"Rais wa misiba"

"Rais wa misiba"

Suo busara kutumia extreme moja kuhalalisha extreme nyingine...
 
Kiongozi lazima awe na ability to delegate tasks.Naunga mkono jinsi serikali ilivyowajibika leo.imefanya vyema
 
Ila jamaa ana roho ngumu sana!! Hili Lazima tulikubali. Kagera hakwenda wakati wa janga, kipindi hiki nacho hajaenda. Watanzania hatujawa na roho ngumu kihivyo!! I think, we made something wrong selecting this guy.
 
Binadamu ni kiumbe changamani sana.

Huo ni ukweli ulio dhahiri ambao wala hauhitaji mtu uwe na 'kipaji maalumu' kuuona.

Hata iweje, binadamu kamwe huwa haridhiki.

Kwa kifupi, ni ndivyo tulivyo!

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu ya yaliyotokea huko Arusha wiki ilopita na kuagwa kwa waliopoteza maisha yao kwenye hiyo ajali mapema leo hii.

Kama ilivyodhaniwa/ ilivyotarajiwa, rais Magufuli hakuwepo kwenye hiyo shughuli.

Hii si mara yake ya kwanza yeye kukosa shughuli kama hii ya leo tangia awe rais.

Watu wengi sana wanamlaumu kwa kukosekana kwake. Kwangu hizo ni lawama halali kabisa.

Naamini ingekuwa ni vyema yeye mwenyewe kuwepo kuliko kutuma mwakilishi.

Sababu za yeye kutokwenda mimi sizijui na wala sitajaribu kuanza kusadiki ni nini kilichomfanya asiende.

Ila pia bado sijasahau kipindi ambapo Jakaya Kikwete alikuwa rais na watu wengi tu [hususan humu JF] walikuwa wakimbeza kuwa eti anapenda sana kwenda misibani kuuza sura kuliko kufanya kazi.

Kuna watu walimbatiza hadi jina kuwa eti ni "rais wa misiba". Na simzushii mtu...bofya hapa usome mwenyewe!

Kikwete alibezwa, akachekwa, akaitwa kila aina ya majina kutokana na kupenda kwake kuhudhuria misiba hata ya watu wa kawaida tu wasio maarufu.

Kuna wengine walidai eti anaweka 'precedent' mbaya na kwamba eti watu watakuwa wanategemea kumwona 'rais' kwenye kila msiba utokeao.

Sasa huyu Ngosha yeye yuko tofauti. Anaonekana si mtu wa kupenda kujichanganya changanya sana na watu.

Misiba mingi tu itatokea katika utawala wake maana huo ndo uhalisia wa maisha. Watu hufa kila siku kwa sababu anuai.

Labda yeye hataki kujenga matarajio kwa watu kuwa kila msiba utokeao na yeye lazima atawepo maana vifo ni vingi mno na ukienda kwenye kifo cha huyu au vifo vya hawa basi kila afapo mtu au wafapo watu, basi na wewe lazima uwepo.

Vyovyote vile, urais ni kazi ngumu sana. Ni kazi ambayo kwa kiasi kikubwa haina shukurani.

Ufanye hili, utalaumiwa na kulaaniwa. Usifanye lile, utalaumiwa na kulaaniwa.

Chochote ufanyacho na chochote usichokifanya, ni lawama na shutuma tu.

Wakati mwingine huwa hata sielewi kwa nini watu huwa wanapenda kuwa marais......
Kuwa rais ni kilele cha mafanikio kwa mwanasiasa yeyote. Ni kazi ambayo unapata mshahara na marupu rupu mazuri sana lakini wewe na familia yako mnakula bure, mavazi bure, ulinzi mkubwa bure, usafiri bure, kulala bure. Yaani unarudi kwenye maisha ya kuwa mtoto mdogo. Wewe kazi yako ni mdomo tu na kuweka sahihi na wakati mwingine kusoma tu ulichoandikiwa. Halafu ukistaafu unaishi kama uko peponi. Huguswi na sheria yoyote kwani katiba inakulinda hata kama ulitoa amri mbovu zilizopelekea watu kuuawa bila kosa. Unaendelea kula na kulindwa kama rais, ulinzi wa uhakika, pension tamu unaendekea kulipwa 80% ya mshahara wa rais aliyepo madarakani wakati umelala zako usingizi nyumbani. Hayo yote mpaka siku utakapojifia na utazikwa kwa heshima zote. Kwanini watu wasigombanie urais tena kwa gharama yoyote hata ikibidi kucheza rafu kama kule visiwani bila haya na dunia nzima inaona
 
Yeah...I suppose.

Ila ni kazi isiyo na shukurani kabisa.
 
Rei Rei.....yaani unajaribu ku rationalize no-show ya Magu??

Huogopi kuitwa mkabila wewe eeeh?

Oh btw, off the top of your head....[no Googling].....what is abatement ab initio? 😛
Hii ishu ya kutokuhudhuria misiba si ya kumlaumu sana Magu.

Hatuwezi kusema kwa kuwa hahudhurii basi anafurahia hiyo misiba. Ana sababu zake ambazo si lazima tuzifahamu.

Na hiyo haimaanishi anachofanya kinafurahisha

Abatement ab initio?...deceased...conviction.. Ngoja kwanza nimalizie hot chocolate yangu hapa nitarudi
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu watanzania viumbe wa ajabu sana lkn pia hiwezi jua kwanini hakufika taasisi ya uaris ni kubwa na inamambo mengi.
Simiyu yetu bila shaka nawe ni Mtanzania, hongera kwa kuwa kiumbe wa ajabu
 
Hii ishu ya kutokuhudhuria misiba si ya kumlaumu sana Magu.

Hatuwezi kusema kwa kuwa hahudhurii basi anafurahia hiyo misiba. Ana sababu zake ambazo si lazima tuzifahamu.

Na hiyo haimaanishi anachofanya kinafurahisha

Abatement ab initio?...deceased...conviction.. Ngoja kwanza nimalizie hot chocolate yangu hapa nitarudi
I hear you!
 
Uzuri wa Rais Magufuli ni mtu ambaye ana misimamo isiyoyumba.

Ni kweli misimamo yake mingine iko kinyume na matarajio ya kisiasa lakini kwa Tanzania ya leo hii misimamo inahitajika sana.

Rais Magufuli amejifunza kwa yaliyotokea kwa Mzee Kikwete wakati akiwa Rais.

Rais Magufuli is the opposite of Rais Kikwete.
Aendelee na misimamo yake isije 2020 akaleta vile clip vyake,
Kwa unyenyekevu kabisa na kwa moyo wa dhati nawaombeani mnichague nitakuwa mtumishi wenu mwema
 
Ila wakuu angeenda inawezekana angetoa hotuba ambayo watu wote wangekimbiana pale msibani,,,,,me me binafsi naona bora mkulu ajaenda tu
 
Uzi wenyewe ulioufanya kama reference kumbe ni wa kipindi karibu na uchaguzi!
Kwani uongo kuwa rais kikwete aliitwa muuza sura? Mpenda camera? Mpenda headlines hata kwenye mambo madogo
 
Kwani uongo kuwa rais kikwete aliitwa muuza sura? Mpenda camera? Mpenda headlines hata kwenye mambo madogo

Nilichokiandika ni ukweli mtupu.

Kikwete alibezwa sana humu ingawa mimi sikuona tatizo la yeye kwenda misibani.

Leo hii huyu Magu analaaniwa kwa kutokwenda misibani.

Ubinadamu ni kazi sana.
 
Sijaelewa kosa la watanzania..
Kikwete alilaumiwa kwa kujali sana kusafiri na misiba ya nje..
au kuibuka kwenye msiba wa ndani wakati alikuwa kama hayupo kwenye
masuala yaliyokuwa gumzo yaliyohitaji kauli yake

Kikwete kupenda misiba na safari hakuhalalishi Magufuli kutokwenda msiba
wowote wa kitaifa..
One's an incident, two's a coincidence, three's a pattern

Kuna akili, maarifa na Busara.
Busara hutawala akili na maarifa kwasababu hutoa mtazamo mpana

Busara inawezesha kutambua wapi iwe incident, wapi coincidence na wapi pattern na inawezekana vipi kutawala vitu hivyo vitatu kama si ku balance

senti moja tu
 
Ndio maana ccm inawazungusha na kuwageuza kama chapati!

2020 itafika na uchaguzi watashiriki kama kawaida halafu baadaye watailaumu tume ya uchaguzi kuwa si huru ilhali walikubali kushiriki huku wakijua jinsi tume ilivyo.

Sasa hivi washaanza kuimba eti Tundu Lisu 2020.....

Ila huwasikii wakitilia mkazo tume huru ya uchaguzi sasa hivi. Sasa hivi wanadandia dandia vijitukio tu....mara Bashite...mara Gwajima...mara Kinana [eti sasa wako so concerned na well being ya Kinana....Katibu mkuu wa CCM]...mara sijui Lema kanyimwa kuongea....mara Roma Mkatoliki....ujinga ujinga tu.

2020 watapigwa tena hao.....watch this space.
 
Duh,umenifanya nikumbuke zile enzi zako Nyani McCain na cupcake wako Kelly1
 
Back
Top Bottom