Kama huyaelewi haya, huwezi kumwelewa Rais Samia

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
69
252
Acha kwanza nikukumbushe tulikotoka japo kwa ufupi,

1. Kipindi cha Nyerere:

Ninaikumbuka kauli ya baba wa taifa alipokuwa akikiri kwamba katika awamu Yao Kuna mazuri na mabaya mengi.

Na sote ni mashahidi, (labda kama huijui historia yetu), mfumo wa utawala wa Mwalim ndio kipindi ambacho Wanafunzi walifaidi huduma ya serikali kuwasomesha bure tena wa Kipata elimu ilivyo bora kabisa.

Ndio kipindi ambacho Tanzania ilijenga viwanda vingi vilivyozalisha ajira kwa wazee wetu.

Kama huamini hili kamuulize mzee wako nyumbani(kama bado yupo) atakuthibitishia.

Lakini pamoja na yote mazuri, hicho ndio kipindi ambacho Tanzania iliishi maisha magumu na ya maumivu haitasahaulika.
Ndio Enzi zilizo shuhuda watanzania wenzetu wakiikimbia nchi Yao kwenda kuishi ukimbizini Ulaya kwa sababu za kisiasa.

Ndio Enzi ambazo watanzania walikamata bunduki mkononi kupigana vita ambayo kama hujui athari zake zinaitafuna nchi mpaka leo.

Kipindi cha Mwalimu ndio Enzi ambazo watu walivaa matairi miguuni huku wakitumia masizi ya mkaa kama dawa ya meno, huku sukari na sabuni vikipatikana kwa foleni.
Tunanshukuru Mwalimu kwa nafasi yake Aliya fanya yake na kwa heshima mpaka leo heshima yake ni kubwa katika taifa hili.

2.kipindi cha Mzee Mwinyi:

Kipindi hiki nilikishuhudia nikiwa na akili zangu timamu.
Wakati nikipitia kitabu cha Mzee WA rukhsa nilikutana na sehemu ya andiko lake lile refu akikiri kuwa na mabaya na udhaifu sehemu nyingi wakati wa uongozi wake.
Ndicho kipindi ambacho kilikuwa neema kwa wafanyabiashara na ikaleta ahueni kwa maisha ya mwananchi wa kawaida. Milango ya kibiashara ilifunguliwa bidhaa nyingi zikapatikana nchini. Uchumi kwa mtu mmoja mmoja ukastawi.
Mambo Mengi yaliyokuwa yamezuiliwa na Mwalim yaliruhusiwa, na ndio ukasikia mzee Mwinyi akaitwa mzee WA RUKHSA.

Vyombo vya habari vikawa huru na watu walitoa maoni yao kila walipohitaji bila hofu, na baadhi walithubutu mpaka kumchora Rais na kumtukana kama ambavyo wachache wanavyofanya hii leo.

Uhuru ukiachwa sana madhara yake wachache wetu huko adabu kwa viongozi wetu.

LAKINI changamoto kwake ikaibuka, ufisadi tukaujua, uchumi wa nchi ukayumba, thamani ya shilingi ikashuka, michango ya huduma za elimu ikaibuka kwa majina tofauti,mfumuko wa bei ikiwemo bidhaa ya mafuta.

Viwanda vyetu vingi vilikata kauli kipindi hiki,ajira ikawa tatizo.

Watu wakapiga sana kelele wanaumizwa na hali ya mambo, Rais akasemwa sana kwamba ni dhaifu na anashauriwa na mkewe

Binafsi kipindi hiki ndio nilijua maana ya neno migomo mashuleni na makazini. Ndio misemo ya magabacholi na walalahoi iliibuka.

Tunashukuru na yeye alitufungulia Dunia, kila laheri mzee wetu, hakuwa na makuu alisamehe hata aliyethubutu kumnasa kibao hadharani(baada ya urais).

3. Kipindi cha Ben Mkapa:

Ilisemwa kwamba uchumi wa nchi kipindi cha Mwinyi hali ilikuwa mbaya sana, Mkapa yeye akaja kama mrekebishaji wa mambo, kisiasa ningeweza kumuita 'Reconstructor'.

Mkapa aliingia kupitia uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995.

Ili kuweka sawa hali ya mambo yeye alikuwa na njia mbili, moja ni sera ya Ubinafsishaji na ya pili ni kuwekeza nguvu kwenye makusanyo ya Kodi.

Hapa ndipo zikazaliwa kodi za aina mbalimbali ikiwemo hii maarufu ya VAT. (kodi ya ongezeko la thamani). Kodi zikawa nyingi kiasi cha Rais kupewa Jina la bwana Kodi.

Licha pia ya kujielekeza kwa sera ya Ukweli na uwazi lakini kiukweli usiri ulitawala sana, mali nyingi za umma zilibinafsishwa ikiwemo nyumba za NBC chini ya msajili wa Majumba.

Badala ya kurekebisha mambo yakazidi kuwa mabaya, pesa zikawa haipatikani, serikali ikajinasibu kuwa tajiri(kinadharia tu) lakini wananchi wake wakawa na hali mbaya. Deni la taifa likakua zaidi.
Ndio kipindi ambacho nikwambie ndio Upinzani ulikuwa na nguvu kubwa sana kuzidi awamu zilizofuata, Democrasia ikayumba na kushuhudia mtutu ukitumika kuwadhibiti wapigania Democrasia, umwagaji damu wa wazi ukadhihiri. Shuhuda mkuu wa haya ni marehemu mwenyewe kupitia kitabu chake cha "My Life, My purpose".

Lakini pamoja na mabaya machache Ben alijitahidi saaana upande wa miundo mbinu, barabara nyingi zilijengwa na serikali yake na kufanya mtandao uliowezesha sehemu nyingi za nchi kufikika kirahisi. Hili lilisaidia kuuinua uchumi.
Uwanja wa taifa kwa Mkapa Ndiyo fahari kubwa zaidi ya awamu ya Mkapa.

4. Kipindi cha J Kikwete:

Alikuwa Rais kijana aliyebeba matarajio makubwa kwa Wananchi, hasa vijana. Ndio wakati ambao ilishuhudiwa Uhuru wa kidemocrasia.

Hakuwa na hiyana Mkwele wa watu akasikiliza na kuheshimu malalamiko ya wengi, akaanzisha mchakato wa Katiba ikiwemo kuunda bunge la katiba na hatimaye rasimu ya katiba mpya ikapatikana.

Mzee Kikwete yeye aliamini sana ukombozi wa uchumi kupitia kilimo, akaja na sera ya 'kilimo kwanza'. Licha ya nia njema aliyokuwa nayo, hakuisimamia vizuri, ikafeli.

Mikataba Mingi ya Uwekezaji ilisainiwa, ikalalamikiwa sana kuhusishwa na ufisadi. Ikaitwa awamu ya Mikataba.

Ndiyo kipindi ambacho kesi nyingi za ufisadi zilifunguliwa mahakamani. Visa vingi na mikasa ya kifisadi vikawa vikisemwa na kujadiliwa kila leo bungeni na mitaani.
Mahospitalini madawa haya kuwepo, huduma za afya zilizorota. Licha ya changamoto zote katika sekta ya afya lakini nakumbuka mfuko wa Bima ulianzia mikononi kwa Jk.

Japo aliitwa Rais mpenda watu, wengine hawakuipenda tabia ile ya kujichanganya na wananchi wake, wakamsimanga kila leo.

Wakamsema kazidi upole, anachekacheka sana na akina dada wakamuita Rais handsome.
Matajiri wengi waliibuka na walifurahia awamu yake.
Deni la taifa lilikuwa zaidi na shilingi ikazidi kuporomoka japo uchumi wa mtu mmojammoja ulikuwa licha ya mfumuko wa bei kusumbua mara kadhaa ndani ya ile miaka kumi. Rais mwenyewe alikaririwa akikiriwa akikiri kwamba hana uwezo wa kudhibiti bei ya mafuta Duniani ambayo mwisho wa siku Ndiyo huathiri uchumi wote kwa kuchochea kupanda bei ya bidhaa mbalimbali.

Wakati akimaliza awamu yake alisema tumemsema sana kwamba yeye Mpole, Sasa anatuletea Chuma

5. Kipindi cha Magufuli:

Zikaja zama za Chuma Magufuli, hakuna aliyemtarajia lakini ndiye akawa mkuu wa nchi yetu.
-Yeye akawa mkali sana kwa mafisadi ambao walitajwa kutawala awamu ya Kikwete,kiasi ikatafsirika kwamba jamaa anachukia Matajiri.

-Kikawa Chuma kweli tena Chuma cha moto, fedha haikupatikana kwa Wananchi, watu wakalia vyuma vimekaza na yeye akawaambia atakayebaki mjini kwa miezi Sita huyo ni Mwanaume.

-Akaapa na kuahidi kumfanya kila aishie kama Malaika aishi kama shetani, serikali ikawanyang'anya pesa wananchi na kweli wale waliokuwa wakiheshimiwa kwa fedha zao haikuwasaidia na wengi wao wakaishia Jela.
-Nidhamu kwa watumishi wa umma ikaimarika sana, waliogopa kutumbuliwa

-Kwa mara ya kwanza tangu Enzi za Nyerere wananchi wakafaidi huduma ya Elimu bure kutoka msingi mpaka sekondari .

-Uwekezaji kwenye miradi mkubwa, barabara, bwawa la Nyerere na treni ya Umeme.

-Ununuzi wa ndege kuifufua ATCL kwa kutumia fedha taslim tena za kwetu wenyewe.

-japo ilianza tangu awamu ya nne, lakini kiukweli uunganishaji wa umeme kwa wenzetu wa vijijini umekuwa na kasi na mafanikio makubwa sana

-Kuinadi na kuisimamia na kulitetea kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda japo kiuhalisia imeonekana kuwa sera ya kinadharia zaidi na haitekelezeki kwa kuwa hata wawekezaji walishaiogopa serikali yetu.

-Serikali ikajinasibu kushinda ufisadi na kufanikiwa kuingiza nchi katika uchumi wa kati.
Serikali ikajinasibu kwa utajiri na uwezo wa kugharamia miradi yake mikubwa kwa fedha zetu wenyewe. Lakini wenye akili zao wakaguna, mh!

-Democrasia ikafinywa, wapinzani wakaufyata na wakaiogopa Siasa ya Upinzani wengi wakakimbilia upande wa chama tawala wakisema wanaunga mkono juhudi za Rais.

-Vyombo vingi vya habari vikafungiwa kwa madai ya kukiuka kanuni, serikali ikawa kali sana pindi ikikosolewa.
Maisha yakawa magumu hata kuku na wanyama ni mashuhuda.

-Deni la taifa likaongezeka maradufu na kwa haraka kuliko nyakati zote japo tuliambiwa kinyume chake.

-Ndugu zetu wengi wakapotea bila serikali kusema wako wapi mpaka leo hii hakuna mwenye majibu.

-Majaribio ya watu kuuawa kwa sababu zinazohisiwa za kisiasa yakafanyika, na Vyombo vya usalama vikawa bubu, Siasa ikawa chungu.

-Mahusiano ya nchi yetu na majirani yakatetereka.

-Ajira za watanzania wengi serikalini zikapeperuka, watanzania wengi wakalazimishwa kuishi bila ajira.

-Biashara nyingi zikafungwa kwa sababu mbalimbali zilizosababishwa na utawala.

-Wawekezaji wengi wakakimbia nchi na kufunga miradi Yao, nchi ikabaki kiwa.

-Miaka Sita ya awamu watumishi serikalini hawakuwahi kuonja tamu ya kupandishwa mishahara wala madaraja, maisha yakawawia magumu.

-Watoto wasichana waliopata ujauzito shuleni hawakuruhusiwa tena kurudi shule hata baada ya kujifungua, wakawa wa mama wa nyumbani, serikali ikaapa kwamba haiwezi kusomesha wazazi.

-Katiba ikapuuzwa na kuvunja kila leo na watawala wakajinasibu na kujifaharisha kufanya hayo, utawala wa sheria ukapuuzwa, mabavu na ubabe vikatawala.

-Magereza zikafurika mahabusu wasio na dhamana, mahakama ikageuzwa kituo cha kukusanya mapato kutoka kwa kila aliyehitaji kununua Uhuru alionyang'anywa kwa kupewa kesi isiyodhaminika na serikali ilifurahia mwenendo huo.

-Wengi walilia na kusaga meno ilhali wachaaache sana walifaidika wakaishi kifalme kufanya watakayo.

-Siasa za ukanda zikatawala

Ni bahati mbaya sana utawala ule ukaishia njiani.
Kikatiba Ikapatikana awamu ya Sita.

6.Kipindi cha MAMA samia:

Wengi kama walistukizwa na hawakutaka kuamini wala kukubali kwamba Sasa tunaenda kuongoza na Rais mwenye jinsia ya kike, Samia Suluhu Hassan.
Kwa kuwa ni awamu ya mwendelezo wa awamu ya Tano kikatiba, ndio kipindi ambacho tumeshuhudia mengi yakifanyika kurekebisha kasoro nyingi zilizoibuka wakati wa awamu ya tano.

-Nafuu ya maisha ikaonekana kuanzia hotuba yake ya kwanza tu baada ya kuapishwa akiahidi kuwaachia watu wote waliopewa kesi za kubambikiza. Na punde tumeshuhudia utekelezaji wa agizo lake.
Malango ya Magereza yakafunguka watu wakarudi uraiani.

-wasichana wote waliofukuzwa mashuleni kwa sababu ya ujauzito wakaruhusiwa kurudi shule na kuendelea na na masomo, tabasamu la furaha likarudi usoni mwa wasichana.

-account nyingi za wafanyabiashara zilizofungwa Enzi za utawala wa awamu ya tano zikafunguliwa na zama mpya za Urafiki kati ya wafanyabiashara na mamlaka za kikodi ikaanza.
Rais akisisitiza kwamba hataki kodi za dhulma na Biashara nyingi zimerudi katika hali yake ya kawaida.

-wafanyakazi wote waliofukuzwa au kuachishwa kazi kwa sababu za vyeti wakasamehewa na Sasa wamerejeshwa makazini kazi inaendelea .

- wafanyakazi wa umma waliahidiwa kuongezewa mshahara ndani ya mwaka mmoja, na hilo limetekelezwa juzi siku ya kilele cha siku ya wafanyakazi Rais alipotangaza kutekeleza ahadi yake na kukubali ombi la wafanyakazi kuongezewa mshahara.

Kwa mantiki hiyo Waka ujao wa fedha mWezi July itashuhudiwa ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi. Kicheko kwa mfanyakazi

-uhusiano wa kimataifa umerudishwa na kuimarika maradufu.

-Demokrasia imeimarika, Rais ameahidi kurudisha Usawa wa kidemokrasia na kisiasa tena akisisitiza hata kama itamgharimu kisiasa, ni kauli ya kishujaa sana.
Serikali kwa makusudi imeshakutana na viongozi wa vyama vya Siasa kwa nia ya kuweka mazingira mazuri ya kisiasa hali ambayo haikuwepo awamu ya tano.

Hivi Sasa tayari Kuna kikosi kazi kilichoundwa kukusanya maoni ya wadau ya namna bora ya kupata kanuni zitakazosimamia mikutano ya kisiasa kwa wadau wote.

-Ndiyo awamu ambayo imekuwa na ujasiri wa kusema ukweli kwamba ile miradi mkubwa tuliyoambiwa kwamba inaendeshwa kwa fedha zetu si kweli, bali illikopwa pesa kubwa kwa ajili yake na Sasa Ndiyo iliyosababisha deni la taifa kuwa kubwa zaidi ya Trilion sabini.

-ule Mchezo wa watu kutekanatekana ovyo na watu kupoteza bila ya sababu Sasa imedhibitiwa, Amani imerejea kwa Mtanzania.

-Uhuru wa kujieleza umerejea, watu wapo huru kila mmoja kueleza alilonalo. Mama hakuwa na hiyana, alitoa Ruhsa anapokosea akosolewe kwa faida ya kujenga.
Wengine wanatumia nafasi hii kutukana kama ilivyo kuwa kwa mzee Mwinyi. Uhuru unaotumika vibaya.

-Vyombo mbalimbali vya habari vilivyofungiwa vikafunguliwa na Sasa wa naendelea na kazi inaendelea.

-mazuri yote ya awamu ya tano ndani ya mwaka mmoja tu mpaka Sasa tumeshuhudia yakieendelezwa, na ndio maana tu nasema kazi iendelee

Tathmin hii ya awamu ya Sita ni kwa kipindi cha mwaka mmoja tofauti awamu zilizo tangulia.

CHANGAMOTO kubwa iliyoikabili awamu ya Sita ni mfumuko wa bei, jambo ambalo ndani ya mWezi mmoja uliopita imesababisha gharama za maisha maeneo mengine kupanda ghafla hali inayomuumiza mwananchi hasa wa kawaida.
MALALAMIKO yamekuwa mengi sana kwa vile Uhuru umeachwa Sasa wengine ndo wanatumia fursa hiyo kutukana na kujitangaza awamu ya Sita kwa mabaya zaidi kuliko mazuri mengi iliyofanya.

Kuna baadhi ambao aidha kwa Imani zao au Mila zao inawapa shida kuongoza na mwanamama, na ni kwa sababu hii ndo wamekuwa kila leo wakiizungumza vibaya serikali na wengine wakijinasibu kutoielewa

Kulielewa jambo wakati mwingine hutegemea utayari wako na nia thaabit kulielewa, Wengi wanalalamika hawako tayari kuielewa serikali kwa sababu zao binafsi na si vinginevyo.
Tena wengine wanathubutu kumlilia marehemu ambaye pia aliwaliza kila leo, ni unafiki wa kiwango cha juu!
Kulielewa jambo lolote ni lazima uelewe historia ya jambo hilo, ulijua kwamba kila serikali ilikuwa na changamoto zake tena za muda mrefu huwezi kujiachia kulalamika kila leo.
Au inawezekana kwa sababu Sasa hivi hakuna vile vishindo na mayowe ya kutangaza kila lililofanyika. Au tunahitaji vile vipindi vya 'Kishindo cha SSH' na magazeti ya propaganda kila leo?
Serikali imelisikia na kulifanyia kazi kwa haraka sana na kuweka ruzuku ya Tshs. Bilion Mia moja na punde gharama za Mafuta zitashuka.

Kama huzielewi awamu zilizopita na changamoto zao, huwezi kumwelewa Mama Samia.
 
Sijasoma yote ila ni licho jua kipindi chote hicho tume tawaliwa na chama kimoja cha kijani......na mama hata apewe miaka 20 hawezi kufanya maajabu as long as CCM ndo ina tawala, na mwenye kulaumiwa zaidi ni mwl Nyerere sio mgine katufikisha hapa tulipo, af bado mambo kumshinda kanyatuka kujifanya mgwana sana
 
Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
Kwanini unatumia nguvu nyingi kiasi hiki kupalilia mbigiri?
 
Sijasoma yote ila ni licho jua kipindi chote hicho tume tawaliwa na chama kimoja cha kijani......na mama hata apewe miaka 20 hawezi kufanya maajabu as long as CCM ndo ina tawala, na mwenye kulaumiwa zaidi ni mwl Nyerere sio mgine katufikisha hapa tulipo, af bado mambo kumshinda kanyatuka kujifanya mgwana sana
Hata apewe miaka 100 hakuna jipya
 
Uzi mzuri umeandika na umefungua mengi kuhusu awamu mablimbali ila ujue nini nguvu uliyotumia kusema both mabaya na mazuri ya awamu zote Tano za nyuma ungetumia pia nguvu hiohio kusemea mabaya na mazuri ya awamu hii wewe ulipofika katika awamu ya 6 umesema mazuri mengiii mabaya machache.

Ndio maana munaitwa MACHAWA uzi huu ungeuandika katika nadharia ya kufanya evaluation halaf ukauacha. Wasomaji tungefanya sisi wenyewe hio evaluation.

Leo unasema Rais amefanya makubwa katika uhusiano wa kimataifa wewe hapo ukikaa bila kutembeleana na Jirani yako ila munasalimiana vizuri tu utapata Shida kwenye maisha yako?

Huyu Rais anasafiri uchwao kwa kodi za watanzania ila kule vyuoni watoto wamekosa mikopo hujui?

Hela zimeletwa hizo za Uviko-19 lakini umesikia zilivyopigwa hujui?

Shida ya Nishati imerudi nisemee Umeme hujui?

Rais kateua watu walewale ambao kila siku wanasemwa wana madudu kwa akili zako chama chenu CCM only Nape na Makamba ndio warudishwe kua viongozi wengine hawawez kua viongozi?

Gharama za mawasiliano zimepanda hujui?

Rais kakosolewa kidogo kamtimua Spika hujui?

Rais kautangazia ulimwengu Nchini kuna Ugaidi na kituko kamuachia Gaidi na akakutana nae pale Ikulu hujui?
 
Andiko refu bovu.
Wazee walipata elimu bora?
Ilisaidia nchi kitu gani?
hawakupata elimu bora, elimu bora ipo leo mashuleni. Nyerere alikua na degree Biology na English. Msekwa alipewa ukuu wa chuo UDSM akiwa na degree moja ya sheria.
 
Haya mambo labda ni mapya kwako ila wengi wetu tumeshayasikia na mnayarudia kila mara.

What matters most is Samia to get things done.

Akishindwa kudeliver watu watasema.
 
Naungana na wewe mtoa mada... Nina mawazo kama yako.. Binafsi sioni ubaya wa huyu mama japo hawez kuwa perfect ila naamini Watanzania ni watu wamezoea malalamiko tu.. Tulipotoka palikua kuzimu Nchi ilikua inaelekea Zimbabwe Jamani tujifunze kuweka akiba ya maneno
 
hawakupata elimu bora, elimu bora ipo leo mashuleni. Nyerere alikua na degree Biology na English. Msekwa alipewa ukuu wa chuo UDSM akiwa na degree moja ya sheria.
Nyerere hakupata degree alipata dip ya kuswahili na biology ndo akaenda Scotland kufanya masters
 
Acha kwanza nikukumbushe tulikotoka japo kwa ufupi,

1. Kipindi cha Nyerere:

Ninaikumbuka kauli ya baba wa taifa alipokuwa akikiri kwamba katika awamu Yao Kuna mazuri na mabaya mengi.

Na sote ni mashahidi, (labda kama huijui historia yetu), mfumo wa utawala wa Mwalim ndio kipindi ambacho Wanafunzi walifaidi huduma ya serikali kuwasomesha bure tena wa Kipata elimu ilivyo bora kabisa.

Ndio kipindi ambacho Tanzania ilijenga viwanda vingi vilivyozalisha ajira kwa wazee wetu.

Kama huamini hili kamuulize mzee wako nyumbani(kama bado yupo) atakuthibitishia.

Lakini pamoja na yote mazuri, hicho ndio kipindi ambacho Tanzania iliishi maisha magumu na ya maumivu haitasahaulika.
Ndio Enzi zilizo shuhuda watanzania wenzetu wakiikimbia nchi Yao kwenda kuishi ukimbizini Ulaya kwa sababu za kisiasa.

Ndio Enzi ambazo watanzania walikamata bunduki mkononi kupigana vita ambayo kama hujui athari zake zinaitafuna nchi mpaka leo.

Kipindi cha Mwalimu ndio Enzi ambazo watu walivaa matairi miguuni huku wakitumia masizi ya mkaa kama dawa ya meno, huku sukari na sabuni vikipatikana kwa foleni.
Tunanshukuru Mwalimu kwa nafasi yake Aliya fanya yake na kwa heshima mpaka leo heshima yake ni kubwa katika taifa hili.

2.kipindi cha Mzee Mwinyi:

Kipindi hiki nilikishuhudia nikiwa na akili zangu timamu.
Wakati nikipitia kitabu cha Mzee WA rukhsa nilikutana na sehemu ya andiko lake lile refu akikiri kuwa na mabaya na udhaifu sehemu nyingi wakati wa uongozi wake.
Ndicho kipindi ambacho kilikuwa neema kwa wafanyabiashara na ikaleta ahueni kwa maisha ya mwananchi wa kawaida. Milango ya kibiashara ilifunguliwa bidhaa nyingi zikapatikana nchini. Uchumi kwa mtu mmoja mmoja ukastawi.
Mambo Mengi yaliyokuwa yamezuiliwa na Mwalim yaliruhusiwa, na ndio ukasikia mzee Mwinyi akaitwa mzee WA RUKHSA.

Vyombo vya habari vikawa huru na watu walitoa maoni yao kila walipohitaji bila hofu, na baadhi walithubutu mpaka kumchora Rais na kumtukana kama ambavyo wachache wanavyofanya hii leo.

Uhuru ukiachwa sana madhara yake wachache wetu huko adabu kwa viongozi wetu.

LAKINI changamoto kwake ikaibuka, ufisadi tukaujua, uchumi wa nchi ukayumba, thamani ya shilingi ikashuka, michango ya huduma za elimu ikaibuka kwa majina tofauti,mfumuko wa bei ikiwemo bidhaa ya mafuta.

Viwanda vyetu vingi vilikata kauli kipindi hiki,ajira ikawa tatizo.

Watu wakapiga sana kelele wanaumizwa na hali ya mambo, Rais akasemwa sana kwamba ni dhaifu na anashauriwa na mkewe

Binafsi kipindi hiki ndio nilijua maana ya neno migomo mashuleni na makazini. Ndio misemo ya magabacholi na walalahoi iliibuka.

Tunashukuru na yeye alitufungulia Dunia, kila laheri mzee wetu, hakuwa na makuu alisamehe hata aliyethubutu kumnasa kibao hadharani(baada ya urais).

3. Kipindi cha Ben Mkapa:

Ilisemwa kwamba uchumi wa nchi kipindi cha Mwinyi hali ilikuwa mbaya sana, Mkapa yeye akaja kama mrekebishaji wa mambo, kisiasa ningeweza kumuita 'Reconstructor'.

Mkapa aliingia kupitia uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995.

Ili kuweka sawa hali ya mambo yeye alikuwa na njia mbili, moja ni sera ya Ubinafsishaji na ya pili ni kuwekeza nguvu kwenye makusanyo ya Kodi.

Hapa ndipo zikazaliwa kodi za aina mbalimbali ikiwemo hii maarufu ya VAT. (kodi ya ongezeko la thamani). Kodi zikawa nyingi kiasi cha Rais kupewa Jina la bwana Kodi.

Licha pia ya kujielekeza kwa sera ya Ukweli na uwazi lakini kiukweli usiri ulitawala sana, mali nyingi za umma zilibinafsishwa ikiwemo nyumba za NBC chini ya msajili wa Majumba.

Badala ya kurekebisha mambo yakazidi kuwa mabaya, pesa zikawa haipatikani, serikali ikajinasibu kuwa tajiri(kinadharia tu) lakini wananchi wake wakawa na hali mbaya. Deni la taifa likakua zaidi.
Ndio kipindi ambacho nikwambie ndio Upinzani ulikuwa na nguvu kubwa sana kuzidi awamu zilizofuata, Democrasia ikayumba na kushuhudia mtutu ukitumika kuwadhibiti wapigania Democrasia, umwagaji damu wa wazi ukadhihiri. Shuhuda mkuu wa haya ni marehemu mwenyewe kupitia kitabu chake cha "My Life, My purpose".

Lakini pamoja na mabaya machache Ben alijitahidi saaana upande wa miundo mbinu, barabara nyingi zilijengwa na serikali yake na kufanya mtandao uliowezesha sehemu nyingi za nchi kufikika kirahisi. Hili lilisaidia kuuinua uchumi.
Uwanja wa taifa kwa Mkapa Ndiyo fahari kubwa zaidi ya awamu ya Mkapa.

4. Kipindi cha J Kikwete:

Alikuwa Rais kijana aliyebeba matarajio makubwa kwa Wananchi, hasa vijana. Ndio wakati ambao ilishuhudiwa Uhuru wa kidemocrasia.

Hakuwa na hiyana Mkwele wa watu akasikiliza na kuheshimu malalamiko ya wengi, akaanzisha mchakato wa Katiba ikiwemo kuunda bunge la katiba na hatimaye rasimu ya katiba mpya ikapatikana.

Mzee Kikwete yeye aliamini sana ukombozi wa uchumi kupitia kilimo, akaja na sera ya 'kilimo kwanza'. Licha ya nia njema aliyokuwa nayo, hakuisimamia vizuri, ikafeli.

Mikataba Mingi ya Uwekezaji ilisainiwa, ikalalamikiwa sana kuhusishwa na ufisadi. Ikaitwa awamu ya Mikataba.

Ndiyo kipindi ambacho kesi nyingi za ufisadi zilifunguliwa mahakamani. Visa vingi na mikasa ya kifisadi vikawa vikisemwa na kujadiliwa kila leo bungeni na mitaani.
Mahospitalini madawa haya kuwepo, huduma za afya zilizorota. Licha ya changamoto zote katika sekta ya afya lakini nakumbuka mfuko wa Bima ulianzia mikononi kwa Jk.

Japo aliitwa Rais mpenda watu, wengine hawakuipenda tabia ile ya kujichanganya na wananchi wake, wakamsimanga kila leo.

Wakamsema kazidi upole, anachekacheka sana na akina dada wakamuita Rais handsome.
Matajiri wengi waliibuka na walifurahia awamu yake.
Deni la taifa lilikuwa zaidi na shilingi ikazidi kuporomoka japo uchumi wa mtu mmojammoja ulikuwa licha ya mfumuko wa bei kusumbua mara kadhaa ndani ya ile miaka kumi. Rais mwenyewe alikaririwa akikiriwa akikiri kwamba hana uwezo wa kudhibiti bei ya mafuta Duniani ambayo mwisho wa siku Ndiyo huathiri uchumi wote kwa kuchochea kupanda bei ya bidhaa mbalimbali.

Wakati akimaliza awamu yake alisema tumemsema sana kwamba yeye Mpole, Sasa anatuletea Chuma

5. Kipindi cha Magufuli:

Zikaja zama za Chuma Magufuli, hakuna aliyemtarajia lakini ndiye akawa mkuu wa nchi yetu.
-Yeye akawa mkali sana kwa mafisadi ambao walitajwa kutawala awamu ya Kikwete,kiasi ikatafsirika kwamba jamaa anachukia Matajiri.

-Kikawa Chuma kweli tena Chuma cha moto, fedha haikupatikana kwa Wananchi, watu wakalia vyuma vimekaza na yeye akawaambia atakayebaki mjini kwa miezi Sita huyo ni Mwanaume.

-Akaapa na kuahidi kumfanya kila aishie kama Malaika aishi kama shetani, serikali ikawanyang'anya pesa wananchi na kweli wale waliokuwa wakiheshimiwa kwa fedha zao haikuwasaidia na wengi wao wakaishia Jela.
-Nidhamu kwa watumishi wa umma ikaimarika sana, waliogopa kutumbuliwa

-Kwa mara ya kwanza tangu Enzi za Nyerere wananchi wakafaidi huduma ya Elimu bure kutoka msingi mpaka sekondari .

-Uwekezaji kwenye miradi mkubwa, barabara, bwawa la Nyerere na treni ya Umeme.

-Ununuzi wa ndege kuifufua ATCL kwa kutumia fedha taslim tena za kwetu wenyewe.

-japo ilianza tangu awamu ya nne, lakini kiukweli uunganishaji wa umeme kwa wenzetu wa vijijini umekuwa na kasi na mafanikio makubwa sana

-Kuinadi na kuisimamia na kulitetea kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda japo kiuhalisia imeonekana kuwa sera ya kinadharia zaidi na haitekelezeki kwa kuwa hata wawekezaji walishaiogopa serikali yetu.

-Serikali ikajinasibu kushinda ufisadi na kufanikiwa kuingiza nchi katika uchumi wa kati.
Serikali ikajinasibu kwa utajiri na uwezo wa kugharamia miradi yake mikubwa kwa fedha zetu wenyewe. Lakini wenye akili zao wakaguna, mh!

-Democrasia ikafinywa, wapinzani wakaufyata na wakaiogopa Siasa ya Upinzani wengi wakakimbilia upande wa chama tawala wakisema wanaunga mkono juhudi za Rais.

-Vyombo vingi vya habari vikafungiwa kwa madai ya kukiuka kanuni, serikali ikawa kali sana pindi ikikosolewa.
Maisha yakawa magumu hata kuku na wanyama ni mashuhuda.

-Deni la taifa likaongezeka maradufu na kwa haraka kuliko nyakati zote japo tuliambiwa kinyume chake.

-Ndugu zetu wengi wakapotea bila serikali kusema wako wapi mpaka leo hii hakuna mwenye majibu.

-Majaribio ya watu kuuawa kwa sababu zinazohisiwa za kisiasa yakafanyika, na Vyombo vya usalama vikawa bubu, Siasa ikawa chungu.

-Mahusiano ya nchi yetu na majirani yakatetereka.

-Ajira za watanzania wengi serikalini zikapeperuka, watanzania wengi wakalazimishwa kuishi bila ajira.

-Biashara nyingi zikafungwa kwa sababu mbalimbali zilizosababishwa na utawala.

-Wawekezaji wengi wakakimbia nchi na kufunga miradi Yao, nchi ikabaki kiwa.

-Miaka Sita ya awamu watumishi serikalini hawakuwahi kuonja tamu ya kupandishwa mishahara wala madaraja, maisha yakawawia magumu.

-Watoto wasichana waliopata ujauzito shuleni hawakuruhusiwa tena kurudi shule hata baada ya kujifungua, wakawa wa mama wa nyumbani, serikali ikaapa kwamba haiwezi kusomesha wazazi.

-Katiba ikapuuzwa na kuvunja kila leo na watawala wakajinasibu na kujifaharisha kufanya hayo, utawala wa sheria ukapuuzwa, mabavu na ubabe vikatawala.

-Magereza zikafurika mahabusu wasio na dhamana, mahakama ikageuzwa kituo cha kukusanya mapato kutoka kwa kila aliyehitaji kununua Uhuru alionyang'anywa kwa kupewa kesi isiyodhaminika na serikali ilifurahia mwenendo huo.

-Wengi walilia na kusaga meno ilhali wachaaache sana walifaidika wakaishi kifalme kufanya watakayo.

-Siasa za ukanda zikatawala

Ni bahati mbaya sana utawala ule ukaishia njiani.
Kikatiba Ikapatikana awamu ya Sita.

6.Kipindi cha MAMA samia:

Wengi kama walistukizwa na hawakutaka kuamini wala kukubali kwamba Sasa tunaenda kuongoza na Rais mwenye jinsia ya kike, Samia Suluhu Hassan.
Kwa kuwa ni awamu ya mwendelezo wa awamu ya Tano kikatiba, ndio kipindi ambacho tumeshuhudia mengi yakifanyika kurekebisha kasoro nyingi zilizoibuka wakati wa awamu ya tano.

-Nafuu ya maisha ikaonekana kuanzia hotuba yake ya kwanza tu baada ya kuapishwa akiahidi kuwaachia watu wote waliopewa kesi za kubambikiza. Na punde tumeshuhudia utekelezaji wa agizo lake.
Malango ya Magereza yakafunguka watu wakarudi uraiani.

-wasichana wote waliofukuzwa mashuleni kwa sababu ya ujauzito wakaruhusiwa kurudi shule na kuendelea na na masomo, tabasamu la furaha likarudi usoni mwa wasichana.

-account nyingi za wafanyabiashara zilizofungwa Enzi za utawala wa awamu ya tano zikafunguliwa na zama mpya za Urafiki kati ya wafanyabiashara na mamlaka za kikodi ikaanza.
Rais akisisitiza kwamba hataki kodi za dhulma na Biashara nyingi zimerudi katika hali yake ya kawaida.

-wafanyakazi wote waliofukuzwa au kuachishwa kazi kwa sababu za vyeti wakasamehewa na Sasa wamerejeshwa makazini kazi inaendelea .

- wafanyakazi wa umma waliahidiwa kuongezewa mshahara ndani ya mwaka mmoja, na hilo limetekelezwa juzi siku ya kilele cha siku ya wafanyakazi Rais alipotangaza kutekeleza ahadi yake na kukubali ombi la wafanyakazi kuongezewa mshahara.

Kwa mantiki hiyo Waka ujao wa fedha mWezi July itashuhudiwa ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi. Kicheko kwa mfanyakazi

-uhusiano wa kimataifa umerudishwa na kuimarika maradufu.

-Demokrasia imeimarika, Rais ameahidi kurudisha Usawa wa kidemokrasia na kisiasa tena akisisitiza hata kama itamgharimu kisiasa, ni kauli ya kishujaa sana.
Serikali kwa makusudi imeshakutana na viongozi wa vyama vya Siasa kwa nia ya kuweka mazingira mazuri ya kisiasa hali ambayo haikuwepo awamu ya tano.

Hivi Sasa tayari Kuna kikosi kazi kilichoundwa kukusanya maoni ya wadau ya namna bora ya kupata kanuni zitakazosimamia mikutano ya kisiasa kwa wadau wote.

-Ndiyo awamu ambayo imekuwa na ujasiri wa kusema ukweli kwamba ile miradi mkubwa tuliyoambiwa kwamba inaendeshwa kwa fedha zetu si kweli, bali illikopwa pesa kubwa kwa ajili yake na Sasa Ndiyo iliyosababisha deni la taifa kuwa kubwa zaidi ya Trilion sabini.

-ule Mchezo wa watu kutekanatekana ovyo na watu kupoteza bila ya sababu Sasa imedhibitiwa, Amani imerejea kwa Mtanzania.

-Uhuru wa kujieleza umerejea, watu wapo huru kila mmoja kueleza alilonalo. Mama hakuwa na hiyana, alitoa Ruhsa anapokosea akosolewe kwa faida ya kujenga.
Wengine wanatumia nafasi hii kutukana kama ilivyo kuwa kwa mzee Mwinyi. Uhuru unaotumika vibaya.

-Vyombo mbalimbali vya habari vilivyofungiwa vikafunguliwa na Sasa wa naendelea na kazi inaendelea.

-mazuri yote ya awamu ya tano ndani ya mwaka mmoja tu mpaka Sasa tumeshuhudia yakieendelezwa, na ndio maana tu nasema kazi iendelee

Tathmin hii ya awamu ya Sita ni kwa kipindi cha mwaka mmoja tofauti awamu zilizo tangulia.

CHANGAMOTO kubwa iliyoikabili awamu ya Sita ni mfumuko wa bei, jambo ambalo ndani ya mWezi mmoja uliopita imesababisha gharama za maisha maeneo mengine kupanda ghafla hali inayomuumiza mwananchi hasa wa kawaida.
MALALAMIKO yamekuwa mengi sana kwa vile Uhuru umeachwa Sasa wengine ndo wanatumia fursa hiyo kutukana na kujitangaza awamu ya Sita kwa mabaya zaidi kuliko mazuri mengi iliyofanya.

Kuna baadhi ambao aidha kwa Imani zao au Mila zao inawapa shida kuongoza na mwanamama, na ni kwa sababu hii ndo wamekuwa kila leo wakiizungumza vibaya serikali na wengine wakijinasibu kutoielewa

Kulielewa jambo wakati mwingine hutegemea utayari wako na nia thaabit kulielewa, Wengi wanalalamika hawako tayari kuielewa serikali kwa sababu zao binafsi na si vinginevyo.
Tena wengine wanathubutu kumlilia marehemu ambaye pia aliwaliza kila leo, ni unafiki wa kiwango cha juu!
Kulielewa jambo lolote ni lazima uelewe historia ya jambo hilo, ulijua kwamba kila serikali ilikuwa na changamoto zake tena za muda mrefu huwezi kujiachia kulalamika kila leo.
Au inawezekana kwa sababu Sasa hivi hakuna vile vishindo na mayowe ya kutangaza kila lililofanyika. Au tunahitaji vile vipindi vya 'Kishindo cha SSH' na magazeti ya propaganda kila leo?
Serikali imelisikia na kulifanyia kazi kwa haraka sana na kuweka ruzuku ya Tshs. Bilion Mia moja na punde gharama za Mafuta zitashuka.

Kama huzielewi awamu zilizopita na changamoto zao, huwezi kumwelewa Mama Samia.
Nitakusahihisha vitatu tu:
1. Deni la nje halikuoanda wakati wa Mkapa bali yeye ndiye aliyefutiwa madeni kwenye awamu yake na kuufanya Nchi itoke kwenye stutus ya High Indebted Poor Countries (HIPC) na kuanza kukopesheka.

2. Bima ya Afya (NHIF) ilianza mwaka 2003 wakati Benjamin Mkapa ni Rais na siyo wakati wa Kikwette

3. Elimu Bure aliyoianzisha Magufuli siyo sawa na Elimu Bure ya wakati wa Nyerere. Ya Magufuli alifuta ule mchango tu wa Tsh 20,000 ila wakati wa Nyerere hata maskini asiye na kipato angeweza kusomesha mwanaye kuanzia darasa la kwanza hadi University alimradi mtoto anapasi mitihani. Ilikuwa kila kitu kinatewa sa Serikali kuanzia nauli za basi, chakula cha njiani, chakula shuleni, mabweni, madaftari, vitabu, kalamu na boom kwa wanafunzi wa vyuo
 
Umenena.
 
Na zaidi xana, Nyerere alionekana kuonyesha nia njema ktk utawala, hakuwa na nia ovu ilofichika kichwani mwake. Aliweka miiko ktk utawala na kupunguza gap ktk mishahara. Viongozi walifanyiwa uchunguzi kabla ya kupewa vyeo na waTz walimpenda kw dhati, hakukua na mapambio ya kusujudu. Tz ilijulikana kw misimamo yake na raslimali za umma zilitumika kw manufaa ya wote. Sasa hivi kla kiongozi anajitahidi kumshinda mwenzie kwa kuwa na mali nyingi, rushwa, ufisadi, dhulma vimeongezeka. waTz wanalia huduma muhimu hazipatkani ispokua kwao, kifupi hali si shwari kwa mlala hoi. Cku hz kla sent ya fedha inayotoka serikalini ni ya mama na viongozi, wanakiri kwamba, kila wanacho tenda, wametumwa na mama. Huenda ndo sbb ya utenguaji na mateuzi yanofanywa na mama kila kukicha - kwamba, usipotenda aliyokutuma, unatupwa nje, mwngne anaingia ...au?
 
Acha kwanza nikukumbushe tulikotoka japo kwa ufupi,

1. Kipindi cha Nyerere:

Ninaikumbuka kauli ya baba wa taifa alipokuwa akikiri kwamba katika awamu Yao Kuna mazuri na mabaya mengi.

Na sote ni mashahidi, (labda kama huijui historia yetu), mfumo wa utawala wa Mwalim ndio kipindi ambacho Wanafunzi walifaidi huduma ya serikali kuwasomesha bure tena wa Kipata elimu ilivyo bora kabisa.

Ndio kipindi ambacho Tanzania ilijenga viwanda vingi vilivyozalisha ajira kwa wazee wetu.

Kama huamini hili kamuulize mzee wako nyumbani(kama bado yupo) atakuthibitishia.

Lakini pamoja na yote mazuri, hicho ndio kipindi ambacho Tanzania iliishi maisha magumu na ya maumivu haitasahaulika.
Ndio Enzi zilizo shuhuda watanzania wenzetu wakiikimbia nchi Yao kwenda kuishi ukimbizini Ulaya kwa sababu za kisiasa.

Ndio Enzi ambazo watanzania walikamata bunduki mkononi kupigana vita ambayo kama hujui athari zake zinaitafuna nchi mpaka leo.

Kipindi cha Mwalimu ndio Enzi ambazo watu walivaa matairi miguuni huku wakitumia masizi ya mkaa kama dawa ya meno, huku sukari na sabuni vikipatikana kwa foleni.
Tunanshukuru Mwalimu kwa nafasi yake Aliya fanya yake na kwa heshima mpaka leo heshima yake ni kubwa katika taifa hili.

2.kipindi cha Mzee Mwinyi:

Kipindi hiki nilikishuhudia nikiwa na akili zangu timamu.
Wakati nikipitia kitabu cha Mzee WA rukhsa nilikutana na sehemu ya andiko lake lile refu akikiri kuwa na mabaya na udhaifu sehemu nyingi wakati wa uongozi wake.
Ndicho kipindi ambacho kilikuwa neema kwa wafanyabiashara na ikaleta ahueni kwa maisha ya mwananchi wa kawaida. Milango ya kibiashara ilifunguliwa bidhaa nyingi zikapatikana nchini. Uchumi kwa mtu mmoja mmoja ukastawi.
Mambo Mengi yaliyokuwa yamezuiliwa na Mwalim yaliruhusiwa, na ndio ukasikia mzee Mwinyi akaitwa mzee WA RUKHSA.

Vyombo vya habari vikawa huru na watu walitoa maoni yao kila walipohitaji bila hofu, na baadhi walithubutu mpaka kumchora Rais na kumtukana kama ambavyo wachache wanavyofanya hii leo.

Uhuru ukiachwa sana madhara yake wachache wetu huko adabu kwa viongozi wetu.

LAKINI changamoto kwake ikaibuka, ufisadi tukaujua, uchumi wa nchi ukayumba, thamani ya shilingi ikashuka, michango ya huduma za elimu ikaibuka kwa majina tofauti,mfumuko wa bei ikiwemo bidhaa ya mafuta.

Viwanda vyetu vingi vilikata kauli kipindi hiki,ajira ikawa tatizo.

