Reincarnation...nazidi kupata uhakika binadamu hatufi

Kwani nani amesema haufi? Hapa mleta mada anamaanisha baada ya kifo, kwamba kuna uwezekano mtu akazaliwa kwenye mwili mwingine
Hakuna tofauti na wanaoamini kuhusu motoni na peponi
Pia unaposema nijiandae na umauti, actually mimi sijiandai na kifo chochote kile, ninaishi kawaida kivyangu mpaka umauti utakaponikuta wenyewe. Kwa nini nijiandae na sijui nakufa lini?
 
Sio tu haufi, au sio tu kwamba utazaliwa tena na tena, unaweza ukafa na ukabaki hapa hapa, isipokuwa mazingira yanabadilishwa kidogo tu wanakuweka kwenye ulimwengu unaofanana na ule uliokuwamo awali.

Kwanza hutajua kama umekufa, utaendelea tu huku wao wanakuchekaaaa!

Hii ni kwa wachache sana.
 
Mabudha wanasema kila nafsi huwa ina mission yake maalum inabidi ikamilishe kabla ya kufa, hivyo kama hujakamilisha utakuwa unazaliwa tena na tena mpaka ukamilishe. Na ukisha kamilisha unaenda kuungana na ufahamu wa ulimwengu na kuwa moja na ufahamu huo.
 
 
Ukifa unazaliwa nch nyingine
 
Kuna maeneo au watu ni kama umeshawahi kuwaona sehemu lakini uwakumbuki....ni kama mlishawahi kuonana au ulishawahi kuishi sehemu fulani fulani lakini huezi elezea na kukumbuka vizuri.....we are not alone on this one!
 
Dhana ya Ukifa hauendi popote ni uongo kwasababu hakuta kuwa na 'wewe' wa kwenda popote. Kama ambavyo hakukuwa na 'wewe' kabla hujazaliwa..ndivo itakavokuwa utakapokufa.

Na hii ni kwasababu hakuna kitu kinaitwa 'wewe'

Kila kitu unachomaanisha usemapo 'mimi' hakipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…