Singida Mpya ya kijani inawezekana - Suphian Juma

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
134
551
SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA - SUPHIAN JUMA NKUWI.

Aprili 17, 2024 nimezindua kampeni ya kupanda miti mkoa mzima wa Singida NILIPOZALIWA iitwayo "SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA" ambapo kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) tumepanda miti 460 shule ya Msingi MULAGWE kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye udhibiti wa mabadiliko ya Tabia nchi ikizingatiwa Singida ni moja ya mikoa ongozi katika ukame nchini.

SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA tumeizindulia Shule ya MULAGWE iliyopo Kijiji cha Minyughe, Wilaya ya Ikungi kwasababu nina historia nayo. Wanyaturu wana msemo; "Munyamuikha njokha uguandia umighuu" (Mmulika nyoka huanzia miguuni). Eneo la shule hii lisilopungua hekari 15 nililitoa bure mimi na familia yangu kama sehemu ya kuunga mkono Serikali kwenye Sekta ya elimu.

Na kipekee nimeishukuru Serikali kwa kuiita shule hii " Mulagwe" kwani MULAGWE ni jina la babu yangu ambaye alikuwa MTEMI akiongoza Kata yote ya Minyughe wakati wa ukoloni.

Nimewasihi wanafunzi kuilea miti hiyo kwani ndio uhai wao na inaweza kuwafanya kutimiza ndoto zao kuu na kuwafanya kuwa yeyote bora vyoyote muda wowote watakavyo maishani.

Aidha nimetoa rai kwa wananchi waliohudhuria na wote wa mkoa wa Singida kuanza utamaduni wa kupanda miti mitano mitano kila kaya kila mwaka ili sote tutairejeshe Singida yenye uoto wenye asili inayovutia.

Shukrani tele kwa ushirikiano usiomithilika kutoka TFS chini ya Mhifadhi Mwandamizi Samweli Matura, Viongozi wa Chama Tawala wakiongozwa na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Singida Bi. Martha Mlata.

Viongozi wa Serikali chini ya Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Dendego (kipekee Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ikungi Mheshimiwa Kijazi aliyewakilishwa na Mkuu wa Idara ya Mazingira, Bwana Richard, Shule ya Msingi Mulagwe chini ya Mkuu wa Shule ndugu Kimaro na Mwalimu wa Mazingira Bwana Lameck, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Mzee Daniel Njoghomi).

Kongole nyingi kwa wananchi wote wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Minyughe, Mzee Noah Ihonde, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Minyughe Wazazi, Mzee Saidi Chima (Said Stori) na Mwenyekiti UWT Kata ya Minyughe, Bi. Elizabeth (Nyazulu) kwa kuipa baraka tele kampeni hii ya SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA.

Mwisho kwa umuhimu, nawashukuru wadau wote walionipa sapoti ya hali na mali kufanikisha uzinduzi huu, na kwa chapisho hili nawakaribisha wadau wengine wa MAZINGIRA POPOTE DUNIANI kunipa ushirikiano wa hali na mali kuendelea kuifanikisha kampeni hii ili sote tutairejeshe Singida mpya ya kijani kibichi.

Michango inaweza kutumwa:

Tigopesa: 0717027973 Jina Suphian Nkuwi

CRDB: 0152519454800 Jina SUPHIAN JUMA NKUWI

Asanteni,

Suphian JUMA NKUWI,
MWANZILISHI - SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA.
Aprili 18, 2024
Singida.
+255717027973

KAZI IENDELEE.

IMG_20240418_120518.jpg
IMG_20240418_120714.jpg
IMG_20240418_120726.jpg
IMG_20240418_120718.jpg
 
Mtu wa kwanza kuisifia zaidi serikali na sio mtu mmoja mmoja

Kuhusu upandaji wa miti duniani ni lazima sana ila kusifia upandaji mdogo hivyo unatia mashaka huna habari na Dunia kabisa

Mwaka 2019 Ethiopia walipanda miti milion 350 kwa siku moja YES siku moja tu
Na hiyo ilikuwa ni rekodi iliyovunjwa duniani
Sasa kusema kila Kaya wapande miti mitano mitano ni michache sana

Kuhusu watoto kuitunza ni sawa ila inahitaji maji
Lazima awachimbie na kisima hapo
Na kama ana malengo yakuifanya Singida kijani inabidi achimbishe mabwawa makubwa kwa ajili ya umwagiliaji

Ethiopia kulikuwa na ukamwe 98% lakini leo ukipita kwenye anga lao na ndege utashuhudia jinsi iliivyo kijani
 
SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA - SUPHIAN JUMA NKUWI.

Aprili 17, 2024 nimezindua kampeni ya kupanda miti mkoa mzima wa Singida NILIPOZALIWA iitwayo "SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA" ambapo kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) tumepanda miti 460 shule ya Msingi MULAGWE kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye udhibiti wa mabadiliko ya Tabia nchi ikizingatiwa Singida ni moja ya mikoa ongozi katika ukame nchini.

SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA tumeizindulia Shule ya MULAGWE iliyopo Kijiji cha Minyughe, Wilaya ya Ikungi kwasababu nina historia nayo. Wanyaturu wana msemo; "Munyamuikha njokha uguandia umighuu" (Mmulika nyoka huanzia miguuni). Eneo la shule hii lisilopungua hekari 15 nililitoa bure mimi na familia yangu kama sehemu ya kuunga mkono Serikali kwenye Sekta ya elimu.

Na kipekee nimeishukuru Serikali kwa kuiita shule hii " Mulagwe" kwani MULAGWE ni jina la babu yangu ambaye alikuwa MTEMI akiongoza Kata yote ya Minyughe wakati wa ukoloni.

Nimewasihi wanafunzi kuilea miti hiyo kwani ndio uhai wao na inaweza kuwafanya kutimiza ndoto zao kuu na kuwafanya kuwa yeyote bora vyoyote muda wowote watakavyo maishani.

Aidha nimetoa rai kwa wananchi waliohudhuria na wote wa mkoa wa Singida kuanza utamaduni wa kupanda miti mitano mitano kila kaya kila mwaka ili sote tutairejeshe Singida yenye uoto wenye asili inayovutia.

Shukrani tele kwa ushirikiano usiomithilika kutoka TFS chini ya Mhifadhi Mwandamizi Samweli Matura, Viongozi wa Chama Tawala wakiongozwa na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Singida Bi. Martha Mlata.

Viongozi wa Serikali chini ya Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Dendego (kipekee Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ikungi Mheshimiwa Kijazi aliyewakilishwa na Mkuu wa Idara ya Mazingira, Bwana Richard, Shule ya Msingi Mulagwe chini ya Mkuu wa Shule ndugu Kimaro na Mwalimu wa Mazingira Bwana Lameck, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Mzee Daniel Njoghomi).

Kongole nyingi kwa wananchi wote wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Minyughe, Mzee Noah Ihonde, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Minyughe Wazazi, Mzee Saidi Chima (Said Stori) na Mwenyekiti UWT Kata ya Minyughe, Bi. Elizabeth (Nyazulu) kwa kuipa baraka tele kampeni hii ya SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA.

Mwisho kwa umuhimu, nawashukuru wadau wote walionipa sapoti ya hali na mali kufanikisha uzinduzi huu, na kwa chapisho hili nawakaribisha wadau wengine wa MAZINGIRA POPOTE DUNIANI kunipa ushirikiano wa hali na mali kuendelea kuifanikisha kampeni hii ili sote tutairejeshe Singida mpya ya kijani kibichi.

Michango inaweza kutumwa:

Tigopesa: 0717027973 Jina Suphian Nkuwi

CRDB: 0152519454800 Jina SUPHIAN JUMA NKUWI

Asanteni,

Suphian JUMA NKUWI,
MWANZILISHI - SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA.
Aprili 18, 2024
Singida.
+255717027973

KAZI IENDELEE.

View attachment 2967191View attachment 2967196View attachment 2967198View attachment 2967199
Kazi itakayofanya ukumbukwe CCM kuzuri hata shavu kidogo limetoka sasa!
 
SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA - SUPHIAN JUMA NKUWI.

Aprili 17, 2024 nimezindua kampeni ya kupanda miti mkoa mzima wa Singida NILIPOZALIWA iitwayo "SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA" ambapo kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) tumepanda miti 460 shule ya Msingi MULAGWE kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye udhibiti wa mabadiliko ya Tabia nchi ikizingatiwa Singida ni moja ya mikoa ongozi katika ukame nchini.
Kwamba ninyi watanzania hamma uwezo wa kujifanyia mambo yenu kwa faida yenu kulingana na mahitaji? Yaani uwezo wenu wa kufikiri, kutenda, kupimga na kushauri ulishakufa na hivyo mlicho baki nacho ni kuunga mkono tu.
Nje ya kuunga mkono hakuna muwezalo?
 
Back
Top Bottom