Mkristo kufunga mwezi wa Ramadhan haikubaliwi ni mpaka aukubali uislamu kwanza: Uliza swali lolote kuhusu Ramadhan nitakujibu

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
594
1,827
Katika nyumba kama mnaishi na Mkristo hakikisheni mnampatia chakula kama ilivyo desturi, Kama kuna Mkristo ambaye anafunga mwezi wa Ramadhani, jambo la kwanza ni yeye kuukubali na kuingia kwenye Uislamu, kwa sababu kufunga bila kuingia Uislamu hakutamnufaisha.

Kwa hiyo ni muhimu kwake, kwanza kabisa, Kuamini MUNGU mmoja na kumwamini Mtume Muhammad (rehema na amani za Allah ziwe juu yake) na kuingia katika Uislamu.

Iwapo atamwamini Muhammad (rehema na amani za Allah ziwe juu yake) na akaingia katika Uislamu, katika hali hiyo atatakiwa kuswali, kufunga, kutoa zakaah, kuhiji na kadhalika. Kuhusiana na kufunga kwake au kusali wakati angali Mkristo, hilo si sahihi; Swalah yake ni batili, Saumu yake ni batili, na haitamnufaisha, kwa sababu mojawapo ya masharti ya ibada hizi ni kuwa Mwislamu. Iwapo ataswali wakati yeye si Muislamu na akafunga akiwa si Muislamu, basi ibada yake ni batili.

Uliza swali lolote kuhusu Ramadhan: Nitakujibu kwa Comment

Ramadan2013_freecomputerdesktopwallpaper_1920.jpg
 
TUSIKUBALI PASAKA INAJISIWE. HATUTAKI KUFUNGAMANA NA DINI YA KIARABU. HII NI DHARAU KIARABU KUKARIRIWA PASAKA. HATUTAKI PASAKA KUNAJISIWA.
Pasaka ipi unayoiongelea?

Yesu Kristo ndo Pasaka yenyewe, alikubali kubeba makosa yetu na kuuwawa Ili tupate ukombozi wa dhambi, yeye ndiye mwanakondoo aliyechinjwa na akafufuliwa na Mungu Mkuu siku ya tatu na Sasa Yuko mkono wa kuume wa Mungu Mkuu.

Pasaka ya Wakristo ambaye ni Yesu mwenyewe hawezi najisiwa.
 
Wengine wanafunga sio kwa mategemeo ya kupata thwawabu au kumfurahisha Allah

Wapo wanaofunga kwa ajili ya kuweka sawa afya zao.

Na wengine hili ni zoezi endelevu sio la siku 30 kwa mwaka kama wewe unavyofanya, kunakuwa na short break ya muda fulani then zoezi linaendelea mpaka pale mtu anapoona amefikia lengo.
 
Aya sasa na islam now mmefunga kwaresima mbona hamjawa Christian?.

Ramadan imewakuta Christian wakiwa kwenye toba (kufunga) ila hamjasem hii sawa but mkirisitu akitaka kufunga kwa sababu amekuta ramadan basi lazima akubali uislam..!! 😳
Ramadhani ni mwezi wa tisa wa kalenda ya mwandamo wa Kiislamu (Inatokana na mzunguko wa mwezi ambao unaweza kuwa siku 28-30 kwa hivyo inabadilika kila wakati kuhusiana na kalenda ya magharibi), na huchukua siku 29 au 30, kulingana na wakati gani mwezi mpevu mpya unaonekana, au unapaswa kuonekana. Kwa hivyo majira yake ya miezi hubadilika ndio maana imekua mwezi wa 3 kuja wa 4
 
Nina warembo zangu wa 2 waislamu wamefunga ila wananiomba pesa kwa ajili ya manunuzi ya chakula kama futari je pesa anayopokea kwangu ni halali au haramu kwake?
Katika Uislamu, kujamiiana kabla ya ndoa (uasherati), pamoja na kujamiiana nje ya ndoa (uzinzi) ni haramu kabisa na kuchukuliwa kuwa madhambi makubwa ambayo yana madhara makubwa duniani na akhera.

Uislamu unaipa ngono hali ya heshima kwa kuiwekea mipaka kwenye uhusiano wa mume na mke.

Ikiwa unawapa pesa kwa mnasaba wa ngono pesa hiyo ni haramu, lakini ikiwa unawapa kwa mnasaba wa kibinaadamu hakuna tatizo.
 
Oooh religion, such a burden to mankind 😔
Uislamu unafundisha wanadamu wote ni sawa mbele ya Mungu, bila kujali rangi, tabaka au utaifa. Maombi na sala za kila siku yanadhihirisha dhana hii huku Waislamu wa tabaka mbalimbali wakisali bega kwa bega,
 
Katika Uislamu, kujamiiana kabla ya ndoa (uasherati), pamoja na kujamiiana nje ya ndoa (uzinzi) ni haramu kabisa na kuchukuliwa kuwa madhambi makubwa ambayo yana madhara makubwa duniani na akhera. Uislamu unaipa ngono hali ya heshima kwa kuiwekea mipaka kwenye uhusiano wa mume na mke. Ikiwa unawapa pesa kwa mnasaba wa ngono pesa hiyo ni haramu, lakini ikiwa unawapa kwa mnasaba wa kibinaadamu hakuna tatizo.
Wao kwa sasa hivi wamefunga na mimi ni ATM yao ya kudownload pesa kwa ajili ya mahitaji ya chakula sasa nimekuuliza je pesa ninayo toa kwa ni halali na mimi na faidika kwa Mungu kwa kuwahudumia hawa warembo kipindi hiki cha mfungo? achana na masuala ya zinaa na usherati
 
Wengine wanafunga sio kwa mategemeo ya kupata thwawabu au kumfurahisha Allah

Wapo wanaofunga kwa ajili ya kuweka sawa afya zao.

Na wengine hili ni zoezi endelevu sio la siku 30 kwa mwaka kama wewe unavyofanya, kunakuwa na short break ya muda fulani then zoezi linaendelea mpaka pale mtu anapoona amefikia lengo.
Tunazungumza wale Wakristo wanaofunga Ramadhan
 
Wao kwa sasa hivi wamefunga na mimi ni ATM yao ya kudownload pesa kwa ajili ya mahitaji ya chakula sasa nimekuuliza je pesa ninayo toa kwa ni halali na mimi na faidika kwa Mungu kwa kuwahudumia hawa warembo kipindi hiki cha mfungo? achana na masuala ya zinaa na usherati
umewaoa?? kama sio wake zako halali ni haram labda iwe unaitoa kwa kuinuia kama sadaka na wao waate ftar
 
Uislamu ungekuwa chini ya watu wa aina yako usingetufikia huku Tanzania, unaonekana una uwezo mdogo wa kufikiri na umejawa na jazba, hekma na busara umekosa. Mtu wa aina yako huwezi kuwavutia watu katika Uislamu
Mkuu umesoma andiko vizuri lakini
 
Back
Top Bottom