JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Akizungumza leo Julai 31, 2025, katika hafla ya uzinduzi wa Bandari Kavu ya Kwala, Kibaha mkoani Pwani, Kunenge ameeleza kuwa idadi ya viwanda katika mkoa huo imeongezeka kutoka 1,387 kabla ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan hadi kufikia viwanda 1,681, huku viwanda vikubwa vikiongezeka kutoka 59 hadi 97.
Ameongeza kuwa viwanda hivyo vimezalisha zaidi ya ajira 21,000 za moja kwa moja, na zaidi ya ajira 60,000 zisizo za moja kwa moja, huku bidhaa mbalimbali zikiendelea kuzalishwa kwa wingi.