Elections 2010 REDET & Synovate hamtaweza kuzuia mabadiliko...

Matokeo ya utafiti yanatoa muongozo wa nani anaweza kushinda, na hayo yanaweza kubaki hivyo endapo upepo utabaki kuwa kama ulivyokuwa wakati utafiti unafanyika.Ikumbukwe kuwa katika ulingo wa siasa muda ni kitu muhimu sana kwani ndani ya wiki moja upepo wa siasa unaweza kutoa ishara tofauti na mwanzo.

Hebu tujikumbushe yaliyotokea wakti ule George Bush alipopambana na John Kerry wa Democratic huko Marekani.Mtakumbuka John Kerry aliendelea kuongoza tangu mwanzo wa kampeni hadi wiki ya mwisho ya kampeni.Lakini mambo yalibadilika zikiwa zimebaki siku saba kupiga kura pale ulipofanyika mdahalo wa mwisho, ambapo John nkerry aliulizwa swali moja la msingi kuhusu msimamo wake juu ya NDOA ZA JINSIA MOJA.

John kerry alijibu kuwa ndoa za jinsia moja ni uhuru na haki ya mwanadamu kuamua.Ikumbukwe kwamba John Kerry ni mkristu Mkatoliki kanisa ambalo linapinga kwa nguvu zote ndoa za jinsia moja. Kwa upande wake George W.Bush alipoona mwenzake kachemsha alipinga huku kionyeshwa kukerwa sana na swali liele kwa maaana kwamba halikupaswa kuulizwa kwani HAIKUBALIKI katika dini ya kikristu na kumbuka Bush ni muumini wa madhehebu ya Mashahidi wa yehova nayo yanapinga.

Baada ya majibu hayo John KERRY upepo ulimwendea vibaya kuliko kawaida yake kwani wakatoliki wote walimhama kwa kuwadhalilisha kukubali kuota uhuru wa watu kuamua badala ya kuzuia kwa nguvu zote.
NA HAPO KERRY ALIANGUKA NA KUMUACHA BUSH AKIPETA.

Ninachotaka kusema kwa upande wa Tanzania ni kwamba, kura za utafiti zilizotolewa kwa mfululizo kwa makampuni mawili tofauti, REDET NA SYNOVATE ndani ya masaa 72, haziwezi kutushawishi moja kwa moja kuwa JK ndiyo atakuwa mshindi, la hasha hizi zinawakilisha muda Fulani tu, zinaweza kubadilika kuendana na kampeni zinavyobadilisha upepo na pia wapiga kura kuendelea kuelimika kwa kusikiliza sera.

Mazingira ya kura hizi pia yanaonyesha kupikwa kwa mtindo wa PROPAGANDA ILI KUWAKATISHA TAMAA WAPIGA KURA.
Tukumbuke JK nimtaalam wa PROPAGANDA na kwamba kaisomea anajua fika namna ya kutumia na ndiyo maana yawezekana matokeao HAYA YAMEMSAIDIA KUMUINUA kwa kiwango Fulani.Lakini baada ya muda watu watasahau.

NINI KIFANYIKE
Wadau/chadema waendelee kuwaelimisha wapiga kura na kuyakataa kwa nguvu zote matokeo kwa kutumia PROPAGANDA PIA, maana dawa ya moto ni moto.Kwa kufuatilia kwangu nimendua matokea hayana IMPACT kwa wapiga kura ila faida ya haya matokeo kwa JK ni kwamba sasa anao uwanja uliobarikiwa kumuwezesha kuiba kura kwani atajitetea hata tifiti zimeonyesha ndiyo maana kafanya tafiti zaidi ya mbili ili kutoa uwanja mpana wa kujitetea.CHADEMA wajizatiti kuimarisha ulinzi wa kura na kuziba mianya yote .YOTE YANAWEZEKANA KWA KUMTUMAINI MUNGU
 
Ukiangalia kwa haraka haraka unaweza ukafikiri kwamba REDET na SYNOVATE wamefanya tafiti zenye matokeo tofauti kabisa kwamba ati REDET wamesema Kikwete atapata 71% na SYNOVATE wamesema Kikwete atapata 61%. Ukweli ni kwamba hawa jamaa tafiti zao zote zinaonyesha kwamba Kikwete atashinda kwa wastani wa asilimia 70. Hii inatokana na ukweli kwamba REDET wamempa Kikwete 71% mojakwamoja (Directly) wakati SYNOVATE wamempa Kikwete asilimia 70 ila kwa maneno ya kujizungusha (Ila lengo likiwa ni 70% na si 61%).

