nilipoingia ndani ya jukwaa na kuzikuta habari za msiba huu wa kamanda, nilitamani sana iwe naota na sii kitu halisi, lakini hata hivyo kumbe ni kweli. Kwa hakika nilikuwa sijawahi kukutana na Regia phisically, lakini kupitia michango yake katika kupigania ukombozi wa mtanzania, ilikuwa kama ni mtu nilie nae kila wakati na popote niendapo. Bwana Mungu na akupumzishe pema kwa kuwa matendo yako mema ya kupigania haki kwa wote, yamekutangulia huko uendako. Aaamen!!
.