Rais Samia usiende China ukaacha nchi haina maji wala umeme

Rais Samia usiende China ukaacha nchi haina maji wala umeme

Kinachoendelea Tanzania ni Uhaini unao fanywa na baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu ya sita, haiwezekani mgao wa maji ufike mpaka Vijijini hivi ninavyoandika nipo Marangu mtoni maji yanatoka kwa Don mmoja aliyechimba maji chini.

Kama hiyo haitoshi Leo ni siku tatu umeme unakatika saa kumi na mbili unarudi muda usio julikana.

Mh Rais tumesikia umealikwa kwenda China tafadhali tunakuomba usiende ukatuacha kwenye Giza na ukosefu wa maji hii ni hatari Kwa Taifa kiusalama.

Mwisho Rais Nina swali kwako na Kwa watawala wenzako hivi Rais Magufuli aliwezaje kuondoka upuuuzi huu UKIWA Makamu ila Leo hii UKIWA Rais unashindwa kumuiga?

Mh Rais usiliache Taifa katika Giza tafadhali!

Kigulu na njia hawezi kukuelewa, mwenzio anaenda shopping, kukosa maji it is your problem not hers
 
Mwisho Rais Nina swali kwako na Kwa watawala wenzako hivi Rais Magufuli aliwezaje kuondoka upuuuzi huu UKIWA Makamu ila Leo hii UKIWA Rais unashindwa kumuiga?

Mh Rais usiliache Taifa katika Giza tafadhali!
Nipo concerned na hili swali. Anawezaje kumuiga mtu anayemnyali kila anaposimama jukwaani?

Teuzi zinaonesha kabisa ni mwendo wa kufutana machozi. Tumeshamueleza sana Mama lakini anachokiamini ni kwamba watu wake wa karibu hawawezi kumuangusha.

Sisi tuliomacho muda wote tunaona na tunasema.

Bora muda upite watatafutana lakini Watanzania watapata mwanzo mpya kupitia kura halali
 
Serikali yetu inayoongozwa na mh Rais wetu mpendwa mama Samia IPO kazini muda wote na kwa kila kitu kinachoendelea hapa nchini inakuwa inakitambua na kukifanyia kazi na mikakatika mbalimbali kuweza kutatua kero hiyo, Urais Ni Taasisi inayofanya kazi hata Rais wetu akiwa nje ya mipaka ya Taifa letu anakuwa anapokea Taarifa muda na Wakati wote na kutoa maelekezo muda wote juu ya Nini kifanyike

Lakini pia watanzania Tuendelee kumwomba mwenyezi Mungu atusaidie mvua ziweze kunyesha ili ukame huu uweze kuondoka, lakini pia watanzania tuanze kujenga urafiki na mazingira yetu kwa kuhakikisha kuwa tunapanda Miti, Hatulimi katika vyanzo vya maji, tujiepushe kuchoma misitu yetu kwa shughuli za kilimo au uwindaji au sababu ya aina yoyote Ile inayo haribu mazingira yetu, mwisho Tuendelee kuelimishana wenyewe kwa wenyewe juu ya utunzaji wa mazingira yetu
Haya maneno yako yana jibu kero ya maji ama umeme??
 
Bagamoyo inagombwaniwa sana
Huku West huku East

Ila bora twende na West
 
Ukame na mahangaiko wanayopitia watanzania kwa sasa ni matokeo ya uongozi uliokataliwa kiroho!
Wachache wenye akili wataelewa hili!

Mfano mwaka juzi kulikuwa na tishio la nzige lakini Tanzania halikufika ,tishio la kimbunga JOBO nalo Mungu akapisha,hatukuwa na uhaba wa mvua kiasi hiki sasa hivi niko kigoma hapa hakuna mvua,Hatukuwa na mjaa na bei za vyakula zilikuwa chini lakini sasa bei ya chakula ilo juu hata mbolea iko juu kabla hata ya vita ya Ukraine!

Mungu amewakataa amini usiamini!

Mwovu atawalapo mahangaiko na mateso hutamaraki na dalili zake ndo hizo!

Ushawahi kujiuliza vipi uongozi huu ungekuwepo kipindi COVID inatokea? Yangefanyika maamzi yakushangaza maana uwezo wao ni mdogo!
Mara zote watu ambao hawana uwezo wa kujenga hoja hukimbilia kwenye dini, ukabila, jinsia.

Hivi Mungu unayemwabudu anaweza kutunyima mvua kwa sababu ya Rais Samia? Rais ambaye amewasamehe waliotengenezewa kesi za uhujumu uchumi, Rais alie wasamehe wapinzani waliopachikwa kesi za ugaidi.

Rais ambaye hakuna mtu anaehofia kutekwa. Acha kulalamika fanya kazi
 
Sijui kama unauona ukame uliopo hivi sasa katika ukanda huu wa afrika ya mashariki au ndio utaratibu ule ule wa kulalamika bila sababu.

Unajuaje kama huko China hakuna suluhisho la matatizo ya maji tuliyonayo kwa sasa?. Uchungu ulionao wewe wa TZ hao wanasiasa wenye majukumu ya kuongoza nchi wanao pia.

JPM msipambe sana mpaka watu wakafikia hatua ya kumkosea adabu, alikuwa binadamu tu kama mimi na wewe.
Vichaa kama hawa wananishangaza sana... nilishasemaga hapa, hakuna mtu angebaki kumsifia JPM kama tozo za kipuuzi zisingeletwa, bei ya vyakula isingepanda, mgao wa maji usingekuwepo, mgao wa umeme usingekuwepo, bei za bundle zisingepandishwa na bei ya mafuta(petroli n.k) ingeregulatiwa na serikali ili kusaidia uchumi.

Hapo sijaongea kuhusu wafanyabiashara wadogo wadogo waliohamishiwa biashara zao pasipo na miundo mbinu au angalau chochote kutoka serikalini ili mitaji yao isiharibike.
 
Sijui kama unauona ukame uliopo hivi sasa katika ukanda huu wa afrika ya mashariki au ndio utaratibu ule ule wa kulalamika bila sababu.

Unajuaje kama huko China hakuna suluhisho la matatizo ya maji tuliyonayo kwa sasa?. Uchungu ulionao wewe wa TZ hao wanasiasa wenye majukumu ya kuongoza nchi wanao pia.

JPM msipambe sana mpaka watu wakafikia hatua ya kumkosea adabu, alikuwa binadamu tu kama mimi na wewe.
Bado lawama hazikwepeki ina maana kwa kipindi chote imeshindikana kutengeneza mabwawa ya kuhifadhi maji ya kutumika kipindi cha ukame?

Tukiondoa bajeti ya kununua ma-v8 kila mwaka na malipo ya wabunge tu wakipangwa kwa kima kinachoendana na hali ya nchi mbona ingetosha kabisa tatizo la maji kuwa historia
 
Anaondoka wakati huku kusini Kuna mgomo wa kuuza korosho.wiki ya pili Sasa wananchi wamegoma kuuza korosho zao kwa sababu ya Bei ndogo inayotolewa na wafanyabiashara. Waziri.

Mkuu yupo nje Hana habari na Sasa rais naye anaondoka, watatetewa na nani
 
Migao haikosekani popote duniani hata ulaya Wana mgao WA gasi
 
Kinachoendelea Tanzania ni Uhaini unaofanywa na baadhi ya Mawaziri wa serikali ya awamu ya sita, haiwezekani mgao wa maji ufike mpaka Vijijini hivi ninavyoandika nipo Marangu mtoni maji yanatoka kwa Don mmoja aliyechimba maji chini.

Kama hiyo haitoshi leo ni siku tatu umeme unakatika saa kumi na mbili unarudi muda usio julikana.

Mh Rais tumesikia umealikwa kwenda China tafadhali tunakuomba usiende ukatuacha kwenye Giza na ukosefu wa maji hii ni hatari Kwa Taifa kiusalama.

Mwisho Rais Nina swali kwako na Kwa watawala wenzako hivi Rais Magufuli aliwezaje kuondoka upuuuzi huu UKIWA Makamu ila Leo hii UKIWA Rais unashindwa kumuiga?

Mh Rais usiliache Taifa katika Giza tafadhali!
John Walker
 
Back
Top Bottom