"Rais wa misiba"

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
93,478
119,292
Binadamu ni kiumbe changamani sana.

Huo ni ukweli ulio dhahiri ambao wala hauhitaji mtu uwe na 'kipaji maalumu' kuuona.

Hata iweje, binadamu kamwe huwa haridhiki.

Kwa kifupi, ni ndivyo tulivyo!

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu ya yaliyotokea huko Arusha wiki ilopita na kuagwa kwa waliopoteza maisha yao kwenye hiyo ajali mapema leo hii.

Kama ilivyodhaniwa/ ilivyotarajiwa, rais Magufuli hakuwepo kwenye hiyo shughuli.

Hii si mara yake ya kwanza yeye kukosa shughuli kama hii ya leo tangia awe rais.

Watu wengi sana wanamlaumu kwa kukosekana kwake. Kwangu hizo ni lawama halali kabisa.

Naamini ingekuwa ni vyema yeye mwenyewe kuwepo kuliko kutuma mwakilishi.

Sababu za yeye kutokwenda mimi sizijui na wala sitajaribu kuanza kusadiki ni nini kilichomfanya asiende.

Ila pia bado sijasahau kipindi ambapo Jakaya Kikwete alikuwa rais na watu wengi tu [hususan humu JF] walikuwa wakimbeza kuwa eti anapenda sana kwenda misibani kuuza sura kuliko kufanya kazi.

Kuna watu walimbatiza hadi jina kuwa eti ni "rais wa misiba". Na simzushii mtu...bofya hapa usome mwenyewe!

Kikwete alibezwa, akachekwa, akaitwa kila aina ya majina kutokana na kupenda kwake kuhudhuria misiba hata ya watu wa kawaida tu wasio maarufu.

Kuna wengine walidai eti anaweka 'precedent' mbaya na kwamba eti watu watakuwa wanategemea kumwona 'rais' kwenye kila msiba utokeao.

Sasa huyu Ngosha yeye yuko tofauti. Anaonekana si mtu wa kupenda kujichanganya changanya sana na watu.

Misiba mingi tu itatokea katika utawala wake maana huo ndo uhalisia wa maisha. Watu hufa kila siku kwa sababu anuai.

Labda yeye hataki kujenga matarajio kwa watu kuwa kila msiba utokeao na yeye lazima atawepo maana vifo ni vingi mno na ukienda kwenye kifo cha huyu au vifo vya hawa basi kila afapo mtu au wafapo watu, basi na wewe lazima uwepo.

Vyovyote vile, urais ni kazi ngumu sana. Ni kazi ambayo kwa kiasi kikubwa haina shukurani.

Ufanye hili, utalaumiwa na kulaaniwa. Usifanye lile, utalaumiwa na kulaaniwa.

Chochote ufanyacho na chochote usichokifanya, ni lawama na shutuma tu.

Wakati mwingine huwa hata sielewi kwa nini watu huwa wanapenda kuwa marais......
 
Uzi wenyewe ulioufanya kama reference kumbe ni wa kipindi karibu na uchaguzi!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kuwa kiongozi Ni pamoja Na kujitaidi Ku "balance" mambo...... Kuna misiba ya kawaida Na matukio(soma misba) ya "kitaifa"

Btw, bongo ukiwa rais wew ndio Killa kitu, anaweza kubomoa Na kuumba vitu......
Uamuzi Ni wake, wapiga kura pia Ni wake....maana alisema "wasimchagulie" not so long ataomba tena "wamchague" yeye Na "wasimchague" yule.....

What goes around comes around..that's life.
 
406513.jpg
 
Sijaelewa kosa la watanzania..
Kikwete alilaumiwa kwa kujali sana kusafiri na misiba ya nje..
au kuibuka kwenye msiba wa ndani wakati alikuwa kama hayupo kwenye
masuala yaliyokuwa gumzo yaliyohitaji kauli yake

Kikwete kupenda misiba na safari hakuhalalishi Magufuli kutokwenda msiba
wowote wa kitaifa..
 
Uzuri wa Rais Magufuli ni mtu ambaye ana misimamo isiyoyumba.

Ni kweli misimamo yake mingine iko kinyume na matarajio ya kisiasa lakini kwa Tanzania ya leo hii misimamo inahitajika sana.

Rais Magufuli amejifunza kwa yaliyotokea kwa Mzee Kikwete wakati akiwa Rais.

Mpaka pale wakosoaji wake watakapofahamu kuwa Rais Magufuli is the opposite of Rais Kikwete ndipo watakapogundua kuwa wanachokifanya ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
 
Umejaribu kuongea vizuri lakini cha msingi ni kwamba raisi lazima aguswe na matukio yanayochukua maisha ya watu wengi kwa pamoja kama majanga na ajali kubwa kama hii.
Suala kwenda kila msiba nalo ni kituko kama alivyokuwa akifanya mkwere.
Kumbuka hadi Kenya wameguswa na rais alidiriki kutuma wawakilishi lakini Rais wetu hajaguswa kihivyo kiasi cha kutuma uwakilishi wa makamu wa rais.

UFIKE WAKATI rais aonyeshe UPENDO kwa watu wake kwa vitendo.
Tuna rais mwenye roho ngumu zaidi ya mfanyakazi wa mochuari, inaumiza na inasikitisha.
Nyani Ngabu
 
Uzuri wa Rais Magufuli ni mtu ambaye ana misimamo isiyoyumba.

Ni kweli misimamo yake mingine iko kinyume na matarajio ya kisiasa lakini kwa Tanzania ya leo hii misimamo inahitajika sana.

Rais Magufuli amejifunza kwa yaliyotokea kwa Mzee Kikwete wakati akiwa Rais.

Rais Magufuli is the opposite of Rais Kikwete.

Ni kweli, jamaa kwenye baadhi ya mambo yupo consistent sana....
 
Umejaribu kuongea vizuri lakini cha msingi ni kwamba raisi lazima aguswe na matukio yanayochukua maisha ya watu wengi kwa pamoja kama majanga na ajali kubwa kama hii.
Suala kwenda kila msiba nalo ni kituko kama alivyokuwa akifanya mkwere.
Kumbuka hadi Kenya wameguswa na rais alidiriki kutuma wawakilishi lakini Rais wetu hajaguswa kihivyo kiasi cha kutuma uwakilishi wa makamu wa rais.

UFIKE WAKATI rais aonyeshe UPENDO kwa watu wake kwa vitendo.
Tuna rais mwenye roho ngumu zaidi ya mfanyakazi wa mochuari, inaumiza na inasikitisha.
Nyani Ngabu

Mimi nimejaribu kuonyesha tu jinsi ambavyo binadamu haturidhiki hata iweje.

Nina imani kabisa kuwa hata kama leo angeenda kwenye kuwaaga hao maiti bado tu wangekuwepo ambao wangemlaumu....

He is damned if he does and damned if he doesn't....
 
Wabongo bana...mlisema ya Bukoba kwenye tetemeko na mwisho wa siku Rais mkamsikia yupo kule akitoa pole.leo mmeanza tena.kweni hauoni katuma muwakilishi tena makamu wake?na pole yake ameitoa,waTanzania kwa kulalama sijui tukoje
 
Binadamu ni kiumbe changamani sana.

Huo ni ukweli ulio dhahiri ambao wala hauhitaji mtu uwe na 'kipaji maalumu' kuuona.

Hata iweje, binadamu kamwe huwa haridhiki.

Kwa kifupi, ni ndivyo tulivyo!

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu ya yaliyotokea huko Arusha wiki ilopita na kuagwa kwa waliopoteza maisha yao kwenye hiyo ajali mapema leo hii.

Kama ilivyodhaniwa/ ilivyotarajiwa, rais Magufuli hakuwepo kwenye hiyo shughuli.

Hii si mara yake ya kwanza yeye kukosa shughuli kama hii ya leo tangia awe rais.

Watu wengi sana wanamlaumu kwa kukosekana kwake. Kwangu hizo ni lawama halali kabisa.

Naamini ingekuwa ni vyema yeye mwenyewe kuwepo kuliko kutuma mwakilishi.

Sababu za yeye kutokwenda mimi sizijui na wala sitajaribu kuanza kusadiki ni nini kilichomfanya asiende.

Ila pia bado sijasahau kipindi ambapo Jakaya Kikwete alikuwa rais na watu wengi tu [hususan humu JF] walikuwa wakimbeza kuwa eti anapenda sana kwenda misibani kuuza sura kuliko kufanya kazi.

Kuna watu walimbatiza hadi jina kuwa eti ni "rais wa misiba". Na simzushii mtu...bofya hapa usome mwenyewe!

Kikwete alibezwa, akachekwa, akaitwa kila aina ya majina kutokana na kupenda kwake kuhudhuria misiba hata ya watu wa kawaida tu wasio maarufu.

Kuna wengine walidai eti anaweka 'precedent' mbaya na kwamba eti watu watakuwa wanategemea kumwona 'rais' kwenye kila msiba utokeao.

Sasa huyu Ngosha yeye yuko tofauti. Anaonekana si mtu wa kupenda kujichanganya changanya sana na watu.

Misiba mingi tu itatokea katika utawala wake maana huo ndo uhalisia wa maisha. Watu hufa kila siku kwa sababu anuai.

Labda yeye hataki kujenga matarajio kwa watu kuwa kila msiba utokeao na yeye lazima atawepo maana vifo ni vingi mno na ukienda kwenye kifo cha huyu au vifo vya hawa basi kila afapo mtu au wafapo watu, basi na wewe lazima uwepo.

Vyovyote vile, urais ni kazi ngumu sana. Ni kazi ambayo kwa kiasi kikubwa haina shukurani.

Ufanye hili, utalaumiwa na kulaaniwa. Usifanye lile, utalaumiwa na kulaaniwa.

Chochote ufanyacho na chochote usichokifanya, ni lawama na shutuma tu.

Wakati mwingine huwa hata sielewi kwa nini watu huwa wanapenda kuwa marais......
Tupe orodha kwa asilimia ya wale waliombeza JK na wale waliomsifia wakati akihudhuria misiba kipindi chake cha urais.
 
Back
Top Bottom