Dr Slaa na Lipumba watafiti wetu wamekuwa na mpishano mkubwa kiasi. Wakati tofauti kati ya REDET na SYNOVATE kwa Dr Slaa ni ~6%, Prof. Lipumba ni 4% ilihali tofauti kwa Bwana Kikwete ni 1%.
Kwa akili ya haraka haraka utaweza kujua kuwa watafiti hawa wanamalengo maalum ya kuweza kuhalalisha wizi utakaofanywa na CCM katika kuiba kura.

Hapa tutakubaliana sote baada ya Octoba 31 kwamba kama hatua za ziada hazitafanyika Kikwete atashinda na ushindi wake utakuwa hivi kimahesabu 65%-75%. Kama tunabisha tutaonana tena November kuhakikisha hili kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

Sasa ni vipi CCM watachakachua kura??? Mimi ni miongoni mwa watanzania wachache sana walioweza kwa muda mrefu kuishi vijijini na mijini mwa nchi yetu. Ile kasumba kwamba vijijini kuna wapiga kura wengi kuliko mjini ni uongo. Ila kilichopo vijijini kikubwa kuliko mjini ni kwamba wananchi wa vijijini wanatishika kirahisi kuliko wa mjini. Nani huyo anayewatisha???

1. Wenyeviti wa vijiji
2. Polisi
3. Watendaji wa vijiji na kata. Hawa wote ni makada mashuuri wa chama tawala (CCM). Sasa ni huku vijijini ambako uchakachuaji hufanyika bila tabu wala shida yoyote.

Ni vijijini ambako hata ofisi za vyama pinzani hakuna. Ni vijijini ambako vyama vya upinzani havina mawakala wa kutosha wa kila kituo. Sasa hapa ndo penyewe, kijiji chenye wapiga kura 1000 watazaliwa 4000 zaidi na kufanya 5000. Haya yote yanawezekana vijijini. Ni vijijini ambako hakuna mfumo mzuri wa barabara wala nyumba za kulala wageni ambako waangalizi wa kimataifa wanaweza kufika. Ni huko vijijini ndiko wapiga kura watakuwa 60% wa wapiga kura wote nchini.

Kwa utafiti wa idadi ya watu unaonyesha kwamba uwiano wa watu wazima na watoto Tanzania ni 2:3 maana katika watu wazima 2 watoto ni 3. Kwa maana hiyo wapiga kura ambao ni watu wazima ni 40% ya idadi ya watu wote. Sasa tume ya uchaguzi imetueleza kwamba tuna idadi ya wapiga kura 19.7m ina maana idadi ya watanzania inakaribia 50m????. Hapa kunaonyesha kuna kura hewa karibu 3m zimeandaliwa. Hizo kura 3m ni wapi zinapelekwa?? Ndio kule vijijini nilikokusema.

Angalizo langu ni kwamba kwa hali ilivyo hivi sasa CCM lazima watafanikiwa kuiba kura na itakoma mpaka pale vyama vya upinzani vitakavyoweza kueneza ofisi zake mpaka kule vijijini kusikofikika kirahisi hapo ndio ushindi kwa upinzani tutauona ala sivyo tusubiri ushindi wa 65%-75% kwa CCM.
 
Ni kweli kabisa mkuu, mimi naona ni mbinu tu ya ccm kujificha nyuma ya pazia ya kura ya maoni ili kuhalalisha hujuma.

Tubaki kumwamini Mungu ili wale wenye kutumwa kwa hujuma ya aina yoyote awageuze nia zao na kujiona kuwa ukombozi unaotafutwa ni kwa ajili yao na watoto wao wenyewe
 
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, amepanda kwa alama nne, huku mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, akishuka kwa alama 10, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Synovate.

Matokeo hayo yanapishana na yale yaliyotolewa siku tano zilizopita na taasisi ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) ambayo ilimpa Kikwete asilimia 71.2, Dk. Slaa (12.3) na mgombea wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (10.3).

Akitangaza matokeo ya utafiti huo, jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Synovate hapa nchini, Agrey Oriwo, alisema utafiti wao wameufanya kuanzia Septemba 5 mwaka huu na umewahusisha watu 2000.
Alisema katika utafiti huo, uliohusisha mikoa 21 ya Tanzania Bara ulifanywa katika wilaya 63 na waliowahoji walikuwa 73 ambao walikuwa wakikusanya takwimu (data) za utafiti huo.

