Rapper King Crazy GK aachana na muziki wa Rap ageukia kwenye kuimba(kubana pua)

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
xVanessa-na-GK-1.jpg.pagespeed.ic.DyLzhpY4Sy.jpg

Rapa mkongwe kutoka kundi la East Coast, King Crazy GK ameamua kuingia Studio kwa Alonem ambapo amebadili maudhui ya uimbaji wake kutoka kurap na kufanya muziki wa kuimba huku video akiifanya na muongozaji Donald kutoka Uganda.

Akipiga story ndani ya eNewz, GK amesema kuwa ushindani uliopo sasa kwenye game la muziki ni tofauti na zamani kwani ushindani ulikuwa wa hapa tu nchini, Ila kwa sasa wameongezeka wasanii mbalimbali wanaotoka hata nje ya nchi ya Tanzania.

“Nimeamua kuimba lakini ni kutokana na game la Tanzania kubadilika, zamani tulikuwa tukishindana sisi wa Tanzania kama Juma Nature, AY na wengine lakini kwa sasa muziki wa Bongo ume’change’ na kuingia mpaka wakina Wizkind, so kubadilika muhimu” amesema GK.

Hata hivyo GK amebadilisha kabisa aina ya muziki wake anaouimba akijikita kutengeneza ngoma zenye mahadhi tofauti kabisa na muziki wake wa zamani wa rap huku mwenyewe akisema anaandaa mashambulizi makali ili kupambana na game la sasa.

Source: Eatv
 
Sijui GK ana bundi gani...ameshindwa kurudi kwenye chart kama zamani ingawa kuanzia mwaka 2014 anajitahidi ila waapi

Halafu hivi hana bifu kweli na AY pamoja na FA?

Nadhani ana bifu na " relics " zake tu ambazo hazimtoi!
 
Hatuna Habari nae tena, Habari ya mjini Ni team kibakuli Na team domoz
 
Sijui GK ana bundi gani...ameshindwa kurudi kwenye chart kama zamani ingawa kuanzia mwaka 2014 anajitahidi ila waapi

Halafu hivi hana bifu kweli na AY pamoja na FA?
na alikua njema kabla ya wao
 
Alikua na hali gani ya Ubongo akiongea maneno hayo!!???
 
GK kurap anarap off key (imagine that). Ataimbaje?
Nilidhani nipo peke yangu kwa hili anakuwa na kama kigugumizi flan hivi kiukweli hakuwahi kunivutia pale katika kundi lao walibebwa na AY na FA kuna kipande anaimba sisi upanga kivyetu na wao kivyao yaani gari gari limekwama sasa linasukumwa.
 
Ni bora angeacha mziki kuliko anachoenda kufanya atajishushia hata hadhi kidogo aliyokuwa nayo aisee.
 
Nilidhani nipo peke yangu kwa hili anakuwa na kama kigugumizi flan hivi kiukweli hakuwahi kunivutia pale katika kundi lao walibebwa na AY na FA kuna kipande anaimba sisi upanga kivyetu na wao kivyao yaani gari gari limekwama sasa linasukumwa.
Madogo wa Upanga tunawajua hawa tangu kabla Professor Jay hajaanza ku rap Hard Blasterz.
 
jina ubeba taswira ya Maisha ya Mtu, sasa jina lenyewe (Mfalme kichaa) unategemea huyo mtu atakuwa wa sampuli gani??
 
Back
Top Bottom