Watu wakapiga sana kelele wanaumizwa na hali ya mambo, Rais akasemwa sana kwamba ni dhaifu na anashauriwa na mkewe

Binafsi kipindi hiki ndio nilijua maana ya neno migomo mashuleni na makazini. Ndio misemo ya magabacholi na walalahoi iliibuka.

Tunashukuru na yeye alitufungulia Dunia, kila laheri mzee wetu, hakuwa na makuu alisamehe hata aliyethubutu kumnasa kibao hadharani(baada ya urais).

3. Kipindi cha Ben Mkapa:

Ilisemwa kwamba uchumi wa nchi kipindi cha Mwinyi hali ilikuwa mbaya sana, Mkapa yeye akaja kama mrekebishaji wa mambo, kisiasa ningeweza kumuita 'Reconstructor'.

Mkapa aliingia kupitia uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995.

Ili kuweka sawa hali ya mambo yeye alikuwa na njia mbili, moja ni sera ya Ubinafsishaji na ya pili ni kuwekeza nguvu kwenye makusanyo ya Kodi.

Hapa ndipo zikazaliwa kodi za aina mbalimbali ikiwemo hii maarufu ya VAT. (kodi ya ongezeko la thamani). Kodi zikawa nyingi kiasi cha Rais kupewa Jina la bwana Kodi.

Licha pia ya kujielekeza kwa sera ya Ukweli na uwazi lakini kiukweli usiri ulitawala sana, mali nyingi za umma zilibinafsishwa ikiwemo nyumba za NBC chini ya msajili wa Majumba.

Badala ya kurekebisha mambo yakazidi kuwa mabaya, pesa zikawa haipatikani, serikali ikajinasibu kuwa tajiri(kinadharia tu) lakini wananchi wake wakawa na hali mbaya. Deni la taifa likakua zaidi.
Ndio kipindi ambacho nikwambie ndio Upinzani ulikuwa na nguvu kubwa sana kuzidi awamu zilizofuata, Democrasia ikayumba na kushuhudia mtutu ukitumika kuwadhibiti wapigania Democrasia, umwagaji damu wa wazi ukadhihiri. Shuhuda mkuu wa haya ni marehemu mwenyewe kupitia kitabu chake cha "My Life, My purpose".

Lakini pamoja na mabaya machache Ben alijitahidi saaana upande wa miundo mbinu, barabara nyingi zilijengwa na serikali yake na kufanya mtandao uliowezesha sehemu nyingi za nchi kufikika kirahisi. Hili lilisaidia kuuinua uchumi.
Uwanja wa taifa kwa Mkapa Ndiyo fahari kubwa zaidi ya awamu ya Mkapa.

4. Kipindi cha J Kikwete:

Alikuwa Rais kijana aliyebeba matarajio makubwa kwa Wananchi, hasa vijana. Ndio wakati ambao ilishuhudiwa Uhuru wa kidemocrasia.

Hakuwa na hiyana Mkwele wa watu akasikiliza na kuheshimu malalamiko ya wengi, akaanzisha mchakato wa Katiba ikiwemo kuunda bunge la katiba na hatimaye rasimu ya katiba mpya ikapatikana.

Mzee Kikwete yeye aliamini sana ukombozi wa uchumi kupitia kilimo, akaja na sera ya 'kilimo kwanza'. Licha ya nia njema aliyokuwa nayo, hakuisimamia vizuri, ikafeli.

Mikataba Mingi ya Uwekezaji ilisainiwa, ikalalamikiwa sana kuhusishwa na ufisadi. Ikaitwa awamu ya Mikataba.

Ndiyo kipindi ambacho kesi nyingi za ufisadi zilifunguliwa mahakamani. Visa vingi na mikasa ya kifisadi vikawa vikisemwa na kujadiliwa kila leo bungeni na mitaani.
Mahospitalini madawa haya kuwepo, huduma za afya zilizorota. Licha ya changamoto zote katika sekta ya afya lakini nakumbuka mfuko wa Bima ulianzia mikononi kwa Jk.

Japo aliitwa Rais mpenda watu, wengine hawakuipenda tabia ile ya kujichanganya na wananchi wake, wakamsimanga kila leo.

Wakamsema kazidi upole, anachekacheka sana na akina dada wakamuita Rais handsome.
Matajiri wengi waliibuka na walifurahia awamu yake.
Deni la taifa lilikuwa zaidi na shilingi ikazidi kuporomoka japo uchumi wa mtu mmojammoja ulikuwa licha ya mfumuko wa bei kusumbua mara kadhaa ndani ya ile miaka kumi. Rais mwenyewe alikaririwa akikiriwa akikiri kwamba hana uwezo wa kudhibiti bei ya mafuta Duniani ambayo mwisho wa siku Ndiyo huathiri uchumi wote kwa kuchochea kupanda bei ya bidhaa mbalimbali.

Wakati akimaliza awamu yake alisema tumemsema sana kwamba yeye Mpole, Sasa anatuletea Chuma

5. Kipindi cha Magufuli:

Zikaja zama za Chuma Magufuli, hakuna aliyemtarajia lakini ndiye akawa mkuu wa nchi yetu.
-Yeye akawa mkali sana kwa mafisadi ambao walitajwa kutawala awamu ya Kikwete,kiasi ikatafsirika kwamba jamaa anachukia Matajiri.

-Kikawa Chuma kweli tena Chuma cha moto, fedha haikupatikana kwa Wananchi, watu wakalia vyuma vimekaza na yeye akawaambia atakayebaki mjini kwa miezi Sita huyo ni Mwanaume.

-Akaapa na kuahidi kumfanya kila aishie kama Malaika aishi kama shetani, serikali ikawanyang'anya pesa wananchi na kweli wale waliokuwa wakiheshimiwa kwa fedha zao haikuwasaidia na wengi wao wakaishia Jela.
-Nidhamu kwa watumishi wa umma ikaimarika sana, waliogopa kutumbuliwa

-Kwa mara ya kwanza tangu Enzi za Nyerere wananchi wakafaidi huduma ya Elimu bure kutoka msingi mpaka sekondari .

-Uwekezaji kwenye miradi mkubwa, barabara, bwawa la Nyerere na treni ya Umeme.

-Ununuzi wa ndege kuifufua ATCL kwa kutumia fedha taslim tena za kwetu wenyewe.

-japo ilianza tangu awamu ya nne, lakini kiukweli uunganishaji wa umeme kwa wenzetu wa vijijini umekuwa na kasi na mafanikio makubwa sana

-Kuinadi na kuisimamia na kulitetea kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda japo kiuhalisia imeonekana kuwa sera ya kinadharia zaidi na haitekelezeki kwa kuwa hata wawekezaji walishaiogopa serikali yetu.

-Serikali ikajinasibu kushinda ufisadi na kufanikiwa kuingiza nchi katika uchumi wa kati.
Serikali ikajinasibu kwa utajiri na uwezo wa kugharamia miradi yake mikubwa kwa fedha zetu wenyewe. Lakini wenye akili zao wakaguna, mh!

-Democrasia ikafinywa, wapinzani wakaufyata na wakaiogopa Siasa ya Upinzani wengi wakakimbilia upande wa chama tawala wakisema wanaunga mkono juhudi za Rais.

-Vyombo vingi vya habari vikafungiwa kwa madai ya kukiuka kanuni, serikali ikawa kali sana pindi ikikosolewa.
Maisha yakawa magumu hata kuku na wanyama ni mashuhuda.

-Deni la taifa likaongezeka maradufu na kwa haraka kuliko nyakati zote japo tuliambiwa kinyume chake.

-Ndugu zetu wengi wakapotea bila serikali kusema wako wapi mpaka leo hii hakuna mwenye majibu.

-Majaribio ya watu kuuawa kwa sababu zinazohisiwa za kisiasa yakafanyika, na Vyombo vya usalama vikawa bubu, Siasa ikawa chungu.

-Mahusiano ya nchi yetu na majirani yakatetereka.

-Ajira za watanzania wengi serikalini zikapeperuka, watanzania wengi wakalazimishwa kuishi bila ajira.

-Biashara nyingi zikafungwa kwa sababu mbalimbali zilizosababishwa na utawala.

-Wawekezaji wengi wakakimbia nchi na kufunga miradi Yao, nchi ikabaki kiwa.

-Miaka Sita ya awamu watumishi serikalini hawakuwahi kuonja tamu ya kupandishwa mishahara wala madaraja, maisha yakawawia magumu.

-Watoto wasichana waliopata ujauzito shuleni hawakuruhusiwa tena kurudi shule hata baada ya kujifungua, wakawa wa mama wa nyumbani, serikali ikaapa kwamba haiwezi kusomesha wazazi.

-Katiba ikapuuzwa na kuvunja kila leo na watawala wakajinasibu na kujifaharisha kufanya hayo, utawala wa sheria ukapuuzwa, mabavu na ubabe vikatawala.

-Magereza zikafurika mahabusu wasio na dhamana, mahakama ikageuzwa kituo cha kukusanya mapato kutoka kwa kila aliyehitaji kununua Uhuru alionyang'anywa kwa kupewa kesi isiyodhaminika na serikali ilifurahia mwenendo huo.

-Wengi walilia na kusaga meno ilhali wachaaache sana walifaidika wakaishi kifalme kufanya watakayo.

-Siasa za ukanda zikatawala

Ni bahati mbaya sana utawala ule ukaishia njiani.
Kikatiba Ikapatikana awamu ya Sita.

6.Kipindi cha MAMA samia:

Wengi kama walistukizwa na hawakutaka kuamini wala kukubali kwamba Sasa tunaenda kuongoza na Rais mwenye jinsia ya kike, Samia Suluhu Hassan.
Kwa kuwa ni awamu ya mwendelezo wa awamu ya Tano kikatiba, ndio kipindi ambacho tumeshuhudia mengi yakifanyika kurekebisha kasoro nyingi zilizoibuka wakati wa awamu ya tano.

-Nafuu ya maisha ikaonekana kuanzia hotuba yake ya kwanza tu baada ya kuapishwa akiahidi kuwaachia watu wote waliopewa kesi za kubambikiza. Na punde tumeshuhudia utekelezaji wa agizo lake.
Malango ya Magereza yakafunguka watu wakarudi uraiani.

-wasichana wote waliofukuzwa mashuleni kwa sababu ya ujauzito wakaruhusiwa kurudi shule na kuendelea na na masomo, tabasamu la furaha likarudi usoni mwa wasichana.

-account nyingi za wafanyabiashara zilizofungwa Enzi za utawala wa awamu ya tano zikafunguliwa na zama mpya za Urafiki kati ya wafanyabiashara na mamlaka za kikodi ikaanza.
Rais akisisitiza kwamba hataki kodi za dhulma na Biashara nyingi zimerudi katika hali yake ya kawaida.

-wafanyakazi wote waliofukuzwa au kuachishwa kazi kwa sababu za vyeti wakasamehewa na Sasa wamerejeshwa makazini kazi inaendelea .

- wafanyakazi wa umma waliahidiwa kuongezewa mshahara ndani ya mwaka mmoja, na hilo limetekelezwa juzi siku ya kilele cha siku ya wafanyakazi Rais alipotangaza kutekeleza ahadi yake na kukubali ombi la wafanyakazi kuongezewa mshahara.

Kwa mantiki hiyo Waka ujao wa fedha mWezi July itashuhudiwa ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi. Kicheko kwa mfanyakazi

-uhusiano wa kimataifa umerudishwa na kuimarika maradufu.

-Demokrasia imeimarika, Rais ameahidi kurudisha Usawa wa kidemokrasia na kisiasa tena akisisitiza hata kama itamgharimu kisiasa, ni kauli ya kishujaa sana.
Serikali kwa makusudi imeshakutana na viongozi wa vyama vya Siasa kwa nia ya kuweka mazingira mazuri ya kisiasa hali ambayo haikuwepo awamu ya tano.

Hivi Sasa tayari Kuna kikosi kazi kilichoundwa kukusanya maoni ya wadau ya namna bora ya kupata kanuni zitakazosimamia mikutano ya kisiasa kwa wadau wote.

-Ndiyo awamu ambayo imekuwa na ujasiri wa kusema ukweli kwamba ile miradi mkubwa tuliyoambiwa kwamba inaendeshwa kwa fedha zetu si kweli, bali illikopwa pesa kubwa kwa ajili yake na Sasa Ndiyo iliyosababisha deni la taifa kuwa kubwa zaidi ya Trilion sabini.

-ule Mchezo wa watu kutekanatekana ovyo na watu kupoteza bila ya sababu Sasa imedhibitiwa, Amani imerejea kwa Mtanzania.

-Uhuru wa kujieleza umerejea, watu wapo huru kila mmoja kueleza alilonalo. Mama hakuwa na hiyana, alitoa Ruhsa anapokosea akosolewe kwa faida ya kujenga.
Wengine wanatumia nafasi hii kutukana kama ilivyo kuwa kwa mzee Mwinyi. Uhuru unaotumika vibaya.

-Vyombo mbalimbali vya habari vilivyofungiwa vikafunguliwa na Sasa wa naendelea na kazi inaendelea.

-mazuri yote ya awamu ya tano ndani ya mwaka mmoja tu mpaka Sasa tumeshuhudia yakieendelezwa, na ndio maana tu nasema kazi iendelee

Tathmin hii ya awamu ya Sita ni kwa kipindi cha mwaka mmoja tofauti awamu zilizo tangulia.

CHANGAMOTO kubwa iliyoikabili awamu ya Sita ni mfumuko wa bei, jambo ambalo ndani ya mWezi mmoja uliopita imesababisha gharama za maisha maeneo mengine kupanda ghafla hali inayomuumiza mwananchi hasa wa kawaida.
MALALAMIKO yamekuwa mengi sana kwa vile Uhuru umeachwa Sasa wengine ndo wanatumia fursa hiyo kutukana na kujitangaza awamu ya Sita kwa mabaya zaidi kuliko mazuri mengi iliyofanya.

Kuna baadhi ambao aidha kwa Imani zao au Mila zao inawapa shida kuongoza na mwanamama, na ni kwa sababu hii ndo wamekuwa kila leo wakiizungumza vibaya serikali na wengine wakijinasibu kutoielewa

Kulielewa jambo wakati mwingine hutegemea utayari wako na nia thaabit kulielewa, Wengi wanalalamika hawako tayari kuielewa serikali kwa sababu zao binafsi na si vinginevyo.
Tena wengine wanathubutu kumlilia marehemu ambaye pia aliwaliza kila leo, ni unafiki wa kiwango cha juu!
Kulielewa jambo lolote ni lazima uelewe historia ya jambo hilo, ulijua kwamba kila serikali ilikuwa na changamoto zake tena za muda mrefu huwezi kujiachia kulalamika kila leo.
Au inawezekana kwa sababu Sasa hivi hakuna vile vishindo na mayowe ya kutangaza kila lililofanyika. Au tunahitaji vile vipindi vya 'Kishindo cha SSH' na magazeti ya propaganda kila leo?
Serikali imelisikia na kulifanyia kazi kwa haraka sana na kuweka ruzuku ya Tshs. Bilion Mia moja na punde gharama za Mafuta zitashuka.

Kama huzielewi awamu zilizopita na changamoto zao, huwezi kumwelewa Mama Samia.
📝🆒🎤🔊👊👍👌👏🤝🙏 🎁💐🗼🎖️🏆🛡️👑
 
Back
Top Bottom