Recipe ya Kauzu wa Kigoma

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,529
19,384
Natafuta Recipe nzuri ya kupika kauzu wa Kigoma; wenye kujua mapishi ya kauzu nisaidieni.
 
Kauzu wa kigoma wanapikwa kwa mafuta ya mawese, kitunguu, nyanya chungu na ndimu.
Umeanza, sasa nipe ukweli wote. Mawese, vitunguu, nyanya chungu na ndimu nitapata tu, wewe nipe ufundi wa kuvichanganya.
 
Sijawahi kuzinakili namba zao.
Ukipata namba ya mmoja wao nitumie haraka sana kwenye pm, nitawapigia. Ninaishi nje ya nchi na majuzi nilipata begi moja la kauzu kutoka Kigoma na natamani sana kuwala ile sijui jinsi ya kuwapika ili niwale.
 
Umeanza, sasa nipe ukweli wote. Mawese, vitunguu, nyanya chungu na ndimu nitapata tu, wewe nipe ufundi wa kuvichanganya.
Loweka dagaa kwa saa moja na uwaoshe kutoa mchanga. Weka mafua jikoni yakipata moto kaanga vitunguu, vikiwa tayari weka dagaa, malizia na nyanya chungu, ndimu na chumvi.
 
Loweka dagaa kwa saa moja na uwaoshe kutoa mchanga. Weka mafua jikoni yakipata moto kaanga vitunguu, vikiwa tayari weka dagaa, malizia na nyanya chungu, ndimu na chumvi.
Ni rahisi namna hiyo? basi Poa, nitakutumia kadi ya dinner siku mbili zijazo.
 
Kauzu wa Kigoma wanapikwa kwa mafuta ya mawese, kitunguu, nyanya chungu na ndimu.
Ngoja nikuulize swali kidogo; je nisipopata mafuta ya mawese naweza kutumia mafuta ya nazi au ya mzeituni?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom