Rais wa Marekani apaswa kuafikiana na Rais wa China ili mkutano wao upate matokeo ya kunufaishana

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111464485800.jpg
Rais wa China Xi Jinping amekutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Joe Biden kabla ya Mkutano wa Viongozi wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasific (APEC) wa mwaka huu, ambayo yamefuatiliwa sana na jamii ya kimataifa..

Mazungumzo yao yanfanyika kwa wakati sahihi kwa upande wa rais wa Marekani Joe Biden, ambaye nchi yake kwa sasa inakabiliwa na upinzani mkali kutokana na kutochukua hatua baada ya Israel kuwaua maelfu ya watu wa Palestina katika ukanda wa Gaza, ikiwa ni kama hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya shambulizi lililofanywa na kundi la Hamas.

Mazungumzo hayo ni ya pili ya moja kwa moja kati ya viongozi hao wa nchi kubwa kiuchumi duniani tangu rais Biden aingie madarakani Januari, 2021, na yanafanyika wakati dunia ikiwa bado inasubiri matokeo ya mkutano wao wa kwanza uliofanyika kando ya Mkutano wa Kundi la Nchi 20 (G20) uliofanyika Bali, Indonesia, katikati ya mwezi Novemba, 2022.

Wakati dunia ikikabiliwa na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa katika karne iliyopita, mkutano kati ya viongozi hao wawili wa nchi zenye nguvu zaidi duniani unaweza kuleta matumaini mazuri kwa jamii ya kimataifa. Uchumi wa dunia unaoporomoka, athari za mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa amani katika Mashariki ya Kati na Ukranine, na migogoro mingine mikubwa ni masuala ambayo yanapaswa kujadiliwa kwa dharura.

Lakini kuna athari chanya kwa uhusiano kati ya China na Marekani. Nchi hizi mbili zimeweka wazi njia za mawasiliano kupitia ziara za viongozi wa ngazi za juu. Mikutano hiyo imesaidia kuonyesha kuwa, wenzi hao wanahitajiana, japokuwa kwa ajili ya utulivu wa dunia.

Dunia inasubiri kwa hamu matokeo ya mkutano wa pande hizo mbili kwa shauku kubwa, ikitumai kuwa Marekani itatumia busara ya msemo wa kale wa nchi hiyo, kuwa “mara ya tatu italeta mafanikio.” Kutokana na juhudi za kurejesha uhusiano mzuri kati ya nchi hizo kushindwa, matokeo ya mafanikio ya mkutano wa dafari hii yatatoa mchango mkubwa katika kuishi kwa pamoja kwa amani kwa nchi hizi mbili kubwa, jambo ambalo sio tu ni muhimu kwa nchi hizo, bali kwa dunia nzima.
 
Back
Top Bottom