Alisema mbinu iliyotumika ni utafiti wa kimahesabu ambapo wahojiwa walichaguliwa kwa njia ya nasibu.

Alisema asilimia 53, waliohojiwa kwenye utafiti huo walikuwa ni wanaume na 47 wanawake ambapo asilimia 60 ya waliohojiwa ni wakazi wa maeneo ya vijijini, huku 40 wakiwa maeneo ya mijini.
Alisema miongoni mwa maswali waliyoulizwa ni “Mtamchagua nani kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano mwishoni mwa mwezi huu?” Ndipo yalipopatikana matokeo kuwa asilimia 61 wangemchagua Rais Kikwete, Dk. Slaa (16)na Profesa Lipumba (05).

Alisema asilimia 13 waligoma kujibu swali hilo, huku asilimia 5 wakijibu kuwa wangewachagua wagombea wa vyama vingine vya siasa.

Alisema katika utafiti huo, wananchi waliulizwa umaarufu wa vyama vya siasa ambapo asilimia 64 walisema CCM iko karibu nao, CHADEMA (22), CUF (7), asilimia 5 walivitaja vyama vingine, huku asilimia mbili hawakujibu swali hilo.

Swali jingine lilikuwa ni kama ingetokea nafasi ya kuwachagua vijana waliojitokeza na wenye vipaji vya uongozi kuwa rais wangemchagua nani, ambapo Zitto Kabwe aliibuka kidedea kwa kupata asilimia 38 akifuatiwa na Husein Mwinyi (15); na Makongoro Nyerere (12).


HABARI ZAIDI>>
 
Angalizo langu ni kwamba kwa hali ilivyo hivi sasa CCM lazima watafanikiwa kuiba kura na itakoma mpaka pale vyama vya upinzani vitakavyoweza kueneza ofisi zake mpaka kule vijijini kusikofikika kirahisi hapo ndio ushindi kwa upinzani tutauona ala sivyo tusubiri ushindi wa 65%-75% kwa CCM.

Ofisi kamwe hazilindi kura ila ni watu na mwaka huu huko vijijini kura zitalindwa mno kuliko mijini kwa sababu Mwenyezi Mungu anataka nchi hii iongozwe na kiongozi mwadilifu na mcha Mungu kama tulivyoomba wenyewe mwaka jana
 
Kuhusu matokeo ya kura za maoni ya Urais wa TZ yaliyofanywa na REDET/SYNOVATE na kutolewa hivi karbuni. Hili swala la kuchakachua jamani!!! Inanipa shida kidogo na naomba wanajukwaa wanisaidie hapa. Hizi in two independent survey on same subject (Watanzania, Inakuwaje ziwe zitatofautiana sana REDET 71 SYNOVATE 61 ni degree gani ya confidence iliyotumika hapa? Navyoelewa mimi ni kwamba kutakuwa na kushabiana kwa kiasi fulani. Si wote wameuliza kuwa kama uchaguzi utafanyika leo ni nani utamchagua kuwa rais wa TZ? Navyofahamu mimi ni kuwa utafiti ni lazima uashirie kinachooneka wazi. Sasa kama CCM ina-score mpaka 70% kwa upande wa urais inakuwaje level of effort inayotumika kumnadi mgombea wake inakuwa kubwa namna hii tunayoona. Kama kuna difference ya 60 in terms of % si sahihi nikisema kuwa CCM hata isipofanya Kampeni itashinda tu. Je ni kweli?
 
Ofisi kamwe hazilindi kura ila ni watu na mwaka huu huko vijijini kura zitalindwa mno kuliko mijini kwa sababu Mwenyezi Mungu anataka nchi hii iongozwe na kiongozi mwadilifu na mcha Mungu kama tulivyoomba wenyewe mwaka jana

Ni kweli kabisa. Je si sifa zipi za kiongozi mwadilifu?
 
SYNOVATE na REDET wasubiri kukabidhiwa The Hague kwa kuchochea wanayoyachochea sasa.
Watu hawatathmini hasara za kueneza uongo kwa taifa.
Ridhisha leo, kesho inakula kwako
 
EPA yaendelea kuwanunua watafiti kwa kasi zaidi nguvu zaidi na ari zaidi.........hongereni ccm ila mwisho wenu ndiyo huu na mfa maji haachi kutapatapa..............subirini maajabu pamoja na kwamba mnataka ushindi wa lazima km mnavyojinadi
 
Ni kweli kabisa. Je si sifa zipi za kiongozi mwadilifu?

