Rais Samia, wananchi wa Kakonko tunaomba barabara mpya ya Kakonko (Kigoma) kwenda Mambali (Uyui)

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,391
1,258
Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu Philip Isdory Mpango

Nawasalimu sana katika jina la JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!

Baada ya Salaam hizi nachukuwa wasaa huu kuwaombea afya ya siha bora Wewe, Rais wetu kipenzi Samia Suluhu, Waziri Mkuu Majaliwa Majaliwa Kassim na viongozi wote wa nchi hii.

Tatu, wananchi wa wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma tumedhamiria kwa dhati kulima na kulisha mikoa jirani na nchi kadhaa za maziwa makuu. Hii ni kutokana na dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais wetu ya kutoa mbolea nyingi za ruzuku mkoani Kigoma.

Nne, ili kuifungua Kakonko na mikoa ya Tabora na nchi jirani ya Burundi wananchi wako tunaiomba Serikali yako Barabara mpya ya (Muganza) Kakonko - Nkongogwa - Mambali (Uyui) - Tabora mjini kupitia pori tengefu la Muyowosi.

Barabara hii itawezesha usafiri na usafirishaji wa watu na mizigo toka nchini Burundi - Kakonko - Tabora bila kuzungukia wilaya za Nzega au Uvinza ambako panakuwa mzunguko mkubwa na gharama kuwa za juu.

Rais Samia na Makamu Philip Isdory Mpango, VP of Tanzania; faida za barabara hii zipo nyingi sana ikiwa ni pamoja na:
  • Kukuza sekta ya usafirishaji,
  • Kuongezeka kwa ajira,
  • Kukua kwa uchumi, na
  • Faida zingine mtambuka.
Nishukuru tena Serikali yako kwa namna inavyolipa suala la maendeleo kipaumbele cha hali ya juu na kuwarahisishia maisha watanzania.

Tunakuahidi kwamba Kakonko ya CCM haitakaa nyuma katika kuisaidia Serikali wakati wa kuwaletea wananchi maendeleo.

Msakila M Kabende
(Masters in Economics) & Former Kagera Regional Statistician Officer
 
Lengo ni upande nafasi tu huna nia njema ya taifa hili zaidi kuwazia tumbo lako
 
Kwa mtazamo wangu, barabara ingejengwa kutoka Tabora,kupitia ulyankulu ipite kwenye hifadhi ya Kigosi na Moyowosi ije kutokea Nyavumbu/Kumhasha, kibondo mjini ikaungane na ile ya Kibondo mjini kwenda border ya Mabamba inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo itapunguza mzunguko mkubwa kwa Kakonko na Kibondo katika kuunganishwa na mikoa ya katikati ya nchi hasa Dodoma.
1695666525428.png
 
Kwa mtazamo wangu, barabara ingejengwa kutoka Tabora,kupitia ulyankulu ipite kwenye hifadhi ya Kigosi na Moyowosi ije kutokea Nyavumbu/Kumhasha, kibondo mjini ikaungane na ile ya Kibondo mjini kwenda border ya Mabamba inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo itapunguza mzunguko mkubwa kwa Kakonko na Kibondo katika kuunganishwa na mikoa ya katikati ya nchi hasa Dodoma.
View attachment 2762288
Rais Samia aone mateso tunayopata ukanda huu
 
Back
Top Bottom