RC Mongella marehemu Omela Wangwe hakupigwa na wananchi wenye hasira. Simamia haki ili waliomuua wakamatwe

Ndugu acha ujinga,
Ina maana wewe ukisema alipigwa ndani ya ofisi ya kata ndio ushahidi tosha. Wewe nani?...
Bwege wewe usie na akili hata kiduchu. Nimekuuliza unao uhakika kuwa aliiba milango?

Mtendaji wa kata anaruhusiwa kisikiliza kesi ya jinai?

Wewe mwizi akikuibia kama ukitaka kuchukua sheria mkononi shauri yako.

Mpuuzi usie na akili unajifanya kujadili masuala usioyajua.
 
Mkuu Mongela hebu rudisha imani ya wananchi kwa serikali badala ya kukumbatia huu uhuni wa mapolisi. Tenda haki ili Mola ane apate kukulinda na kukupa heshima.
 
Mambo ya kihuni nakutakia mema !!. Kikubwa haya ndiyo mambo jamii inayalalamikia. Kuna watu walioko ndani ya taasisi zetu , wako juu ya sheria.

Ujue tunapolalamikia TL kupigwa risasi 38 mchana saa saba lakini hamna uchunguzi mpaka leo !!. Ndugu zake wanajisikaJe ?!. Hilo ndiyo imemkumba huyo Omela wa huko buswelu
Nashukuru Odhiambo cairo umemkumbusha mwanajukwaa mwenzetu huyu chagu wa malunde kuhusu TUNDU LISSU kushambuliwa na kikundi cha wasiojulikana chini ya Bashite. Siku zote tukimuambia Serikali inahusika anatuambia LETE USHAHIDI. Nilimuambia siku moja kuwa asubiri siku mtu wake wa karibu auliwe ndiyo atajuwa kuwa nchi hii inaendeshwa kiholelea. Yamempata tayari
 
Huihui2 natamani kuona Chadema na viongozi wake wanachukua hatua kuhakikisha waliompiga risasi TL wanajulikana, kama Polisi Tanzania hawatachukua hatua juu ya ishu ya TL zipo hatua za kufuata kuanzia hapa nyumbani mpka UN. Kulalamika kwenye media haisaidii huku mmekunja miguu.
 
Nashukuru Odhiambo cairo umemkumbusha mwanajukwaa mwenzetu huyu chagu wa malunde kuhusu TUNDU LISSU kushambuliwa na kikundi cha wasiojulikana chini ya Bashite. Siku zote tukimuambia Serikali inahusika anatuambia LETE USHAHIDI. Nilimuambia siku moja kuwa asubiri siku mtu wake wa karibu auliwe ndiyo atajuwa kuwa nchi hii inaendeshwa kiholelea. Yamempata tayari
Na yamemkuta huyu Kada . Inaonekana huyo Omela yaonekana ni ndugu ye wa karibu. Ndiyo ameujua uchungu wa uonevu.

Wanachama wa Cdm, Act na Cuf wameumizwa vya wengine wameuliwa kisa tu, wanaitikadi tofauti na wenye nchi . Wengi leo wapo magerezani, kwa kesi za kubumba, Lakini @ Chagu wa Malunde hajawahi kujisikia uchungu alionao leo kwa ndugu yake kuuliwa !!.

Nchi hii ni ya watu wote. Wanaotuhumu na wanaotuhumiwa. Na si kweli kuwa wanaotuhumu wana haki kuzidi wengine
 
Ni mwaka sasa tangu marehemu Omela Wangwe auwawe kwa kupigwa na Mwanajeshi ndani ya ofisi ya kata ya Kahama wilayani Ilemela.

Marehemu hakukamatwa kwenye tukio lolote, bali alipigiwa simu ili aje aeleze wapi alipata milango aliyokuwa anaiuza kama dalali na alikamatwa na watuhumiwa wanne na kupelekwa ofisi ya kata Kahama Ilemela baada ya kupigiwa simu aje asaidie upelelezi.

Alitokea mwanajeshi ambae alikuwa amepanga njama za kupata watu waliomuibia TV kwake. Na huyu mwanajeshi akishirikiana na migambo wa kata kwa ruhusa ya mtendaji wa kata walimpiga Omela Wangwe wakimhisia kuiba Tv ya mwanajeshi,ambae baadae alifariki Sekoutore Hospital.

Polisi kirumba walidanganya kuwa alipigwa na wanachi wenye hasira kali. Mke wa marehemu alikuona wewe mkuu wa mkoa. Uliagiza upelelezi ufanyike. Mwezi wa nne mwaka huu wapelelezi walienda Kata ya Kahama na walichukua maelezo watu walioshuhudia hili tukio,ukweli ulifahamika kuwa Omela Wangwe alipigwa ndani ya ofisi ya kata.

Jalada la kesi lilifunguliwa kwa mwendesha mashitaka wa mkoa wa Mwanza, mke wa marehemu aliambiwa watuhumiwa walitakiwa wakamatwe ili hatua stahiki zichukuliwe. Kwa mujibu wa mke wa marehemu Rco wa Mwanza alitoa amri watuhumiwa wasikamatwe.

Mke wa marehemu alikuja kukuona wewe mkuu wa mkoa ili umsaidie,na inasemekana bado mnafanya uchunguzi. Uchunguzi gani mnafanya kwa mtu aliyeuliwa kwa kupigwa mchana kweupe ndani ya ofisi ya kata?

Wewe kama mkuu wa mkoa umeshindwa hata kufanya mkutano wa hadhara ili kupata ukweli juu ya hili tukio?

Cc Wapenda haki wote.

Pia soma
-
Mwanajeshi awatesa vijana na mmoja kufariki akiwatuhumu kumwibia tv yake. Je, hii ni haki?

- Polisi Mwanza mnaoshughulikia hii kesi, kuweni makini hii ni awamu ya tano, mtakuja kuumbuka
Mimi nakushauri peleka hili suala kwa Waziri Mkuu au kwa Mhe. Raisi mwenyewe.
 
Hawa jamaa sio wa kawaida, akiongozwa na katibu tawala wa mkoa wake wanakauli mbiu yao, "Duniani sheria, haki mbinguni", pathetic.
 
Back
Top Bottom