Real life problem!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Saa ya ukutani ya bwana khalifa iliishiwa betri kisha ikawa haifanyi kazi.Khalifa alitoa betri zilizokwisha na kuweka mpya kwenye hiyo saa,kisha ikaanza kufanya kazi.Lakini saa ya khalifa ilishapoteza majira!,khalifa hana redio,tv wala jirani yeyote wa karibu,anaishi peke yake kama jangwani.Alichofanya bwana khalifa ni kwenda kwa rafiki yake anayeishi kilometa 10 kutoka kwake ambaye pia ana saa.Alipofika kwa rafiki yake,alikaa kwa masaa 10 kisha akaanza safari kurudi kwake.Alipofika nyumbani kwake,aliweza kurekebisha muda wa saa yake.Je,aliwezaje/alitumia mbinu gani kurekebisha muda?
 
Unless kama inachukua saa moja kutoka kwake hadi kwa rafiki yake, otherwise nadhani mentor yuko sahihi kabisa.
 
aliweza kuirekebisha kwa kutumia kanuni aliyoifanya mwanzo, alifika kwake na kukaa masaa kumi then akajumlisha na ule muda wake wa kukaa kule masaa kumi, akapata muda maalumu wa kuiset saa yake..
 
tunawaza kusaka mahela nilipe nisepe no mo discussions sasa ww unataka tuumize vichwa weeeeeeee,y?kwann?
 
Leo umekujaje? Nipo kwenye gari nikishuka nitajaribu kurekebisha ya kwangu halafu nitarudi na jibu
 
inaweza kuwa hivi; Alinote muda kwenye saa yake kabla ya kuondoka, kisha akaanza safari, alivyofika kwa rafiki yake akanote muda pia na akakaa hadi masaa kumi, kisha akanote muda wakati anaondoka, assumption muda aliotumia kwenda na kurudi ni sawa, alipofika kwake akaangalia time lapse toka ameondoka hadi alivyorudi, masaa yaliyopatikana atatoa kumi kisha atagawanya kwa mbili,halafu ataset saa yake exact kwa muda aliondoka kisha ataongeza idadi ya masaa ambayo aliyatumia kurudi.

Nipe maksi na unigongee thanks.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom