Rais wangu Samia, unataka upate tabu kama Mzee Kikwete?

WhoWeBe

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
2,301
4,243
Aliwakaribisha mpaka ikulu kunywa juisi lakini hawakuacha kumharibia;

1. Serikali ilipowaambia wananchi 'tufanye hivi, wao dakika hiyohiyo walipita na, kwa ubabe mkuu, wakasema 'msifanye hata kidogo'. Watz, wengi wao, ni wasioona mbali, hawakufanya na maendeleo yakadorora.

2. Wafanyakazi, hususani madaktari na wanafunzi, hususani wa vyuoni wakahamasishwa waandamane kila siku, kazi zikawa hazifanyiki, serikali ikatikisika, almanusra ishindwe.

3. Adabu ikatoweka, serikali ikaitwa legelege. Sitosahau 'watoto' wa chuo kikuu cha Dar es Salaam walivyomdhalilisha kikwete kwa kumtupia mawe na kumzomea mbele ya wageni, how furious Museveni was! Sitosahau maandishi makubwa yaliyoandikwa barabarani pale Dar, KIKWETE NCHI IMEKUSHINDA.

JPM, akijifunza kutoka kwa Kikwete, alijua kuwa kwa kucheka na nyani hawa, ni mabuaxpekee ndicho atakachovuna akawakunjia sura, no juice ikulu no kuwachekechekea. NI KAZI TU. Aliyekuwa hampendi JPM ndani ya ccm alishindwa kupitisha taarifa zake huko upinzanini sababu hakukuwa na nafasi ya kubwabwaja.

Matokeo? Kazi zikafanyika kwa raha zake; wasaidizi wakajifanyia kazi zao kwa raha mustarehe bila kulazimika kuzuia maandamano. Of course hofu ilikuwa kwa jpm tu mwenyewe ukitembelewa naye.

Miradi ulioachiwa unaiendeleza vizuri tu, kuna wachache tu wenye matatizo ya kijinsia ndiyo wanajifanya hawaioni, hofu yangu, wak8anza hao kupita mabarabarani humu basi wafanyakazi watalazimika kusubiri masaa kadhaa yapite maandamano yao kabla ya kufika kazini. Hapo delayment iliyosababishwa nao itakugeukia wewe. HAJAFANYA CHOCHOTE!
 
Hakuna kitu kama hicho.

Nadhani una namna ya ajabu ya kufikiri.

Nchi zote zilizoendelea zina ruhusu mawazo mbadala.

Mawazo mbadala yanaongeza uwazi na kukuza tija katika utekelezaji.

Nchi hii ni yetu sote, pamoja na sisi tusio na vyama.

Lazima mawazo ya watu wote yasikilizwe
 
Shida mnataka demokrasia then hamjui kazi ya vyama vya upinzani. Kama lengo ni kuwa na mawazo sawa si vingefutwa kibaki chama kimoja kuliko kuchoma fedha za kodi kwa ruzuku.

Na upinzani wa siasa si ugomvi eti kiasi anayetawala asikae na mpinzani wake wala kunkaribisha kama vile ni jeshi la serikali dhidi ya waasi.

Hizi mentality za watu wakiwa vyama tofauti ni uadui wa hadi kutoana meno sijui mmezitoa wapi.
 
Ficha ujinga wako basi,

Kelele za WAPINZANI wasio na Jeshi, hawana mbunge hata mmoja bungeni, hawatumii hata manati, ni midomo tu,

Yaani watu kama hao watasababisha vp Nchi isitawalike!!!
 
Ndio kusema CHADEMA watakwamisha miradi ya maendeleo inayojengwa sasa? au Magu alikuwa mwizi wa mali za umma aliogopa kushushuliwa
 
Back
Top Bottom