Rangi za bendera ni ujumbe, uzalendo au urembo?

Uzalendo umekwisha. Leo hii angalia shule za msingi nyingi ni za binafsi (English Academy) hakuna mchakamchaka, mambo mengi ni ya mataifa ya ulaya tu, unategemea kutakuwa na uzalendo? Yani Tanzania majanga sana.

Nilikuwa namuuliza mtoto mmoja bendera ya Taifa ina rangi ngapi na zina maana gani hajui wala haelewi sasa haya mambo sisi tulianza kufundishwa mapema sana then nyimbo za Tazama Ramani,Tanzania Tanzania ni nyimbo zilizokuw zinaonyesha uzalendo
 
pita karibu na kambi ya FFU ukute wao wana shusha alaf we tembea, uje utu ambie kama hii amri bado ipo au la
 
Mkuu, mimi nilikamatwa kwa ajili ya kutembea wakati bendera inashushwa. Ilikuwa ile siku ya mechi kati ya Tanzania na Ivory Cost. Walinikamata pale makao makuu ya Jeshi la Magereza Posta, pembezoni mwa Chuo cha IFM. Walinikomalia ili wanipige Pingu, wakaniuliza maswali mengi sana, umri wangu, elimu yangu, naishi wapi n.k ila niliwaomba msamaha mpaka wakanisamehe.
 
Nilikuwa namuuliza mtoto mmoja bendera ya Taifa ina rangi ngapi na zina maana gani hajui wala haelewi sasa haya mambo sisi tulianza kufundishwa mapema sana then nyimbo za Tazama Ramani,Tanzania Tanzania ni nyimbo zilizokuw zinaonyesha uzalendo
tena hizi nyimbo nakumbuka tulikuwa tunaziimba assembly ground kama yakuingia madarasani
 
ni janga janga kubwa ukimsikiliza mwalimu katika speech zake anasema kila taifa lina tamaduni zake na lina taratibu zake. taifa lisilo na tamaduni ni vigumu sana kusimama maana tamaduni yoyote ya mwingine huweza kulimeta taifa hili. leo hii unaweza ukaenda miji ya watu au nchi utashangaa wanavyoheshimu mambo sheria taratibu za nchi hizo na wako makini kwelikweli hawaruhusu yoyote mwenyeji wala mgeni kuharibu mambo hayo kwa vizazi vilivyopo na vijavyo. leo hii tunabadilisha majina ya barabara na kuweka majina ya wageni wajao kwa muda na kutoa majina ya waasisi na wenye maaana na historia ya nchi. taifa letu limekosa mwelekeo ni meli iliyotoboka toboka na kuzama.
 
nakumbuka tulikuwa tunakimbia kuuzunguka uwanja wa shule zaidi ya mara tatu tukiimba nyimbo za azimio la arusha, vita vya kagera tukisifu nchi yetu na kuiombea mema, wakati tunaimba tunawataja wazalendo waliopigania nchi yetu kwa namna moja au nyingine, morali na mzuka ukipandishwa na "mchakamchaka chinja " tulipenda kufanya hivyo na tulikuwa wakati huohuo tukijifunza historia na kutambua mambo mbalimbali.

siku hizi ukimkimbiza mtoto mama yake anakuja juu, ukiwakimbiza watoto mchakamchaka wanakununia na kukuona wakuja hii ni tatizo tunajenga taifa lisilojitambua.
 
tunajifanya wakileo mno tunasahau kuwa hao tunaotaka kufanana nao wana tamaduni zao na mila na desturi wanazozithamini na kuzitunza hadi sisi tunazitamani na kuziiga. tuamke tupende vya kwetu ndio wengine watapenda. tutaishia kudandia dandia vitu vya watu hadi lini.
 
ni janga janga kubwa ukimsikiliza mwalimu katika speech zake anasema kila taifa lina tamaduni zake na lina taratibu zake. taifa lisilo na tamaduni ni vigumu sana kusimama maana tamaduni yoyote ya mwingine huweza kulimeta taifa hili. leo hii unaweza ukaenda miji ya watu au nchi utashangaa wanavyoheshimu mambo sheria taratibu za nchi hizo na wako makini kwelikweli hawaruhusu yoyote mwenyeji wala mgeni kuharibu mambo hayo kwa vizazi vilivyopo na vijavyo. leo hii tunabadilisha majina ya barabara na kuweka majina ya wageni wajao kwa muda na kutoa majina ya waasisi na wenye maaana na historia ya nchi. taifa letu limekosa mwelekeo ni meli iliyotoboka toboka na kuzama.

Wapi Kilwa Road,Nyerere Road,Morogoro Road,Bagamoyo Road,
 
nakumbuka tulikuwa tunakimbia kuuzunguka uwanja wa shule zaidi ya mara tatu tukiimba nyimbo za azimio la arusha, vita vya kagera tukisifu nchi yetu na kuiombea mema, wakati tunaimba tunawataja wazalendo waliopigania nchi yetu kwa namna moja au nyingine, morali na mzuka ukipandishwa na "mchakamchaka chinja " tulipenda kufanya hivyo na tulikuwa wakati huohuo tukijifunza historia na kutambua mambo mbalimbali.

siku hizi ukimkimbiza mtoto mama yake anakuja juu, ukiwakimbiza watoto mchakamchaka wanakununia na kukuona wakuja hii ni tatizo tunajenga taifa lisilojitambua.

Au tukisifia Mbuga zetu,ya kwanza ni Serengeti,Ngorongoro manyara na Mikumi ooh Tanzania Oyeeee
 
Wapi Kilwa Road,Nyerere Road,Morogoro Road,Bagamoyo Road,

chezea wewe baraka obama road, mwai kibaki road. utamwambia nini mwano akikuuliza eti kwa nini hii inaitwa hivi ahhh alikuja mgeni toka nchi.... rais akaamuru iitwe hivi.

unaonaje akiuliza kwa nini nyerere road? akianza kumueleza kwa kina na huku akaja akamsoma katika civics au uraia na kila akipita anaona mantiki ya kupewa jina hili kwenye barabara hiyo.

haya nayo yamo.
 
Au tukisifia Mbuga zetu,ya kwanza ni Serengeti,Ngorongoro manyara na Mikumi ooh Tanzania Oyeeee

ilikuwa inaimbwa hivi

mbuga za wanyama tanzania ya kwanza ni serengeti ngorongoro manyara na mikumi ohh tanzania oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Tuache utani lakini ule ulikuwa uzalendo wa kipekee uko wapi siku hizi?sijui watoto wetu watajifunza nini...so vitabu vya siasa aka civics vitakuwa vimebadilishwa maana swali hilo lilikuwa halikosekani std III ...

Mkuu wakati ule unaona fahari kusimama wakati bendera ya taifa inashushwa.. Yaani watu wakisikia filimbi automatically wananchi wanasimama.. Ule ulikuwa ni uzalendo wa kweli..
 
hata town usije ukabugi kutembea wakt wana shusha au pandisha bendera.

town ya wapi mkuu?
kuna siku napita mahali fulani magomeni bendera inashushwa huku mdundiko nao unapita wamama na wadada wako "namwaga radhi mie radhi mieeeeeeeeeeeeeeeee mtaa huuu ananijua nani " kigoma kinaendelea watu hawana habari kabisa. hata mshushaji nae anashangaa mdundiko.
 
town ya wapi mkuu?
kuna siku napita nahali magomeni bendera inashushwa huku mdundiko nao unanipa wamama na wadada wako "namwaga radhi mie radhi mieeeeeeeeeeeeeeeee " kigoma kinaendelea watu watu hawana habari kabisa. hata mshushaji nae anashangaa mdundiko.
du nimeimagn ule mgandisho wa ngoma Kindi kindi ndi ndii.. huku bendera inashushwa..then mshushaji anasmile
 
kwikwiwkwiiii mshushaji bendera anashangaa ngongingo za akina mama waliovaa kanga tu.
 
Back
Top Bottom