Rangi za bendera ni ujumbe, uzalendo au urembo?

Rangi za bendera ni ujumbe, uzalendo au urembo?

kwikwiwkwiiii mshushaji bendera anashangaa ngongingo za akina mama waliovaa kanga tu.

Na unakuta hata kama mama ni ngongingo lakini kiuno huwa kinaenda yaani waswahili sijui huwa wanaendaga course?
 
mimi pamoja na kusoma nilikosoma na zaidi ya nilivyosoma hapa mungu akinijalia zaidi na zaidi sitadharau mambo haya ya kunitambulisha utaifa wangu. na hata mila zisizo na madhara.
na nitawafundisha watoto wangu na nimesha nunua vitabu mbalimbali vinavyoeleza mambo mengi ya nchi yangu. pamoja na speech za mwalimu nyerere kwani naamini zina mafundisho mema kwa wenye kutafakari na kuelewa alichokuwa anamaanisha mzee yule. nitawaachia urithi huo kazi kwao wenyewe.
 
na nimeprint nyimbo zote mashuhuri nimehifadhi, tanzania tanzania, tazama ramani, na mungu ibariki nimeshaona itafika siku huko tuendako kukakosekana aujuae. bora nitunze kabisa kwa ajili ya wanangu
 
mimi pamoja na kusoma nilikosoma na zaidi ya nilivyosoma hapa mungu akinijalia zaidi na zaidi sitadharau mambo haya ya kunitambulisha utaifa wangu. na hata mila zisizo na madhara.
na nitawafundisha watoto wangu na nimesha nunua vitabu mbalimbali vinavyoeleza mambo mengi ya nchi yangu. pamoja na speech za mwalimu nyerere kwani naamini zina mafundisho mema kwa wenye kutafakari na kuelewa alichokuwa anamaanisha mzee yule. nitawaachia urithi huo kazi kwao wenyewe.

Tukipatikana watu kumi wazalendo kila mkoa..elimu ya Uraia haitashuka hasa kwa hawa .com
 
du nimeimagn ule mgandisho wa ngoma Kindi kindi ndi ndii.. huku bendera inashushwa..then mshushaji anasmile

ah nilikua natafuta namna ya kuwasilisha mdundo wa kigoma kile umenifurahisha sana
 
Tuache utani lakini ule ulikuwa uzalendo wa kipekee uko wapi siku hizi?sijui watoto wetu watajifunza nini...so vitabu vya siasa aka civics vitakuwa vimebadilishwa maana swali hilo lilikuwa halikosekani std III ...
hakuna cha uzalendo kaka, maisha yenyewe magumu ntaheshimuje bendera inayopepea juu?
 
Uzalendo nchi hii ni sifuri mkuu. Hata viongozi wa nchi wanavyotudharau utadhani sisi ni vinyesi kabisa. Viongozi kwa matendo yao ndiyo wamesababisha hali ya kuua uzalendo. Binafsi mara ya mwisho kusimama ilikuwa kipindi hicho nasoma A-Level Jite Ute. Naipenda nchi yangu ila nakuwa disappointed sana na mwenendo wa uzalendo wa viongozi wa serikali.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ile bendera ya taifa inarangi nne ambazo zinamaana!ukitaza kwa kina tanzania tumebaki na zile rangi tu lakin vitu vinavyowakiliashwa na zile rangi hatunufaiki navyo!con xababu ya kuheshimu vitambaa vyenye rangi ziczo na maana kwetu
 
Juzi nilipita mahali Bendera ya Taifa inashushwa...sasa mind yangu ikakumbuka haraka miaka ya zamani tulikatisha kituo cha polisi saa kumi na mbili wanashusha Bendera almanusura turushwe vichura kisa hatukusimama imeadiately....cha ajabu hii ya juzi naona hata polisi wenyewe wanaendelea na shughuli zao ndipo nimeamua kuuliza hii sheria imekuwa zilipendwa ama?
kweli kabisa ndugu yangu sio kituo cha polisi pekee sehemu yoyote ile yenye bendera ya taifa ilikuwa ikipulizwa filimbi lazima usimame mpaka ishuke.kunajamaa yangu alishawahi kukutana na zahama ya kurushwa kichura nusu saa na mienyesho mingine kama kujiviringa kwenye vumbi toka kwa askari baada ya kukiuka(1996).

Sasa mimi mwenyewe jana nimepita hapa NSSF Plaza Mwanza mida ya saa 12,ikawa imepulizwa filimbi nikaganda baadae nashangaa mtu ananipita na wengine wanatembea kama kawaida,ujue nilijiona kama mjinga haikuchukua muda ikabidi nitembee na mimi...

Naweza kusema hili jambo lilizama hasa katika uzalendo siku hizi hakuna uzalendo tena mtu haoni haya kumfananisha mnyama na utanzania
 
hakuna cha uzalendo kaka, maisha yenyewe magumu ntaheshimuje bendera inayopepea juu?

makosa si ya bendera mkuu
makosa ni yetu sisi tulio waweka vihio wanaochakachua rasilimali zetu zilizotakiwa kutunufaisha mimi na wewe.
kuheshimu nchi yetu na vile vinavyotutambulisha sisi vitabaki kuwa palepale. tubadili viongozi na kuweka wale watakaotufanya sisi kuheshimu mambo haya.
 
Mkuu, mimi nilikamatwa kwa ajili ya kutembea wakati bendera inashushwa. Ilikuwa ile siku ya mechi kati ya Tanzania na Ivory Cost. Walinikamata pale makao makuu ya Jeshi la Magereza Posta, pembezoni mwa Chuo cha IFM. Walinikomalia ili wanipige Pingu, wakaniuliza maswali mengi sana, umri wangu, elimu yangu, naishi wapi n.k ila niliwaomba msamaha mpaka wakanisamehe.

Ni kweli, pale Magereza HQ ni wafuatiliaji kwa watu wanaotembea wakati bendera ina shushwa.. i let pedestrians beware!
 
ilizikwa na chama kimoja mkuu...sasa hivi ni huria holela tu, hata mawaziri hawajui ni nchi zipi ziliungana kuunda tanzania.
 
Juzi nilipita mahali Bendera ya Taifa inashushwa...sasa mind yangu ikakumbuka haraka miaka ya zamani tulikatisha kituo cha polisi saa kumi na mbili wanashusha Bendera almanusura turushwe vichura kisa hatukusimama imeadiately....cha ajabu hii ya juzi naona hata polisi wenyewe wanaendelea na shughuli zao ndipo nimeamua kuuliza hii sheria imekuwa zilipendwa ama?
katiba imetoa uhuru wa kuabu tupo akina sisi hata kama tutakufa hatupo tayari kuabudu bendera ya serikali za wanadamu
 
Ndugu msomaji husika na kichwa hapo juu.

Tumezoea kuona bendera ya Taifa ikipandishwa asubuhi na kushushwa jioni kila siku. Hivi kuna mantiki gani ya kupandisha na kushusha bendera kila siku?

Je, kupandisha bendera asubuhi kunaimanisha kwamba Taifa na Serikali yake limeamka kutoka usingizini? Je, kushusha bendera kila jioni kunaimanisha SERIKALI inaenda kusinzia?

Ni masuala ambayo huwa najiuliza nashindwa kuelewa.
 
Ni utamaduni tulioletewa na wenyewe. Watemi wetu (tumeambiwa na tumeaminiswa kuwa ni washenzi) walikuwa hawateremshi bendera zao.
 
Kwa kweli huwa nakosaga jibu kwa kitu kama hiki!
Hata isingepepea yote sawa tu!
 
huu uzi ungeenda intelliigence unafaa sana.. hii mambo ni ukoloni tu hamna sababu yoyote zaidi ya ukoloni
 
Back
Top Bottom