Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Mwezi Novemba 2003, Baada ya vita kufukuta nchini Iraq, Rais wa Marekani alifanya ziara ya kushtukiza kwenye eneo la vita Yaani nchini Iraq
Kwa Wamarekani ile ilikuwa sehemu ya fursa ya kuitangazia Dunia kuwa ni kwa Jinsi gani wana uwezo wa kijeshi na kiulinzi wa kumsafirisha Rais wao hadi eneo la vita na akarudi salama hadi Marekani.
Jambo lile liliipa sifa Marekani ulimwenguni, wana habari wa Rais walikuja kutoa taarifa ile Rais Bush akiwa njiani kurudi Marekani na walionesha kwa Jinsi gani mbinu mbalimbali za kiulinzi zilitumika kurusha ile ndege hadi Iraq
Huku Tanzania jana Rais Samia kafanya ziara naweza sema ya ghafla nchini Msumbiji tena katika moja ya eneo korofi nchini mle yani jimbo la Pemba. Ziara hii haikutangazwa Kwa sababu wengi tumeshuhudia Rais akiwa anapokelewa nchini Msumbiji. Hii ilikuwa fursa katika mkakati wa Rebranding Tanzania.
Kama nchi ya Afrika inayojiinua na kutaka kuonekana duniani lazima tuioneshe dunia kuwa tuna uwezo mkubwa wa kiulinzi hadi kuweza kumsafirisha kiongozi wetu hadi eneo la vita.
Lile tukio lingeandaliwa hata makala kuonesha kwa Jinsi gani Rais alisafirishwa na hata mngeweza kuandaa kikao kifupi cha Mhe Rais na wanajeshi wetu walioko kule akizungumza nao. Tena hata yeye mngempiga kombati
Mnaweza dhani kuwa hizi zingekuwa ni mbwembwe tu ila amini nawaambia kwenye kujibrand ili kuionesha dunia nyie ni kina nani na mna uwezo gani, ni lazima mfanye vitu kama hivi ili kujitengeneza huko nje na kuvutia watu wa maana kuja kwenu
Muwe na weekend njema!
Zaidi soma: Rais Samia amefanya ziara ya kikazi ya siku moja Nchini Msumbiji (28/01/2022)