RC Mongella marehemu Omela Wangwe hakupigwa na wananchi wenye hasira. Simamia haki ili waliomuua wakamatwe

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Ni mwaka sasa tangu marehemu Omela Wangwe auwawe kwa kupigwa na Mwanajeshi ndani ya ofisi ya kata ya Kahama wilayani Ilemela.

Marehemu hakukamatwa kwenye tukio lolote, bali alipigiwa simu ili aje aeleze wapi alipata milango aliyokuwa anaiuza kama dalali na alikamatwa na watuhumiwa wanne na kupelekwa ofisi ya kata Kahama Ilemela baada ya kupigiwa simu aje asaidie upelelezi.

Alitokea mwanajeshi ambae alikuwa amepanga njama za kupata watu waliomuibia TV kwake. Na huyu mwanajeshi akishirikiana na migambo wa kata kwa ruhusa ya mtendaji wa kata walimpiga Omela Wangwe wakimhisia kuiba Tv ya mwanajeshi,ambae baadae alifariki Sekoutore Hospital.

Polisi kirumba walidanganya kuwa alipigwa na wanachi wenye hasira kali. Mke wa marehemu alikuona wewe mkuu wa mkoa. Uliagiza upelelezi ufanyike. Mwezi wa nne mwaka huu wapelelezi walienda Kata ya Kahama na walichukua maelezo watu walioshuhudia hili tukio,ukweli ulifahamika kuwa Omela Wangwe alipigwa ndani ya ofisi ya kata.

Jalada la kesi lilifunguliwa kwa mwendesha mashitaka wa mkoa wa Mwanza, mke wa marehemu aliambiwa watuhumiwa walitakiwa wakamatwe ili hatua stahiki zichukuliwe. Kwa mujibu wa mke wa marehemu Rco wa Mwanza alitoa amri watuhumiwa wasikamatwe.

Mke wa marehemu alikuja kukuona wewe mkuu wa mkoa ili umsaidie,na inasemekana bado mnafanya uchunguzi. Uchunguzi gani mnafanya kwa mtu aliyeuliwa kwa kupigwa mchana kweupe ndani ya ofisi ya kata?

Wewe kama mkuu wa mkoa umeshindwa hata kufanya mkutano wa hadhara ili kupata ukweli juu ya hili tukio?

Cc Wapenda haki wote.

Pia soma
-
Mwanajeshi awatesa vijana na mmoja kufariki akiwatuhumu kumwibia tv yake. Je, hii ni haki?

- Polisi Mwanza mnaoshughulikia hii kesi, kuweni makini hii ni awamu ya tano, mtakuja kuumbuka
 
Ahaa, mitano inahusiana vipi na haki za watanzania?
Tunashukuru kwa kuamua kujitenga na uovu, kwa taarifa yako wapinzani wengi wameuwawa na kupata vilema, huku viongozi na Mamlaka husika zikifumbia macho mambo hayo toka utawala awamu hii imeingia madarakani. Lakini kwa bahati mbaya umejitenga na uovu kinafki, wakati tayari shetani ameshapata nguvu japo za muda mfupi.
 
tindo uongo na ukweli hautangamani. Huwezi kuamini,polisi kirumba waliandika barua ya uongo kuwa Omela wangwe alipigwa na wananchi. Mkuu wa mkoa alituma wapelelezi na kila kitu kiko wazi. Hapa kuna tatizo kubwa.
 
Ahaaa,jaduong acha mambo ya kihuni.
Mambo ya kihuni nakutakia mema !!. Kikubwa haya ndiyo mambo jamii inayalalamikia. Kuna watu walioko ndani ya taasisi zetu , wako juu ya sheria.

Ujue tunapolalamikia TL kupigwa risasi 38 mchana saa saba lakini hamna uchunguzi mpaka leo !!. Ndugu zake wanajisikaJe ?!. Hilo ndiyo imemkumba huyo Omela wa huko buswelu
 
Jaduong,kuna mtanzania aliyefurahi kilichompata TL? TL alikuwa na nafasi ya kuwakabaka waliokuwa wanamfuatilia mpaka akachimba mkwara.

Vipi huyu Omela Wangwe ambaye alipigiwa simu, na kuuliwa kwa kuhisiwa kuiba Tv? Mke wake muuza nyanya sabasaba ana nini cha kubishana na wauaji? Mke wake amepambana kudai haki, leo hii anadhurumiwa!

Tl wapi amedai haki ya kushambuliwa? Acha ushabiki.
 
tindo uongo na ukweli hautangamani. Huwezi kuamini,polisi kirumba waliandika barua ya uongo kuwa Omela wangwe alipigwa na wananchi. Mkuu wa mkoa alituma wapelelezi na kila kitu kiko wazi. Hapa kuna tatizo kubwa.

Nasema hivi, kwa sasa umeamua kijitenga na uovu, lakini wapinzani wameuliwa, kuachwa na vilema, ikiwemo kutupwa jela. Na Mamlaka ndio zimekuwa zikipindisha ukweli ili haki za wananchi zipotee. Hakuna mamlaka sasa hivi hazitoi taarifa za uongo ili kupoteza haki za wananchi. Hata uchaguzi wa juzi si mamlaka zote zimeshiriki uharamia ule? Watu si wameuwawa na vyombo vya kimamlaka?

Chama cha CUF si wametoa taarifa leo kuwa huko Liwale kuna unyama wa hali ya juu, na vyombo vya dola ndio vinaendesha hayo? Huko kwa waziri Mkuu na spika, wote si wamepita bila kupingwa baada ya washindani wao kufanyiwa unyama? Unashangaa hayo wakati kwa sasa chini ya awamu hii hiyo ndiyo tabia?
 
Nasema hivi, kwa sasa umeamua kijitenga na uovu, lakini wapinzani wameuliwa, kuachwa na vilema, ikiwemo kutupwa jela. Na Mamlaka ndio zimekuwa zikipindisha ukweli ili haki za wananchi zipotee. Hakuna mamlaka sasa hivi hazitoi taarifa za uongo ili kupoteza haki za wananchi. Hata uchaguzi wa juzi si mamlaka zote zimeshiriki uharamia ule? Watu si wameuwawa na vyombo vya kimamlaka?...
tindo kwenye hili naomba utofautishe ishu za kisiasa na zinazohusu wananchi wanyonge.

Nakuambia Polisi kirumba walidanganya marehemu alipigwa na wananchi wenye hasira baada ya kukamatwa akiiba.
Na waliandika barua ukiiona ni aibu tupu.

Mke wa marehemu alimuona mkuu wa mkoa,ukweli ukajulikana,baada ya jalada kufika kwa mwendesha mashitaka ni mizengwe.
 
Back
Top Bottom