Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,596
Sasa rais hatakikusikia habari mbaya, kashasema hilo.Ona sasa...mwingine huyu kimsingi anasema haoni ubaya wa Magufuli kutokwenda la kama angekuwa na uwezo wa kufufua watu.
Kwake cha muhimu zaidi ni kuangalia namna ya kuepusha ajali kama hiyo iliyotokea....
Lakini si ajabu nawe ukaitwa mkabila.....
Mnataka kumlazimisha?
Kama hamumtaki rais wa hivyo mtoeni.
Rais mwenyewe msema ovyo, si ajabu akaja msibani na kusema maneno ya ovyo na kuzua mjadala hasi.
Sijaona Magufuli kwa roho yake ya korosho angefanya nini cha ziada kwenye msiba huo.
Ndiyo maana nikasema labda kama angekuwa ana uwezo wa kufufua watu ningeona ana umuhimuwa kuwepo.
Zaidi ni kuingiza siasa katika msiba tu. Tushaona kina Lema wanazozana na uongoziwa CCM kuweka siasa katika msiba.
Mimi mtu atakayeihoji serikali ya Magufuli inafanya nini kuhakikisha ajali hizi zinadhibitiwa nitamuona anafanya la maana kuliko anayehojikwa nini Magufuli hajaenda msibani.
Hususan kwa sababu kuna muwakilishi mkubwa sana wa serikali kaenda, makamu wa rais.
Kwa hiyo hatuwezi kusema serikali ngazi ya taifa imesusa kwenda msibani.
Kwani lazima msibani aende Magufuli? Tunajuaje kama rais na Makamu hawajagawana majukumu na Makamu kupewa jukumu la kufariji misibani wakati rais anaendelea na kazi nyingine kuhakikisha hiyo misiba haijirudii?