RC Chalamila: Rais Samia amewaona waliodandia Treni

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiona ‘video clip’ ya abiria wa treni Jijini Dar es Salaam maarufu kama treni ya ‘Mwakyembe’ wakid andia na kuning’inia milangoni usiku.

Kutokana na hatua hiyo, RC Chalamila amesema amefanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya reli na treni hiyo leo ili kuzungumza na abiria wenyewe wamueleze kero na changamoto wanazozipitia.

“Mheshimiwa Rais Samia ameona Watu ambao wanadandia hii treni na alipokuwa ameona hilo na ndiye aliyeniambia ebu fuatilia hilo, hiyo treni ikoje kwahiyo mguu huu ni mguu wa Rais Samia Suluhu Hassan yeye ndiye aliyeliona hilo na ameona Watu wakidandia usiku usiku na nimekuwa nikipigiwa simu

Millard Ayo
 
RC mzima hawezi detect na kugundua matukio mkoani mwake ..hadi rais ampe maelekezo ? Lilivyo boya linasema weakness zake......huyu hamnazo....hana ubunifu mkoa umemzidi x 10 times...
Halafu hajui unaweza kuwa mtego anajisifa ujinga eti huu mguu wa Raisi, kwahiyo Raisi asingeona hilo tatizo lingedumu miaka mingapi!?,na mangapi hajayaona Raisi!?,huyu jamaa anaonekana anapenda sana ma camera halafu anafanya kazi kichawachawa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiona ‘video clip’ ya abiria wa treni Jijini Dar es Salaam maarufu kama treni ya ‘Mwakyembe’ wakid andia na kuning’inia milangoni usiku.

Kutokana na hatua hiyo, RC Chalamila amesema amefanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya reli na treni hiyo leo ili kuzungumza na abiria wenyewe wamueleze kero na changamoto wanazozipitia.

“Mheshimiwa Rais Samia ameona Watu ambao wanadandia hii treni na alipokuwa ameona hilo na ndiye aliyeniambia ebu fuatilia hilo, hiyo treni ikoje kwahiyo mguu huu ni mguu wa Rais Samia Suluhu Hassan yeye ndiye aliyeliona hilo na ameona Watu wakidandia usiku usiku na nimekuwa nikipigiwa simu

Millard Ayo
Kwani mkurugenzi wa TRC hawamjui? Yaan stunt zingine hizi ni za kichko kabisa
 
Ndo mwelekeo kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app

Sina shida na hiyo Mkuu.
Ni kweli kwamba Mheshimiwa asingeona hii clip na kuwaona wananchi wakigombea train wasingekuja na mkakati wa kutatua hii kero?

Hapo Kuna nia ya kweli ya kutatua tatizo kweli?
 
Utendaji kazi wa kichawa ni tatizo hapa nchini.
Umeniwahi. Ni nani katuloga jamani? Hivi nchi ina mazezeta kama haya halafu eti tutarajie maendeleo? Yeye kakalisha li-kitambi lake mpaka rais aone kasoro ndiyo akurupuke? Huu ni ujuha wa level ya juu sana. Ubaya ni kuwa wananchi hawaoni ujuha kama huu au hata wakiona hawachukui hatua...
 
Back
Top Bottom