"Rais wa misiba"

"Rais wa misiba"

Watu wakisema hawaoni kwa sababu wamepewa Radio waves badala ya visible light, ukiwapa Gamma Rays unakuwa bado hujatatua tatizo lao.

675px-EM_Spectrum_Properties_edit.svg.png

Mshikaji anasema anapishana na mimi lakini hata sioni tunapopishana.

Ndo mambo ya [1] kusoma kitu bila kuelewa na [2] kusoma jambo bila kuwa na an open mind na badala yake kuongozwa na preconceived notions.

Some folks are really funny.
 
Nyuzi na mabandiko ya Kikwete kuitwa 'rais wa misiba' ni nyingi/ mengi mno humu.

Kwa sisi tuliopo muda mrefu humu na tulio na kumbukumbu nzuri tunayajua hayo.
Nyani Ngabu mimi nakuelewa vema sana mkuu, ID mpya ndio hazikuelewi.
 
Mshikaji anasema anapishana na mimi lakini hata sioni tunapopishana.

Ndo mambo ya [1] kusoma kitu bila kuelewa na [2] kusoma jambo bila kuwa na an open mind na badala yake kuongozwa na preconceived notions.

Some folks are really funny.
Wengine hawajapita kwa ngariba hawa bado si bure.
 
Unajua kila nikifikiria ili jambo na wale wanaotetea Rais kutokuenda kwenye huu msiba nashindwa kuwaelewa. Tunazungumzia watoto thelathini maisha yao yamefupishwa na hii ajali. Rais hajaona umuhimu wa yeye kwenda kuwapa pole hawa wazazi. Hivi ni nini haswa maana ya kuwa kiongozi wa nchi kama hauwezi kushiriki na wananchi wako katika kipindi kama hiki?
 
Hata mimi sielewi kwa nini hakwenda kwenye hiyo hafla ya kuwaaga hao maiti.

Sometimes optics matter...and in this case I think they do matter a lot.

Not everyday as many people die in a single incident like that....
Aisee. Nimesikitika sana baba mwenye nyumba kutokwenda
 
Binadamu ni kiumbe changamani sana.

Huo ni ukweli ulio dhahiri ambao wala hauhitaji mtu uwe na 'kipaji maalumu' kuuona.

Hata iweje, binadamu kamwe huwa haridhiki.

Kwa kifupi, ni ndivyo tulivyo!

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu ya yaliyotokea huko Arusha wiki ilopita na kuagwa kwa waliopoteza maisha yao kwenye hiyo ajali mapema leo hii.

Kama ilivyodhaniwa/ ilivyotarajiwa, rais Magufuli hakuwepo kwenye hiyo shughuli.

Hii si mara yake ya kwanza yeye kukosa shughuli kama hii ya leo tangia awe rais.

Watu wengi sana wanamlaumu kwa kukosekana kwake. Kwangu hizo ni lawama halali kabisa.

Naamini ingekuwa ni vyema yeye mwenyewe kuwepo kuliko kutuma mwakilishi.

Sababu za yeye kutokwenda mimi sizijui na wala sitajaribu kuanza kusadiki ni nini kilichomfanya asiende.

Ila pia bado sijasahau kipindi ambapo Jakaya Kikwete alikuwa rais na watu wengi tu [hususan humu JF] walikuwa wakimbeza kuwa eti anapenda sana kwenda misibani kuuza sura kuliko kufanya kazi.

Kuna watu walimbatiza hadi jina kuwa eti ni "rais wa misiba". Na simzushii mtu...bofya hapa usome mwenyewe!

Kikwete alibezwa, akachekwa, akaitwa kila aina ya majina kutokana na kupenda kwake kuhudhuria misiba hata ya watu wa kawaida tu wasio maarufu.

Kuna wengine walidai eti anaweka 'precedent' mbaya na kwamba eti watu watakuwa wanategemea kumwona 'rais' kwenye kila msiba utokeao.

Sasa huyu Ngosha yeye yuko tofauti. Anaonekana si mtu wa kupenda kujichanganya changanya sana na watu.

Misiba mingi tu itatokea katika utawala wake maana huo ndo uhalisia wa maisha. Watu hufa kila siku kwa sababu anuai.

Labda yeye hataki kujenga matarajio kwa watu kuwa kila msiba utokeao na yeye lazima atawepo maana vifo ni vingi mno na ukienda kwenye kifo cha huyu au vifo vya hawa basi kila afapo mtu au wafapo watu, basi na wewe lazima uwepo.

Vyovyote vile, urais ni kazi ngumu sana. Ni kazi ambayo kwa kiasi kikubwa haina shukurani.

Ufanye hili, utalaumiwa na kulaaniwa. Usifanye lile, utalaumiwa na kulaaniwa.

Chochote ufanyacho na chochote usichokifanya, ni lawama na shutuma tu.

Wakati mwingine huwa hata sielewi kwa nini watu huwa wanapenda kuwa marais......
Yeye anasemaaa...."Ajali, vifo, misiba na matetemeko havijaletwa na serikali yake, na wala yeye hakuchaguliwa kuleta misiba, matetemeko na mengine yanayofanana na hayo"...inawaudhi tukisema ila haina budi kukumbusha alichowahi kutamka yeye mwenyewe kwa mdomo wake huo usio na breki!
 
Japo angehutubia taifa kupitia redio nakutoa siku tatu za maombolezi
 
Ni kweli, jamaa kwenye baadhi ya mambo yupo consistent sana....
Mkuu Nyani Ngabu signature yako inajieleza wazi kabisa, hizi lawama za Mh Raisi kutohudhuria zimeanzia USA, na kwa kuwa wameambiwa basi utaonekana unabisha tu.
 
Unajua kila nikifikiria ili jambo na wale wanaotetea Rais kutokuenda kwenye huu msiba nashindwa kuwaelewa. Tunazungumzia watoto thelathini maisha yao yamefupishwa na hii ajali. Rais hajaona umuhimu wa yeye kwenda kuwapa pole hawa wazazi. Hivi ni nini haswa maana ya kuwa kiongozi wa nchi kama hauwezi kushiriki na wananchi wako katika kipindi kama hiki?
Kitu gani ambacho ni cha kumlazimu sana rais kwenda pale ambacho hawezi kukifanya bilakwenda pale siku hiyo?

Kama serikali imewakilishwa na Makamu wa Rais, kwa nini Rais alazimike kuwepo?

Rais ana uchawi wa kufufua wafu na kutokuwepokwake kumefanya waliofariki wakose kufufuliwa?

Kimsingi, msiba wa raia wanasiasa hawatakiwi kujazana,hawatakiwi kutoa hotuba.

Kwa sababu wakijazana na kutoa hituba, watafanya msiba uwe ni jukwaa la siasa.

Na attention itaondokakwa waliofiwa na waliofariki.
 
Na attention itaondokakwa waliofiwa na waliofariki.[/QUOTE]

Sidhani kama umesoma ulichoandika...
 
Mshikaji anasema anapishana na mimi lakini hata sioni tunapopishana.

Ndo mambo ya [1] kusoma kitu bila kuelewa na [2] kusoma jambo bila kuwa na an open mind na badala yake kuongozwa na preconceived notions.

Some folks are really funny.
Nyani Ngabu uko too defensive kwenye ulichokiandika, Otherwise ukiruhusu akili yako Kuwa Huru utaelewa Kuwa Kuna ninapoungana na wewe na Kuna ninapotofautiana nawe.

Unapo refer "Rais wa Misiba" argument's ni kama unahalalisha Kuwa Kwa Kuwa yule alienda sana na akaitwa "wa Misiba" basi ni sahihi huyu kutokwenda. Jambo ambalo nimelipinga na nime declare Kuwa Mimi ni miongoni mwa tuliomuita yule "Rais wa Misiba" kutokana na hulka yake iliyopitiliza kushiriki Misiba ya ndani na ya nje iwe mikubwa au midogo jambo ambalo lililigharimu Taifa as you know kwamba akienda yeye huambatana na msururu wa Watu protocol inataka hivyo.

Nilichokubaliana na wewe ni Kuwa ni sahihi kwamba Rais huyu Alipaswa kushiriki Misiba ya Kitaifa iliyotokea Ule Wa Maaskari wetu na Huu wa Watoto wetu kwani Yeye ndiye Mfariji wetu Mkuu.

Nawasilisha.
 
Rais ana uchawi wa kufufua wafu na kutokuwepokwake kumefanya waliofariki wakose kufufuliwa?

Kimsingi, msiba wa raia wanasiasa hawatakiwi kujazana,hawatakiwi kutoa hotuba.

Kwa sababu wakijazana na kutoa hituba, watafanya msiba uwe ni jukwaa la siasa.

Na attention itaondokakwa waliofiwa na waliofariki.

Sidhani kama umesoma ulichoandika...[/QUOTE]
Wewe hudhani.

Mimi najua hujajibu maswali niliyouliza.

Kwa ninini muhimu sana rais awepo in person, licha ya kutuma ujumbe mkubwa wa makamu wake?

Rais ana nguvu za kufufua wafu?
 
Kitu gani ambacho ni cha kumlazimu sana rais kwenda pale ambacho hawezi kukifanya bilakwenda pale siku hiyo?

Kama serikali imewakilishwa na Makamu wa Rais, kwa nini Rais alazimike kuwepo?

Rais ana uchawi wa kufufua wafu na kutokuwepokwake kumefanya waliofariki wakose kufufuliwa?

Kimsingi, msiba wa raia wanasiasa hawatakiwi kujazana,hawatakiwi kutoa hotuba.

Kwa sababu wakijazana na kutoa hituba, watafanya msiba uwe ni jukwaa la siasa.

Na attention itaondokakwa waliofiwa na waliofariki.
Al Watan upo vizuri mkuu
 
Sidhani kama umesoma ulichoandika...
Wewe hudhani.

Mimi najua hujajibu maswali niliyouliza.

Kwa ninini muhimu sana rais awepo in person, licha ya kutuma ujumbe mkubwa wa makamu wake?

Rais ana nguvu za kufufua wafu?[/QUOTE]

You have raised questions which frankly showcased how myopic you are!
 
Al Watan upo vizuri mkuu

Kuna mtoto mmoja wa rais Theodore Roosevelt wa Marekani, alikuwa anachukizwa sana na tabia ya baba yake, rais Roosevelt,kuwa kila akienda kwenye msiba, harusi au hata ubatizo wa mtoto, ana hijack shughuli na attention yote inatokakwenye maharusi, wafiwa au mtoto anayebatizwa, inaenda kwa rais.

Shughuli inageuka hotuba ya rais.

Akasema msemo mmoja upo mpaka leo maarufu kwa jina lake.

Alisema.

"My father always wanted to be the corpse at every funeral, the bride at every wedding and the baby at every christening."

Naona wanasiasa wengi wa Tanzania wako kama huyu rais Theodore Roosevelt.
 
Watu ni wa ajabu sana aisee.

Kwa aliyenisoma vizuri ataona kabisa nimesema wazi kuwa naamini ingekuwa ni vyema kama yeye binafsi angeenda kwenye hafla ya kuaga hao maiti.

Lakini mijitu bado inakuja na habari sijui za ukabila...mara sijui za kutaka kuhalalisha matendo ya Magufuli kupitia matendo ya Kikwete...

Oh well...
Jiwe limerushwa gizani, kumbe limekupata mwenyewe . . ?!
 
Back
Top Bottom