelewa nini? Au serikali inapotekeleza ujenzi wa mabwawa ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao huwa unaelewa nini? Au serikali inapoagiza matrekta na kuyatoa kama mikopo kwa vikundi vya wakulima kwa bei nafuu huwa unaelewa nini?, au serikali inapoendesha vituo vya utafiti wa mbegu bora zinazovumilia ukama na kutoa mazao mengi kwa muda mfupi huwa unaelewa nini? Nk.nk.nk.nk.; au huwa unafikiri hivyo vitu havina gharama? Serikali huchangia moja kwa moja katika uzalishaji wa hayo mahindi, hivi wamehusika na mahindi kuwa mengi na bei kushuka, toa hayo makonokono kichwani and think straight! Tena kwa hasira naenda kununua kila 100 za unga naweka ndani, just incase mahindi yakapanda bei, shenzi kabisa!
 
Waliozuia kuuza nje wao wanakula vya super market tu.......hii nchi viongozi wamelaaniwa si bure.
Acheni kuongea kinafku wapendwa ,kwan hamkumbuk mwaka jana tulikua na mgogoro na Kenya Mara ng'ombe Mara vifaranga,Mara wakasema baba yetu anataka kuingilia uchaguz wao...sasa dawa yao ilikua kuwanyima mahindi ili wakome...kwan mmesahau kuna msemo usemao adui muombee njaa?????
 
Msimu huu mama lishe watauza mboga tu ugali watagawa bure [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Nacheka lakini naumia maana mkulima wa mahindi hajawahi kutabasamu kipindi kirefu sana. Fikiria hiyo mahindi mkulima anauza bei gani kwa wachuuzi [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Usishangae ikawa 7000.
 
Back
Top Bottom