RC Mongella marehemu Omela Wangwe hakupigwa na wananchi wenye hasira. Simamia haki ili waliomuua wakamatwe

tindo kwenye hili naomba utofautishe ishu za kisiasa na zinazohusu wananchi wanyonge...

Haki inaangalia mwanasiasa au asiye mwanasiasa? Kwahiyo ukiwa mwanasiasa una haki ya kuuwawa, maana kwa tafsiri yako ukiwa mwanasiasa sio mnyonge? Huna unalotetea hapa bali unataka kujionyesha tu kuwa una utu, wakati huna lolote.
 
Hujanielewa,acha kupanic dogo. Wanasiasa na watu wakawaida sote tuna haki.

Lakini wanasiasa wana backup kubwa. Utalinganisha na mtu ambae huma mbele wala nyuma.

Hivi unadhani akifa kiongozi wa Cuf,Act au Cdm ndani ya ofisi ya kata au apigwe ndani ya ofisi ya kata, nini kitatokea?
Tumia utu na busara.
 
Nini kitatokea, kapigwa Lisu risasi kwenye makazi ya wabunge yenye ulinzi 24hrs, kipi kilitokea?
Kuna mtu alifurahia juu ya Tundu kushambuliwa?

Hata Omela kila mtu amesikitika,je kwa nini mke wa marehemu alimuona Rc Mongella?
 
tindo uongo na ukweli hautangamani. Huwezi kuamini,polisi kirumba waliandika barua ya uongo kuwa Omela wangwe alipigwa na wananchi. Mkuu wa mkoa alituma wapelelezi na kila kitu kiko wazi. Hapa kuna tatizo kubwa.
Kama ngazi ya mkoa imeshindwa bhas either kuna maelekezo kutoka juu au ngazi ya mkoa yenyewe iko complicated. Anayesema yeye ni kiongozi wa anayependa haki na kiongozi wa wanyonge asikie kilio hiki, sio kutamka tu hayo maneno katika vipaza sauti
 
Maelezo yako hayajitoshelezi.

Unasema wezi wa milango mara TV, ila unashindwa kusema kama au ikiwa Omela Wangwe alikuwa mwizi wa milango.

Je, ni kweli Omela aliiba milango? Historia yake ni mwizi? Kwanini wamhisi na wamwite yeye na sio wewe mwanzisha uzi?

Taarifa yako imeegemea upande mmoja zaidi kujaribu kushinikiza jambo lifanyike. Tambua jeshi na wanajeshi hawataniwi na mkuu alishasema chezea vingine usifike mahali ucheze na mali za jeshi hii ni dharau. (Alikuwa akiongelea waliokopa matrekta SUMA JKT hawalipi).

Watu wenye hasira kali sio lazima wawe 20, wanaweza kuwa watatu au wanne.

Wizi ni mbaya na unarudisha nyuma maendeleo binafsi na taifa. Wezi wanafaa kunyang'anywa vitu na silaha zao harakaharaka na kuvisalimisha polisi ili kuhakikisha hawarudii tena kuiba.
 
Ni mwaka sasa tangu marehemu Omela Wangwe auwawe kwa kupigwa na mwanajeshi ndani ya ofisi ya kata ya Kahama wilayani Ilemela.....
Hapa ndipo shida yetu ilipo, ukweli wenye mashaka. Unaposema amefia kwenye ofisi ya kata na hapo hapo unasema amefikia Sekou Toure, unaweka mashaka makubwa kwenye maelezo yako. Inapunguza umakini wa ufuatiliaji. Tutulie na kutoa maelezo ya kina na haja popote haki ilipoonekana kuminywa
 
Unajua kusoma?
 
Suala sio kufurahi, hatua gani zimechukuliwa?
Lissu alishambuliwa, lakini kabla ya hapo alisema hadharani kuna watu wanamfuatilia na anawajua. Alipaswa kuripoti polisi ili hao watu wakamatwe.

Ameshambuliwa, wewe na wanaCdm mmechukua hatua gani? Hata kama hamna imani na polisi wa ndani, mngeanza nao alafu kama wanazingua hatua zinazofuata zichukuliwe.

Hata aliemuua Mwangosi alikuwa analindwa lakini waandishi wa habari walikomaa mpaka kikaeleweka.
 
Maelezo yako hayajitoshelezi.

Unasema wezi wa milango mara TV, ila unashindwa kusema kama au ikiwa Omela Wangwe alikuwa mwizi wa milango.

Je, ni kweli Omela aliiba milango? Historia yake ni mwizi? Kwanini wamhisi na wamwite yeye na sio wewe mwanzisha uzi?

Taarifa yako imeegemea upande mmoja zaidi kujaribu kushinikiza jambo lifanyike. Tambua jeshi na wanajeshi hawataniwi na mkuu alishasema chezea vingine usifike mahali ucheze na mali za jeshi hii ni dharau. (Alikuwa akiongelea waliokopa matrekta SUMA JKT hawalipi).

Watu wenye hasira kali sio lazima wawe 20, waaweza kuwa watatu au wanne.

Wizi ni mbaya na unarudisha nyuma maendeleo binafsi na taifa. Wezi wanafaa kunyang'anywa vitu na silaha zao harakaharaka na kuvisalimisha polisi ili kuhakikisha hawarudii tena kuiba.
Tumia akili unapokuja kujibu hoja za wanaume. Nini maana ya kuwa na kuwa na utawala wa sheria. Kama ni mwizi mtu akifika ofisi ya kata ndio apigwe? Sheria za Tanzania zinaruhusu kuchukua sheria mkononi?

Acha kushabikia upuuzi wa kijinga,hata kama ukiiba mali za jeshi, sheria zinasema unatakiwa upelekwe mahakamani ufungwe.

Kwa nini wanadanganya alipigwa na wananchi? Si waseme kweli kuwa alipigwa ndani ya ofisi ya kata kisha akafariki akiwa hospital.

Unao uhakika kuwa aliiba milango?
 
Ndugu acha ujinga,
Ina maana wewe ukisema alipigwa ndani ya ofisi ya kata ndio ushahidi tosha. Wewe nani?

Anayesema alipigwa na wananchi wenye hasira kali haijalishi ni wawili au watatu, haijalishi ni nje ya ofisi au ndani, wanaweza kuwa sahihi kama wewe unavyojiona sahihi kulazimisha unachokiamini.

Hauwezi kutulazimisha kuamini hicho unachokiamini bila ushahidi. Hata wenzio wa upande wa pili wana hoja ambazo pia hatuwezi kuziamini bila ushahidi.

Suala la mwizi na kitendo cha kuiba, hukumu ya upendeleo ni kifungo, lakini adhabu sitahiki ni kifo.

Mimi nikimpata mwizi amejichanganya kwenye anga zangu nammaliza.

Unataka utawala wa sheria, kwani yeye wakati anaiba hakujua kuna utawala wa sheria na kuiba ni kosa kisheria na anavunja sheria. Kwanini mimi nikivunja sheria iwe taabu. Mwizi na auawe tu hakuna namna.
 
Back
Top Bottom