Rebranding Tanzania: Hongera Rais Samia, ni dhahiri Tanzania inaenda kuonekana kwenye ramani ya Dunia kiuchumi

Wacha hasira, hiyo ni alert tu umepewa, punguza kusifia kama mlevi hata kabla matunda ya unachokisifia hayajaonekana, mambo ya uchumi sio issue ya usiku mmoja.
Nilivyosema kuanzia 2025 tutaanza kuona maendeleo makubwa kutokana na programs uliekewaje?
2025 ni usiku mmoja?
 
Naona mbwembwe za siku mia....

Anajibrand kama bidhaa,kwa nani na lengo lipi? Watanzania awamfahamu au?
 
Amani iwe nanyi wadau!

Leo napenda kuongelea kuhusu suala la program aliyoibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kui rebrand nchi yetu na faida ya programu hii kiuchumi huko mbeleni.

Kwanza kabisa napenda kutoa pongezi kwa Mama Samia na huu ubunifu wake. Kwa uzoefu wangu, nchi chache sana duniani zilifanya programs hii na channel kubwa kama CNN. Nchi hizi ni Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, Singapore, Malyasia, India, Taiwan, Uturuki, China( kwa Hong Kong na Shanghai) na Pia nchi za Afrika za South Africa na Rwanda.

Kwa nilivyookuwa naona kipindi cha kuanzia miaka ya 2005 , program hii kwa CNN na BBC inahusisha vyombo hivi vikubwa vya habari vinavyotazamwa zaidi duniani kuandaa vipindi mbalimbali vinavyoelezea mambo mbalimbali ya nchi husika, ikiwemo utalii, siasa, viwanda biashara na maisha kwa ujumla.

Kama wanabodi wa JF mliopo humu, najua mtaafikiana na Mimi kuwa moja ya sababu za hizi nchi kupaa sana kiuchumi katika miaka kuanzia 2000- 2015 ni hizi nchi kujitangaza vizuri Kwa dunia kupitia program hizi maalumu.

Nchi ya karibuni kutumia hii program na kupata faida sana kiutalii ni Rwanda ambapo pamoja na kujitangaza kiutalii, walitumia program hii kutangaza bidhaa zao hasa kahawa ambayo kwa sasa inauzwa sana nchini Ufaransa ikiwemo kwenye uwanja wa Mpira wa klabu ya PSG.

Kupitia program hii pia Rwanda walienda mbele hadi kuingia mkataba na klabu ya Arsenal ambapo kwa sasa kila mwaka baadhi ya wachezajii na wafanyakazi wa Arsenal wana kwenda kutembelea Rwanda na kutangaza hayo dunia nzima.

Hizi ni akili kubwa sana ambazo kusema kweli Tanzania tulikuwa tumezikosa akiwa muda mrefu sana na hadi kufikia Leo kama tungezitumia mapema ni hakika tungekuwa mbali sana.

Hatuwezi kujisifu kuwa tuna madini tu Au mbuga au Misitu au bidhaa za shambani wakati soko kubwa na Hilo bidhaa ni nje ya nchi na sie hatujitangazi kwa dunia. Kusema kweli Mama Samia amenikosha sana kwenye hili na tuseme ukweli, endapo programu hii ikifanywa vizuri tutaona matunda makubwa sana kufikia 2025 kwa bidhaa zetu nyingi kujulikana na kupata masoko nje, watalii wengi sana kuja Tanzania na mapato ya Taifa kuongezeka na mwisho wawekezaji wengi serious na genuine kuja Tanzania na kuleta ajira na mapato mengi.

Katika kuelekea kuanza programu hii, ningependa mamlaka kuu za Tanzania kufanya ya yafuatayo;

1. Wizara ya Maliasili na Utalii
Tumieni programu hii vizuri hasa kuvitangaza vivutio vyetu. Mbuga za Serengeti, Ngorongoro, Manyara, Tarangire, Selous, Mikumi, Ruaha na hata Game reserves zetu

Mtangaze Pia Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Maua Kitulo.

2. Wizara ya Viwanda na Biashara
Kuna bidhaa kubwa na Nzuri zinatengenezwa Tanzania, Kuna viwanda vikubwa, vitangazeni kwa u sahihi na promo Nzuri kabisa

3. Wizara ya Uwekezaji
Tangazeni fursa za uwekezaji, kuanzia kilimo, madini, na hata kwenye miundombinu

4. Wizara za Nishati na Madini
Huu ndo wakati wenu sasa kutangaza madini yote yaliyopo Tanzania, kuanzia Tanzanite, Dhahabu, nikel, Almasi bila kusahau gesi na mafuta.

Tanzania, amkeni, wakati ni huu
Kwa kumbukumbu zangu, hakuna nchi ninayoijua iliyotumia vyema programu hii na unafeli. Tuitumie vyema.

Tuwatumie wataalamu wetu, wanaopiga kimombo vizuri, wadada mashallah wanaoweza kujieleza vizuri Maana hao ndo wanaovutia watu kuja kweli.

Nimalize kwa kusema Mama Samia, watu waliokudharau kuwa huwezi, utawashangaza sana. Kwa akili zako na mipango yako, naiona Tanzania ikiwa mbali sana kimaendeleo kuanzia 2025 na kuendelea.

Hongera Mama
Unaupiga Mwingi sana!


Nyongeza

5. Kwa Air Tanzania
Hiki pia ndo kipindi murua cha kutangaza Ndege zetu mpya na Nzuri ili zifahamike na kujulikana duniani. Tumieni hii fursa vizuri, tangazeni vizuri sana ndege zetu, ubora huduma kwa wanaozitumia bila kusahau bei Nzuri. Hii programu itazipa wateja ndege zenu.

6. Kwa Wafanyabiashara
Naomba msimuangushe Mama, mafanikio ya programu hii ndo mafanikio ya biashara zenu na uwekezaji wenu. Msiache kumuunga mkono kama kupitia hii programu.


Uzuri wa Mama ni kwamba amechukuwa mazuri yote ya Hayati na kuongezea uzoefu wake wa kufanya kazi kimataifa. Lakini vilevile anajua sana mawasiliano kuliko Hayati hii itasaidia nchi sana. Hayati katusaidia sana lakini Mama atafanya marekebisho machache tu na Tanzania itapaa sana
 
Uzuri wa Mama ni kwamba amechukuwa mazuri yote ya Hayati na kuongezea uzoefu wake wa kufanya kazi kimataifa. Lakini vilevile anajua sana mawasiliano kuliko Hayati hii itasaidia nchi sana. Hayati katusaidia sana lakini Mama atafanya marekebisho machache tu na Tanzania itapaa sana
Magufuli angeacha mambo yake ya ajabu na akafanya mazuri yake na kuendeleza mazuri ya wenzake bila kusahau kuruhusu ubunifu angekuwa vizuri sana.

Aliyotakiwa kufanya Magufuli ndo anayofanya Samia saivi. Ukali kiasi, umakini mkubwa, akili zaidi badala ya nguvu na ubunifu zaidi.
 
Back
Top Bottom