Rashid Othman: Umeshindwa Jiuzulu!

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,327
2,000
Hadi gazeti la Guardian litutangazie kuwa Waziri wetu ameficha Bilioni kisiwani Jersey (thanks Yebox2) wao kina RO walikuwa wapi?

Hadi Kamati Teule ilipotuambia rasmi kuwa RDC ni kampuni hewa RO na timu yake walikuwa wapi?

Niendelee kuorodhesha ushahidi wa uzembe uliokithiri na uvivu wa kufikiri wa taasisi nyeti ya Usalama wa Taifa? Kama wameshindwa kugundua matukio ya economic sabotage yanayoendelea nchini wana faida gani? Hii ya kusafiri na Rais na kutumia vi ear pieces na makoti marefu kama vile wao Secret Service?

Rashid Othman ajiuzulu kwa ajili ya Usalama wa Taifa!!!

yes I said it!
 

Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,848
0
Hadi gazeti la Guardian litutangazie kuwa Waziri wetu ameficha Bilioni kisiwani Jersey (thanks Yebox2) wao kina RO walikuwa wapi?

Hadi Kamati Teule ilipotuambia rasmi kuwa RDC ni kampuni hewa RO na timu yake walikuwa wapi?

Niendelee kuorodhesha ushahidi wa uzembe uliokithiri na uvivu wa kufikiri wa taasisi nyeti ya Usalama wa Taifa? Kama wameshindwa kugundua matukio ya economic sabotage yanayoendelea nchini wana faida gani? Hii ya kusafiri na Rais na kutumia vi ear pieces na makoti marefu kama vile wao Secret Service?

Rashid Othman ajiuzulu kwa ajili ya Usalama wa Taifa!!!

yes I said it!

RO ni nani vile?
 

Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,738
1,225
Mama,

RO ni Head wa Intelligence Tanzania.

Mwanakijiji sasa RO kazi yake namba moja ni kuhakikisha usalama wa mafisadi, wewe unategemea nini?
 

Nurujamii

JF-Expert Member
Jun 14, 2007
414
195
Na ndio maana hata mhariri wa mwanahalisi (Kubenea) imedhihirika wazi waliohusika kumhujumu na kutaka kumtoa roho ni vijana wa RO ili kuwalinda Mafisadi (akina Lowasa)
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,327
2,000
ndio maana aondoke afuatane nao huko wanakotumbua fedha za Taifa hili. How can an intelligence agency be unintelligent?
 

KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
1,225
Mwanakijiji kwenye Makala yako moja ya nchi imetekwa kuna aliyetamka kuwa unajua aliyeiteka?

Mmojawapo ni RO
 

Nikifufukammekwisha

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
260
0
Mzee Mwanakijiji,

Kama the whole system kuanzia juu kabisa is incompetent kama matukio yanayorindimana yalivyotuonyesha na yatakavyoendelea kutuonyesha, how would you expect RO to be different?
 

Ant Ru

Member
Apr 16, 2008
12
0
Kaka Mwanakijiji ,

Kwanza nakupa Hongera, Huu ndio ujasiri tunaoutaka humu ndani ya JF.

Na nilazima awachie ngazi ama auelezee umma Manufaa gani Umma unapata kwa kuwepo kwake hapo, Kama anashindwa hata kupata dondoo tu ya mambo hasa katika wakati wa Utandawazi.

Iweje Usalama wa MIAKA ile ya mwalimu wawe wanaweza kunusa taarifa mapema kuliko hawa akina RO. Nilazima kuna namna.

RO tueleze SISI kama wanajimii tunafaidika vipi na uwepo wako. NA Jee credibility ya Taasisi unayoiongoza unaipeleka wapi.

Thanks, Mwanakijiji, Tuendeleze Kusema ingawa hawa jamaa kwa kawaida wanataka waropokwe wao tu , wewe ukisema .............
 

