RC Singida: Serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayehatarisha amani ya nchi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi amesema serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayehatarisha amani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.

Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo alipohutubia wananchi, wazazi na wanafunzi wakati wa sherehe za mahafali ya kuhitimu kidato cha nne kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mandewa wanaosali Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), mjini Singida jana.

"Kuna watu fulani fulani wanazungumza maneno yenye kila aina ya viashiria vya uvunjifu wa amani wakidhani huenda kipindi hiki cha kampeni serikali haipo kazini. Niwatahadharishe kamwe wasithubutu kufanya hivyo wataishia kwenye mkono wa sheria," alisema na kuongeza:"Mpaka mda huu serikali ipo, na Rais wetu sote bado ni Dk. John Pombe Magufuli.

Katika hatua nyingine, 'Mama' Nchimbi alimpongeza Rais kwa ujasiri,na maono yake kwa namna ya pekee alipofanikiwa kulivusha salama Taifa dhidi ya janga hatari la Corona.

"Haya maamuzi sio mepesi mepesi tazameni nchi nyingine zinavyoendelea kuteseka mpka sasa...kwakweli tunamshukuru sana Rais na Mwenyezi Mungu aendelee kumuongoza na kumjalia hekima na busara ili mapenzi yake ya dhati kwa watanzania wenzake yazidi kushamiri."
 
Mmmmh. Hapo alitakiwa kuwaasa vijana wetu wakawe raia wema baada ya kuhitimu masomo kwa ngazi husina wJiepushe na bangi.,madawa ya kulevya uvivu. Mimba za utotoni na zaidi wajiepushe na fisiemu. Ila hoyo mengine atuachie sisi wazazi wao tulolipa ada.
 
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi amesema serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayehatarisha amani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu..
Wewe Rehema wewe acha hizo! Kwa wale wahenga kama miye! Alikuwepo RC Iringa Dr Kleruu aliwaletea wahehe za kuleta akauawa kama mbwa akawekwa kwenye buti ya gari lake mwenyewe!

Alikuwa mwingine Mara Nsa Kaisi. Wakurya waliizunguka ikulu akatoroka kwa mtumbwi kupitia Ziwani. Hizo zote zilikuwa zama za giza la chama kimoja kilichoshika hatamu na mwenyekiti wa kuabudiwa pamoja na fikra zake. Sembuse leo hii wewe mama acha hizo utaumia sana trust me
 
Kwa sasa wanaohatarisha amani ya nchi ni ccm na jeshi la polis, muda wote polis ni kubambikizia kesi wafuasi wa upinzani, Kule tarime wamewabikizia kesi ya timu yote ya kampeni ya John heche, kinachonishangaza viongozi wa chadema wanalalamika tu kimyakimya.walipaswa kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya jeshi la polis.
 
Kwa sasa wanaohatarisha amani ya nchi ni ccm na jeshi la polis, muda wote polis ni kubambikizia kesi wafuasi wa upinzani, Kule tarime wamewabikizia kesi ya timu yote ya kampeni ya John heche, kinachonishangaza viongozi wa chadema wanalalamika tu kimyakimya.walipaswa kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya jeshi la polis.

Police wanafanya kazi nzuri Sana ya kuibomoa ccm kwa kupandikiza chuki ili watz waendelee kuichukia ccm,polisi wanaihujumu ccm,cheki ilivyotumika kuuwa upinzani, kushughulikiwa kwa upinzani na police kwa miaka 5 kumesaidia Sana kuujenga upinzani.
 
Alpoteuliwa tu kuwa RC wa Singida alimweka Mganga Mkuu wa wilaya lock up masaa 24 eti kwa sababu hajatatangaza karantini kutokana na kipindupindu! Kwa hiyo RC ndiye anajua cha kufanyika kuliko Mganga Mkuu. Alipotoka tu lock up yule Daktari akatoa taarifa ya masaa 24 kuacha kazi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom