Rais Samia usilalamike, unachokisikia ndio kinasemwa nchi nzima, kubali tu yaishe!

Mkuu 'Galileo_Gaucho', mimi ndio leo nakusoma humu JF, kwa vile umeni'quote', sijapata kamwe hata siku moja kujuwa uwepo wako.

Sasa unaponiambia mimi nisahihishe nilichoandika mimi mwenyewe kwa ufahamu nisioutilia mashaka kabisa, nakuona wewe kama 'juha' (ashakhum si matusi, sina neno bora zaidi ya hilo).
Inawezekana sana, kwa elimu hizi za siku hizi uwe hujui maana ya hilo neno "DIKTETA", vinginevyo wewe utakuwa ni 'chawa' tu wa Magufuli aliyekuwa akikunywesha uchafu ili uweze kwenda chooni.
Usihangaike, sijibishani na watu wa aina fulani humu JF.
Mimi si wewe na wewe si Mimi ufahamu Wangu wa kijuha Magufuli hakuwa na hatakuwa Dikteta ni maoni yangu. Serikali haipigwi dole baya.
 
EeeeenHeeee!
Hakika "ni maoni yako", kama nami nilivyo na maoni yangu kwamba Magufuli alikuwa ni Dikteta, tena dikteta mtoa roho za watu.
Asingefanya hayo, pengine wewe na mimi tungekuwa pamoja tukimkumbuka kwa yale mengine ambayo sote tuliyapenda alipokuwa akiyahimiza.
 
Uzuri wa watz huwa hawajali nani yuko madarakani na ni wa chama gani, wao wanachojali ni maisha yao yaende tuu.

Uzuri wa watz hawaandamani road ila huo msusio watakaokupa utajuta mwenyewe, utapigwa vita ya kidiplomasia ndani kwa ndani mpaka ukome.

Sasa mama walimuingiza chaka kwenye haya mambo:

1. Tozo za miamala
2. Kuwafurusha wamachinga
3. Mfumuko wa bei unaopanda kila mwezi hasa mafuta
4. Kubwa kuliko ni kesi ya ugaidi ya FAM, ambayo hata darasa la 7 anaona "hapa hamna kitu".
5. Kuendelea kufanya kazi na 90% ya awamu iliyopita.

Hayo mambo juu yasiposawazishwa 2025 % ya kushinda ni <20% hata atumie goli la mkono.
Hapo kwenye WAMACHINGA umechemka
 
EeeeenHeeee!
Hakika "ni maoni yako", kama nami nilivyo na maoni yangu kwamba Magufuli alikuwa ni Dikteta, tena dikteta mtoa roho za watu.
Asingefanya hayo, pengine wewe na mimi tungekuwa pamoja tukimkumbuka kwa yale mengine ambayo sote tuliyapenda alipokuwa akiyahimiza.
Nasimamia Magufuli hakuwahi kuwa Dikteta, muhimu kutokukubaliana nayo ni afya pia kukubali kutokukubaliana.
 
Pengine unayo maana yako ya kipekee inayoelezea maana ya neno "dikteta"ni nini. Lakini kama unatumia maana ile ile inayotumiwa na wengi, Magufuli hawezi kutokuwa Dikteta.
Haitoshi tu kukubali kutokubaliana wakati jambo linajieleza lenyewe.
 
Uzuri wa watz huwa hawajali nani yuko madarakani na ni wa chama gani, wao wanachojali ni maisha yao yaende tuu.

Uzuri wa watz hawaandamani road ila huo msusio watakaokupa utajuta mwenyewe, utapigwa vita ya kidiplomasia ndani kwa ndani mpaka ukome.

Sasa mama walimuingiza chaka kwenye haya mambo:

1. Tozo za miamala
2. Kuwafurusha wamachinga
3. Mfumuko wa bei unaopanda kila mwezi hasa mafuta
4. Kubwa kuliko ni kesi ya ugaidi ya FAM, ambayo hata darasa la 7 anaona "hapa hamna kitu".
5. Kuendelea kufanya kazi na 90% ya awamu iliyopita.

Hayo mambo juu yasiposawazishwa 2025 % ya kushinda ni &lt;20% hata atumie goli la mkono.
hawezi kushinda 2025
 
Back
Top Bottom