Rashid Othman ndiye Boss wa Usalama

Rashid Othman ndiye Boss wa Usalama

Status
Not open for further replies.
Nakubali CV itasaidia ikiwekwa hadharani ingawa sio lazima kwa vile kule ni usalama, hatutakiwi kujua vyote, Lord Denninf jaji maarufu hapa uingereza aliwahi kusema those who are entrusted with the security of our country should be the one to decide on national safety no one should intervene'' nchi yetu usalama wake kakabidhiwa RO tumuachie, halafu najua kuwa RO sio show off kama mahiga sidhani kama tutaipata cv, tumeambiwa kuna watu humu wana critical political information basi tuwaombe hao watuwekee hapa!

Nimkejiunga mtandaoni hapa baada ya kuona ni blog bora na walau ina hoja hoja. I will join anything to debate my country's future, nimejiunga hivi punde tu hivyo bado ni mgeni humu ndani. Nategemea makaribisho mazuri kwa vile ni mgeni, lakini nimeguswa na uongo mwingi unaowekwa humu na ES nikaona nichangie.

Kama huwa unasoma meseji nyingine huwa nachangia sana, tunakwenda katika mtiririko mmoja wa mawazo na ES katika China na nashukuru nae pia ameniunga mkono lakini haina maana maoni yake ni sahihi by default tu hivyo akiwa sawa tutamuunga mkono akichemka ataambiwa, huu ndio uhuru wa mawazo.

Lakini kuna watu wengine wa ajabu sana,mimi kwa kutaka fair treatment kwa wahusika ie Jakaya na RO naambiwa natetea interest zangu, wale wanaomfagilia Mahiga kwa ''dont even go there'' na Kibelloh hao hawana neno!

ejama tuweni fair
 
Mimi kwa maoni yangu ni jk, kachemsha kwa kumteua huyu jamaa kuwa kwenye nafasi nyeti kama hii.

Mimi nimekuwa karibu sana na huyu jamaa hapa London hii ni pamoja na kuwa na ukaribu kwenye mambo ya starehe na ya kikazi pia, uwezo wake ni duni sana, pia hata kujieleza kwake kunalenga kwenye habari nyepesix2.hoja nzito hana ujanja nazo, na hili ni hatari sana kwa Taifa Jk.

Kwa kiasi kikubwa yeye alikuwa ni mpambe wa mambo ya kibinafsi ya hao waliomuweka madarakani na hii inathibitishwa na kutotoa wasifu wake na hata maelezo yake ya kwanza eti nitapambana na ujambazi kwa nguvu zote! kunaashiria yeye kutojua mipaka yake..

Mimi sina mgogoro na Jk kuwapa wanawake nafasi nyingi za uongozi kwani hakuna asiyejua ukaribu wake na akina mama huko nyuma! ...ila mgogoro wangu ni kuwa watu kama wakina Othman wanapopewa nafasi nyeti kama hizi kunazua maswali mengi sana juu ya aina ya Serikali tuliyonayo!..kama ni fadhila Jk..basi ungempa hata Ubalozi kwani watu wangesema kisha wangeenda kulala ila kwa hili hapa Umechemsha kichizi.. kama aliweza kuwaleta Kilimanjaro Band wana njenje kwenye Harusi ya Mtoto wake Hapa London kwa kutumia Mgongo wa Ubalozi nawe ukiwa Waziri wake ukaminya nini kitatokea sasa....ni kwa Akina yakhe na washikaji wote wa Readings na vitongoji vyake kufurahia kwani .........usalama wa Taifa uko kwa Mtoto wa Mjini...

Mungu Wabariki Watanzania Wote Walioko Vyuo Vikuu Ili Wakihitimu Washike Nafasi Kama Hizi......
 
Ndotokiwenyi
Wewe ndiye jibu la swali la Mzeeshughuli Bwana .Maana CV haitolewi . Mimi huyu RO simjui ila baada ya kuoa mabishano na hasa swali la Mzeeshughuli niliamua kuingia London kujua ukweli . London kona mimi ni mwenyeji sana . Basi nimekutana na ndugu mmoja akasema huyu uzuri wake ni kijichanganya na watu kila kichochoro .Hii ndiyo sifa yake kubwa .

