Elections 2010 REDET & Synovate hamtaweza kuzuia mabadiliko...

Wabongo bana nimewavulia kofia.. hizi tafiti uchwara zinashikiwa bango kana kwamba ni kijito cha maji jangwani. Kweli uono wa typical mbongo unaeza kweli hauzidi pua yake.

Hamjapata urais mnatutukana wabongo namna hivi, sasa je tukiwapa si mtakunya katika vichwa vyetu.

Jamani hawa wenzetu bado wanahitaji muda, maana ni wachanga, tena wachanga kweli kweli.

Mmmm ninamashaka na hawa wenzetu!!!!!
 
Mapungufu ya utafiti wa Synovate

Wakuu kwa mujibu wa tovuti ya wavuti, nimeona nachoweza kukiita matokeo rasmi ya utafiti wa Synovate. Bofya Hapa for further details. Kinachoshangaza kuna utitiri wa makosa ambayo aidha yanaipunguzia hadhi ripoti hiyo au kuifanya ionekane ya kupikwapikwa fasta fasta. Kwa taasisi kama hiyo yenye kaulimbiu inayoonyesha iko makini na ya kuaminika this is absolutely no good.

Kwa kuperuzi upesiupesi nimekutana na mushkeli zifuatazo.

  1. Typos. Ripoti ina utitiri wa typos as if imechapishwa na vile vi-secretarial bureau vya sinza. Mifano:
  • Ukurasa wa nane una swali kuhusu baadhi ya vijana waliojitokeza na wenye vipaji vya uongozi kuwa maraisi. Cha kushangaza kuna jina la Jakaya Kikwete na amekuwa wa mwisho with only 1% na kukubalika kwake in urban centers ni 0%. Sasa Synovate mtuambie hiyo 61% amepataje?
  • Ukurasa huo huo wa nane, who is Shyrose "Bhange"
  • Ukurasa huo huo tena wa 8 who the f**k is DR/RTA nafasi ya tatu
  • Ukurasa wa 11, who is "Chris" Mziray?
  • Ukurasa wa 11, who is "Fahoni" Dovutwa
  • Ukurasa huo huo wa 11, who is this Mutamwega "Mugaiwa"
  • Uk wa 12, who is "Wasila"
  • Uk wa 12 tena, who is "Nemroid" Mkono
2. Ukurasa wa 3 ni kuhusu utendaji wa serikali katika masuala ya jamii. Wakati JK na Kapuya wanatamba kuzalisha ajira zaidi ya 1,200,000. Utafiti huo wa Synovate unaonyesha 82% ya wananchi hairidhiki kabisa na utoaji wa ajira. Cha kushangaza zaidi watafiti wanasema eti watanzania wameridhika sana na utoaji elimu ya msingi na sekondari kutoka serikalini. Lakini ukiangalia jedwali uk wa 3 it is otherwise. Mimi nilifikiri kuridhika sana ni "Very satisfied" kama watafiti walivyoainisha kwenye jedwali lao.

3. Ukisoma uk. wa 12 inaonekana ni wazi watanzania hawaridhiki na utoaji wa huduma za jamii kwa serikali, on average approva iko on some 45%. Sasa inakuwaje kiongozi wa serikali hiyo hiyo aonekane yeye ni mchapa kazi???

4. Ukurasa wa 4 watafiti wanasema watanzania 78% wanaridhishwa na utendaji wa JK, na 77% na utendaji wa Shein (Kwa lipi?). Na kama hii nni kweli sasa mbona hii inakinzana na suala zima la uwajibikaji kama ambavyo watafiti wenyewe wameainisha. Inakuwaje watanzania hao hao wasioridhika na utendaji wa taasisi za serikali na na kuuona uko chini ya average of 45% waridhiswe na viongozi wa serikali hiyo hiyo????

5. Uk wa 4 kuna swali linauliza unaziamini vp taasisi zifuatazo, mojawapo ya hizo taasisi ni TUCTA, gimme a break TUCTA inaingiaje hapa kwa nini isiwe TAMICO, au kile chama cha wahadhiri. TUCTA haiwahusu wafanyakazi wote let alone watanzania wote. Tunachofahamu ni kwamba TUCTA imekuwa na msuguano na serikali kwa muda kiasi kuhusu maslahi ya wafanyakazi na wanaotakiwa kuiamini au kutoiamini ni wanachama wake sasa mtanzania mkulima aliyeko Maneromango, Tandahimba au Nkasi TUCTA inamuhusu nini?

My Take:
Kama hii ndiyo ripoti rasmi basi ingekuwa ni mchezo tungeomba turudishiwe kiingilio. Hawa jamaa wanaonyesha hawako serious kabisa na kuna kila dalili hii ripoti yao imepikwa.
 
Mods pls mnaweza kunirekebishia hiyo heading, bdala ya syovate isomeke synovate!
 
Utoto mtupu kamanda, Synovate wameshurutishwa kutoa matokeo yao haraka na mteja wao ili kuzidi kuangamiza saikolojia za wapiga kura ionekane kwamba mkulu ndiye chaguo.
Sisi tafiti yetu tutaifanya kwenye sanduku la kura walah!
 
Utoto mtupu kamanda, Synovate wameshurutishwa kutoa matokeo yao haraka na mteja wao ili kuzidi kuangamiza saikolojia za wapiga kura ionekane kwamba mkulu ndiye chaguo.
Sisi tafiti yetu tutaifanya kwenye sanduku la kura walah!

Yea yaani it's so funny!!!!!!!!
 
REDET walisema JK ana-drop na Kinana kukubaliana nao ila si kwa asilimia 100 na Dr. Slaa anapanda (Mwananchi 9/10/2010). Sijui REDET walifanya lini na Synovate lini, lakini kama REDET walianza, wakafuata Synovate basi ni kweli JK ana-drop tena kwa kasi, na kufikia 31 October 2010 atakuwa kwenye 40% na Dr. Slaa 45%!!!!!!!!!!!!!!
 
mapungufu ya utafiti wa synovate

wakuu kwa mujibu wa tovuti ya wavuti, nimeona nachoweza kukiita matokeo rasmi ya utafiti wa synovate. Bofya hapa for further details. Kinachoshangaza kuna utitiri wa makosa ambayo aidha yanaipunguzia hadhi ripoti hiyo au kuifanya ionekane ya kupikwapikwa fasta fasta. Kwa taasisi kama hiyo yenye kaulimbiu inayoonyesha iko makini na ya kuaminika this is absolutely no good.

kwa kuperuzi upesiupesi nimekutana na mushkeli zifuatazo.

  1. typos. Ripoti ina utitiri wa typos as if imechapishwa na vile vi-secretarial bureau vya sinza. Mifano:
  • ukurasa wa nane una swali kuhusu baadhi ya vijana waliojitokeza na wenye vipaji vya uongozi kuwa maraisi. Cha kushangaza kuna jina la jakaya kikwete na amekuwa wa mwisho with only 1% na kukubalika kwake in urban centers ni 0%. sasa synovate mtuambie hiyo 61% amepataje?
  • ukurasa huo huo wa nane, who is shyrose "bhange"
  • ukurasa huo huo tena wa 8 who the f**k is dr/rta nafasi ya tatu
  • ukurasa wa 11, who is "chris" mziray?
  • ukurasa wa 11, who is "fahoni" dovutwa
  • ukurasa huo huo wa 11, who is this mutamwega "mugaiwa"
  • uk wa 12, who is "wasila"
  • uk wa 12 tena, who is "nemroid" mkono
2. Ukurasa wa 3 ni kuhusu utendaji wa serikali katika masuala ya jamii. Wakati jk na kapuya wanatamba kuzalisha ajira zaidi ya 1,200,000. Utafiti huo wa synovate unaonyesha 82% ya wananchi hairidhiki kabisa na utoaji wa ajira. Cha kushangaza zaidi watafiti wanasema eti watanzania wameridhika sana na utoaji elimu ya msingi na sekondari kutoka serikalini. Lakini ukiangalia jedwali uk wa 3 it is otherwise. Mimi nilifikiri kuridhika sana ni "very satisfied" kama watafiti walivyoainisha kwenye jedwali lao.

3. Ukisoma uk. Wa 12 inaonekana ni wazi watanzania hawaridhiki na utoaji wa huduma za jamii kwa serikali, on average approva iko on some 45%. Sasa inakuwaje kiongozi wa serikali hiyo hiyo aonekane yeye ni mchapa kazi???

4. Ukurasa wa 4 watafiti wanasema watanzania 78% wanaridhishwa na utendaji wa jk, na 77% na utendaji wa shein (kwa lipi?). Na kama hii nni kweli sasa mbona hii inakinzana na suala zima la uwajibikaji kama ambavyo watafiti wenyewe wameainisha. Inakuwaje watanzania hao hao wasioridhika na utendaji wa taasisi za serikali na na kuuona uko chini ya average of 45% waridhiswe na viongozi wa serikali hiyo hiyo????

5. Uk wa 4 kuna swali linauliza unaziamini vp taasisi zifuatazo, mojawapo ya hizo taasisi ni tucta, gimme a break tucta inaingiaje hapa kwa nini isiwe tamico, au kile chama cha wahadhiri. Tucta haiwahusu wafanyakazi wote let alone watanzania wote. Tunachofahamu ni kwamba tucta imekuwa na msuguano na serikali kwa muda kiasi kuhusu maslahi ya wafanyakazi na wanaotakiwa kuiamini au kutoiamini ni wanachama wake sasa mtanzania mkulima aliyeko maneromango, tandahimba au nkasi tucta inamuhusu nini?

my take:
kama hii ndiyo ripoti rasmi basi ingekuwa ni mchezo tungeomba turudishiwe kiingilio. Hawa jamaa wanaonyesha hawako serious kabisa na kuna kila dalili hii ripoti yao imepikwa.

ahsante
 
Tatizo ccm na vibaraka REDET & SYNOVATE wako busy kuzuia maji ya mto kwa wavu wa kuvulia samaki! Shida ndiyo iko hapo.
 
SYNOVATE NI KAMPUNI ILIANZA LINI SHUGHULI ZAKE:
Synovate inaonekana ni kampuni 'iliyojikita ktk tafiti za kimasoko'. Synovate haijawahi kufanya utafiti thabiti wa kutabiri matokeo ya chaguzi za kisiasa nje ya Afrika.
Synovate ni kampuni isiyokuwa na ofisi ijulikanayo kama makao makuu yake (No Headquarterrs). Kampuni dizaini hizi ni kwa ajili ya kupromoti bidhaa za kibiashara na kwa Tanzania wamekuja kwa ulaji tu, maana hawana uzoefu wowote ktk siasa na chaguzi. Tizama hata timu yao iliyokutana na waandishi wa habari kutoa 'ripoti', wowote ni vijana wadogo kama mimi wenye uzoefu mdogo kiutendaji. Hebu sasa tutembelee webusaiti mbalimbali hapa chini kujiongezea haki ya kuwa na mashaka na hawa jamaa wa Synovate :
Synovate Kenya

google map
Physical Location: Riverside Drive Westlands
Postal Address: 68320
Postcode: 00200
City: Nairobi
Country: Kenya
Telephone: +254 20 445 0190 to 0196
Email: info@synovate.com
Fax: +254 20 442 6432
Website: Global Market Research | Synovate


Founded in 2003
No headquarters
62 countries
5,968 staff*
31,359 projects across the globe*
31 million+ interviews worldwide*
263,638 focus groups / in depth interviews*
*as of December 2009
We help our clients meet the commercial challenges of the information age by constantly creating innovative ways of gathering facts, and turning that data into strategic business insights. If there's no existing method of finding out what you need to know, we'll invent it.
International

Being international is not the same as being global. We are a company built on borderless cooperation. Our structure fits wherever our people are based and fits the needs of clients wherever they are based.

Integration

Integration means our geographies, practices, industry verticals and teams work as one to power Synovate's growth. Our strength lies in involving and learning from each other.

Innovation

Innovation is about challenging the norm and stretching boundaries in order to create a more efficient and better quality business. It's not just about research techniques and big initiatives; innovation can come from anyone and anywhere within our business.
Source: Advertising and Public Relations - Synovate Kenya

www.synovate.com Synovate Research Reinvented
Global market intelligence from the world's most curios people
Award-winning market research

We consistently strive to be the best. Our clients always come first, driving us to continually develop more innovative research solutions that predict actual business results. Our people, processes and solutions have been recognized around the world as being best in class
2010 Agency of the Year Award: Quantitative Research and Qualitative Research

Marketing Magazine
Synovate Hong Kong was voted the number one market research company by senior client-side marketers in Marketing Magazine's annual Agency of the Year Award. To be recognized by clients in this way reinforces our unyielding focus to create and deliver the most innovative research solutions to help solve their most pressing business issues. Above all, we thank our clients for helping us achieve this top honour.
Read more »

mrsnz.jpg

The Supreme Award 2010

MRSNZ Market Research Effectiveness Awards
Synovate New Zealand was recognised for work on projects with Air New Zealand, Commonwealth Bank of Australia, SPARC, Astra Zeneca and several other top companies.
Read more »

most.engaged.jpg

North America's 50 Most Engaged Workplaces 2010

I Love Rewards
Synovate Canada was honoured to be named one of North America's 50 Most Engaged Workplaces. It is our people that make our business a success, and we continually strive to create an environment conducive to personal growth.
Read more »

david.winton.award.jpg

David Winton Award for Innovation 2008

MRS
Synovate won the coveted 2008 UK Market Research Society David Winton award for Innovation in Methodology for the paper "A New Measure of Brand Attitudinal Equity based on the Zipf Distribution". Published in the International Journal of Marketing Research, the authors, including Synovate's Jan Hofmeyr, and Paul Holtzman, describe a new measure of attitudinal brand strength for use as a dependent variable in survey questionnaires. This new approach predicts share-of-wallet behaviour at the respondent level for all brands in a survey.
Read more »


Who could be the Synovate's client in this case? CCM, I presume Angalia rangi nyekundu na ni wazi wapo kibiashara zaidi na wanajenga mazingira ya kibiashara
 
Wana JF, salamu kwenu nyote.

Kama tulivyoona tarifa ya utafiti wa REDET, hayo yaho yamejitokeza kwa SYNOVATE
"STUDY zao sio representative enough". HAitoshi kutuambia uliwahoja wanawake na wanaume achilia mbali uchache wao...lazima watuambia NYUMRI na ELIMU ZAO na ikiwezekana UKEREKETWA WAO maana kuhoji watu kwenye mkutaano wa kampeni wa ccm lazima majibu waliyoyatoa yatajidhihirisha.

Baada ya kusoma ripoti ya SYNOVATE nashindwa kuelwewa vitu vichache...nitanukuuu gazeti la daily news kama walivyomnukuu bossi wa synoivate, shangaaaa....

1. It was conducted from September 5 to 16, this year. Leo ni 1 month tangu wamalize kukusanya data....majobu wanayatoa 1 month later kwamba ndio hali ilivyo sasa.

2. the study involved 2,000 respondents from 63 districts in 26 maana yake watu 2000/wilaya 63 = watu 31 hii ni adadi ndogo sana, less than idadi ya watu kwa kijiji kimoja ( maana yake ni watu wa mabalozi 2 maana ile dhana ya balozi 1 watu kumi ilishakufa...leo ni zaidi ya hiyo...

KAMA DATA ZAO NDIZO HIZI wanapata wapi kiburi cha kutuambia kuwa hii ndio hali halisi na kwamba kama uchaguzi ungefanyika leo basi CCM ingepata 90%?

NAsikitika taaluma ya utafiti imeingiliwa....
 
Mwakani tunatimiza miak 50 tangu tupate UHURU. Tumetawaliwa na watu wale wale kipindi chote hicho, na sasa tuko hoi. Hakuna Mtanzania asiyejua hilio.

Sidhani kama kuna Mtanzania wa kawaida anayependa tuanze miak 50 mingine na chama tawala kile kile kilichotudidimiza kasi hiki. Lazima tubadilishe, kwani tukichagua watu wale wale hali itaendelea kuwa ile ile ya UFISADI, USANII mtupu!

Sasa kama hivyo ndivyo, hao Watanzania wa ajabu ambao wameonwa na REDET na Synovate kwamba wanataka tusibadili chochote wako wapi?

Opinion poll zote ambazo ni huru (kwa maana ya kuwa hazipitii mkononi kwa mtu - ya JF, ya Daily News, ya Majira) zinaonyesha Slaa anapata kwenye 70%.

Bila shaka basi huu upuzi wa Redet na Synovate ni maandalizi ya wizi wa kura. Tuwe macho wananchi. Tumetawaliwa na CCM bila maendeleo kiasi cha kutosha. Sasa tunataka kuwangoa.

Itabidi CHADEMA, na sisi wananchi tutafute mbinu za kuzuia kuibiwa kura zetu. Kama hesabu za kura mahali zinaonyesha Slaa kapata 91, 100 basi na huko kwenye majumuisho ya mwisho ifike hiyo 91,100, na sio ifike 9,100 badala yake.
 
Hawa ndo pweza wetu, kama yule wa Kombe la Dunia.

Hata kama ni utafiti wa kubuni wangejitahidi kutumia usomi wao. Unatafiti, sample size yao haifikii hata 40% halafu wanatoa matokeo na kuyabariki. Wanajiita wasomi!.

Hapo UD jamani, hicho chuo kweli ndo kile kilichowatoa akina Museveni, Garang, nk. Hapo ndo walipokuwa akina Rodney? UD yenye patriotism imekuwa ni ya hypocrisy.

Kumbe ndo umuhimu wa kuwa na vyuo zaidi ya 30 nchini. UD mumetuangusha kabisa!

Niliwahi kuandika hapa kwamba Dr Benson wa REDET sioni kama ana qualities zozote za kuwa 'msomi.' Au hiyo PhD? No! Hata ukimuangalia usoni haonyeshi dalili za intelligence, na huyo ndo brain engine ya REDET. Anao ufahamu wa kawaida tu lakini si kwa kiasi cha kutushawishi kwamba kasema tusiyoyajua. Au alipewa favour kwa ukabila maana nasikia nalo ni tatizo.

Angalia hata arguments zake anapohojiwa kwenye TV. Jamani!

Poleni wanafunzi wake.
 
Matokeo ya utafiti yanatoa muongozo wa nani anaweza kushinda, na hayo yanaweza kubaki hivyo endapo upepo utabaki kuwa kama ulivyokuwa wakati utafiti unafanyika.Ikumbukwe kuwa katika ulingo wa siasa muda ni kitu muhimu sana kwani ndani ya wiki moja upepo wa siasa unaweza kutoa ishara tofauti na mwanzo.

Hebu tujikumbushe yaliyotokea wakati ule George Bush alipopambana na John Kerry wa Democratic huko Marekani.Mtakumbuka John Kerry aliendelea kuongoza tangu mwanzo wa kampeni hadi wiki ya mwisho ya kampeni.Lakini mambo yalibadilika zikiwa zimebaki siku saba kupiga kura,Pale ulipofanyika mdahalo wa mwisho, ambapo John nkerry aliulizwa swali moja la msingi kuhusu msimamo wake juu ya NDOA ZA JINSIA MOJA.

John kerry alijibu kuwa ndoa za jinsia moja ni uhuru na haki ya mwanadamu kuamua.Ikumbukwe kwamba John Kerry ni mkristu Mkatoliki kanisa ambalo linapinga kwa nguvu zote ndoa za jinsia moja. Kwa upande wake George W.Bush alipoona mwenzake kachemsha alipinga huku kionyeshwa kukerwa sana na swali lile kwa maaana kwamba halikupaswa kuulizwa kwani HAIKUBALIKI katika dini ya kikristu na kumbuka Bush ni muumini wa madhehebu ya Mashahidi wa yehova nayo yanapinga vikali.

Baada ya majibu hayo John KERRY upepo ulimwendea vibaya kuliko kawaida yake kwani wakatoliki wote walimhama kwa kuwadhalilisha kukubali kutoa uhuru wa watu kuamua badala ya kuzuia kwa nguvu zote.
NA HAPO KERRY ALIANGUKA NA KUMUACHA BUSH AKIPETA.

Ninachotaka kusema kwa upande wa Tanzania ni kwamba, kura za utafiti zilizotolewa kwa mfululizo kwa makampuni mawili tofauti, REDET NA SYNOVATE ndani ya masaa 72, haziwezi kutushawishi moja kwa moja kuwa JK ndiyo atakuwa mshindi, la hasha hizi zinawakilisha muda Fulani tu, zinaweza kubadilika kuendana na kampeni zinavyobadilisha upepo na pia wapiga kura kuendelea kuelimika kwa kusikiliza sera.
Kwa mfano:utafiti umefanyika septemba muda ambao JK alikuwa hajamnadi.Rostam, Mramba, Lowasa, chenge na wengine Mafisadi, tukumbuke sasa hivi watu wanalalamika kwa nini afanye hivyo hata wana CCM wenyewe.Rejea jana hotuba ya Sumaye pale AR-KKKT

Mazingira ya kura hizi pia yanaonyesha kupikwa kwa mtindo wa PROPAGANDA ILI KUWAKATISHA TAMAA WAPIGA KURA.
Tukumbuke JK nimtaalam wa PROPAGANDA na kwamba kaisomea anajua fika namna ya kuitumia na ndiyo maana yawezekana matokeao HAYA YAMEMSAIDIA KUMUINUA kwa kiwango Fulani.Lakini baada ya muda watu watasahau.

NINI KIFANYIKE
Wadau/chadema waendelee kuwaelimisha wapiga kura na kuyakataa kwa nguvu zote matokeo kwa kutumia PROPAGANDA PIA, maana dawa ya moto ni moto.Kwa kufuatilia kwangu nimendua matokea hayana IMPACT kwa wapiga kura ila faida ya haya matokeo kwa JK ni kwamba sasa anao uwanja uliobarikiwa kumuwezesha kuiba kura kwani atajitetea hata tifiti zimeonyesha ndiyo maana kafanya tafiti zaidi ya mbili ili kutoa uwanja mpana wa kujitetea.CHADEMA wajizatiti kuimarisha ulinzi wa kura na kuziba mianya yote .YOTE YANAWEZEKANA KWA KUMTUMAINI MUNGU
 
We must ask themselves, Who pays for the research and for whose interests! After knowing that, everything will be vivid! Kwa nini REDET, na Synovate watoe matokeo kama hayo. All I know ni kwamba wanatumikia kafiri mwanharamu apite ila wanajua ukweli ni upi! Aluta Continua
 
Yes kwa hiyo inamaaana mpaka 31 atakuwa negative! wanahaha hao kutafuta njia za kuiba duuu!
 
Hawa jaama REDET na synovate ni wapuuzi sana na wanatangaza upuuzi wao kwa kuwasaliti watanzania na mijitu kama hii ndio chanzo cha fujo kutokana na tamaa ya kula hela za mafisadi
 
Back
Top Bottom