Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman astaafu, Nafasi yake yakaimiwa na George Madafa

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,240
4,465
Rais Kikwete akiwa na Rashid Othman Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.JPG


MKURUGENZI Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Rashid Othman amestaafu rasmi wadhifa huo.

Amestaafu rasmi wadhifa huo Agosti 19, mwaka huu akiwa ameiongoza taasisi hiyo tangu Agosti 20, 2006 ikiwa ni takribani miaka 10.

Kiongozi huyo aliteuliwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa Mkurugenzi Mkuu ili kuziba nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa wakati huo, Cornel Apson Mwang’onda.

Aliapishwa Ikulu Dar es Salaam Agosti 21, 2006. Kabla ya uteuzi wake, Othman alikuwa Mkuu wa Utawala na Utumishi wa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa na kufanya kazi nzuri, iliyochangia kumwezesha kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.

Awali, Othman alitakiwa kustaafu mwaka 2013 kwa mujibu wa sheria, lakini aliendelea kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja mmoja hadi alipokubaliwa kustaafu rasmi Ijumaa iliyopita. Othman atakumbukwa kwa kazi nzuri, aliyoifanya kwa Taifa tangu alipoingia katika utumishi wa umma.

Chanzo cha kuaminika kimeliambia Gazeti la Mtanzania kuwa nafasi ya Rashid Othman kwa sasa inakaimiwa Mkurugenzi wa Mambo ya Ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa, George Madafa.

Chanzo: Mtanzania

 
Kuna kustaafu na kustaafishwa. Kuna moja kati ya hilo limetendeka. Na inaleta ukakasi zaidi kuwa habari imetoka leo wakati alistaafu tokea Alhamisi.
 
Hongera sana kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi kwa kazi kubwa ya kuilinda nchi yetu. Hongera kwa vyombo vyote ulinzi na watendaji wote kwa kazi kubwa wanayoifanya.
 
Tunampongeza kwa kustaafu salamaMungu ampe nguvu na heri kwenye mapumziko yake, Tunamuombea sana kwa mungu atakaepokea kijiti chake. Mungu ni mwema .
 
Kuna kustaafu na kustaafishwa. Kuna moja kati ya hilo limetendeka. Na inaleta ukakasi zaidi kuwa habari imetoka leo wakati alistaafu tokea Alhamisi.
Mkuu unadhani hicho chombo ni NSSF mpaka upate habari zao kirahisi rahisi.. ? Ndio maana kinaitwa secret service... ! By the way.. Wale wanaoshangaa kama kastaafu or kastaafishwa wakasome katiba inasemaje kuhusu the appointed director wa chombo hicho.. ! Sio kuropoka tu as long as you can..!
 
Back
Top Bottom