Juu ya uwezo wake mimi sina la kusema niliyo yapata basi nimeamini kwaba Mzee RO anaweza kuwa kilaza wa nguvu zote .Kutoa CV si dhambi ama maelezo ya kina lakini pia unaweza kuwa kwenye system kwa kuwa ni kazi umeajiriwa lakini mchapo halisi usiuweze.Sina kundi kama mnavyo dai ila huyu RO kweli kuanza na neno majambazi kulinifanya nijiulize sana uelewa wake wa kazi yake. Ujambazi haukuwa real jamani maana majambazi wote ama walikuwa wanachangiajia wakubwa wa CCM ama walikuwa wanakula na Mahita . JK he knew all na baada kuwakemea watu ambao walikuwa wanakula nao leo hii ujambazi ni mmoja mmoja maaa ule wa mradi umesha kufa maaa hakuna ambaye hakujua kwamba ulikuwa na mradi wa wakubwa .

Nina wasi wasi na RO lakini maamuzi ya Rais ni ya mwisho . Madai yako Es kwamba jamaa alikuwa mkaribu wa mambo binafsi ninayakubali maana wengi London wanajua hata TZ .Tuendelee
 
Yaliyomkimbiza Mahiga usalama na nchi kwa ujumla ni majungu kama hayo yako, na sio yeye tu waliowahi kukimbizwa na majungu bongo, kuna kina mzee Masha aliyekuwa katibu wa TANU, akaenda kuwa mkurugenzi wa habari wa UN, Professor Rweyemamu, aliyekuwa mshauri wa rais akaenda kuwa mkurugenzi UN, Nsilo Swai, Mama Tibaijuka, na wengine wengi,

Mahiga hakuomba kwenda UN, isipokuwa serikali yetu ya jamhuri ndiyo iliyokwenda kumuomba rasmi UN, mshahara aliokuwa anapata UN na anaopata sasa hivi ni kechekesho kikubwa, na a big joke!, Na inaoenekana humfahamu maana kwa yeyote anayemfahamu anajua kuwa hana huo ujinga wa kujipeleka magazetini, kwani yeye sio mjinga wa kujua kuwa wanaopewa hizo nafasi sasa hivi ni WAISILAMU,

Kama ni CV, huwezi hata ianguke mvua ya mawe ukamlinganisha Mahiga na RO, Mahiga ni Mwalimu wa Mlimani, akawa Mwalimu tena Canada, Mahiga ni former Director of Administration wa usalama bongo, Mahiga ni Mtanzania wa kwanza duniani kuwa Director wa UN, Refugeees in Europe,

I do not remmember hata siku moja nchi yetu ilitaka kupinduliwa kwa sababu ya Mahiga kuwa usalama, ninajua kuwa ilitaka kupinduliwa na watu waliokuwa na problem na siasa za Mwalimu lakini sio Mahiga, unless unataka kusema kuwa wanajeshi walipotaka kuleta vurugu ile miaka ya 60s ilikuwa ni kwa sababu ya Mahiga? Au unataka kusema kina Ngaiza, Bayona na wengine walikuwa na beef na Mahiga? Hilo nilikuwa silijui na hakuna history ya bongo mahali popote inayo-suggest hivyo,

Halafu Mkapa unayemsifia kuwa alikuwa babu K, ilikuwaje akaenda kumuombea Mahiga UN, kwa niaba ya jamhuri yetu, kiongozi bomu kiasi hicho kuwa balozi wetu UN, na mpaka kuwa Mwenyekiti Wa Baraza la Usalama La Dunia? Kiongozi kama Mahiga, ambaye ameweza kuliendesha Baraza La Usalama La Umoja Wa Mataifa, UN na kuliletea sifa za ajabu taifa letu leo hawezi kuwa mkuu wa usalama wa bongo? Are you serious au unatania?

Mtanzania wa mwisho kushika nafasi hiyo ya Mahiga Mzee Salim he almost became katibu mkuu wa UN, na akaja kuwa PM, baadaye Waziri wa Ulinzi, na hata kuwa Katibu wa OAU, leo utamlinganisha Mahiga na Othman? You must be kidding? Kama ni umri ninajua umri wa ku-retire serikalini hata wa rais wetu mpya unazidi, vijana ni kina Sumaye, Freeman, Masha, Nchimbi, JJ, lakini sio JK, RO, wala Mahiga, kwa hiyo hiyo hoja ya umri ni empty kabisaaaa,

Wewe tuwekee CV ya Othman jinsi alivyosoma masters huko UK, na ni lini alichaguliwa kuwa msaidizi wa Abson, kwani ninajua kuwa mpaka wakati wa uchaguzi mwaka jana alikuwa agent mdogo sana pale London, je amekuwa msaidizi kwa muda gani? Abson amekuwa msaidizi toka enzi za Mwinyi, akafanyiwa majungu kibao wakati wa Mwinyi ili apewe Muisilamu, na kweli Mwinyi akaamua kumhamishia u-China, ndipo wazee wa nchi wakamuita Mwinyi na kumuonya aache huo ujinga mara moja, ndipo Mzee Abson amabye alikuwa amebakiza siku mbili kwenda u-China akaambiwa haendi huko na atakuwa Director mpya, wakati wa Mkapa alikuwa anajitayarisha ku-retire, mkapa tena akaonywa na kumuacha mapaka mwisho, JK alimtaka akae kwa miaka miwili lakini akakataa na kumwambia August 1, ndio ungekuwa mwisho wake, sasa utamlinganisha vipi Othman na hawa wazee kina Abson na Mahiga?

Othmasn alirukaje toka u-Agent wa kawaida kule London mpaka kuja kuwa Assistant wa Director bongo, mpaka leo kuwa Director? Wakati mwaka jana October alikuwa agent wa kawaida ule London, yaani between October mwaka jana na leo August, miezi kumi tu tayari ameshakuwa good enough kuwa Assistant Director na leo kuwa Director kamili?

Kama sio mazingaombwe ni nini? Nyinyi mnaokuja kutafuta heshima humu you have a long way to go mimi ninakuja kulichangia taifa langu, na wala sio heshima ninamwaga vitu and let the chips fall where they may, waziri alijaribu kila njia kumuondoa Kibello pale, hilo linathibitishwa na ukweli kwamba hawa kina Nyami walipokuja juu kule bungeni, waziri wa nje alinyamaza kimyaa badala ya kumtetea mtu wa wizara yake, hayo ndiyo yaliyotusaidia kumtetea mbele ya Mkapa, baadaye akamletea issue ya nyumba, nayo hivyo hivyo ushahidi ukaonyesha kuwa hiyop nyumba ilikuwa chini ya usalama na hasa Othman, nayo pia tukampelekea Mkapa kesi ikafa kinyemela, Jk leo ameshindwa kumuondoa kwa sababu moja kubwa nayo kazi aliyomuomba ya kumsaidia Shija kuingia Commonwealth ambayo yeye JK alikuwa ameshinikizwa na Mtandao wenziwe, manake Shija ni mtu wa karibu na Diallo, na Karimagi, na wala sio kitu chochote kingine kwani the next opportunity atamrudisha bongo kama mbwa, hilo tunajua bro, ndio maana kwa maneno ya majungu ni kweli Kibello hafai, lakini inapokuja kwenye Maandishi na Facts zinazohusu kazi iliyompeleka huko ogopa, hamna kitu bro!

Othman pamoja na kupewa hiyo kazi, ninarudia kuwa hana uwezo wa kuifanya ipasavyo, na ninasema kuwa hana qualifications za kutosha na huko Usalama kuna watu wanazo za kumzidi isipokuwa amepewa tu kwa kujuana na JK, ana alikwisha muahidi mapema kwani yeye Othman alishasema mara nyingi kwenye viwanja, kwa mara ya kwanza ilisemwa kule BCS, mwaka jana wakati bado akiwa London, tafadhali nenda kule utayakuta!

Tepu unazozililia sina sababu ya kuzito, nilikuwa ninasubiri vitu vyako kwanza na hamana kitu bro, ndio maana wanabodi humu umewaona kuwa biased maana kama mimi hawajaona kitu na bado tunaendelea kuwapotezea muda uless tutaweka CV ya Mzee anayekutuma Othman, hebu mwambie akupe uiweke hapa!
 
Mimi Mzee Mugishagwe
Sijakielewa hiki kipendele hebu Mzee Es fafanua tafadhali maana umesema haya

Mahiga hakuomba kwenda UN, isipokuwa serikali yetu ya jamhuri ndiyo iliyokwenda kumuomba rasmi UN, mshahara aliokuwa anapata UN na anaopata sasa hivi ni kechekesho kikubwa, na a big joke!, Na inaoenekana humfahamu maana kwa yeyote anayemfahamu anajua kuwa hana huo ujinga wa kujipeleka magazetini, kwani yeye sio mjinga wa kujua kuwa wanaopewa hizo nafasi sasa hivi ni WAISILAMU,
 
Mzee Muggy,

Heshima yako mkuu,

Mzee Mahiga baada ya kupigwa majungu hapa bongo, aliamua kwenda Canada na kuwa mwalimu wa university, na baadaye on his own akaweza kuwa Mkurugenzi wa wakimbizi wa Umoja wa mataifa, yaani UN, stationed in Geneve ingawa alikuwa akiishi zaidi Italy,

Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano, ikaamua kwenda kumuomba UN ili atoke kule na kuwa balozi wetu huko NY, Mahiga akakubali na kusacrifice maana mshahara aliokuwa anapata kule UN, ni karibu dola 15,000 kwa mwezi kulinganisha na dola 7,000 kwa mwezi za bongo anazopata sasa, na hata marupu rupu hayafanani kabisaaa, ndio tunaema kuwa ni a big joke! yeye kutaka kuwa usalama ambako mshahara ni mdogo zaidi kuliko hata huko UN aliko sasa, hakuomba wala kujiweka magazetini huo ni uzandiki!

Nafasi nyeti zote zilizobaki sasa hivi ni kwa ajili ya WAISILAMU, hiyo sio siri na yeye hawezi kuwa mjinga kwamba hajui hilo, ndio maana ninasema kuwa hakuhusika kabisa na hizi hadithi zilizotolewa magazetini kuhusu yeye kupewa, kwani sisi tulikuwa tunajua toka mwaka jana kuwa Othman ameahidiwa hiyo nafasi, na tulisha lijadili hili la Othamn kule BCS, wala sio jipya na ni mwezi uliopita tu nilisema kuwa hii nafasi atapewa MUISILAM, kama vile Polisi alivyopewa SHEMEJI, na katibu wa CCM alivyopewa MTANI!
 
Duh !!! Mimi macho wazi kinywa kitupu akili imeniruka mwili tetemeka na nguvu sina jasho kibao kwenye baridi baada ya maneno yako haya sasa unataka kusema Mkuu wa Majeshi pia ni Muislam anatakiwa ? Wakurya wanasema Machesi duh!!

Je do u know what is the motive wa yeye JK kugawa vyeo kwa waislam what does want shoe or prove ? Je atajenga vipi hoja mwaka 2010 maana tunaona na tutahoji? Hebu nisaidie hapa .
 
Mzee Tafiti,

Huo ndio ushahidi uliokuwa unapikwa na wanaokutuma, sasa pamoja na evidence kali kiasi hicho Kibelloh hakufukuzwa kazi na ndio kwanza anahamishiwa Parieeee!

Maana huo ushahidi wako ni babu kubwa ikawaje mzee makni kama Mkapa unavyomuita akashindwa kumrudisha?

