JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mgomo uliofanywa na Wabeba Mizigo hao, jana Asubuhi Juni 23, 2025 ikidaiwa kuwa wanadai jumla ya kiasi cha Tsh Milioni 18.
Akizungumzia hali hiyo awali, Meneja IFS Consulting Limited Kagera, Godfrey Ismail amesema “Changamoto ni stahiki za Wafanyakazi wetu kudai fedha zao, tunaendelea kupambana, mpaka sasa tumefanikiwa kupata Sh Milioni 6.”
Baada ya maelekezo ya Mkuu wa Mkoa, wabeba mizigo hao wameendelea na kazi wakiisubiri, Jumatano Juni 25, 2025 kujua kitakachotokea.
Ilivyokuwa awali ~ wafanyakazi Wanaobeba mizigo Bandari ya Bukoba wafanya mgomo wakidai malipo yao
Chanzo: Azam TV