ESCORT 1

JF-Expert Member
Dec 7, 2015
1,267
2,519
Leo tujikumbushe kwenye historia ya nchi yetu tangu tulipoungana na wenzetu wa Zanzibar mwaka 1964.

1. Ni watu wawili tu wamewahi kushika madaraka hayo zaidi ya mara moja ambao ni Edward Sokoine na Cleopa Msuya
Edward Sokoine akishika madaraka hayo mwaka 1977 mpaka 1980.
Kwa mara pili akachukua wadhifa huo mwaka 1983 mpaka mwaka 1984 mauti yalipomkuta.

Cleopa Msuya yeye alishika mwaka 1983 mpaka 1985. Awamu yake ya pili akishika mwaka 1994 mpaka 1995.

2. Ni Mzanzibar mmoja tu kuwahi kushika wadhifa huo.
Si mwingine ni mzee wetu, Salim Ahmed Salim. Hapajatokea tena mtu mwingine kutoka visiwani kushika wadhifa huo.

3. Ni Waziri Mkuu mmoja tu ambaye ameweza kuhudumu kwa miaka 10
Huyu si mwingine bali ni Fredrick Sumaye ambaye alianza na Mkapa akamaliza nae.

4. Waziri Mkuu mmoja aliwahi kujiuzulu. Edward Lowassa mwaka 2008 alijiuzulu nafasi hiyo baada ya kuibuka kwa skendo ya Richmond.

5. Kassim Majaliwa awa Waziri Mkuu wa kwanza kuhudumu kwa Marais wawili tofauti.
Amehudumu kwa John Pombe Magufuli na baadae kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

6. Ni Waziri Mkuu mmoja tu aliwahi kufariki akiwa madarakani. Huyu ni mpendwa wetu Edward Sokoine mara baada ya kupata ajali pale Dumila na kupelekea kifo chake.

7. Edward Sokoine anabakia kuwa Waziri Mkuu ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa sana na anatajwa kama bora wa muda wote katika nafasi hiyo, alikuwa na uthubutu mkubwa sana. Na ndio maana haishangazi kushika wadhifa huo mara mbili.

8. Waziri Mkuu aliyeshika madaraka hayo kwa muda mfupi zaidi ni Cleopa Msuya tena mara mbili.
Katika nafasi hiyo ameshika madaraka hayo kwa kila kipindi kuwa muda wa mwaka mmoja, mwaka mmoja tu.

9. Rashid Mfaume Kawawa anatajwa kama Waziri Mkuu mtiifu pengine kuliko wote katika historia ya nchi yetu. Aliweza kukaimu nafasi ya Urais wa nchi wakati Mwalimu Nyerere alipoamua kwenda kujenga chama kwanza punde baada ya nchi kupata uhuru. Mwalimu aliporejea alimkabidhi nafasi yake ya Urais na yeye akaendelea kushika madaraka yake ya Uwaziri Mkuu. Kawawa alikuwa loyal sana mwalimu Nyerere.

10. Hakuna Waziri Mkuu aliyewahi kuja kuwa Rais. Pamoja na kwamba wamepita manguli wa kila namna kuanzia enzi za Kawawa, John Malecela, Edward wote wawili, Sumaye na hata Mtoto wa mkulima hakuna aliyefanikiwa. Hajatokea bado labda siku za usoni.

MWISHO
 
Kwahiyo kwenye hizo historia Mizengo Pinda hana rekodi yeyote? Msimfanyie hivo nyie watu hahah
 
Back
Top Bottom