Serikali imekamilisha maandalizi ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

SERIKALI KUWA NA IMANI NA SERA YA TAIFA YA UGATUAJI WA MADARAKA KATIKA MAWANDA YA USHIRIKISHWAJI WA WADAU

Serikali imekamilisha maandalizi ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ambapo wadau mbalimbali wameshirikishwa na kutoa maoni yao ambapo Rasimu hiyo imewasilishwa katika ngazi ya maamuzi kwa mapitio na maelekezo zaidi.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Deogratius Ndejembi wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Mhe. Ally Mohamed Kassinge alilouliza kuwa “Je, lini Serikali itatunga Sera ya Ugatuaji wa Madaraka na kutunga Sheria ili kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mtaa? Mhe. Kassinge

“Serikali imekamilisha maandalizi ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ambapo wadau mbalimbali wameshirikishwa na kutoa maoni yao ambapo Rasimu hiyo imewasilishwa katika ngazi ya maamuzi kwa mapitio na maelekezo zaidi” Mhe. Ndejembi

Kufuatia Majibu hayo ya serikali yakamsimamisha mbunge huyo kuuliza maswali mawili ya Nyongeza kutokana na kuwa na mashaka na majibu hayo ya Serikali katika Mawanda ya ushirikishwaji wa Wadau huku akiisisitiza Serikali kuwa makini katika utungaji wa Sera hiyo ndiyo itakayoenda kujibu ibara ya 146 ya Katiba Ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ni kiwango gani wadau katika Mikoa, Wilaya na Halmashauri lakini kwa upeke wa madiwani wameshirikishwa katika utungaji wa sera hii?, swali la Pili Je? serikali iko tayari kutoa Commitment hapa Bungeni kwamba katika mchakato huu kabla ya maamuzi sera hii ipitiwe na Wabunge kama tulivyopitia sera ya elimu kwa lengo la kuboresha utungaji wa Sera hii? Kassinge

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri Ndejembi amemtoa shaka kwani Serikali inaimani kubwa na sera hiyo na Wizara hiyo itaendelea kusimamia sera hiyo ya ugatuaji wa madaraka kwenye Halmashauri ili ziweze kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yao wenyewe kwa kushirikiana na wataalamu ambao wanapelekwa na hapa anaeendelea kutoa majibu.

“Baada ya mwongozo huu kufanyiwa mapitio tutaileta kwenye kamati ya Bunge ya TAMISEMI ili nao waweze kupitishwa kwenye ule mwongozo ambao upo lakini tutabaki katika D by D kwajili ya kuwapa nguvu waheshimiwa madiwani kufanya maamuzi yao katika Halmashauri zao” Ndejembi.

ftgyuhuhwer.jpg
yxfcyguuhwqer.jpg
 
Back
Top Bottom