George Kahangwa

JF-Expert Member
Oct 18, 2007
547
250
Mwandishi mmoja aliwahi kuandika kuwa licha ya kuwepo chombo kiitwacho usalama wa Taifa,taifa letu si salama. Mbaya zaidi chombo hiki licha ya kwamba ni idara tu, kinaendeshwa kwa gharama kubwa sana,budget yake ya mwaka inazidi budget za wizara kadhaa zinazohusika na utoaji wa huduma za jamii.
 

KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
1,225
Tatizo la RO siku hizi kuna technologia mpya ya iCT hivyo anapoteza muda mwingi kuchunguza wachangiaji wa JF ni akina nani wakati huo akiwapa mwanya makusudi mafisadi wanafanye vitu vyao.

kama kweli ni mtanzania tunayetegemea atusaidie kulinda nchi yetu katika hujuma mbali mbali mimi kama Mtanzania wa kawaida naona kashindwa kazi, Lakini pia hiyo kazi kuna watanzania wengi wanaiweza. Asipate taabu kukiri.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,327
2,000
Nadhani wakati umefika wabunge wetu wamtolee uvivu. Hivi mnakumbuka jinsi gani wakurugenzi wa CIA na FBI walivyokuwa grilled kuhusu "the failure of intelligence". Kosa moja liliigharimu marekani maisha ya karibu watu 3000, sisi wakurugenzi wetu wamefanya mangapi? na matokeo yake yakoje.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,726
2,000
Nadhani wakati umefika wabunge wetu wamtolee uvivu. Hivi mnakumbuka jinsi gani wakurugenzi wa CIA na FBI walivyokuwa grilled kuhusu "the failure of intelligence". Kosa moja liliigharimu marekani maisha ya karibu watu 3000, sisi wakurugenzi wetu wamefanya mangapi? na matokeo yake yakoje.

Ahahahahahahaha....Wamarekani Ndivyo Walivyo na sisi Ndivyo Tulivyo....bwahahahahahaaaa
 

Dua

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
3,233
2,000
Urais sio lelemama leo hii tunayaona. Kila kona ya nchi kunanuka rushwa na uvundo wa kila aina.
 

Icadon

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
3,583
0
Hivi chimbuko la kuporomoka kwa ufanisi wa TISS ni nani hasa?

Na ilikuwaje RO akawaruka wakuu wa vitengo kadhaa TISS(wengine wako very competent) mpaka kupewa uDG pamoja na kuwa alikuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 8 1/2, kipi kikubwa alichofanya alivyokuwa Zanzibar na Uingereza?
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,726
2,000
Nyani.. huo msemo wako huwa unanidepress kweli kiasi nikiosoma nafikiria kutundika kamba yaishe!

Samahani kaka...kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa kwenye nchi zetu wakati mwingine mtu unalazimika (hata kimya kimya) kuwaza mambo kama hayo (ya ndivyo tulivyo au la?).....
 

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
10,228
2,000
....kikwete anafanya kosa sana kuweka marafiki kwenye nafasi nyeti...huyu RASHIDI alikuwa kuwadi wake tangu wakiwa zanzibar hadi alipokuwa london ...ni mpenda raha na mabibi tu kama kikwete..

tangu amerudi hakuna anachofanya zaidi ya kukesha anacheza muziki..huku akulindwa na ma undercover boardguards na magari nje.....hana maadili kabisa kwa mtu wa nafasi yake...

...intelligence ameiuwa..kama intelligence ingekuwa inafanya kazi inayotakiwa mawaziri wenye kashfa kama chenge mafaili yao yasingefika kwa rais...hata kama kwa hilo rais alishinikiza...ni udhaifu mkubwa sana waziri mwenye kashfa kusafiri na rais hadi nje ...pasipo na mtu wa kumshauri rais angalau asiambatane naye kwa kuwa kashfa yake inatarajiwa kutoka nje....unless rais alikaidi...hata baada ya kushauriwa kutoongozana na chenge ziarani..
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom