kalimbwane
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 708
- 697
Usiwe mbinafsi kiasi hiki kijana kuwa na upendo na Jirani zako,ninachokiongea Mimi ni kile ninachokiona na kukisikia,sicho kinachonipata Mimi Bali kina wapata wengine,Mimi na feel maumivu yao kwasababu ni wanadam wenzangu! Mtu mzima aliyebakiza miaka miwili kustaafu amelitumikia taifa hili kwa miaka Yake yote Leo hii anaambiwa ameliibia taifa kwa sababu hana cheti,niambie uchungu anaoupata mzee huyu je atakuwa na upendo kutoka moyoni kwa kiongozi wake?Kijana ni nani?unanijua?fanya kazi wewe ndugu,usipoteze muda kupiga porojo.Rais huyu ndo tuliwahi kimtaka ktk nchi hii.sasa hv mnapiga kelele za nini?ni kweli maisha ni magumu sote tunajua lakini ni lini maisha yaliwahi kua rahisi toka dunia imeumbwa?miaka yote kuko hivi hivi.nyamaza bwana na ufanye kazi
Wana Kagera walipatwa na majanga,kauli ya kwanza kutoka kwa kiongozi wao ni wafanye kazi wajenge miundo mbinu na nyumba zao kwasababu tetemeko halijaletwa na serikali,michango ya kuwasaidia mkaipeleka kwenye ujenzi wa miundombinu ya serikali wao kama wananchi wakaachwa walalie majani ya migomba.
Upendo wa mwanadam huyu kwa kiongozi wake utatoka wapi? Kijana jitahidi kulichukulia hili jambo liwe kama limekupata wewe.
Tumuogope Mungu,unafiki kitu kibaya sana palipo na ukweli ongea ukweli ila iwe ni kweli kutoka moyoni.
Manung'uniko yao ndio ishara ya kukata tamaa na kiongozi wao.