Rashid Othman ndiye Boss wa Usalama

Rashid Othman ndiye Boss wa Usalama

Status
Not open for further replies.
Yes Mzee ES great facts, wao acha wajimalize bila kujua. Labda wataikimbia/wataihama nchi kama alivyofanya SUmaye eti anaenda kusoma!

Ni kwa nini wameachama tu wanatunisha matumbo yao. hii vita ya umasikini hata kama mnasema ni viini macho anyesema sema ni rais peke yake. Wenzake wanamcheka tu na kusema tunakusubiri tukuonyeshe jinsi tunavyojua kujizolea utajiri kwa waliolala.
 
Mimi mpaka hapa sijaona kipya alichokiandika huyu Mzee Es,anajaribu ku divert topic..mara Radhia Msuya muhuni...mara wawekezaji wanaanza kuchomoa bongo tangu JK alipokuwa Raisi lakini ameshindwa kutoa hata mfano wa kampuni walau moja iliyoondoka. ameambiwa akachukue data Tanzania trade centre London aone jinsi opurtunities zinavyongezeka ameingia mitini. Mara oh! RO kidhugu hakipandi hivyo atakuaje DG wa usalama. Hizi ni hoja za kitoto.

Lets assume kama hakipandi japokuwa na juwa kinapanda vizuri tu kwani amefanya kazi na kusoma nje(masters yake ameichukulia UK,Sheffield). Kwani viongozi wangapi hawapandishi lugha za kigeni na bado ni viongozi wazuri tu kwenye nafasi zao. Kwani kiingereza ninini?inaelekea kijana wewe ni mtumwa wa kiingereza. Kwa taarifa hayo ya lugha kutokupanda ni majungu tu kama humfahamu anapandisha lugh vizuri tundo maana UK wakampa masters na akaaminiwa kuakufanya kazi kwa waingereza miaka nane.

Kuhusu hiyo habari ya watoto wa JK wanakaa wapi wakija UK naona ni irrelevant kujadili maana ni majungu tu.Lakini lakuzingatia kama ulivyielezwa ni uzalendo wa Raisi wetu licha ya influence tangu akiwa waziri na angewasomesha watoto wake nje from sec mpaka vyuo kama wafanyavyo viongozi wengi tu lakini wapi.Hii tosha inaonyesha kama jamaa sio mbadhirifu na anaunchungu na nchi yake.Majuzi tu alitangaza kama atahakikisha viongozi wanatibiwa nchini badalaya ya kwenda nje kwa kuboresha hospitali zetu.

Kuna mtu aliandika mwanzoni kama eti jama alikuwa akijifutua JK alipokuja USA ndo watu wakasema kama yule jamaa anatoka London..huu ni upuuzi RO aliondoka UK hata kabla JK hajakuwa raisi na hata kama alikwenda na JK kule USA alikuwa hatokei LONDON.Kuna mwingine amedai kama kwa nini huo uDG amepewa bwana mdogo..jamaa ana miaka 54 almost sasa ndo kijana mdogo hapa.Kuna wengine eti wanasema kama angepewa Dr Maiga yeye ndo anafaa zaidi.Lakujiuliza huyu mzee anayestaafu ana miaka 62 na Mahiga ana miaka 61 tofauti iko wapi sasa lazima apatikane mtu atakayekwenda na mwendo mdundo wa nguvu mpya. Na nyie mnaodai kama huyu bwana hafai kuwa DG hebu tutajieni anayefaa sasa katika hizo ranks za usalama..na hapa tumeshaona kama Mahiga kutokana na umri hafai.acheni chuki za kitoto kama mnauchungu rudi Tz na tufanye kazi sio kuendeleza chukia za kitoto.

Na kuhusu matusi nimefuatilia mjadala wa mzeeES na tujadili nilichokiona mzee ES ndo aliekuwa wa kwanza kutoa mananeno machafu na ya matusi.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Mimi nakubaliana na maneno ya Mugishagwe kabisa kwamba meno ya mba hayaumani.Sasa nimekaa kimya sana nimeona nitie kaneno . Mimi nasema hapa ni mahala hasa na muda wa sisi kusoma na kuoima yanayosemwa. Ndugu jadili hili jamvi lina wakubwa na wenye heshima kama sisi . Unasema ulisema ni mijadala ya kitoto baadaye umeamua kuja baada ya kuona hakuna utoto labda ulikosea kudhani hayo . Hapa kuna watu wamekomaa na ana data . Tunajadili Nchi . Ikiwemo sisi na Rais .

Umesema majina fulani hayafai ? Hapana umekosea kipendacho roho bwana .Jina lake kalipenda kabla na hata sasa wewe ni nani hadi umchagulie jina ? Hili ni kosa . Fikiaduni ana mambo yake na kusema wacha jina hilo unavuka mipaka ndani ya nyumba yake .

Sasa nasema naungana na Mugusha kuomba watu wakae mpambane na sisi wenyeji wa jamvi hili tutachambua na kujua nani mkweli na nani anatumiwa kutuvuruga .

Namaliza ka kuoma CV ya RO ndugu Jadili hapo nitakuwa nimepata kitu kimoja wapo amacho nakitafuta . Naomba CV yake maana ndiye chanzo ha mjadala .
 
Mchango wako wa tatu unaanza kuelekea kuielewa hii forum sasa,

Mzee Salim ana Degree ngapi? Lakini amesoma wapi, hiyo kusoma kwa akina Nchimbi ndio utamlinganisha na Mahiga ambaye ameshakuwa Professor Canada, na Mlimani? Na Director wa Wakimbizi Europe?

