Rasimu ya sera mpya ya Elimu; Tunachezewa kama yale ya Kilimo kwa vijana

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,698
4,693
Nimemsikiliza waziri wa elimu akisisitiza kwamba sera mpya inatimiza matakwa ya rais. Sasa hapo ndo mwanzo wa ujinga wetu. Rais siyo mtaalamu wa elimu. Sera siyo ya rais, kwa nini sera mpya iwe inayotoa majawabu kwa rais?

Sera hii kama itapitishwa kama kawaida yetu kwa vision ndogo ya aina hii, ni sawa na kilimo cha Waziri Bashe.

Mitaala yetu haina tatizo, tatizo ni ufundishaji. HUwezi kutegemea waalimu wanaonyanyasika kukufundishia watoto wako. Pesa zote zinapelekwa kwenye siasa. Ktk kila kijiji leo hii tuna wanasiasa wengi kuliko waalimu na madaktari, halafu unategemea sera iinue elimu. Tuache hadithi za akina KIshimba Bungeni. Elimu ina misingi yake na haitrakiwi kuwa ni komedi za bungeni ndo zitunge sera na mitaala.

Nimeisoma rasimu, inasikitisha. Ni sera inayoleta makundi nchini; watakaosoma kwa Kiswahili na wale watakaosoma kwa kiingereza. Uhakika ni kwamba wao, hawa viongozi, watasomesha watoto wao kwa kiingereza. Je, nani wanamtungia elimu kwa Kiswahili?

Ni kwa nini hatukusema iwe ni Kiswahili kila mtu? Kwa sababu viongozi wetu wanaamini kiingereza kwa watoto wao ni bora zaidi. Kwa kuogopa hadithi za kisiasa wameamua kutunga mifumo miwili. Huu ni ujinga.
 
Binafsi sijaelewa nini inamaanisha ngoja waje wezangu lakini Nina maswali machache
1: Sera ni ipi?

2: anayekubali kubadilisha sera bila idhini ya raisi ni nani

3: ufundishaji wa namna gani?

4: Nani kasema walimu hakuna tanzania?
 
Nimemsikiliza waziri wa elimu akisisitiza kwamba sera mpya inatimiza matakwa ya rais. Sasa hapo ndo mwanzo wa ujinga wetu. Rais siyo mtaalamu wa elimu. Sera siyo ya rais, kwa nini sera mpya iwe inayotoa majawabu kwa rais...
Kafundishe mtoto wako Kiswahili
 
Mi nasema hawa mawaziri ndo wanaharibu wizara zote. Sielewi kwa nini madaraka ya kitaalamu yamehamishwa toka kwa makatibu wakuu, kwenda kwa mawaziri. Siku hizi mawaziri ndo wanajionesha kuwa wataalamu wa wizara bdala ya makatibu wakuu.

Mramba aliharibu elimu, Bashe anaharibu kilimo, Mkenda anaharibu elimu..... sijui nini kinampa raha rais kuwa na mfumo wa aina hii.
 
Nimewasikiliza watoa mada.
Rasimu iko vizuri sana, wanufaika ni shule binafsi.

Mfano kuondoa Biology na Geography katika ulazima wa kusoma

Kuongeza masomo kwenye tahasusi

Kufanya kiingeleza kusomwa kuanzia darasa la kwanza

Walimu kuanza internship ya mwaka mzima

Walimu kuwa na bodi itayowapa vyeti

Wanafunzi kusoma kwa lazima hadi Form 4
 
Nimemsikiliza waziri wa elimu akisisitiza kwamba sera mpya inatimiza matakwa ya rais. Sasa hapo ndo mwanzo wa ujinga wetu. Rais siyo mtaalamu wa elimu. Sera siyo ya rais, kwa nini sera mpya iwe inayotoa majawabu kwa rais?

Sera hii kama itapitishwa kama kawaida yetu kwa vision ndogo ya aina hii, ni sawa na kilimo cha Waziri Bashe.

Mitaala yetu haina tatizo, tatizo ni ufundishaji. HUwezi kutegemea waalimu wanaonyanyasika kukufundishia watoto wako. Pesa zote zinapelekwa kwenye siasa. Ktk kila kijiji leo hii tuna wanasiasa wengi kuliko waalimu na madaktari, halafu unategemea sera iinue elimu. Tuache hadithi za akina KIshimba Bungeni. Elimu ina misingi yake na haitrakiwi kuwa ni komedi za bungeni ndo zitunge sera na mitaala.

Nimeisoma rasimu, inasikitisha. Ni sera inayoleta makundi nchini; watakaosoma kwa Kiswahili na wale watakaosoma kwa kiingereza. Uhakika ni kwamba wao, hawa viongozi, watasomesha watoto wao kwa kiingereza. Je, nani wanamtungia elimu kwa Kiswahili?

Ni kwa nini hatukusema iwe ni Kiswahili kila mtu? Kwa sababu viongozi wetu wanaamini kiingereza kwa watoto wao ni bora zaidi. Kwa kuogopa hadithi za kisiasa wameamua kutunga mifumo miwili. Huu ni ujinga.
Mkuu wala usiwaze sana. Hii nchi ni ya kipuuzi sijapata kuona. Hivi masomo ya ufundi yatawezaje kufundishwa ilhali walimu wa ufundi na miundombinu ya kufundishia ni gharama sana kuisimika? Ikiwa capitation grant tu ni rahisi lakini haipelekwi shuleni kama inavyotakiwa itawezekanaje mtaala mpya kutekelezwa kwa ufanisi? Hii nchi imelaaniwa na Mungu.
 
Nimewasikiliza watoa mada.
Rasimu iko vizuri sana, wanufaika ni shule binafsi.

Mfano kuondoa Biology na Geography katika ulazima wa kusoma

Kuongeza masomo kwenye tahasusi

Kufanya kiingeleza kusomwa kuanzia darasa la kwanza

Walimu kuanza internship ya mwaka mzima

Walimu kuwa na bodi itayowapa vyeti

Wanafunzi kusoma kwa lazima hadi Form 4
Sasa hapa kuna uzuri gani au na wewe umerogwa?
 
Mitaala yetu haina tatizo, tatizo ni ufundishaji. HUwezi kutegemea waalimu wanaonyanyasika kukufundishia watoto wako.
Mkuu una tatizo..

Jitafakari. Mtaala wetu ni wa kikoloni, uliokuwa ukituandaa kuwa servants of the colonial masters..think of being employed as you were prepared with no life skills..

A stupid colonial curriculum is what is felt all over Africa continent. That u go to school to be employed than harnessing individual's talent.

Amka.. muda ni SASA. TUMECHELEWA Sana.
 
Tutahangaika sana na haya mambo ya mitaala sijui na mkorokoro gani.

Kenya, Uganda na hata Rwanda kwa sasa wanatuzidi kielimu kwa mbali sana. Kwa nini tusicopy na kupest hiyo mitaala na hata mbinu za kudeliver pia?

Leo hii ukimsimamisha mkenya wa kawaida au mganda wa kawaida na anaejiita msomi wa kitanzania ukawahoji jambo lolote la kuhusu nyanja yoyote majibu yatakuambia hii nchi siyo ya kusomeshea mtoto.

Utapata critical thinking, kujiamini, exposure ya mambo mengi sana kwa hawa majirani zetu.

Sasa kama mitaala haitajibu hizi changamoto itatulazimu kuandaa mtaala mpya 2031 mama atakapokuwa ameondoka.
 
Mkuu una tatizo..

Jitafakari. Mtaala wetu ni wa kikoloni, uliokuwa ukituandaa kuwa servants of the colonial masters..think of being employed as you were prepared with no life skills..

A stupid colonial curriculum is what is felt all over Africa continent. That u go to school to be employed than harnessing individual's talent.

Amka.. muda ni SASA. TUMECHELEWA Sana.
Wewe unafuata yale ya kule bungeni unapokutana na watu wa komedi. Au hivi vi-clip vya video vinavyohoji kusoma grasshopper. Nchi gani duniani ambayo haimfundishi mtoto mambo ya aina hiyo? ulaya wanafundisha hadi historia ya Timbuktu!

Wewe leo hii unasema elimu ya mkoloni! Kisayansi gravity, density, force, nk. vitabaki ktk mafunzo ya vijana milele. Ndo mwanzo wa fikra pevu za sayansi.

Tatizo ni uongo munaofundisha kwenye huo uzalendo wenu. Mkwawa anapigwa risasi, mijitu inasema alijinyonga. Majina ya akina Kambona yanafutwa makusudi ili kuinua umuhimu wa Nyerere. Okelo anaisaidia Zanzibar, munakuza umuhimu wa Karume. Hovyo!!
 
Naileta kwenu kama nilivyopokea.

MAPENDEKEZO YA RASIMU YA RIPOTI YA KAMATI YA KITAIFA YA MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU* .

Na Baltazari Luhanga.

1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).

3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa Kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa shule za English medium.

5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa.

11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na
uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
-kilimo na ufugaji
-umakenika
-biashara na ujasiriamali
-sanaa bunifu
-elimu ya michezo
-ufugaji wa nyuki
-uchimbaji wa madini
-urembo

13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
-hisabati
-elimu ya biashara
-kiingereza
-historia ya Tanzania na maadili

15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
-cheti cha amali (NACTVET)

16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.

19. Coding itafundishwa shule ya msingi.

20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.

21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.

25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
-sanaa
-lugha
-muziki
-michezo
-TEHAMA

28. Masomo ya O-level yatakuwa:
-biology
-physics
-chemistry
-history
-geography
-historia ya Tanzania na maadili
-hisabati
-kiswahili
-english
-elimu ya biashara
-utunzaji wa taarifa za fedha
-computer science
-bible knowledge
-elimu ya dini ya kiislamu etc

29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.

31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

32. Walimu watakaofundisha mkondo wa amali (ufundi) watakuwa Wahitimu wa kozi mbalimbali za amali na watapewa astashahada
(cheti) ya ualimu huo kwa miezi 6.

33. Vyuo vya elimu ya juu vitaanzisha kozi za ualimu wa uandisi, urembo, uvuvi, sanaa bunifu nk. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika maeneo hayo ya ufundi.

34. Kutakuwa na internship kwa walimu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumaliza ualimu ili wawe
na umahiri zaidi. Kisha walimu watapata leseni.

35. Mafunzo kwa vitendo ya walimu tarajali yatafanyika katika shule zilizo karibu na vyuo vya ualimu ili zifanyike kwa umakini zaidi.

36. Kutakuwa na motisha kwa walimu na upandaji wa madaraja utakuwa kwa utaratibu mzuri.

37. Bodi ya usajili wa walimu itaanza kufanya kazi.

38. Utekelezaji wa mtaala mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 itaanza kwa awamu kwa darasa moja moja katika kila level. Hii itasaidia kwenda sawa na bajeti kwasababu kuanza kwa madarasa yote na levels zote ni gharama kubwa sana. Utekelezaji utaanza mwaka 2024 kama sera na mtaala zitapitishwa kama ilivyo.
 
Back
Top Bottom