Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,241
- 17,954
Toa vichwa (hii kwa mimi japo wenyewe wa Kigoma hawatoi),
Chemsha maji ya moto weka dagaa zako kiasi cha upendacho, acha wakae kwenye hayo maji ya moto huku waandaa viungo vingine,
Kata kitunguu maji cha kutosha,
Nyanya chungu na Bamia (ukipenda)
Karoti na Hoho (ukipenda)
Nyanya maji,
Ndimu au Limao,
Mafuta ya Mawese/Alizeti/Pamba/Mzeituni
Waweza kuweka tui la nazi au Karanga,
Chumvi,
Jinsi ya kupika,
Toa dagaa zako kwenye maji waweke pembeni,
Weka chombo chako cha kupikia kwenye moto, kikipata moto weka mafuta kiasi, weka dagaa zikaange kama dakika mbili au tatu maji maji yakauke, weka vitunguu maji, kaanga hadi viive, weka nyanya chungu, bamia, karoti na hoho, changanya vizuri mchanganyiko wako hadi viive, kisha weka nyanya maji na chumvi changanya acha ziive,
Baada ya dakika tano utaweka limao/ndimu na maji kidogo acha tena kwa dakika tatu hakikisha viungo vyako yaan nyanya chungu na bamia vimeiva kisha epua tayari kwa kuliwa,
Kama utahitaji kuweka tui la nazi au karanga basi hapo ndio muda wake sahihi, badala ya kuweka maji kidogo utaweka tui na kulipoza lisikatike hadi liive na tayari kwa kuliwa,
Waweza kula kwa Ugali, Wali hata Chapati.