Please leave Mahiga alone, huyo ni moto wakuotea mbali Tanzania ingekuwa na viongozi WATANO TU! kama yeye nchi ingesogea mbele tena sana, ndio maana yeye pamoja na kutokuwa na kambi yoyote kati ya kambi za siasa bongo, bado JK hana hata mpango wa kumuondoa pale maana huyo ni BABU KUBWA, miaka 61 ndiyo miaka inayotakiwa kwa kiongozi wa uasalama wa nchi au SPY CHIEF, je Negroponte ambaye sasa ndiye boss wa Usalama Us ana umri gani? Wewe umewahi kumuona Mahiga, ni mtu anaonekana kijana mdogo licha ya umri wake kwenye numbers, halafu huyu Mahiga hufanya kazi at least masaa 16 kwa siku kule kwenye baraza la usalama alipokuwa mwenyekiti, itakuwa bongo, huyu mzee ameiletea Tanzania heshima mpya kabisaa Bongo kule UN, yaani do not even go there bro, kwa Mahiga NY sasa hakuna majungu tena wala uswahili swahili wa balozi aliyepita!

RO alikwenda US kabla JK hajawa rais, akiwa bado stationed London mtu wa usalama wa NY yule Mhaya (ambaye sasa amehamishiwa London, na hivi ninavyoandika yuko bongo), alikuwa amesafiri, na kwa sababu Mkapa akiwa rais alikuwa anaenda kwenye GA NY, ndio RO akaombwa aende kule kumsimamia, hakuenda JK akiwa rais kwa sababu kwa taarifa yako JK hajawahi kukutana na wananchi wa NY toka awe rais, kwa hiyo mzee umechanganya FACTS hapo, na alipokwenda siku ya mkutano ndipo akawa anajiweka weka sehemu za kutafuta attention na ku-act very childish, to the point hata mimi nilikuwepo kwenye huo mkutano ndio nikamjua kwa mara ya kwanza kwamba ni usalma anatoka London, kwa taaraifa yako pale kwenye mkutano kulikuwa na usalama kibao ambao walikuwa wame-cool, wala usingweza kuwajua!

JK hela ya kuwasomesha watoto akiwa waziri hakuwa nayo, isipokuwa ya kuwahonga kina Honeymoon hiyo kweli, ndio kwanza juizi wamechukuliwa na wazungu huko UK, mmoja amepelekwa Oxford, mmoja akapelekwa kwa wazungu kuishi, akakuta wanaishi na MBWA ndani ya nyumba akakataa kuwa hawezi kuishi na MBWa, ndio wazungu wamemuhamishia kwenye apartment wanayomlipia, na ni hao wazungu waliowaalika watoto hao juzi kwenye hafla ya Courtyard, ambayo balozi alihudhuria, lakini hakuna ofisa wa hapo aliyealikwa. Huko kwenye hafla kulikwa na wawekezaji kibao wa bongo hasa wahindi, ambao watoto wa JK wakiwepo walitulia kimya wakati huyu mkubwa akijigamba jinsi anavyofanya kazi sana na kwamba baba yake hana mfano kwa kazi, walipoondoka tu huku nyuma waliwaachia wawekezaji kichekesho, tena jaribuni kuwafundisha namna ya ku-behave mbele ya wazungu ambao wanajua kila kitu ndani ya bongo, halafu unajaribu kuwadanganya, huu uhusiano na hawa wazungu JK ameuanza lini?

Mzee Kibelloeh amefanya kazi nzito sana hapo katika kuisadia Tanzania, I must admit kwa wananchi wengi wenzangu humu na pengine kuwa Kibelloh hata siku moja hana appeal nzuri kwa wananchi wa kawaida, hilo siwezi kumtetea, lakin I am proud kusema kuwa ametujengea heshima kubwa sana na wawekezaji, ndio maana huu mwezi mzima wazungu wamekuwa wakimuita kila kona kumuaga, huyu mzee amepigana mpaka Mzee Shija amepewa kazi nzito akiwa mwafrika wa kwanza kupewa kazi hiyo Commonwealth, halafu angalia historia je ni viognozi gani waliwahi kuwa mabalozi London kutoka Bongo,

Nsekela - Director National Bank,NBC
Nyakyi - Katibu Mkuu Foreign,
JM - Foreign Minister,
Mchumo - Minister Industries and Commerce,
Dr. Shariff - Director ZNZB
Kibelloh - Katibu Mkuu foreign,

Hii ni kukuonyesha kuwa hicho kituo sio cha mchezo kiasi sasa cha kupeleka Private Advocate, wewe huoni kuwa hiyo ni a big joke? Yaani inaonyesha huko Dar kuna uongozi mpya wa aina gani kama sio uozo?

Kwa kumaliza ninasema hivi, niyinyi tuchezeeni tu Watanzania, ila siku ya siku itakapofika wewe na hao viongozi wanaoukutuma mtashangaa kuwa wananchi wanyonge tuna ushahidi wa kutosha wa kuwahukumu kuwatundika risasi pale Sanamu monument!

Anyway this time mchango wako wa tatu was better kuliko ile miwili ya mwanzo, karibu bro na this was a great debate now as usual nina move forward na next topic!
 
