Rav 4 vs Xtrail

Mkuu inaonesha gari unazonunuaga ni vimeo....uliza wangapi wenye magari walishawahi kubadili hizo mambo zaidi ya kuskia tu kwa watu kama nyie

soma uelewe....nimesema natumia hizo gari kibiashara....kwa mwezi inaenda mtwara,tabora,mwanza,mikumi,serengeti etc[zaidi ya km 5000] kwahio ni vitu vya kawaida kubadili vitu vya kwenye matairi.
 

Kwenye uuzaji RAV4 linauzika kirahisi kuliko hiyo xtrail
 

Kweli SBT japan magar yao mazuri sana hayasumbui kabisa na unapata gar haijatembea kilometre nyingi
 
Nimefuatilia kwa karibu mjadala na kura yangu japo si muuliza swali naona nimeshawishika na x-trail. Naomba wenye uzoefu mnilinganishie kati ya x-trail na ford escape, tuseme ford ya kati ya 2001-2006, 1980cc. katika ulaji mafuta, spare, comfortability na durability
 
Hata mimi jamani hako ka uoga ka kununua magari ya Nissan ninako lakini nazipenda sana and not only Nissan napenda sana magari ya Honda lakini vitisho ninavyovipata kwa the so called wajuzi wa magari imenibidi niendelee na mi Toyota.
 
Nissan xtrail mpango mzima..
Kwa ujumla nissan wana magari mazuri sn yani
 
Sio kweli, ulaji wa mafuta wa xtrail ni around 10km/L, usipotoshe wenzio

Tuwe specific basi, mm nina Rav4 3s engine ya mwaka 1996. Nikienda mkoa inakula wastani Wa 12 km/lita ya gas. Ila hapa Dar nafoleni hizi za Mbezi Kimara inakula 5lts per litle- hapo full Ac kila mahala.
Sasa spea, rav 4 bei chip, tena watakuambia original, Bt hazidumu. Garage kila mara, hasa chini huko kwenye mineso.
Sijatumia e trail Bt nadhani is far better in everything than Rav 4. Maana hata hizi Rav 4 new models za engine AZZ hazifanyi vyema barabarani kuliko Extrail, pia zinakula mafuta zaidi maana Na 2400cc. Second generation Rav 4 japo zinakula mafuta vizuri kidogo lkn nyingine ni 2wheel na pia hazifanyi vyema kwenye lough roads as compared to Extrail.
Kama nilivyosema, Etrail sijaitumia Bt ninavyofuatilia Na kusoma naona is far better tht Rav4
 
Habari wadau,
Naombeni msaada wenu kati ya rav4 na xtrail..ipi iko nzuri brbrb ie fuel consumption,speed,durability ,spares na ubora,kama 4wd au 2wd?

Kwa spare na mafuta ni bora uagize rav 4( recreational active vehicle 4wd) ila baada ya kuona watu wengi hawapendi full time 4wd kama jina la rav 4 lilivo, waliamua kuzifanya rav4 nyingi kuvutia mbele tu. Ila nyingi pia ni AWD kitu ambacho si faida kwa consumption ya mafuta. Kama mara nyingi hutumii 4wd chukua rav4 ila angalia second generation kwani ina VVTi (variable valve timing with intelligence) ambayo inaongeza fuel efficiency.

Nissan xtrail ina 4wd engageable (yani inavutia mbele, FF, by default ila ina button ya 4wd ukitaka kutumia. Ni vizuri kwa hivo ila engine yake ni more consuming than rav 4). spare zake ni ngumu ila ikikuharibikia jiandae kutumia pesa nyingi kuirekebisha.
 
nina xtrail ya 2004 toka sbt japan, hii ni ya ukweli sana barabarani kwenye comfortability na stability vilevile inachapa sana mwendo. sina uzoefu na rv4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…