Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Chakula kikiwa bei nafuu mnakasirika badala ya kufurahi. Kweli nyie ziro kabisa. Kwa taarifa yenu wakulima wadogo wadogo ambao ni wengi wanalima mazao ya chakula kwa ajili ya matumizi binafsi na siyo kuuza.
Una hakika au kwakua mwenzetu unapewa bukusaba ushavimbiwa au hujaishi huko hivi unajua mkulima huyo mdogo unaemsemea wewe maihataji yote mhimu kama sukari, mafuta ya kupikia, chumvi, majani ya chai, nguo, matibabu, na mengine mengi ambayo hayatokani na kilimo anatengea auze mazao hayo ili apate fedha na kununulia hayo mahitaji

Mbali na hayo mtaji kwa kulimia msimu ujao usifikiri mazao ni magugu yanaota yenyewe yanahitaji mbegu, mbolea, palizi, viwatilifu.

Usishikiwe akili hafu usike na wewe ni uvccm mbunge na waziri ajaye kweli watz tunasafari ndefu sana
 
Je wangeruhusu yauzwe nje kisha gunia moja likiwa 120,000/= na kilo ya mahindi ikawa 4,000/= ungelaumu serikali?, kwenda zako huko
Ilitakiwa iwe win win situation nasio mwingine ale hasara hafu wewe uvimbiwe
 
Aisee, umefikiri sawa sawa.

production cost per standard bag(100kg) ni Tshs 45,000/= maeneo yaliyo mengi nchini kutokana na hizi gharama hapa chini ndani ya ekari moja.

-kukodi shamba 100,000/=
-kulima 60,000/=
-kupanda 30,000/=
-mbegu 48,000/=(4bags @12,000/=)
-palizi 60,000/=(2 @30,000/=)
-kuvuna 60,000/=

jumla 358,000/=
hapa ekari moja inakadiliwa kutoa (8-10) bags chini ya uangalizi mzuri japokuwa sijaweka gharama za mbolea na madawa.

ukigawa hapo utakuta 1bag ni 44,750/=, sasa njoo kwenye mauzo.

gunia 20,000/=-44,750/=(-24,750/=)

huyu mkulima bado unashangilia aendelee kulima na kuuza kwa bei hiyo halafu unaona raha tu au ndo kunywa maji yaliyofuliwa hizo bendera zenu.

acheni ushabiki usiokuwa na tija. nilifikiri mtu kama wewe uje na ufumbuzi wa kuwasaidia hawa wakulima labda serikali ihimize hawa watu wafanye food processing ili chakula kisiharibike wakingojea soko likae vizuri.
Umeandika vizuri sana kwa hawa mapunga wanao waza siasa na kula siasa hawatakuelewa
 
mimi nimepata hasara kijimzigo changu cha tsh 2M ndo nilikuwa naanza hii biashra.
katika huo mtaji wa tsh 2M, mim nilikuwa nina 1.5M nikakopa Laki 5 kuongeza
mwisho wa siku nimeuuza mzigo wote kwa laki tano ili nrejeshe pesa niliyokopa
hali ni mbaya ndugu zangu ahapo bado expenses za kufanyia storage
hii hali imenirudisha nyuma sana Lakini Allah ndo mpangaji atanijalia njia nyingine
 
You are just advertising your foolishness shamelessly.Inahitaji wendawazimu kujibu maswali ya kitoto namna hyo
Sasa kama majibu unayajua kelele za nini? Kilimo ni biashara, na basically business in faida na hasara, mwaka jana wakati kilo ya unga inauzwa 2,500/= mlipata faida nankushangilia, mwaka huu mmepata hasara, its ok, thats business
 
Sasa jiulize watapataje mitaji ya kulima miaka ijayo kama wamekula hasara au wewe mwenzetu umepata teuzi au unakula buku saba za lumumba zinakufanya usitumie akili zako
Bei itapanda maana wachache watakopa na kulima, its business
 
Ila huoni kwamba masikini sasa wana uhakika wa kupata walau milo miwili kwa siku?

Bei ya unga ingepanda pia ungelaumu serikali kwamba mnakufa njaa, bei ya mahindi na unga inashuka pia mnalia, mnataka nini nyinyi kasuku?
Kumbuka huyohuyo mkulima anataka auze mahindi alipe ada,apate mboga,anunue mboga na hivi vitu bei juuu
 
Kumbuka huyohuyo mkulima anataka auze mahindi alipe ada,apate mboga,anunue mboga na hivi vitu bei juuu
Sasa kwanini hakulima mboga ambayo ni bei juu, badala yake analima mahindi ambayo ni bei chini? Kilimo ni biashara jamani..
 
Hizi taarifa hazina uhalisia! Kwenye mitandao kila mtu anasema lake. Juzi nimenunua dona 25kg Dar kwa 19,000. Sasa unataka kuniambia gunia la kilo 100 liuzwe bei sawa na kilo 25?? Unamdanganya nani?
Mkuu kama hujui chochote ni bora ukae kimya.. Mimi mwenyewe nimeamua kuyauza mahindi yangu niliyonunua sh 50,000/ kwa @ gunia. Now nimekubali kuyauza 30,000@ gunia ili pesa niifanyie mambo mengine.. Nakuhakikishia km unahela njoo nikupeleke upate mahindi hata tani 200 kwa 27,000 hadi 25,000 kwa gunia huku UNYAMWANGA RUKWA
 
hebu wakulima jitokezeni tununue mjini njaa au ndo mmezira.
 
Kama yameruhusiwa yatapata soko tuu. Mahindi yanayolimwa kwenye ardhi ya frika mashariki yana ladha nzuri sana . Hayo ya bara la amerika ni testless
Mwngo mkubwa. Latin Amerika has better quality
 
Sasa kwanini hakulima mboga ambayo ni bei juu, badala yake analima mahindi ambayo ni bei chini? Kilimo ni biashara jamani..
Mwaka juzi mikoa mingi miezi kama hii mahindi debe 1 liliuzwa kwa tsh.18000/=--23000/= wakulima wengi walihamasika na kulima kwa wingi wakitarajia mauzo mazuri lakini ndo hivyo tena
 
Back
Top Bottom