Haya maneno ya watanzania kuchezewa juzi nimeona Murangira anamweleza Fillga na leo yanarudiwa na Es nadhani sasa tuko serious .Haya mazinga ombwe na hotuba za kuiga sauti ya mwalimu iko siku tutahojo Tanzania ni yetu sote .Sasa mambo haya ni kwa zamu nasema alianza mkoloni na leo ni JK kesho anaweza kuwa Mkira ama mandela ama Fikiraduni basi mjue tutahoji kila kitu bila kificho wala kusema kwamba tutaleta vurugu Nchini .
 
Kingwele

Labda wewe ni mgeni au tulikuwa wote toka huko nyuma tulikotoka. Hapa hakuna mtu anayekatazwa kusema chochote anachotaka. Ila ukisema kitu chochote ambacho kina ulakini lazima uwe tayari kudhibitisha otherwise we will come on you. Mimi naweza kukili kuwa I am vey limited na RO nawasikiliza ninyi nijue ukweli ni upi. Ila lazima ujue haya mambo yapo. Kuna mtoto wa waziri mkuu mmoja mstaafu alikuwa ananiambia jinsi alivyokuwa anahudumiwa na kampuni moja uingereza vitu vingine hata baba yake alikuwa hajui ili tu wawe karibu na baba yake.

Huwezi kusema tusijadili watoto wa JK eti kwa kuwa ni majungu. Kama ni majungu tuambie ni kivipi na majungu. Umesema JK hajawahi kupeleka watoto wake US! Naomba nisahishe kama nimekuelewa vibaya. Je unajua JK alishindwa kulipa kiasi gani cha fedha kwa mtoto wake aliyekuwa anataka kurudishwa bongo toka US? Hata huyo mtoto wa hapo kwenu UK anayesoma masters unajua kwamba alipewa offer ya nyumba ya million 150 bongo mara tu baba yake alipokuwa rais, au na haya ni majungu?

Kamuulize Mahita na Nchimbi tulivyowafanya tukiamua kudhibitisha tunayosema siyo majungu. For now, we do not want to stress them too much, tunawaachia wafanye kazi za maendelea ila tunarekebishana kidogo kidogo pale wanapokosea.

Mwisho, lazima mtambue kwamba hii forum siyo ya chama fulani cha siasa au forum ya vyama vya upinzani au ya CCM. Wanachama wa CCM waliomo humu ndani ni wale wanaotambua ili CCM na serikali ifanye vizuri lazima ikosolewe kwa yale mabaya inayofaya na kusifiwa kwa mazuri.
 
I love this joint man. I have to agree with Mzee ES huyu Othman Rashid VS Mahiga himself doesn't make any sense hasa ukiangalia facts kwamba JK was trying to promote him since Mkapa days.

Nadhani CV ya huyu jamaa ikianikwa hadharani will tell kama ana shule au miyayusho tu.

Swali nilalouliza waungwana, kwa nini JK amkomalie huyu jamaa despite of his "deficiencies"??
 
Lakini wakati mwingine watu wanashangaza!!!

Selemani Kagombee urais wa Tanzania ili umchague Mkuu wa usalama wako!!

Jamaa ana haki kikatiba sasa tararila za nini?. Facts anazotoa Mzee Es ni sawa lakini alishasema kuwa Jamaa JK katiba inamruhusu ila tu kachagua vibaya kwa maoni yake na ya wengine.

Sasa selemani unakuja eti JK kamkomalia RO!!!!
Ameisha chagua hawezi kuondoa kwa kelele zako. Labda ungelisema unapiga kelele katiba ibadilishe na siyo kama unavyosema, inasikitisha
 
Mzee Mkwawa,

Heshima yako mkuu,

I am not sure kuwa majibu yako kwa Mzee Selemani, ambaye ni mchango wake wa kwanza humu ni ya heri na amani, if that is the case basi na wewe ungehitaji kwenda kugombea urais na sisi wote, ili tuwachague viongozi tunaowataka,

maana kila siku humu tunakosoa viongozi wa nyanja mbali mbali za serikali yetu, Je jawabu lake ni kwenda kugombea urais ili tuchague viongozi tunaowataka?

Tuwaheshimu wanachama wanaoingia kwa ustaarabu kama Mzee Selemani, na tuwakaripie wale wanaoingia na matusi na kejeli na wanaotumwa kuja kutuvuruga, yeye ameuliza swali tu na ameomba CV na kuna wengine pia walishaomba hiyo CV, sasa noma ya nini?

Mzee Selemani ninapenda kuchukua nafasi hii kukuomba radhi iwapo majibu haya ya mwanabodi mwenzetu yamekukatisha tamaa, unakaribishwa kutoa michango yako bila ya wasi wasi na ujisikie uko bongo hapa, nyumbani pa FREE SPEECH AT BEST!
 
Mzee ES
Nadhani kati ya Mkwawa na Selemani kuna tofauti kidogo ya kuelewana. Selemani ameonekana kuamini maneno yako zaidi kuliko ya tafiti, lakini bado ana wasiwasi na maelezo yenu kuhusu elimu ya RO ndiyo maana ameomba CV. Swali lake la mwisho nadhani ndili linalochanganya "amkomalie" hata mimi sijui alikuwa ana maanisha nini? Kama alikuwa anataka kujua ni kwa nini JK ameamua kumchagua yeye pamoja na udhaifu wake nadhani ni swali zuri ambalo anatakiwa kujibu. Nadhani tumpe Selemani nafasi ya post yake ya pili kutuelezea vizuri alichokuwa anataka kujua. Karibu Selemani umefika nyumbani.
 
Waungwana;
Kwanza kabisa mi nilikuwa msomaji mkubwa tu kuanzia enzi za BCS, na kuingia humu ndani.

Swali linalonichanganya ni the fact that (according to ES) JK alihakikisha Mkapa anam-promote huyu RO ili aweze kumpa u-chief, also ukilinganisha Mahiga na RO havilingani, ni sawa na Zidane na Lunyamila. Swali langu pamoja na waungwana wengi humu ndani ni kwamba RO is unproven, there is no proven evidences kwamba he deserve this post compared to Mahiga...sasa what earned him zis job????
 
Mzee ES, niko positive kwenye mchango wa selemani,

MCHANGO WA SELEMANI NI MZURI ILA TU LILE NENO "KUMKOMALIA". JK katiba inamruhusu ila sisi tuweke mabaya yao wazi ajue tunajua.

Niko pamoja nanyi ila ni msisitizo tu KATIBA YA NCHI INABIDI IANGALIWE UPYA ILI RAIS APUNGUZIWE BAADHI YA MADARAKA. kWA MFANO YA UTEUZI WA NAFASI NYETI KAMA HIYO BILA HATA KUPELEKWA BUNGENI KUTHIBITISHWA. ILA LINATAKIWA BUNGE MAKINI SIYO KAMA HILI LETU!

WOTE HATUWEZI KUGOMBEA URAIS ITAKUWA CHAOS, ILA TUNATAKA VIONGOZI WABADILIKE NA WAJUE KUWA UWEZEKANO WA WAO KUFUNGWA UPO PIA SIKU ZA BAADAYE KAMA WATAENDELEA KUVURUNDA KWENYE MALI ASILI ZETU. AKIJA MTU NA BUNGE LAKE KATIBA ITABADILISHWA NA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.

TUNAENDELEA ALUTA CONTINUA!
 
Naona humu ndani tunaenda tukizunguka kiasi baadhi naona wanashindwa kujua tunajadili nini,ES ulianza na ushambulizi kuwa huyu jamaa kapewa hii nafasi ''eti kwa sababu ya kumfixia JK vimwana'' then ukaja ukamuingiza na Mama Radhia Msuya kisha ukaanza kupiga ndogondogo humu eti kuwa Rothman kwa sifa hamfikii Mahiga.

Haya yote umeshindwa kuyathibitisha kila tukikutaka utoe hizo tepu zako za uthibitsho unakuja na mengine sijui watoto wa JK walikaa hoteli gani au walihudhuria party gani.Hivi sio crucial kwangu katika kupima utendaji wa JK, nashindwa kuvijadili kwa sasa kwani vipo nje ya context ya mada yetu. Anzisha au mwambia admin afungue topic nyingine ya maadili ya viongozi nitaweka ya kwangu humo, kwa sasa tudeal na hili la madai yako eti RO hafai.

Naona watu wengi humu ndani wapo very biased kwa sababu wanazozijua wenyewe, watu wanadai rekodi ya mahiga ni impeccable na kwamba RO hamfikii, wakati huo huo watu wanaomba CV ya RO, sasa mmejuaje kuwa RO hamfikii Mahiga wakati CV mliyonayo ni ya mahiga peke yake? Subirini mkishaona CV ya RO ndio muanze kuchambua na kuconclude.Hwezi kuamua kesi ukiwa na hoja za upande mmoja...

Mzee ES unadai eti Ooh tungekuwa na kina Mahiga watano tu basi nchi ingekwenda mbele kuliko sasa?haya ni yale yale ya wale wanaosema tungekuwa na kina Lipumba watano tu tungefika mbali, CV ya lipumba huwezi kulinganisha na Mahiga hata siku moja,zipekueni mtwambie nani bomba.

Naam Mzee ES na wengineo wanaodai CV mnayo haki ya kikatiba kueleza yanayowakera na tukubali kuwa kwa sasa tuna uhuru mkubwa wa kutoa mawazo yetu kuliko huko nyuma na pia tuna access to so much information. Alipoapishwa Mzee Apson kuna aliejua? Mbona hamjahoji CV ya Mzee Apson kujua profile ya Mkurugenzi huwa inakuwaje?Sasa hivi tumepata Rais ambae anachapa kazi na anakwenda sambamba na wananchi kwa kuwapa wanayostahili kupitia vyombo vya habari, ukweli kuwa tumekaa tunachangia kuhusu uteuzi wa RO ni ushahidi tosha kwamba tumepewa enough information.

CV ya Mahiga ipo nje kwa vile na yeye alikuwa analilia hii nafasi, akaona akiiuza kwenye vyombo vya habari basi kila kitu kitumuendea vyema kabisa,kasahau kuwa umri siku hizi nao ni factor!Kama alivyosema kingwele kuwa mheshimiwa mkurugenzi anayeondoka ana miaka 62 na mzee Mahiga ana umri wa miaka 61, sasa badala ya mzee Mahiga kufikiria kustaafu akapumzike na watoto/wajukuu if any kaamua kuuza cv yake tena kwa waandishi eti watu waone alivyomchapa kazi!

Sasa mzee Apson ameshikilia nafasi ile kwa takriban miaka kumi meaning he was just 52 wakati anateuliwa, a very good age kwani unaweza kuchapa mzigo sio mchezo, ndio maana Mkapa alipoingia tena akasema naomba tuungane pamoja.Sasa usalama wa taifa letu umekuwa entrusted kwa mkuu RO basi watu wanadai eti JK ndio aliekuwa akimhimiza mkapa amchague huyu bwana awe Mkrugenzi wa Utawala, hivi nyinyi mnadhani Mkapa alikuwa kikaragosi au Rais? hivi kweli Ben anaweza kutiwa presha akakubali? sijawahi kusikia popote katika miaka kumi ya Ben kwamba aliwahi kulazimishwa afanye jambo fulani yule ni msomi anafanya kazi kwa conviction ya hoja kapelekewa wasifu wa RO akaona huyu ndio anaetufaa, beside ni yeye ndio alieridhia R0 aende London as Ofisa mwandamizi pale sasa kelele za nini, thibitisheni hoja zenu dhaifu ES!

Katika baadhi ya hoja uliwahi kudai mlimuonya Mzee Kibelloh kuhusu RO na Salva na mbinu zao, hivi unadhani iwapo JK ataamua balozi aondolewe na yeye akiwa kama waziri wakati ule angeshindwa kweli? Au sasa kama angekuwa hamtaki kibelloh angempa ubalozi Paris? Usilete majungu yasiyokuwepo? Halafu hoja zako Mzee ES zinakinzana mno manake mara Mkapa katiwa shinikizo amteue RO halafu mara Mkapa huyo huyo kakataa umbea wa kumuondoa Kibelloh hapa, what do you take Mkapa for? kama aliweza kufanya zito la kumteua DG wa usalama atashindwa 'dogo' la kumuondoa Kibelloh? Tafiti then Jadili mzee ES

Nimefurahi kuwa hii forum inasemwa haina chama wala mwelekeo wowote wa kisiasa na kama wapo wanachama basi wanatambua kuwa ili kuwa imara ni lazima tukosoane, naam mimi naamini hivyo, kwa sasa sina chama ila naamini to have a healthy democracy we must scrutinize each and everything na kwa ndio maana nikaona nijiunge na blog hii, haina maana kwa kuwemo humu ndio kigezo cha hoja kali kama anavyodai Mzee ES, naheshimu sana ukongwe wenu wa kushiriki katika mijadala lakini hio isiwe ni hoja ya kutetea hoja dhaifu...kuwahi sio kupata bali ujanja kupata kama hoja makini hata akitoa mtoto zinafaa!

Tuwe fair tunapotoa mijadala na tunapopima as well.
 
Jamani nimekuwa nikufuatilia siasa za DRC na hasa uchaguzi.

Inaonekana THE FORMER REBEL LEADER MR BEMBA NI MKAIDI SANA.!

KWANZA VITA YA KONGO YA WAKATI HUO IMEPELEKEA WATU ZAIDI YA MILIONI 3 KUPOTEZA MAISHA. NA WAHUSIKA NI HAWA HAWA AKINA BEMBA NA RAFIKI YAKE MSEVENI NA MWINGINE KAGAME ANALIYEKUWA ANAMUUNGA MKONO AZARIA RUBERWA!

HAPA KWETU BWANA MKUBWA BMW ALIKAA KIMYA AU ALIWAUNGA MKONO AKINA M7!

KWA UPANDE WANGU NINADHANI TUKIWA NA DRC HURU YENYE AMANI WATANZANIA TUAWEZA KUFAIDIKA NA MENGI IKIWAMO KUFANYA KAZI HUKO, BIASHARA NK!

KWA HIYO NINAOMBA SAFARI HII SERIKALI YETU ISIFANYE MAKOSA. MAANA TUNAATHRIKA SANA NA MIZIGO YA WAKIMBIZI NA MAJAMBAZI YENYE SILAHA KUZAGAA NCHINI MWETU. NI VEMA NASI TUPELEKE JESHI MPAKANI MWETU KIGOMA NA KUWAZUIA WAKIMBIZI WA KONGO KUINGIA KWETU NA PIA UGANDA NA RWANDA WASITUVURUGE SAFARI HII! TUNAOUMIA NI TANZANIA WAO WANANUFAIKA NA WIZI WA MADINI. UGANDA NA RWANDA SIYO MEMBER WA SADCC.

WITO KWA JK TUMIA NAFASI ULIYONAYO SADCC! IKIBIDI ATAKAYEKIUKA AFIKISHWE THE HEGEL. BEMBA SIYO MUNGU. AKINA TAYLOR WAKO THE HEGEL IWEJE YEYE?

KAMA AMEPTA 22% SASA VURUGU ZA NINI NA AMEENDESHA KAMPENI KWA UKABILA NA UKANDA.

USHAURI MWINGINE KWA DRC. UCHAGUZI UKIISHA WAANZE TARATIBU ZA KUHAMISHIA MAKAO MAKUU YAO KATIKA YA NCHI?

NINAOMBA MICHANGO YENU LABDA MESSAGE ITAMFIKA JK NA AKAYAFANYIA KAZI!
 
Wana Bodi,
Samahanini.

Nimeweka Hapa Kimakosa. Mchango Huo Hapo Juu Ni Topic Mpya!

Kama Kuna Mchangiaji Achangie Kwenye Topic Mpya.
 
MZEE ES
HII NDIO STORY NILOKWAMBIA NIMEIONA KWENYE GOOGLE, wajumbe wengine mkisearch kwenye google mtaona uchafu wa huyu balozi ambae ni kambi ya Mzee ES na amekuwa akimtetea sana.

Sasa Mzee ES tuambie Salva kahusika vipi?!!!