SIFA ZA KIONGOZI MWADILIFU-TZ
1: Awe ni Mtanzania
2: Awe Mchukia Rushwa (Kwani rushwa ndio adui wa haki)
3: Awe anajua matatizo ya wananchi wake na matatizo ya Nchi
4: Awe ni Mzalendo na Uchungu wa Rasilimali za nchi hii
5: Kama kweli ni mzalendo basi afuate Miiko ya uongozi ile iliyoko kwenye Azimio la Arusha
6: Aitetea na kuilinda KATIBA YA NCHI
7: Afuate sheria za nchi zilizopo

Zingine nanyi muziongezeee wana JF

 
Sina imani sana na tafiti hizi maana kimuonekano zinaonekana zimeegemea upande mmoja na kuonesha kuwa chama kinachotawala bado kinathaminiwa na kuaminiwa na wananchi wengi,lakini hali halisi inaonesha kuwa kwa sasa wananchi wengi wameonekana kuwa na msimamo tofauti na tafiti hizi zinavyotuambia.
Inaonekana ni njia mojawapo ya kumsafishia mgombea wa chama husika njia ya kuendelea na kutawala ila watanzania kwa sasa hawaongozwi na tafiti kama hizi bali wanataka maendeleo ya kweli katika maisha yao.
Tusubiri tarehe ya kupiga kura na tuone ni nani ataibuka kidedea.
 


SIFA ZA KIONGOZI MWADILIFU-TZ
1: Awe ni Mtanzania
2: Awe Mchukia Rushwa (Kwani rushwa ndio adui wa haki)
3: Awe anajua matatizo ya wananchi wake na matatizo ya Nchi
4: Awe ni Mzalendo na Uchungu wa Rasilimali za nchi hii
5: Kama kweli ni mzalendo basi afuate Miiko ya uongozi ile iliyoko kwenye Azimio la Arusha
6: Anei itetea na kuilinda KATIBA YA NCHI
7: Ane Fuate sheria za nchi zilizopo

Zingine nanyi muziongezeee wana JF


Sifa hizo ninazo. Endeleeni kuomba niwe kiongozi wenu.
 
Mumesahau mwaka 2005 alikuwa anaongoza kwenye kura za maoni gazeti la majiri rai nk ,anatumia mbinu zile zile kama alivyotumia za mafiga matatu amabazo sasa hivi wananchi hawataki hata kuzisikia
 
Hawa ndo watafiti wetu, ndo maana hatuendelei tz kutokana na watafiki watiochakachuliwa, wenye fikra zilizochakachuliwa, kutoka kampuni/taasisi zilizochakachuliwa, obvious, matokeo pia yamechakachuliwa.Usiumize kichwa nawe usije ukachakachua msimamo wako wa kumdondosha jk.
Tusilaumu sana watz ndo tuna matokeo halisi ya nani rais wa tz, wasitubabaishe hawa maana hawajui wanachokifanya bali wanatimiza wajibu waliotumwa na bwn wao ie baba riz1.
Mustakabali wa nje yetu tunaujua sisi wazalendo wa kweli si vibaraka hivi vya uchakachuaji....... Watz tusije tukajuta kuwachagua mafisadi, tujitokeze kwa wingi tukapige kura tuwaangushe majizi hawa wataifilisi nchi yetu.
 
Ndugu zangu wana JF na wapiga kura wenzangu, matokeo ya tafiti zote hizi hayana maana kwetu sisi na kura zetu ambazo ni siri ya moyoni. Fuatilia kampeni kwa makini na tumia kura yako ya siri kwa busara. Msifuatilie kampeni za Kikwete, Lipumba na Slaa peke yao, kuna wagombea wengi. Pimeni kwa busara maana kura zenu ndizo zitakazoamua hatima ya nchi hii kwa miaka mitano ijayo. Tumuenzi Baba wa taifa kwa kupeleka Ikulu mtu tunayeaamini atapigania maslahi ya utaifa (sovereignty) na uzalendo (patriotism) na kuwajali watu. Asanteni
 
Hakuna kulala!hizo tafiti za kujifungia chumbani ,hazitomnusuru JK rais legelege!
 
Wapenzi wa mageuzi na mabadiliko, matokeo ya tafiti hizi lengo lake ni kukatisha watu tamaa, sasa ndio zitakuwa changamoto na chachu zaidi ya kutaka mabadiliko, hiyo October 31, watu watashangaa hao Redet na Synovate, watatafuta pa kuficha sura zao na pasionekane!.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom