"Rais wa misiba"

"Rais wa misiba"

Watanzania ni wanafiq sana aisee..nakumbuka baadhi ya watu walitoa mfano et BARRACK OBAMA hakwenda kwny msiba wa MICHAEL JACKSON ingawa anajulikana dunia nzima...wakamponda KIKWETE kwenda kumzika mtangazaji wa Radio tanzania(TBC)..RESTITUTA BUKORI..watu walimponda sana KIKWETE aisee..sisi watanzania ni watu wa ajabu..tunabadilika kama vinyonga vile..tuna ndimi mbili..this is too bad!!!
 
  • Thanks
Reactions: nao
You have raised questions which frankly showcased how myopic you are!

By not even mentioning those questions, and showing their fallibility, so it could either be refuted or accepted, you are being blind and pointing an accusing finger at a supposed myopic.
 
Watanzania ni wanafiq sana aisee..nakumbuka baadhi ya watu walitoa mfano et BARRACK OBAMA hakwenda kwny msiba wa MICHAEL JACKSON ingawa anajulikana dunia nzima...wakamponda KIKWETE kwenda kumzika mtangazaji wa Radio tanzania(TBC)..RESTITUTA BUKORI..watu walimponda sana KIKWETE aisee..sisi watanzania ni watu wa ajabu..tunabadilika kama vinyonga vile..tuna ndimi mbili..this is too bad!!!
Inawezekana ukaambiwa unakwenda kasi sana spidi ya 160 km/hr punguza kasi, utaua watu, ukasimamisha kabisa gari, ukalalamikiwa kwamba umesimamisha gari, watu hawatafika wanakoenda.

Inawezekana hapo katikati kuna speed nzuri ambayo haihatarishi watu na pia itawafikisha safari.
 
Haya mambo ya kusema watu wachache.ndo kuchukuliwa kama kauli ya watanzania.sio sahihi.niliwahi kusema kikwete anamzidi magufuli kitu kidogo sana UKARIMU.
Hicho Kikwete alichomzidi Magufuli sio kidogo, UKARIMU unabeba na tabia nyingine nyingi njema . .
Mtu mkarimu ana UPENDO, FADHILA, HURUMA, MPOLE na ana UOGA WA MWENYEZI MUNGU . . !
 
Inawezekana ukaambiwa unakwenda kasi sana spidi ya 160 km/hr punguza kasi, utaua watu, ukasimamisha kabisa gari, ukalalamikiwa kwamba umesimamisha gari, watu hawatafika wanakoenda.

Inawezekana hapo katikati kuna speed nzuri ambayo haihatarishi watu na pia itawafikisha safari.
Logic
 
2020 itafika na uchaguzi watashiriki kama kawaida halafu baadaye watailaumu tume ya uchaguzi kuwa si huru ilhali walikubali kushiriki huku wakijua jinsi tume ilivyo.

Sasa hivi washaanza kuimba eti Tundu Lisu 2020.....

Ila huwasikii wakitilia mkazo tume huru ya uchaguzi sasa hivi. Sasa hivi wanadandia dandia vijitukio tu....mara Bashite...mara Gwajima...mara Kinana [eti sasa wako so concerned na well being ya Kinana....Katibu mkuu wa CCM]...mara sijui Lema kanyimwa kuongea....mara Roma Mkatoliki....ujinga ujinga tu.

2020 watapigwa tena hao.....watch this space.
Nchi inaangamia kwa kuendelea kuikumbatia ccm, wewe unasema "watapigwa hao . . " as if wewe ni mkenya . . !
 
Kuna misiba ambayo rais anaweza kuhudhuria na ile ambayo rais ana-delegate watu wake kama mkuu wa mkoa ama waziri fulani. Msipende kulalama tu kila kukicha, Mh. Magufuli ni rais mwenye akili sana na anajielewa. Hata huyo Kikwete si kwamba alikuwa anakwenda kwenye kila misiba ya watanzania, lahasha. Yeye alikuwa anakwenda kwenye misiba inayomuhusu yeye tu kama majirani zake, rafiki, nduguze. Acheni ujinga wa kumpaka Mh. rais matope wakati hastahili. Hasira za vyeti fake na kutumbuliwa isiwe chanzo cha kuleta ujinga humu JF, mbona sie wenye vyeti sahihi tupo poa tu?
 
Nchi inaangamia kwa kuendelea kuikumbatia ccm, wewe unasema "watapigwa hao . . " as if wewe ni mkenya . . !

Ndio Tatizo letu hilo tuwapo safarini Huko Uhamishoni tunajikuta kama Vile Sisi Sio RAIA wa Tanzania na kule kana kwamba huwa tunakuwa Tumeambatana koo zetu zote.

Ni maneno ya kawaida Kwa aina hiyo ya watu miongoni mwao.
 
Nyani Ngabu uko too defensive kwenye ulichokiandika,

Nah...wala sipo defensive. Hiyo ni figment ya imagination yako tu.

Wewe au yeyote yule akipotosha maneno yangu nitam-check.

It's called setting the record straight.

Otherwise ukiruhusu akili yako Kuwa Huru utaelewa Kuwa Kuna ninapoungana na wewe na Kuna ninapotofautiana nawe.

Ni ama huna uwezo mzuri wa kujieleza na ukaeleweka au una tatizo la kusoma na kuelewa. Ila pia huenda unazo hizo sifa zote. Nitakuonyesha kwa nini hapo chini.....

Unapo refer "Rais wa Misiba" argument's ni kama unahalalisha Kuwa Kwa Kuwa yule alienda sana na akaitwa "wa Misiba" basi ni sahihi huyu kutokwenda.

Unasema 'ni kama nahalalisha' kuwa kwa vile yule alienda sana na akaitwa rais wa misiba basi ni sahihi huyu kutokwenda...

La hasha! That couldn't be farther from what I said let alone what I meant. Nadhani ndo maana nimesema una tatizo la kusoma na kuelewa.

Kwanza unasema 'ni kama nasema' na si nasema. Huna hata uhakika na hicho unachokiona ambacho unadai unapingana nacho.

Mimi nilikuwa naweka katika perspective jinsi binadamu tusivyoridhika na chochote. Ni dhahiri hilo hujalielewa na ndo maana umekuja na habari ya 'ni kama'.

Jambo dogo lililowekwa kwenye perspective na nuance za hapa na pale umeshindwa kuling'amua. That speaks a lot to your ability....intellectual that is.

So let me dumb it down for you! Ni hivi....hapana, sikuwa kama nasema hivyo. Sikuwa nahalalisha chochote hapo bali nilikuwa naweka katika muktadha sawa hoja yangu ya jinsi binadamu tulivyo changamani hususan katika mintarafu ya kuridhika.

Jambo ambalo nimelipinga na nime declare Kuwa Mimi ni miongoni mwa tuliomuita yule "Rais wa Misiba" kutokana na hulka yake iliyopitiliza kushiriki Misiba ya ndani na ya nje iwe mikubwa au midogo jambo ambalo lililigharimu Taifa as you know kwamba akienda yeye huambatana na msururu wa Watu protocol inataka hivyo.

Umepinga jambo ambalo hata halipo kwenye hoja yangu/zangu! Unachekesha

Nilichokubaliana na wewe ni Kuwa ni sahihi kwamba Rais huyu Alipaswa kushiriki Misiba ya Kitaifa iliyotokea Ule Wa Maaskari wetu na Huu wa Watoto wetu kwani Yeye ndiye Mfariji wetu Mkuu.

Nawasilisha.

Hahaaaaa okay.

Ila unachodai kupingana na mimi hakipo. Kama kipo basi kipo kichwani mwako tu.

Hakika kusoma na kuelewa au sawia zaidi kusoma na kutokuelewa ulichokisoma ni janga la taifa.

Mtu kwa mbwembwe zote unadai eti unapingana na mimi ilhali hakuna popote pale unapopingana nami kwa mujibu wa ba/mabandiko yako humu.....al junun funun
 
Magu mtu mmoja safi sana kwenye nafasi aliyo nayo. Kwenye hii nafasi inabidi uwe na ngozi ngumu kama mamba. Kwanza malalamiko mengi ya waTZ huwa hayatoki moyoni. Kutokana na unafiki wetu uliomo kwenye DNA mtu akikwambia unafanya vibaya ujue hapo ndo unafanya vizuri. Akikwambia umepatia ujue hapo umekosea.

Magufuli amekaa serikalini miaka kibao akisoma gemu na namna za waTZ. Na kitu cha kwanza alichohakikisha anakifanya vyema ni kutorudia makosa ya wenzake wa nyuma. Na kosa kubwa kulifanya ukiwa Rais ni kuamini kwamba kuna jambo lolote utakalofanya kwa waTZ likupe shukrani. Magu hilo kajifunza na ndio maana style yake ni "dont listen to their vibes (they dont mean it anyway), just do what you think is right). And boy, it works!
 
Mbona kamtuma Samia ata kwetu tunawatuma wanawake watangulie kwenye misiba
 
Binadamu ni kiumbe changamani sana.

Huo ni ukweli ulio dhahiri ambao wala hauhitaji mtu uwe na 'kipaji maalumu' kuuona.

Hata iweje, binadamu kamwe huwa haridhiki.

Kwa kifupi, ni ndivyo tulivyo!

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu ya yaliyotokea huko Arusha wiki ilopita na kuagwa kwa waliopoteza maisha yao kwenye hiyo ajali mapema leo hii.

Kama ilivyodhaniwa/ ilivyotarajiwa, rais Magufuli hakuwepo kwenye hiyo shughuli.

Hii si mara yake ya kwanza yeye kukosa shughuli kama hii ya leo tangia awe rais.

Watu wengi sana wanamlaumu kwa kukosekana kwake. Kwangu hizo ni lawama halali kabisa.

Naamini ingekuwa ni vyema yeye mwenyewe kuwepo kuliko kutuma mwakilishi.

Sababu za yeye kutokwenda mimi sizijui na wala sitajaribu kuanza kusadiki ni nini kilichomfanya asiende.

Ila pia bado sijasahau kipindi ambapo Jakaya Kikwete alikuwa rais na watu wengi tu [hususan humu JF] walikuwa wakimbeza kuwa eti anapenda sana kwenda misibani kuuza sura kuliko kufanya kazi.

Kuna watu walimbatiza hadi jina kuwa eti ni "rais wa misiba". Na simzushii mtu...bofya hapa usome mwenyewe!

Kikwete alibezwa, akachekwa, akaitwa kila aina ya majina kutokana na kupenda kwake kuhudhuria misiba hata ya watu wa kawaida tu wasio maarufu.

Kuna wengine walidai eti anaweka 'precedent' mbaya na kwamba eti watu watakuwa wanategemea kumwona 'rais' kwenye kila msiba utokeao.

Sasa huyu Ngosha yeye yuko tofauti. Anaonekana si mtu wa kupenda kujichanganya changanya sana na watu.

Misiba mingi tu itatokea katika utawala wake maana huo ndo uhalisia wa maisha. Watu hufa kila siku kwa sababu anuai.

Labda yeye hataki kujenga matarajio kwa watu kuwa kila msiba utokeao na yeye lazima atawepo maana vifo ni vingi mno na ukienda kwenye kifo cha huyu au vifo vya hawa basi kila afapo mtu au wafapo watu, basi na wewe lazima uwepo.

Vyovyote vile, urais ni kazi ngumu sana. Ni kazi ambayo kwa kiasi kikubwa haina shukurani.

Ufanye hili, utalaumiwa na kulaaniwa. Usifanye lile, utalaumiwa na kulaaniwa.

Chochote ufanyacho na chochote usichokifanya, ni lawama na shutuma tu.

Wakati mwingine huwa hata sielewi kwa nini watu huwa wanapenda kuwa marais......
Alijua Lowassa Angehudhuria Alijua Lowassa angeshangiliwa, He can not stand mtu mwingine anapewa sportlight mbele yake. Hiyo ndio sababu akaingia Mitini anajua Alipokonya Urais wa Lowassa, Anajua Lowassa anapendwa na Kuheshimkwa Kuliko yeye, Ndio sababu ya Kuzuia Mikutano Kisa Mtu mmoja tu Lowassa! Magufuli amemkimbia Lowassa Arusha Period!
 
Alijua Lowassa Angehudhuria Alijua Lowassa angeshangiliwa, He can not stand mtu mwingine anapewa sportlight mbele yake. Hiyo ndio sababu akaingia Mitini anajua Alipokonya Urais wa Lowassa, Anajua Lowassa anapendwa na Kuheshimkwa Kuliko yeye, Ndio sababu ya Kuzuia Mikutano Kisa Mtu mmoja tu Lowassa! Magufuli amemkimbia Lowassa Arusha Period!
Unaota wewe! Si bure!
 
Tatizo humu wengi hawajamuelewa mtoa mada kamaanisha ili kufikisha ujumbe wake kuhusu kiti cha Urais.

Pitieni hata mara 3 mtaelewa jamaa anavyomaanisha..
Wala hajamtetea Rais na pia katoa maoni kuhusu msiba huu wa taifa.
 
Tatizo humu wengi hawajamuelewa mtoa mada kamaanisha ili kufikisha ujumbe wake kuhusu kiti cha Urais.

Pitieni hata mara 3 mtaelewa jamaa anavyomaanisha..
Wala hajamtetea Rais na pia katoa maoni kuhusu msiba huu wa taifa.
Thank you a gazillion times my friend!

Kwa aliyenisoma kwa utulivu bila jazba huku akiwa na mtazamo huru atakuwa kanielewa vizuri kabisa.

Bahati mbaya si watu wote wenye uelewa mwepesi.

Ndo walimwengu tulivyo.
 
Back
Top Bottom