BALOZI KIBELLOH ALININYANG'ANYA PASSPORT YANGU


06/28/2005
Na Saidi Yakubu, London, Uingereza


Balozi wa Tanzania nchini hapa, Hassan Kibelloh ameingia matatani tena baada ya kumnyang'anya pasi ya kusafiria ya mpishi aliyemuagiza toka Tanzania, imebainika.

Bhoke Mgoyo (31) aliyekuwa mpishi wa Balozi huyo toka 3 julai 2002 mpaka ajira yake ilipositishwa bila maelezo 31 Agosti 2002, amesema alinyang'anywa pasi yake ya kusafiria namba A032585 bila maelezo ya msingi.

Bhoke Mgoyo na mwenzie aliefahamika kwa jina moja Rua walikuwa wakifanya kazi katika hoteli ya Bahari Beach wakati Balozi Kibelloh anateuliwa kuja Uingereza. ‘Balozi Kibelloh alikuja pale hotelini akitafuta mpishi atakaeambatana nae kuja hapa Uingereza, aliongea na meneja wangu pale hotelini George Liwolweki na kwa bahati nilichaguliwa mimi na mwenzangu'

‘Baada ya kukutana na Balozi aliniambia niende wizara ya mambo ya nje nikamuone DAP [Director of Administration] au msaidizi wake aitwae Tungaraza aweze kushughulikia safari yangu na kama hao wawili hawapo alisema nimuone Bi Mgana au Bwana Yahya Simba'.

Hata hivyo Bhoke alisema Balozi hakumueleza malipo yao yatakuwaje wala kutoa ufafanuzi wa mkataba wao wa kazi kwa maelezo kuwa kila kitu kitashughulikiwa akifika Uingereza.

Bhoke anaeleza kuwa alikwenda Wizara ya mambo ya nje waliompa barua ya kwenda kuombea visa ubalozi wa Uingereza na waliwasili London tarehe 3/7/04 na makazi yao yalikuwa ni nyumbani kwa balozi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Bhoke anasema walifanya kazi katika mazingira magumu sana chini ya usimamizi wa mke wa Balozi Kibelloh, Bi Amina na walijaribu kuvumilia kwa matumaini kuwa mambo yangekuwa mazuri lakini ajira yao ilisitishwa kwa hila tarehe 30/08/02.

‘Kazi ilikuwa haina muda maalum wa kumalizika, tulianza kazi saa 12 na nusu asubuhi mpaka saa mbili usiku bila mapumziko. Kibaya zaidi tulikuwa tunakula mara moja tu kwa siku kwani mama Balozi alikuwa haturuhusu kula kabla ya watoto wake na hivyo tulikuwa hatuwezi kula mpaka wao warudi shule mchana'.

‘Mapumziko pekee tuliyokuwa tunapata ni masaa nane tu kila baada ya wiki mbili, mazingira ya malazi yalikuwa sio mazuri kwani tulikuwa tunalazwa jikoni katika nyumba ndogo (apartment) ya mpishi kwa maelezo kuwa vyumba vyote ni kwa ajili ya wageni'

Kwa mujibu wa maelezo ya Bhoke nyumba ya Balozi ni ghorofa mbili yenye vyumba kumi,bwawa la kuogelea na uwanja wa mpira wa kikapu katika eneo la bustani na juu kwenye ghorofa ya pili kuna nyumba ndogo ya mpishi yenye chumba, choo, bafu na jiko.

‘Nilikuwa nikiishi katika nyumba hiyo ndogo ya mpishi kwenye ghorofa ya pili ambayo inajitegemea, mama balozi alinikataza kulala kwenye chumba kwa maelezo kuwa kitatumika na wageni wake wakija hivyo nilale jikoni na mwenzangu Rua alikuwa akikaa katika moja ya vyumba vya chini ' alisema.

Bhoke ambaye hivi sasa anaishi katika mji wa Doncaster alisema hawakuwa wakiruhusiwa kumiliki simu wala kugusa simu za nyumba hiyo na hawakuwa na ruhusa ya kuonana na mtu yeyote.

‘Nilipouliza Ni Kwa nini tunafanyiwa hivyo jibu lilitoka kwa mke wa Balozi kuwa hayo ndiyo masharti ya nyumba yake asiyeweza mlango upo wazi, kwani wapo wafilipino kibao wanatafuta kazi za ndani' Raia wa Philines ni maarufu mjini hapa kwa kufanya kazi za ndani kutokana na kuwepo makampuni kadhaa yanayofanya biashara ya kuwaingiza kwa kazi hizo.

Inaaminika kuwa watumishi wa ndani wa Balozi Kibelloh ni wafilipino.

‘Wiki mbili baada ya kuanza kazi, mke wa balozi alituambia anahitaji passport zetu kwa vile balozi anazihitaji kwa ajili ya kushughulikia work permit, wakati tayari tulikuwa nazo kwenye visa zetu tulizopata Dar, hata hivyo kwa kutojua taratibu tulimpa'

‘Tulimuuliza mama Balozi kwa nini tumeanza kazi bila contract alitujibu ‘mna haraka gain kwani hamli? Kipindi chote hicho ukumbuke ndugu mwandishi tulikuwa hatujalipwa na wala hatujui malipo yetu yatakuwa ni kiasi gani kwa wiki'

‘Baada ya wiki moja tena kufika Mama Balozi alituita na kutuambia kuwa tunahitajika kuchangia malipo ya gas,nyumba,umeme na maji kwa hiyo tutakapoanza kulipwa mshahara na yeye tumlipe kiasi, tulishindwa kubisha kwani tulikuwa hatuna contract (mkataba).'

Bhoke alieleza kuwa baada ya mwezi mmoja na nusu, walifika maofisa wawili wa ubalozi, mkuu wa utawala, Bwana Rajab Gamaha (sasa Balozi wa Tanzania nchini Uganda) na Bwana Kiondo walifika kuwaletea mishahara yao na mkataba wao wa ajira. Walisema tusaini na kuandika tarehe ya nyuma kwa maelezo kuwa tarehe inabidi kuwa ya siku waliyoanza kazi.

‘Wakati maofisa hao wanakuja tayari tulikuwa tumefanya kazi wiki sita lakini tulilipwa mshahara wa wiki mbili tu.'alisema Bhoke.

Katika mkataba huo ambao mwandishi wa habari hizi amepata nakala yake unatanguliwa na barua yenye kumbukumbu namba TZL/P.213 iliyoandikwa tarehe 3 julai 2002 inaeleza kuwa wamepewa ajira ya miaka miwili toka tarehe 4 julai 2002 mpaka tarehe 3 julai 2004 na inaeleza kuwa watalipwa kiasi cha paundi 180 kwa wiki na malipo ya paundi 50 kwa wiki za kazi ya ziada na hivyo kufanya malipo yake kuwa 230 kwa wiki.

Aidha katika barua iliyomambatana na mkataba huo Bhoke alitakiwa kujitegemea kwa chakula na gharama zake binafsi kam vile chakula, nguo na matibabu na gharama za nyumba anayoishi za maji,umeme na gesi zingelipiwa na ubalozi.



Mzee ES haya lete ushahidi kama ninavyokupa uthibitisho wa hoja zangu.
 
Balozi wetu Kibello wa UK,

Tulisikia kilo cha watu wengi ni mshenzi sana kwanza wengine mpaka sasa hatumuelewi Jk kumhamishi huyo balozi huko Paris. Amempa ulaji badala ya kumrudisha nyumbani.


Kibello amewahi kuikimbia hadi kamati ya bunge!!!

ninadhani la kibello ingelikuwa wanapigiwa kura tu za maoni zingelitosha kumuondoa. Sidhani kweli wote hao walihongwa kumchafua!

mengine mimi simo ila Kibello kama yanayosemwa ni kweli anapaswa tu kurudishwa nyumbani.

Humu nina imani tunajadili maovu ya watu na si ushabiki labda wengine wanafanya hivyo lakini ushabiki wa vyama na watu tumekemea sana humu.
 
Mzee Tafiti/Kangwale,

Kama nilivyosema, nina move on na next topic siwezi kurudia yale yale kila siku unless kama kuna mapya, lakini nitagusa machache tu,

(1). Kingunge - Waziri mpya wa serikali ya awamu ya nne ana umri gani?

(2). Mahiga - Ni former Director wa Usalama Administration & Acting, Mkapa rais alikwenda kumuomba UN, ambako alikuwa ni Director wa Wakimbizi Europe, sasa kutokana na Mkapa kumuomba kwa Kofi Anaan, ilibidi a-retire kule UN ili kuwa balozi wetu UN, huyu ni moto wa kuotea mbali do not even try! Mahiga mtu ambaye sometimes inabidi alale hotel kwa ajili ya shughuli za Un kuwa nyingi badala ya kwenda nyumbani muda wa kujitangaza bongo ataupata wapi?

No way JK angempa hiyo kazi I mean angefiti vipi na kina Makamba na Kingunge?

(3). Back to Mkapa, eti hajawahi kushinikizwa kuamua asiyoyataka? Bro unakaa nchi gani? sina hata haja ya kuligusa hilo maana hiii forum nzima kila mtu anajua!

Kwa kumaliza, mengine sina mpango maana itakuwa ni boring kwa waanabodi, hiii bodi sio bias hata siku moja,

(a). ina watu wenye upeo mkubwa tena sana na access to critical political informations, kwa hiyo unless una ukweli sio rahisi kuwadanganya,

(b). yale matusi kwenye mchango wako wa kwanza katika hii forum ndio yaliyokupunguzia respect ya vitu vyako ambavyo vilikuwa almost convincing, na kwa sababu watu humu wako experienced na watu waliowahi kutumwa na viongozi kuja kuvuruga humu, ukafiti aina ya wale watu kuwa umetumwa,

(c). Kutumia majina mawili kwa wakati mmoja wakati maneno ni yale yale, haikuwa strategy nzuri katika hii forum, halafu uliposema kuwa mlidhani hizi forum ni za kitoto, hapo ndipo ulipowaudhi karibu watu wote humu hata wanaonichukia,

(d). Hukuwa na Facts, ila ulikuwa una some hadithi ambazo ulijaribu sana kuzifanya ziwe facts, na I am sorry kuwa hazikuhold scrutiny ya hii forum, kwa sababu you have to understand kuwa kuna watu wengi humu ambao they cannot wait siku atakapotokea a hero wa kuni-crash, na most of them thought you were the one kwa hiyo umewa-dissapoint sana "hao watu" na you can see frustrations zao kwenye hizi posting za mwisho mwisho, na utaendelea kuziona

Kwa hiyo sio kweli kuwa humu kuna bias, hapana, isipokuwa RESPECT for trying, na unaonyesha kuwa ni open minded person na willing ku-adjust according to the environment, kwa hiyo ndugu karibu kwa mikono miwili na watu wenye access kama wewe ndio asset ya hii forum, lakini it was agreat debate ambayo ilikuwa ina-miss humu for a while,

Kwa wale ndugu zangu wengine, kuhusu Kibelloh kama nilivyosema mambo yake mengine ya binafsi siwezi kuyatetea,

Salaam kwa wazee wote, tuendelee kuelimisha taifa na kuelimishana!
 
Mimi Mzeesghuli Bwana wakati nakuja kuuliza swali hil nilitegemea wote mnaobishana haa mngalinisaidia kwa kunipa CV ya huyu ndugu . Mzee tafiti unasema kwamba tuna bahati ya kumjua huyu RO kwa kuwa JK ni mchapa kazi na anaendana na matakwa ya watu wanavyo taka una uhakika ?Wakati Mzee Apson anakuja bado tulikuwa tunaingia kwenye uhuru wa kusema lakini bado uhuru ue Mkapa aliukataa na alikuwa mbabe ba hadi sasa anajulikana kwa ubabe .Aliwahi kuomba ushahidi wa rushwa kwenye mkutano wa hadhara pale Singida.Ndiy ubabe huu wa kuilinda rushwa na marafiki zake .

JK kama ni mkweli basi amwambie huyu jamaa yake aweke CV all we need is his CV tuna haki kabisa ya kumjua .Sasa kama kateuliwa kirafiki ama kidini sisi tutampima kwa kazi maana hapo tutakuwa na la kusema . Mimi muda wote nimekaa kimya nawasoma .Kuna makundi hapa yanateta interest zao.Umesema umekuwa msomaji tangia huko hadi hapa sawa but what prompted you kuanza kuchangia ? Kama miaka yote hujawahi kujiunga na sasa umejitokeza kwa ajili ya RO tu unataka tuelewe vipi kama na wewe habari zako si maslahi binafsi ?Bado nasema naoma CV na ni wakati sasa wa kumpunguzia Rais madaraka na kaba ya kuwa na watu kama RO ni lazima kujulikana maana ana serve Tanzania .Huko nyuma we never questioned about Apson maana pamoja na kutajwa kwake hakuzua mawazo ya ajabu .Kwanza kubwa kuliko wote watu wanalia na dalili za udini hili nazo ni jambo ambalo linasababisha watu wajiulize . Serikalini kuna seniority vipi kwa nafasi kama hizi hilo hakuna ?

Mimi sina kundi na sihitaji kundi nabaki kuwa Mtanzania na sina Chama cha Siasa ila issue tutazikata mtake msitake .
 
Nashukuru kusikia kama Es amekiri kama huu mjadala uishe.Lakini pia kwa faida tumepata picha ya Es kwenye forum hii jinsi wanavyo mchukulia kama akisemaa yeye ndo mijipoint Facts na akitokea mtu wa kumcrush atakuwa amewadisapoint wengi. Tafiti mchango wako wa mwisho ambao umemvunja nguvu hata Es nimeupenda kama haiwezekani ukiwa unasema fulani hafai kama Cv yake hujaiona..hi tu inamaanisha chuki.maana unavyomjuwa wewe RO ni yule aliyekuja BM USA na akawa anajifutua huku kavaa miwani myeusi jambo ambalo lina maanicha kutomjuwa vyema.RO akiwa kama afisa mwandamizi wa usalama logically hana haja ya ku act hivyo..kama ungesema alikuwa ni bodyguard tungekuelewa yeye ni tu wakuwaambia vijana wake wafanye nini..hivyo kauli zako kama alikwenda USA na Beni na akawa anajifutua mkutanoni kiasi watu wote wakabaini kama yeye ni usalama kutoka London ni matusi.

Naona mada imekwisha vizuri tu baada ya kushindwa kukiri kama je mzee Apson alivypchaguliwa CV yake iliwekwa hadharani?hawa ni secret service kama unavyowaita na miongoni mwa kazi wanazozifanya katika kutumikia jamii ni za hatari huwezi kuanika hadharani kutaja tasks walizowahi kufanya,nk.Ila kwa kuwa teuzi zake huwa zinafanywa na Raisi aliyeaminiwa kupewa ridhaa za wananchi tena kwa rekodi(kishindo) ndo maana tunakuwa na imani naye.

Simvunjii heshima Mzee Mahiga kwa sababu ni sawa na mzee wangu lakini huwezi kumlazimisha JK kwa ma CV ndo lazima amteue.Duh basi kama ni kama alivyotueleza Tafiti kama huyu mzee alifukuzwa usalama baada ya kesi ya uhaini na yeye kuwa shahidi x, hii tosha nikuwa hatufai. Siji kama haya ni majungu au nikweli lakini nitaamini kama si majungu ikiwa yeye mwenyewe hatakuja kukanusha mpaka sasa naamini kama alifukuzwa ua asistant DG miaka hiyo kwa kushindwa kuinusuru serikali na kesi ya kupinduliwa. Na kusuhu usomi wake wa udokta basi baraza la mawaziri wangejaa maprofesa wote wachuo kikuu maana hawa CV zao zinatisha.JK amemuona RO anafaa inatosha kama alivyosema Mkwawa kama hupendi subiri zamu yako uwe Rais na umuweke unayemtaka lakini kelele zako kama hafai ni za bure.

Hongera JK kwa kuchaguliwa kwa Kishindo na RO kuteuliwa kuwa Usalama DG.

Mwisho nasema slogan ni ileile nguvu mpya..........Historia kwisha,kwisha kwissha kabisa,

Mjadala umefungwa rasmi natoa hoja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom