Rayvanny afunguka kuhusu Harmonize, Paula, lebo ya NextLevel na mengine kuhusu muziki wake

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,528
7,381
Akiwa katika live interview na radio namba moja kwa sasa WASAFI FM, Ray amefunguka yafuatayo

" Wakati ananikandamiza (Hamonaizi) na kuchochea kwa kusema nimekosea sikuwa najua Chuki yake inatoka wapi . Lakini imekuja kunishangaza sana kuja kuona kumbe yeye ndio anafanya mabaya zaidi ya aliyokua nayakemea "

" Alikuwa anawapigia simu viongozi wa serikali akipambania nifungwe miaka 30...mimi nna mtoto, nna wazazi nna watu wananitegemea hata kama ni chuki hapa alikuwa amevuka mstari"

"Sina muda wa kutafuta Kiki, sihitaji Kiki ili kuuza muziki wangu kwasababu Napendwa na Mashabiki . Bali lengo ni kumfunza kuwa alichokifanya si sahihi na anatakiwa kuomba radhi "

"mimi kwenye mambo ya kiki sipo ila inapofikia point mtu kaingia kwenye maisha yangu siwezi kukaa kimya mimi nitaingia kwenye haki"

" Nikifanya show zangu anaenda mtandaoni kukejeli....alishawai iita show yangu mkutano wa hadhara....wakati mimi na yeye hatukuwai gombana"

"Kuna watu amewaumiza kwa alichokifanya, Familia ya Watu inatukanwa mitandaoni, nilitegemea aombe radhi lakini ndio kwanza akaitumia kama Kiki na kwenda kutoa wimbo "


"Mimi sishindani na mtu. Huyo mtu wanaesema nashindana nae angalia Subscribers wake na wangu, angalia Views zangu na Zake, angalia mauzo yangu na yake ..
Mimi ndio msanii ninaengoza kwa Kusikilizwa Boomplay na Kutazwamwa YouTube kwa Mwaka huu "


"Kipindi anamatatizo na Uongozi mara nyingi alikua ananipigia kulalamika . Na mara nyingi nilikua nakaa upande wake, ila tukizungumza kwenye simu na kuwasema Viongozi wanapokosea mwenzangu akawa ananirekodi kwenye Simu..... Mimi napigania kitu cha kwako alafu wewe unaenda kunirekodi una Plan gani?"

"Kuhusu Sound From Africa, nina Video 20 mpaka hivi sasa ambazo zipo tayari . Yaani mapambano ndio kwanza yameanza na kuanzia sasa hizi ni kudondosha Mawe tu "

" Siwezi kumuongelea Paula kwa heshima ya Familia yake . Kwasababu nikiongea chochote watu wanaweza kutafsiri vibaya na ikawaletea matusi mitandaoni, sitaki kitu hicho kitokee "

Kuhusu kama ana mahusiano na Paula " Paula anaenda chuo hivi karibuni mambo mengine mtayaona wenyewe wala hamtaitaji kupewa maelezo...Naweza ongea kwa nia njema watu wakatafsiri tofauti wakaenda kuwatukana"

" Next Level Music ni ya kwangu...yule Mzimbabwe ni rafiki yangu na business partner wangu hausiki kwenye umiliki wa lebo"

"Sipendi kuzungumzia au kuweka wazi mambo yangu ninayofanya . Kama nikitaka naweza kufungua Lebo kama Next Level zaidi ya moja , na hivi karibuni nazindua Club ndani ya Mbeya"
 
Tuhuma za unafiki alishazisemea pia Rich mavoko , Konde ni wa kupiga nyundo kabisa Yule si wa kumhurumia , Bora umnyanyue Marioo kuliko huyo mtu pori
mnafiq sana ndio maana vitu vyake havinyooki anaishi kwa kutegemea huruma za mashabiki.
 
Video zipo za kumwaga zinatolewa taratibu.
Kwa iyo mdau mmakonde kafanya kipi kibaya mpaka van kuvujisha picha zake za utupu.....iyo kupelekwa polisi ama na mbona kesi yenyewe iliisha juu kwa juu...


Ukikaa chini na kutafakari utaona kabisa nani ni mbaya kwa mwenzie
 
Hilo Nyakyusa halina akili..mashabiki wako ni wa Mondi..Toka Wasafi tuone
laiti wangekua mashabiki wa momd, basi mondi ndo angeongoza mauzo platform zote, ray anamzid mond mauzo kwenye platform zote isipokua youtube pekee.

hapa ni sawa nakusema ibra amshinde mauzo boss wake kwenye digital platform alafu ulete kisingizio mashabiki ni wa boss wake akati mwenye mashabiki hao kashindwa kufanya hivo.
 
Ukweli Mchungu Rayvanny kimziki hamgusi Harmonize. 😂
Mbona msanii anayeongoza kuwa na viewers wengi youtube ni Rayvanny ukimtoa diamond, ukija kwenye mauzo ya mziki Rayvanny ndio msanii anayeongoza kuwa na stream nyingi kuliko msanii yoyote wa Tz kwenye platform zote za kuuza mziki huo mziki aliyompita ni upi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom