Rashid Othman ndiye Boss wa Usalama

Rashid Othman ndiye Boss wa Usalama

Status
Not open for further replies.
Jasusi,
Itakapotokea hiyo kitu ndio itakuwa mwisho wa wananchi kuwaamini hata jirani zao. Lakini kama ulivyopendekeza ni ukweli tu ndio utatufanya tuwe huru.
 
Jasusi,
Kuunda tume ya Ukweli ni ngumu maana walaji ni wao wenyewe. Vitu kama PCB, Tume ya Warioba yote ilikuwa viini macho. Actually nadhani PCB ni kujikosha tu mbele ya donors. Why have PCB while we already had Usalama wa Taifa kila kona ya nchi? and so far what significant achievement can PCB be proud of in terms of convicting anyone involved in the so called mega-corruption?
 
Nadhani kuna watu humu hawana hakika na wanayoyasema.

Mfano huyu jamaa anaedai kuwa ofisa huyu alikuwa na njama za kumuondea Balozi Kibelloh. Habari hii bila shaka kabisa haikufanyiwa utafiti na mtu hajui atendalo.

Habari zile nimeona kwenye google katika utafiti nilofanya na sisi tuliopo london tunajua nani aliandika.Kuna mwandishi hapa anaitwa Saidi Yakubu aliandika ikiwa ni mfululizo wa tafiti zake baada ya nyumba ya balozi kuvamiwa.
Ni vigumu kuona salva rweyemamu alihusika vipi na hizo njama hebu tuelezwe hizo njama walikuwa vipi.

Inadaiwa mama Radhia alihusika, huyu mtuma meseji haelewi kuwa mama radhia msuya nae alikuwa akitajwatajwa humo.

Halafu wanadai ashakum si matusi ati huyu mkurugenzi alikuwa akimfixia vimwana JK! Yani hizi ni hoja mtu mwenye akili yake hawezi kukaa akaziandika labda na yeye ikiwa ni mmoja wa hao vimwana waliofuatwa. watu wengine pumbaf sana! Tuthibitishie hili kama huna hakika kaa kimya. Waingereza wanasema ''it is better to keep quiet and let people think you are a fool than to open it and let people confirm that you are a fool''.

Haya mwingine humu anadai ati huyu jamaa alijifanya spy alipokuwa marekani kwa kuvaa miwani myeusi kwenye mkutano, nadhani huyu mtu anadhani usalama wa taifa ni kujidai james bond! Yani huyu mtu alieaminiwa na rais mkapa akamteua Director of Administration basi imekuwa leo hafai kwa vile kateuliwa na Jakaya! Mkumbuke nafasi za usalama level ya udirector nyingi ni appointment za viongozi sasa basi Mkapa nae kampendelea?!

Nawaunga mkono wale wanaodai kuwepo na CV yake hadharani, hili ni jambo la kufutatiliwa kwa kweli wananchi tujue mheshimiwa mkurugenzi ana wasifu gani, elimu yake, rekodi yake nk.

Lakini imetia moyo sana kusikia kasema atakuwa beneti na waandishi hii poa, big up mzee Othman chapa kazi kwa ari mpya.

At last nadhani sasa watz tupo huru kusema chochote, hii ni hatua kubwa.
 
Wewe tafiti,
hakuna mtu aliyesema RO hafai. and please no matusi please!!
 
MZEE RS:
Nasikitika bado unaendelea kutoa shutuma ambazo unashindwa kuzithibitisha. Hoja nyingi unazotoa za chini ya mkanda umeshindwa kuzithibitisha. ooh mama msuya hivi jk kapotea hoteli nk,mpe mwanakijiji hizo tepu tuzisikilize manake una maelezo mengi ya majigambo bila ukweli nakuchallenge umpe hizo tepu tuzisikie, elimu nzuri ni kuweka kichwa huru kupokea mawazo mapya hivyo nimeweka fikra wazi tuwekee hizo tepu tuchambue pumba na mchele.

Kuna maelezo umeyatoa hayana msingi ila ni hoja naweza kujibu baada ya kukuachia upuuzi mwingi kwako. Mkapa sio aliemteua Mwanyika kuwa AG, Mwanyika katika wadhifa wake wa kuwa mwanasheria mkuu kapewa na mheshimiwa jakaya kikwete within a week baada ya kuapishwa. Rashid Othman alirejea nyumbani baada ya kuteuliwa na Rais Mkapa kuwa Mkuu wa utawala na utumishi usalama wa taifa kwa kipindi kirefu, sijui kateuliwa lini lakini najua kuwa aliondoka UK mwisho wa mwaka jana hivyo hata kabla Jakaya hajawa Rais huyu alikuwa tayari ni mkurugenzi wa usalama katika idara ya utawala. Ujue kuwa kwa nafasi hiyo anakuwa ni second in command na huwa anakaimu nafasi hiyo ya ukurugenzi mkuu mara kwa mara.

Kumbe Mzee ES[huu uzee sijui ni wa umri au kupenda kujishaua shaua tu manake shaban robert aliwahi kusema mvi sio kipimo cha busara], huna data ni kauli za hear say tu. Huyo mzee wa ccm tutajie jina hizi ni enzi za uwazi na ukweli kama umeweza kumtusi mama radhia msuya ''kwa kulala na rupia na msabaha'' kweli unashindwa kusimamisha hoja yako ya msingi ya kumcrush RO kwa kusema tu mzee wa CCM?!!

Yani hoja zako nyingine zinachekesha sana, eti wazee wa usalama huko majuu wamekuwa wakiwasumbua sana viongozi wetu kuwauliza kama huyu RO ndiye aliekuwa London...!!Ngoja nikupe darasa kidogo la itifaki na diplomasia:

Mtu ambae ni presidential appointee anaepelekwa katika ubalozi kwa cheo chochote kuanzia minister counsellor ambae anapelekwa nchi ngeni kuwakilisha taifa lake basi hawezi kwenda huko mpaka hapo nchi husika inapotoa go ahead kumkubali mtu huyo. Hili la go ahead hawalitoi kijinga jinga tu ni kwamba wanaangalia rekodi ya mtu na kufanya tafiti zao wakiridhika basi ndio wanampitisha na kumruhusu ukweli kuwa rashid othman amekuwa hapa london kwa miaka kadhaa ni dalili kuwa serikali ya kwini imemkubali na sio kama usemavyo, ni uongo dhahiri kabisa.

Imeshawahi nchi kadhaa kukataa baadhi ya maofisa, Rwanda ilipeleka jina la kiongozi mmoja wakitaka aende kuwa balozi wao ujerumani lakini ikabainika mtu yule yupo ubalozi wa tanzania nigeria akiwa na hadhi ya kidiplomasia wakamkataa, nakumbuka alinyang'anywa uraia pamoja na kina jenerali ulimwengu wakati wa utawala wa mkapa.

Haya unadai huyu rashid othman english haipandi, wewe ni Mzee ES aidha ni mwehu au humjui rashid othman manake otherwise usingesema hivyo, hivi serikali ya Tanzania itapeleka mtu katika kituo muhimu kama London wakati language haipandi?! this allegations is beneath discussion kwa kweli,tafiti kabla hujajadili mzee ES!!

Nyumba ya ubalozi bila shaka kadhia yake huijui. Nyumba ile ipo namba three denewood road, about three minutes walk kutoka katika makazi ya kifahari ya balozi kibelloh ambae hupita hapo kila siku.Hili ni eneo la Highgate, aliekuwa anahusika na uchakavu wa nyumba ile huku akikataa kuchukua hatua yoyote ni balozi kibelloh ambae ana rekodi ya kukataa ushauri toka kwa subordinates wake. Hali ya nyumba hiyo huijui wewe Mzee ES manake ungekuwa unaijua usingesema maneno ya JK kukaa na vimwana, nyumba haijakaliwa tangu mwaka 1996! na baada ya hapo ilikua haina hadhi ya kukaliwa na maofisa wa hadhi ya kibalozi hivyo balozi Kibelloh aliwapa wapishi wakae pale,ambao pia walifukuzwa mmoja wapo ni mpishi hapa anaitwa Marco Chongwe, muulize huyo akuambie...Then kesi haikuisha kimya kimya manake ilienda mahakamani na waliovamia waliamuliwa kuhamishwa ambayo ilitoka mpaka nipashe na majira na bbc..walikuja vibopa hapa kuisort out na haikuwa tatizo na aliekuwa the centre of row alikuwa ni kibelloh othman alikuwa kishaondoka hapa london!! halafu hoja zako zinajigongagonga manake mara jakaya hupotea akija london maafisa hawamuoni halafu mara anatumia nyumba ya ubalozi kujistarehesha na vimwana, alisema shaban robert...elimu chache udhia...ningependa kujua elimu yako mzee ES manake isijekuwa ni zile digrii za kununua katika Ebay if at all you have one!

Sasa unataka kusema Jakaya kwa nafasi aliyonayo anashindwa kumlipia mtoto wake kuishi hapa? Maofisa wangapi wa tanzania na wafanyabiashara wana watoto wao hapa, kufika ulaya ndio nini? nauli ni milioni moja au chini ya hapo,kweli mtu aliekuwa waziri miaka zaidi ya kumi na tano na kuwa ofisa miaka kadhaa anashindwa kumpeleka/kuwapeleka watoto wake ulaya ajabu iko wapi, ujue kuwa mtoto wake Ridhiwani kamaliza digrii ya sheria pale mlimani wakati vijana wengine tangu sekondari wamesomea ulaya au kenya na uganda. Mtoto wake mwingine Salma bado yupo muhimbili hapo akisomea udaktari. Sasa unataka rais gani alie down to earth kama huyu.

Binafsi nadhani kwa mara ya kwanza tumepata rais ambae alikuwa akifanya homework kuwa rais na sasa tunaona namna anavyoweka mambo sawa, kishatoa darasa kwa viongozi wake wakuu mawaziri na sasa ameenda level ya marc, madc na maras tukitoka hapo rais wetu anatupeleka vizuuuri kabisa timu yote ikiwa inaelewana kama chelsea vile... subiri uone mambo ari mpya haiongopi kwa sasa namuunga mkono rais kwa kazi nzuri na uteuzi mzuri na akija kutetereka mwanzo utaniona mimi nikiwa wa mwanzo kumpinga hapa hapa katika forum.

Mzee ES don't fungua domo bila research kuna vitu kwenye mwili unaweza kufungua bila utafiti vifungue hivyo....
 
Mzee ES, BIG salute for your post.

Now I understand even better the meaning of this quote ''it is better to keep quiet and let people think you are a fool than to open it and let people confirm that you are a fool''
 
mTz

Kwanza nasema meno ya mbwa hayaumani.
nakushauri japokuwa ni haki yako kaa pembeni kwamba tule data .Hawa jamaa hawagombani japokuwa huyu mgeni kaja na maneno ya kejeli kwa Es . Toeni data wote sisi tuchambue ukweli wa habari . Sasa mimi Mzee Mugisha nasema naomba wengine tusome kwanza ndipo tuanze kuingilia huu mgogoro . Matusi hapanaaaaaaaaaaaaa.
 
Mzee Mugisha nimekupata asante kwa ushauri.
 
Mtz,

Nilichogundua ni kuwa, ES anaongelea FACTS na mwenzetu anaongela LOGIC!.

Halafu ameshambulia saana bila kujibu maswali na FACTs, mfano ES hajasema JK hana hela ya kusafirisha wala kuwaweka hotelini watoto wake au mkewe. ES kauliza kwanini wanafikia huko wanakofikia. Ndugu Mtafiti, jaribu kusoma between the lines, kisha jibu maswali yoote, acha kutumia LOGIC, siasa haina LOGIC, siasa ni uongo uliokomaa!!!

Ahahahahahah

FD
Mtumia ungo kupembua Mchele na Pumba!!
 
Mugishagwe said:
mTz

Kwanza nasema meno ya mbwa hayaumani.
nakushauri japokuwa ni haki yako kaa pembeni kwamba tule data .Hawa jamaa hawagombani japokuwa huyu mgeni kaja na maneno ya kejeli kwa Es . Toeni data wote sisi tuchambue ukweli wa habari . Sasa mimi Mzee Mugisha nasema naomba wengine tusome kwanza ndipo tuanze kuingilia huu mgogoro . Matusi hapanaaaaaaaaaaaaa.
Mugisha na MTZ kama mlivyosema ninabidi tuone vita hivi nani anaongea pumba. Mimi nadhani jadili amejaribu kukosoa aliyoeleza MZee ES sasa anachotakiwa kufanya ni kutetea. Ameeleza kwa kirefu nani alikuwa responsible na ile nyumba ya ubalozi na jinso Othman alivyokuwa hahusiki na suala la kushambuliwa kwa kibello si Othman si Salva aliyehusika. Tunataka haya majungu yaishe na tuone ukweli uko wapi mwisho tutaconclude kama hata il mitusi kama Radhia Msuya alitembea na Msabaha na JK kumbe ni majungu tu nachuki binafsi. Hizi ni zama za uwazi toa hizo facts..na logically haiwezekani kama kumbe hilo jumba lilikuwa chakavu watu wene wakafanye mambo yao. Haya ni majungu tu na bila shaka Mzee Es ataingia mitini tu kwenye hii topic kama bado yupo basi amjibu tujadili. Halafu kuhusu mitusi mie nadhani aliyetukana zaidi ni huyo anayejiita mzee. Kamshambulia mama wa watu..na maneno kama malaya,nk. Acha matusi mzee ES otherwise tutakuona una boa tu.
 
Hi Kingwele:
You are looking onesided, but insults are lesser meaniful than what we are dicovering now. Let us say Mzee ES has been teasing this guy to come up and open his mouth, we are learning points which we should be commenting now, for example:


1. Haya unadai huyu rashid othman english haipandi, wewe ni Mzee ES aidha ni mwehu au humjui rashid othman manake otherwise usingesema hivyo, hivi serikali ya Tanzania itapeleka mtu katika kituo muhimu kama London wakati language haipandi?! this allegations is beneath discussion kwa kweli,tafiti kabla hujajadili mzee ES!!
ANSWER: I 'VE SEEN MANY!

2. Hali ya nyumba hiyo huijui wewe Mzee ES manake ungekuwa unaijua usingesema maneno ya JK kukaa na vimwana, nyumba haijakaliwa tangu mwaka 1996! na baada ya hapo ilikua haina hadhi ya kukaliwa na maofisa wa hadhi ya kibalozi hivyo balozi Kibelloh aliwapa wapishi wakae pale,ambao pia walifukuzwa mmoja wapo ni mpishi hapa anaitwa Marco Chongwe, muulize huyo akuambie...

QUESTION: ELEZEA HII NYUMBA KAMA WAPISHI WALIIISHI, MTU MWENYE HADHI YA UBALOZI ATASHINDWAJE KULALA HUMO? ILIKUWA MBOVU KULIKO ZILE NYUMBA ZA MAPIPA/ KIGOGO?

3. Manake mara jakaya hupotea akija london maafisa hawamuoni halafu mara anatumia nyumba ya ubalozi kujistarehesha na vimwana,

QUESTION: WHAT MAKES YOU THINK HE DIDN'T DO THAT? WHAT IS YOUR POINT HERE?

4. Sasa unataka kusema Jakaya kwa nafasi aliyonayo anashindwa kumlipia mtoto wake kuishi hapa? Maofisa wangapi wa tanzania na wafanyabiashara wana watoto wao hapa, kufika ulaya ndio nini? nauli ni milioni moja au chini ya hapo,kweli mtu aliekuwa waziri miaka zaidi ya kumi na tano na kuwa ofisa miaka kadhaa anashindwa kumpeleka/kuwapeleka watoto wake ulaya ajabu iko wapi, ujue kuwa mtoto wake Ridhiwani kamaliza digrii ya sheria pale mlimani wakati vijana wengine tangu sekondari wamesomea ulaya au kenya na uganda. Mtoto wake mwingine Salma bado yupo muhimbili hapo akisomea udaktari. Sasa unataka rais gani alie down to earth kama huyu.

FACT: ONDOA WAFANYABIASHARA. IS AN ISSUE WHEN YOU COME TO GOVERNMENT OFFICIALS, THEIR EARNINGS ARE VERY LIMITED, ARE YOU TRYING TO PROVE SOMETHING HERE? YOU'RE NOT TALKING OF ONLY A CHILD BUT CHILDREN. IT TAKES NOT LESS THAN A FORTUNE TO PAY PER ANNUM!

5. Binafsi nadhani kwa mara ya kwanza tumepata rais ambae alikuwa akifanya homework kuwa rais na sasa tunaona namna anavyoweka mambo sawa, kishatoa darasa kwa viongozi wake wakuu mawaziri na sasa ameenda level ya marc, madc na maras tukitoka hapo rais wetu anatupeleka vizuuuri kabisa timu yote ikiwa inaelewana kama chelsea vile... subiri uone mambo ari mpya haiongopi kwa sasa namuunga mkono rais kwa kazi nzuri na uteuzi mzuri na akija kutetereka mwanzo utaniona mimi nikiwa wa mwanzo kumpinga hapa hapa katika forum.

INTERESTING.......!
 
Kama siku zote huweka fikra huru kupokea mambo mapya naomba MZEE ES pamoja na uthibitisho niliokuomba umtumie mwanakijiji kama unavyodai una tepu(hizi tepu unaimply kama na wewe ni shushu vile au umenyimwa kazi nini?) basi ongezea na kutupatia ushahidi wa kutosha juu ya haya:

Tuthibitishie ni makampuni mangapi hayo ambayo yanaondoka bongo kwa vile JK ni rais? Mimi naona ndio kwanza interest zinaongezeka za wafanyabiashara kutaka kuja hapa bongo, ongea na Yusuph Kashangwa director wa tanzania trade centre london akwambie!Hapo kuna ma-offer na ma-interest kibao ya wafanyabiashara kibao.

Nadoubt ukweli kuwa balozi anaweza kuuliza kwenye kikao cha leo/jana kwamba mashushu wa ubalozi wapo wapi? hawa hawapo kwa takriban mwezi sasa halafu balozi aulize leo ilhali kuna vikao kila siku kujadili daily agendas? Inawezekana kweli watendaji wa ubalozi ingawa ni mashushu waondoke bila kuaga? hata kama ndio kuna sababu gani balozi aulize jana ilhali kuna kipindi kirefu kimepita? usijifanye una contacts ubalozini wakati huna lolote.

Kwangu mimi kama nilivyokwambia akili yangu ni huru kupokea ushawishi wowote wa hoja unaoutoa basi nakiri kutokujua nani kawaleta watoto wa jakaya na wapo wangapi hapa sijui naweza kukutajia wale ninaowajua wapo hapa, najua Miraji yupo hapa na mwingine Ridhiwani yupo Birminghaam akipursue masters yake..nani kamleta sijui as I said bali nilikuwa na presumption of innocence kama tunavyotakiwa kuwa kumhisi mtu vizuri hivyo sioni kama kikwete anashindwa kumsomesha mwanae.

Mzee ES tuambie wanapokaa kama una uthibitisho tusioujua? Hoja zako unazijenga kwa mtindo wa fallacy? unataja majina na kujidai unapiga simu wakati ni uongo lakini watu wengine waamini!!

Tusaidie tena Mzee ES mama kikwete akija anakaa wapi manake tujuavyo mara ya mwisho kapita na mzee hapa walikaa hotelini masaa machache kabla ya kurejea bongo na ni hotel ya Hayyatt pale central london waandishi kadhaa walikwenda na baadhi ya picha tumeziona magazetini hapa, jambo london moja wapo. Kabla ya hapo mama kikwete alipita kutibiwa hapa alikaa katika rented apartments za pale green park akiwa na wasaidizi wake na zililipiwa na ikulu bila shaka kama anavyostahili mke wa kiongozi. Sasa hapa nukta ni alikaa wapi tusihoji mantiki ya kulipiwa na serikali or not manake that is a valid argument bot not in this discussion,[binafsi sioni kama ni maridhawa mawaziri na viongozi kutibiwa nje lakini nareserve comments kwa sasa], sasa kama Mzee ES unajua otherwise tuambie basi.akili zetu huru kama hoja zinamake sense.

Nashawishika kuchangia hoja za wengineo humu kwa azma safi kabisa:

Mugishagwe:
Naomba watu wote waruhusiwe kuwa huru kuchangia manake hii ni forum waachie kina Mtz kama wana kitu cha kuchangia basi watoe manake ndio uhuru wa mawazo, tuchukulie hii kama debate then kuna opposer na proposer halafu kuna waongeaji wengine.

FikiraDuni:
[jina badilisha yakhe manake linatoa impression mbaya kabla hata ya kuanza kusoma hoja zako, ni nzuri lakini nikianza kusoma ''fikira duni'' says naona kama unajishusha hadhi wakati mzee una mapoint, jiite hoja muruwa kama unadhani huna hoja kali] nashukuru kwa ushauri uliotoa na nikiri kwanza nimependa hata hii slogan yako ''mtazama pande zote za shilingi'' ingawa nadhani hujapata. unasema jamaa Mzee ES ana facts zionyeshe basi tuzione manake naona mzee katoa maneno sio mazuri na hayana hoja.

Haya mzee ES huko Afrika ulipo katika bara letu lenye raslimali za kutosha zinazohitaji kuendelezwa tupe michango yako safari hii uwe na hoja sio shutuma na kuita watu mbuzi na malaya uwe na lugha nzuri utapata lugha nzuri ukienda chini ya mkanda mimi ntakupa an eye for eye!
 
FikiraDuni,
Nimependa jina lako la ubatizo. Kuanzia sasa nitakuita Hoja Muruwa
 
ndugu yangu Jadili naona huyo mzee ES ameingia mitini maana hoja unazotoa umeshamtoa udhu..ndo maana yuko kimya hana lolote anajidai yuko Afrika eti Angola,mwongo. Yuko Marekani na huu mjadala anaufuatilia ila anaona yamemfika pabaya. Unajuwa hatukutaka kuingia kwenye foums hizi kwa kuwa tulidhani kuna utoto mwingi nilichuogundua vijana kama huyu anayejiita mzee Es wanatoa mbegu mbaya hivyo inabidi wajibiwe kwa hoja za nguvu mpaka waingie mitini kama walivyoingia sasa hivi. Kama kuna mwingine mwenyehoja kama za kwake amsaidie basi mana mjadala una boa jamaa ndo yameshamishinda,shuwain. Anataka kuleta utoto na majungu ya vijiweni hapa..pumbaff
 
tafiti,
Nilikuwa najua umefanya utafiti kabla ya kuingia kwenye hii forum? Inaonekana wewe unasikiliza maneno ya majukwaa ya kisiasa. Wewe si unapenda kutafiti, hebu tuambie ni kwanini mtoto wa JK alirudishwa bongo na ni kiasi gani JK alishindwa kumlipia, wote tutumie logic unazotumia. Another logic, kwa kuwa JK alitumia rushwa kupata urais basi anajua njia zote za kupambana na wana rushwa. The great president. Anyway, this is sam. Karibu.
 
Mzee ulikuja na matusi, na kama kawaida yetu hurudisha mara mbili, halafu no question kuwa wewe ni huu usalama mbuzi wa bongo, I am not mimi sio usalama kama unavyosema mimi ni mwananchi mwenye uchungu na nchi yangu na kwa bahati siku zote ninazo data za yanayofanywa na wakubwa mpaka wadogo wa nchi yetu,

(1). Kwanza ulikuwa unajaribu na bado unajaribu kumuosha huyu mwanamama hapo London, ukweli ni kwamba huyo mama si lolote ni muhuni, na haya mambo ya kujihusisha na kuwaharibia viongozi sio mara yake ya kwanza kwani kule NY pia aliwahi kuhusika na kumuondoa Mzee Nyakyi, tepu zilitolewa na kwenye magazeti ziliandikwa, hilo hukuligusa mzee wa utafiti!

(b). Halafu huyu mwanamama, pia alihusika na zile kesi za upatu zilizowahusisha kina mama Rupia, na wengine wengi hapo bongo, yeye akapona baada ya kuzirudisha zile pesa karibu shillingi millioni 5, hilo vipi?

(c). Huyo mama toka JK apate achaguliwe Dodoma, anapoenda bongo huwa anamuaga nani hapo ubalozini? Mbona huko nyumbani kuna ripoti kwamba hupotea tu na kutokea bongo na hakuna wa kumuuuliza?

(d). Bwana Salva, huyo mama, na RO wanahusika sana na kupandikiza mbegu za fitina against Mzee wangu Kibelloh, lakini kwa bahati nzuri tulishamuonya Mzee Kibelloh mapema toka yule mbunge Nyami alipoenda bungeni kudai hafai na aondolewe kwa sababu anaringa sana, ilibidi tumpelekeee Mzee BM orodha ya wabunge waliopita London kwa mwezi ule alioudai huyu mbunge ambazo zilionyesha kuwa yule mbunge hajawahi kukanyaga London katika maisha yake, ndio maana Mzee Kibelloh anapeta mpaka leo na sasa anahamia Parieeee!

(2). Mwanyika alichaguliwa na rais Mkapa, JK asingeweza kumchagua mwanasheria mkuu, kabla hajaapishwa kuwa rais wa jamhuri nenda uangalie vizuri data, Mwanyka alichaguliwa na rais wa jamhuri kwa mujibu wa sheria, rais hakuwa JK!, halafu kwenye kikao maalumu cha wazee wa nchi wakati JK anadai EL awe PM, kilio chake kilikuwa ni pamoja na kwamba hakumchagua Mwanyika, wala Shein, na bado wanataka kumuongezea wengine akasema siwezi kufanya na mtu yoyote zaidi ya EL!

(3). RO alipewa hiyo kazi kwa shinikizo la rais mtarajiwa ambaye alikuwa bado hajakabidhiwa rasmi madaraka, huyu ndiye aliyemfanyia JK kazi nyingi akiwa London, kwa sababu Mzee Kibelloh sio mtu wa kambi ya JK, hayo niliyasema toka BCS, na hata JK mwenyewe kabla ya kuwa rais, akiwa waziri naye pia alijaribu kila mbinu kmhujumu huyu balozi, lakini akapiga chini maana tulikuwa tunafuatilia kwa makini njama zote against huyo balozi, mpaka memo kadhaa za JK kwa rais BM, kutaka aondolewe zipo lakini ni nyara za serikali, hatuweki hadithi tuuu hapa! RO alikuwa ndiye mtu wake pale, kuanzia vimwana mapaka contact za akina Tido Mhando huko BBC na zile poll za magirini kuwa yeye anaongoza, Je unajua kipindi kile Mzee JM alikuja mara ngapi pale London na huyu RO akajificha kabisaaa hakuonekana?

(4). Hayo maneno ya diplomasia ni upumbavu wa hali ya juu, maana mzee Nyirabu alikataliwa na US lakini serikali ikaweka mguu chini, kwani US ilisema haiwezi kumruhusu balozi ambaye central Benki imeungua under his watch, lakini serikali yetu ikaweka mguu chini kuwa ni huyo tu na akawa? Mbona unataka kuwadanganya watu hapa na diplomasia kama vile hatuijui? Balozi Seif Idd mbona alienda kuwa balozi Uchina na hakipandi kabisaa na sasa ni waziri? Mbona Kissoky alikuwa RC na kilikuwa hakipandi? Muhogo mchungu je?

(5). Hiyo nyumba unasema haijakaliwa toka 1960, je JM alipochaguliwa kuwa PM na kuondoka hapo London, watoto wake wawili waliokuwa wanamalizia shule zao mbona walikaa hiyo nyumba mpaka wakamaliza shule?

(6). Watoto wa rais walialikwa na nani kwenye hiyo party ya Courtyard? Je niynyi watu wa ubalozi mlialikwa? Mbona hili hukuligusa? Huyu mmoja huko Oxford amepelekwa na nani? Na huyu mwingine ile familia ya wazungu inamjuaje mpaka kumleta huko? Na kumlipia kwenye apartment anayokaa sasa baada ya kukataa kukaa nao kwa sababu ya kuwa mbwa? Mbona hayo hujasema? Halafu toka lini mtu wa usalama wakati akisafiri nje ya ubalozi anamuaga balozi? Hiyo system ilianza lini au ni wewe umeianzisha huko London hivi karibuni?

Mwisho ni kwamba wewe ni mjinga na utaendelea hivyo hivyo kupigwa tuu miti na hawa jamaa wenye nguvu lakini masikini ya Mungu hata cheo hawakupi, wanakupiga dana dana, JK ana uzuri wake na matatizo yake mojawapo ni hili la mara tu watoto wameshachukuliwa na kupelekwa na wazungu hata mwaka kwenye urais haujaisha, je miaka kumi ijayo itakuwaje?


wazungu huko walikuwa bado wanajaribu kutafakari juu ya wakili kuwa balozi hapo, sasa hawajakaa vizuri huyooo RO, ndio maana simu zimekuwa zikimiminika huku kuwa eti hiyo kazi yake mpya ni equivalent to CIA, KGB, na M16 au ni tofauti? Ninarudia tena, kuwa RO kama bosi wake mpya uwezo wao ni mdogo, the matter of fact hawana kabisaa, lakini nchi yetu itajiendesha yenyewe bila tatizo kama vile miaka 10 ya Mwinyi, tulijiongoza wenyewe, RO hana kabisaa qualifications alizonazo Mzee anayeondoka tena ni aibu hata kusema kuwa anachukua nafasi ya Mzee anayeondoka, ndio maana hata JK pamoja na hasira naye kipindi chote cha uchaguzi na kuapa kuwa akipata tu atamuondoa kwanza, ilibidi abane mwenyewe na hata kumpa mtoto wake unbunge wa bure, maana huyo alikuwa sio mtu wa mchezo, mwambie RO najua ndiye anayekutuma kuwa hana uwezo wa kuwa SPY CHIEF hana!

Kuhusu tepu zipo na wala hakuna haraka nazo, kwa sababu so far huna ukweli ila ni mtu tu unayetumwa kuja hapa kuwadanganya wananchi, huko nyumbani hakuna biashara mpya, juzi juzi zimetumwa shillingi billioni kila mkoa ili kuanzisha ajira mpya, guess what hizo hela zimeshaanza kuliwa kwani ajira ikishindwa serikali kuu za mikoa zitaweza vipi? Huo ndio tunauita uwezo mdogo alionao kiongozi wetu mpya, pamoja na ahadi nyingi hewa, ndio lakini atatuongoza for the next ten years na pembeni yake wapuuzi kama wewe!
 
Mzee Kingwele,

So far unayo michango miwili tu katika hii forum tukufu, mahali ambapo tunachangia hoja za maendeleo na ubadhirifu unaofanywa na viongozi wa nchi yetu,

Hebu angalia tena hiyo michango yako inaelekea kwenye hilo lengo, au umetumwa kuja kuharibu majadiliano ya kujenga nchi yetu?

Mahali nilipo sio tatizo, just deal with my message, sisi mzee tulianzia hukoooooo kwney mti, yaani BCS hatukuanza leo, mimi nikikimbia ujue mwisho wa dunia umefika, ila sishidni humu wakati wote lakini I love it wanapokuja humu majuha kama wewe na kubadili badili majina mimi siku zote ni Mzee Es never change, hebu toa michango ya kusadidia nchi yetu kama huna kaa pembeni wanaume waendelee hapa! Kazana na michango mingi ndio uwahukumu the SENIORS hapa,

Na sisi tunasema wembe ni ule ule, na ole wenu nyinyi wajinga wa usalama mbuzi siku nchi hii itakapogeuka, maana kila siku tunakusanya ushahidi tu hatuna haraka tena kawaambie na hao wanaokutuma, kuwa hatujalal, na hapa umefika in one month utakuwa umepata somo la kutosha kuwa wabongo hawajalala, eti hizi forum za kitoto? Muulize Mahita, na Sizzla wake mbona alienda ikulu analia alikuwa analilia nini? Moto ulianzia kwenye hizi forum na bado tutaendelea kumwaga vitu hapa hatishiki mtu hapa hata wote huko usalama yenu mje hapa hakimbii mut hapa, ninasema kuwa hatukimbii wajinga hapa!
 
Mzee ES
Inaonekana wageni wanaingia kichwa kichwa, hawakufahamu. They will soon get used to the standard of the forum. Your data are convincing.
 
Mzee Invincible,

Heshima yako mkuu, ukweli ni kuwa bongo ni nchi yetu na regardless ya the odds kuwa against wananchi for the last 20 Years, kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho, mimi ninasema huu uharamia tunaofanyiwa wananchi wa bongo sasa unakaribia mwisho, maana hawa viongozi wetu sasa wako karibu kumaliza kila kitu, na sasa hivi watafikia mahali kutakuwa hakuna kitu tena, wewe nafikiri unaelewa kuwa watu waliokumbwa na mawimbi ya bahari wakatupwa hukooooo kusikokuwa na kitu kwanza hula majani na wadudu, na hatimaye kulana wenyewe kwa wenyewe, na ndiko tunakoelekea sasa it is coming,

Angalau enzi za Mwalimu ndio kulikuwa na viongozi wadokozi wa hapa na pale lakini sio wachotaji kama waliokuja kipindi cha Mwinyi, na wakwapuaji wa enzi za BM, na sasa ndio kabisaaaa tumekwisha, sasa itafikia mahali hakutakuwa na cha kuiba tena, hapo ndio tutageukana wenyewe kwa wenyewe, sasa kazi tunayofanya hapa sio ujinga hata kidogo,

ndio hawa viongozi wana nguvu, lakini hatuwezi kuwapa nafasi ya kulala lazima tuwatupie mawe na nafikiri by now umeshagundua kuwa mawe yakiwa ya kweli yakiwagusa huwa wanatuma watu wao hapa, tena hapa ninamuomba admin awe imara.

Sisi tutaendelea kuwazungumzia wanyonge wasioweza kuzungumza na kujizungumzia wenyewe maana hii bongo ni nchi yetu, na hatuwezi kutishwa na yoyote hata awe usalama, ukweli ni kwamba JK anaendelea kushusha hadhi ya serikali yake mwenyewe kwa kuwachagua viongozi wasiokuwa na uwezo, kitu ambacho kinadhihirisha kuwa yeye ni kiongozi wa namna gani na amezungukwa na akina nani,

si wazungu wanasema nionyeshe rafiki zako nitakujua wewe ni nani?

Aluta continua bro, na hakuna kulala, kama alivyosema Mr. Freee!
 
Message Sent! and Delivered

Inaonekana serikali inapata ujumbe. Ni vizuri kama huyo tafiti ni moja wa watu serikalini. nathani ujumbe utafikishwa . na wakishajua kwamba forum hii ina exist na haina watoto. Itakuwa home page yao wanapowasha computer zao kila siku.

Kuna DC moja kilasiku anaingia humu, namjua sana..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom