Nashangazwa sana na baadhi ya wabunifu wetu wa vazi letu la taifa.wengi wao ubunifu wao ni kwenye rangi za bendera ya taifa. Naona hii sio sawa,mimi ningeshauri tubuni vazi ambalo litakua la kipekee hapa duniani lakini lisilo na rangi za bendera ya tanzania.mfano wenzetu uk, scotland,india,nigeria,saudi arabia n.k. Mavazi yao ya taifa hayana rangi za bendera zao isipokua upekee au utofauti wa mavazi yao na mavazi ya mataifa mengine ni aina ya mitindo ya mavazi hayo.ningeshauri tutafute aina ya mavazi ya asili ya makabila yetu mawili,moja kutoka zanzibar na moja kutoka tanganyika ambayo yalikua yanavaliwa hapa nchini pekee na kuyachanganya kiubunufu, kuyatilia, maboresho na nakshi za kisasa na kulifanya hilo kuwa vazi la kitanzania. Kwa bara mfano,uvaaji wa kimasai ungeweza kuwa mfano mzuri wa ninachofikiria lakini wamasai wapo na nchi jirani hivyo kuondoa upekee ninaoufikiria.rangi za taifa zibakie kwenye vitu vingine.hata hivyo tuzingatie athari za vazi, rangi na muungano wetu.je muungano ukivunjika vazi letu litakua bado linaweza kuendelea kuwepo? Ni mchango na mawazo yangu tu. Naomba kutoa hoja.