As of me, hapana hata siku moja sijihusishi na ushahidi kama huo wako wa kuokota kwenye Google, ina maana kila kinachoandikwa huko google ni kweli na ushahidi kamili wa kumfumga mtu au kumfukiuzisha kazi?

Je umeona hapo juu wajumbe wa hii forum wameanza kulifanyia kazi hili la Othman, na kumjua kuwa ni mtu wa aina gani? Au na wao ni mimi?
 
naanza kujiulia una uhusiano gani na mahiga kiasi unapoteza pumzi ndefu namna hii!

Yani umeanza na kutupa mishahara! hivi wewe n mahiga mkoje mpaka unajua mishahra yake, kama umeipata katika public domain basi tunajua kuwa mahiga ni show off, kama kakwambia mwenyewe tuthibitishie pia humu ndani kwani hakukutuma kuchafua kazi nzuri ya urais.

Kuhusu issue za uislamu nipe muda nafanya utafiti nitakuja na nyeti hapa hapa, mimi sikurupuki huwa natafiti kwanza.

Ama kweli hoja zako siku zote zinakwepa kwepa hili nakupa heko, unasema nchi haikuwahi kupinduliwa? sikusema hivyo nilichosema ni kwamba nchi ilijaribiwa na ndio maana kukawa na kesi ya uhaini, mzee mahiga sikusema alitaka kupindua au nchi kupinduliwa kwa kuwa yeye ni mkurugenzi usalama nilichosema ni kwamba hakulihandle suala lile vizuri ndio maaana wakamuondoa. Sasa kama haya ulikuwa unayajua mbona hukusema awali? au unamfichia maovu yake.

Sipo interested na kina professa Tibaijuka hao nawaheshimu na najua utendaji wao vizuri.

Mzee ES njoo na hoja.

Wewe unajua mzee Kibelloh kwa nini anabakia madarakani licha ya mascandle?
uliza ujibiwe!
 
tafiti,

Kwanza kabisa lazima utambue kuwa siyo kwamba Mzee ES hapingwi humu ndani, naye huwa anapingwa vile vile kwenye baadhi ya hoja zake. FD yuko pembeni anasoma.

Lakini kwenye hili nadhani watu tunashindwa kukuamini na data unazotoa. Wakati mwingine ninaanza kuamini hoja zako ila inapofika mahali unapoingiza eti Mahiga aliuza CV kwenye vyombo vya habari ninaanza kujiuliza hata ukweli wa mambo niliyokuamini kabla au unaposema eti JK hajawai kuwapeleka watoto wake US hapo ninazidi kujiuliza sijui wewe una define vipi watoto.

Hiyo inatupa shida sana watu tusiomjua RO kukuelewa na kukuamini. Kama alivyosema Mzee ES usije kuombea hawa watu unaowaona humu ndani waamue kumshugulikia RO. Umediliki kusema eti CV ya Lipumba ni bora kuliko Mahiga, sijui tukisema CV tunamaanisha nini?

Wengi humu tunatambua kuwa rais ameshamchagua yeye kelele zetu humu haziwe kumfanya amuondoe, pengine atakuwepo pale kwa miaka 10 ijayo, kitu ambacho tunataka kujua mtu aliyepo kwenye nafasi muhimu kama ile ni mtu wa namna gani na uwezo wa rais tuliomchagua kuteua watu kwenye nafasi muhimu na sisi tujue kama 2010 tumpigie debe tena au la.
 
Off course ninamjua Mahiga na ninawajua viongozi karibu wote wa serikali na CCM,

kusema sipingwi humu ni njia ya kutafutwa kuungwa mkono na watu humu bila hoja,

Ukiziweka CV za Mahiga na Othman, nina wasi wasi mmojawapo kati ya wawili hao akawa messenger wa mwingine!
 
tafiti then jadili,
kosa la Mahiga lilikuwa ni nini haswa wakati wa "jaribio" la kumuangusha Nyerere? mbona inaelekea usalama walifanya kazi nzuri ya kuwapeleleza wakina Uncle Tom na Hatty McGhee.

kwa upande wangu naona kama Mahiga & Co., walifanya kazi nzuri kuliko Marehemu Emilius Mzena wakati wa maasi ya 1964.

Vilevile, "jaribio" la 1980 lilisabishwa na frustrations za hali ugumu wa maisha na hali mbaya ya uchumi wa wakati ule. Hoja yako inaelekea kumbebesha mzigo wa lawama Dr.Mahiga.

CV ya Dr.Mahiga imetoka baada ya kuteuliwa kuwa Mwakilishi ubalozini UN. Haielezwi kwamba aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Angekuwa mtu kujikweza angeweka wazi kwamba aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Usalama.

Labda utendaji wa Dr.Mahiga kama mkurugenzi wa usalama ulikuwa na dosari, lakini wako Watanzania wachache sana wenye elimu, uzoefu, na hata bahati, aliyonayo Dr.Mahiga.

Sijui una maoni gani kuhusu uteuzi na utendaji wake kama mwakilishi wetu UN. Mkapa pamoja na mapungufu yake ninaamini asingeweza kuchagua wawakilishi wasiofaa pale UN.

Mwisho, unaweza kutupatia wasifu mfupi wa Rashid Othman. Ni mzaliwa wa wapi, amesoma wapi, kiwango cha juu cha elimu yake? Ni kipindi gani alikuwa hapo London, na ni muda gani amekuwa Mkurugenzi makao makuu ya usalama?
 
Mugishagwe said:
Duh !!! Mimi macho wazi kinywa kitupu akili imeniruka mwili tetemeka na nguvu sina jasho kibao kwenye baridi baada ya maneno yako haya sasa unataka kusema Mkuu wa Majeshi pia ni Muislam anatakiwa ? Wakurya wanasema Machesi duh!!

Je do u know what is the motive wa yeye JK kugawa vyeo kwa waislam what does want shoe or prove ? Je atajenga vipi hoja mwaka 2010 maana tunaona na tutahoji? Hebu nisaidie hapa .
Wewe Muhaya kama mnavyoamini kama akuna aliyesoma kama Muhaya..yaani huoni kama Waislamu wana deserve kupewa nafasi.Sasa tuambie ni dini gani basi inayofaa kuongoza nchi. Bm huyu aliepita likuwa ni wadini gani?nanyi bado mnamlaumu.

Sasa Mahiga ambaye aliondolewa na Nyerere akiwa deputy sec gen ofisi ya Raisi ndo haya unayoyaita majungu..basi kama ni majungu aliyaanza baba yetu nyerere ambaye alimuona hafai kuwepo ofisi ya raisi. Mahiga mwaka 82 aliondolewa ofisini pale baada ya kushindwa kuihandle ile issue ya uhaini na yeye akiwa shahidi x...anajuwa wazi kama hawezi kufit anachofanya nikuwatuma nyie watuwake mpige kelele tu lakini anajuwa wazi kama hawezi kutia pua tanzania ya leo.

Mwisho sidhani kama kuna alielinganisha CV ya Othman na ya Mahiga tunjuwa ana phd na amefanya kazi un na kuwa mwalimu lakini tunachokisema ni Raisi amemuona Othman anafaa wenye nafasi ile.Labda chakusaidiana ni kwanini mlitaka Mahiga awe DG wa usalama wakati hayumo kwenye idara ya usalama?sasa mnataka mtu from no where achukuliwe kwanini msiseme asihaguliwe kuwa balozi au bunge wa kuteuliwa na baadae kuwa waziri..lakini mnasisitiza kama yeye ndo anafaa..hapa kuna kitu mnakitafuta.

Na huyo Mhaya hapa juu anasema kama kwa nini JK nafasi zote anawapa waislamu amesahau kama siku ile wameapishwa watu watatu na wawili walikuwa ni wakristo ?
 
Tafiti;
This is a million dollar question ambalo mzee ES ameuliza.

"Othman alirukaje toka u-Agent wa kawaida kule London mpaka kuja kuwa Assistant wa Director bongo, mpaka leo kuwa Director? Wakati mwaka jana October alikuwa agent wa kawaida ule London, yaani between October mwaka jana na leo August, miezi kumi tu tayari ameshakuwa good enough kuwa Assistant Director na leo kuwa Director kamili?"


If u can come up with the logic behind the "not so experienced" RO kupata kuwa director wa usalama bongo wakati few years ago alikuwa mzushi tu wa kawaida hapo london then I will believe you, otherwise utakuwa unatuzingua tu, PLUS this guy is UNPROVEN hatuijui elimu yake and we all know hana experience.
 
Kingwele
Ama hujui ulichokisoma ama una chuki sasa au ni jazba ama watu wamegusa mahapa pako . Uhaya na wahaya hapa vinatoka wapi na kwa nini ulete haya .Nimesoma sana habato ya Mugishagwe hajataja kisomo na wala hajamtaka Mahiga awe mkuu wa usalama . Maswali yake yako wazi na si Uhaya wala ukabila wala udini . Hebu fafanua ni aina gani ya ujumbe ulitaka kuwapa watu hapa ukumbini badala ya kukimbilia kuwanyooshea wahaya vidole .
 
hii cv nimesema tupo wote manake tungefurahu kujua sifa za mkurugenzi wetu.

Sijakanusha kuhusu watoto wa jk kwenda US. nimesema sina data katika hilo na nikaomba proof. Aliekaa na data ni Mzee ES ambae anajidai kwamba zipo ila kazizuia wakati meseji ya mwanzo ambayo watu hawakuhoji alisema anazo tepu! kwa vile waliokuwemo mwanzo humu ni wale ambao hawakuwa wakihoji for proof! naamnini kwa sasa huna data unashindwa kuziproduce sasa nasema hivi nitakubali hoja inayoletwa na uthibitisho huna kaa kimya, mimi huichukulia hii forum kama open court hivyo kila ninachosema huwa naweka na ushahidi au reference, nimekuletea ya mzee kibelloh umedai ni suala binafsi, nimekuambia kuhusu mahiga kufukuzwa umekuja na issue za kwamba hakufukuzwa aliondoka! kumbe unajua mbona hukusema? au ulikuwa unacapitalize na watu kutokuwafahamu?

Sasa wamejitokeza watu humu nani na nashukuru binafsi nimepokelewa uzuri tumeanza kuchangia mzee ES unahaha kwamba nafasi yako ya kuheshimiwa hoja zako kwisha!

Tangu alipoteuliwa ndio umekuja na la uislamu sasa hivi? waislamu nawaheshimu sana na kwa kweli siwezi kuthubutu kuweka baadhi ya vitu humu vitakavyowaoffend najaribu kufanya utafiti kuona hizi allegations za udini unazoweka sasa hivi facts zake ni vipi na kama kweli lipo ni kwa kiasi gani? natumai waislamu mliopo humu mtatusaidia, hoja zangu nitazileta naahidi na mimi ni muungwana sivunji ahadi.

kingwele humu ndani alihoji tena baada

Mzee ES tupe uhalisia wa knowledge yako ya hao viongozi wengine manake unajua mshahara wa Mahiga, viongozi gani wengine unajua mishahara yao manake la mahiga umelishupalia mno wakati ni zilipendwa tu.

humu umekuwa ukidai nirejee BCS umeshajadili nipe data za huko nitazichambua humu humu usiniambie nisake kitu unachoweza kucut and paste!

lete data tujadili!
 
selemani said:
Tafiti;
This is a million dollar question ambalo mzee ES ameuliza.

"Othman alirukaje toka u-Agent wa kawaida kule London mpaka kuja kuwa Assistant wa Director bongo, mpaka leo kuwa Director? Wakati mwaka jana October alikuwa agent wa kawaida ule London, yaani between October mwaka jana na leo August, miezi kumi tu tayari ameshakuwa good enough kuwa Assistant Director na leo kuwa Director kamili?"


If u can come up with the logic behind the "not so experienced" RO kupata kuwa director wa usalama bongo wakati few years ago alikuwa mzushi tu wa kawaida hapo london then I will believe you, otherwise utakuwa unatuzingua tu, PLUS this guy is UNPROVEN hatuijui elimu yake and we all know hana experience.

Tafiti nisaidie na hilo swali hapo juu, am curious to see your perspectives koz It doesn't make any sense huyu RO kupata hiyo kazi basing on his background infos that we know.
 
selemani said:
Tafiti nisaidie na hilo swali hapo juu, am curious to see your perspectives koz It doesn't make any sense huyu RO kupata hiyo kazi basing on his background infos that we know.
Bro Sele unadhani inaingia akilini kama tu atoke kuwa agent wa kawaida na achaguliwe kuwa DG usalama. Japokuwa watanzania tumaskini lakini si maskini wa aina hii serikali haiendeshwi hivyo. Maana kila mtu angepiga kelele ni kisema mtu simaanishi hizi kelele za Es.Habari zilizopo jamaa yuko kwenye idara zaidi ya miaka 25 na ameshawahi kabla ya kuja UK kuwa mkurugenzi katika moja ya idara za pale(siji ni idara gani) ni msomi wa masters degree tena ana UK qualificatiion from UK univ,sio za kununua kwenye web amekwenda darasani.

Sasa hizi kelele kama alikuwa ni agent wa kawaida ni za kitoto tu.wewe mtu mwenye MA awe agent wa kawaida usalama..sijapata kuona.Ila the formal CV kama haja ipo kuondoa hii adha ni vyema ikawekwa wazi japokuwa kwa maoni yangu bado nawaamini viongozi wetu.

Mugushagwe nimekutaja kwa kabila lako kwa sababu umetoa dharau kama kwanini waislamu wanachaguliwa kushika nyadhifa serikalini?inamaana kama hawastahili au hawakusoma kama mlivyosoma nyie?Sitaki malumbano na waislamu wenyewe wakiiona hii hoja yako ndo maana nikaona nikuonye mapamema.

Halafu nimezidi kukariri kama ikiwa huyu jamaa hafai nani basi mnaona anafaa kwenye zile ranks za watu wa usalama kule nyumbani kuwa DG?
 
unajua bwana selemani kwa kweli mimi nashindwa hasa kujua kazi za usalama beyond zile post na titles zao, humu ndani mimi nimekuwa advocate wa unfair treatment anayopewa huyu mkurugenzi na ningefurahi kuona cv.

Sasa watu wanapodai alikuwa agent wa kawaida London nadhani wameconfuse usalama wa taifa na hadithi za kubuni za James Bond ndio utaona kuna watu wanajifanya eti alikuwa marekani kavaa miwani myeusi! yani hawa nadhani hata kihaiba hawamjui RO manake yeye sio mlinzi, ni mabodyguard wa viongozi ndio pengine huvaa miwani!

Halafu kingine naweza kukusaidia kwa knowledge yangu kwa sasa ni kwamba hufikia wakati mtu akawa kituo cha nje lakini akawa na level ya ukurugenzi au kama vile mabalozi wana hadhi tofauti kuna ambao wanaitwa minister pleniponitentiary ambae kwa kiswahili tumwita balozi, kuna wengine ni mabalozi lakini wana hadhi ya ukurugenzi wizarani, sasa nadhani ujue kuwa vyeo vya usalama hatokuja kujua nani anafanya nini.

Humu kuna watu wanaonekana kutojua hasa usalama wanafanya nini manake kwa vile mkurugenzi kaamua kwamba ujambazi atakwenda nao sambamba baadhi wanasema hajui mipaka yake? hivi nyinyi mliotoa hivyo mnajua mipaka ya idara ya usalama?

labda tusaidiwe hawa jamaa wanaomuunga mkono mahiga watupe vigezo vinavyotumiwa kua mkuu usalama manake kama wanaweza kujua mishahara yao basi hili hawatoshindwa.

things are getting tighter for liers...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom