Hotuba ya Rais Samia yalituliza Taifa na Kukata kiu ya Watanzania juu ya changamoto ya umeme

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
20,924
15,141
Ndugu zangu Watanzania,

Leo Rais samia Amekata kiu ya watanzania na kulituliza Taifa ambapo muda mwingi walikuwa wanataka kusikia kauli yake juu ya changamoto ya kukatika kwa umeme. Kwa utulivu ,upole,uthabiti na uimara wa hali ya juu sana amelieleza Taifa sababu ya chagamoto hiyo na mikakati ya serikali yake kuimaliza. Ameliambia Taifa kuwa hali hiyo imetokana na serikali kufanya ukarabati na matengenezo ya mitambo ambayo ilikuwa haijafanyiwa matengenezo kwa muda mrefu. Hivyo serikali inalazimika kuzima mingine na kuwasha mingine ambayo inakuwa haitoshelezi umeme unaohitajika.

Lakini pia Amelieleza Taifa kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yameathiri uzalishaji wa umeme kutokana na nchi kukumbwa na ukame kwa baadhi ya maeneo na hivyo maji yanayohitajika katika mabwawa yetu kuwa pungufu.Hata hivyo ameelezea jitihada za serikali yake kumaliza changamoto hiyo ambayo itabakia historia katika Taifa letu baada ya miezi sita tu. Ambapo kwa sasa serikali inajitahidi kuongeza na kutumia vyanzo vingine vya umeme kama vile umeme wa gas na jua.

Naamini watanzania wenzangu sote ni mashahidi wa namna jua linavyowaka kwa kipindi hiki na namna maeneo mengi yanavyoendelea kuwa kame na kukauka maji .sote tunakubaliana na ukweli kuwa hata shughuli za uchumi zinazotegemea umeme zimeongezeka kwa kiasi kikubwa sana kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi wetu, unaotokana mazingira mazuri na sera nzuri za serikali yetu katika kuchochea ukuaji wa uchumi na Biashara.

Tuendelee kuwa wavumilivu katika miezi hiyo sita ambayo mh Rais na serikali yake wanaendelea kupambana kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini ,lakini pia Tuendelee kumuomba Mungu atuletee mapema mvua zenye baraka zisizo na madhara zitakazo jaza mabwawa yetu.lakini pia tukumbuke pia mwakani bwawa la mwalimu Nyerere litaanza nalo uzalishaji wa umeme na hivyo kufanya Taifa kuwa na umeme wa kutosha na mwingine kuuza nje ya nchi kama vile kenya na nchi nyingine zenye uhitaji wa umeme.

Rais samia ni kiongozi mkweli sana ,Ni kiongozi ambaye anaendana na Baba wa Taifa Hayati mwalimu Nyerere ambaye alikuwa haoni haya kuusema ukweli kutwambia watanzania,kama ambavyo amewahi kutuambia kuwa Tufunge Mikanda. Huo ndio uongozi na huo ndio uungwana .Rais samia Hataki kuendesha serikali kwa udanganyifu na ulaghai wakati anajuwa mwisho wa siku ukweli hujitenga na uongo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Badala ya Kumtayarisha Raisi na matamshi na maneno na kauli zake akiwa Jukwaani, mnabakia kufanya Damage Control akiwa....

Ameshaboronga, na wapiga kura wanajua hayo.

Urudishe Kadi ya Uanachama wa CCM na Uchague kwa umakini mkubwa 2025

Tanganyika inahitaji mapinduzi ya haraka.
 
Mimi nipo humu naendelea kuleta ukweli na kupinga upotoshaji wa aina yoyote ile unaoletwa na wenye dhamira mbaya kwa Taifa letu.
Mh. January alipokuwa Waziri alitangaza Siku kadhaa za kufanyia Matengenezo mitambo na Umeme tukawa tunapata kwa shida.

Kwahiyo tangu wakati huo hadi Sasa Matengenezo bado yanaendelea?

Sababu ya Pili ya katizo la Umeme nakubaliana na Mh. Raisi ila ya Kwanza ametupiga na kitu kizito.


Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Yaani watanzania tupo gizani na hapa tulipo hatuna umeme, halafu mama anasema shida ya umeme iendelee hivi hivi mpaka baada ya miezi sita ndio atakuja kufanya tathmini kuona imepungua, kuongeza au amekwisha! Hapa hapana kabisa. Mama ameteleza kwa 100%.

Watanzania tunataka umeme wa uhakika sasa.
 
Banza Stone alisemaga ukweli .
Bora ukose Mali upate Akili.
Mnyiha wewe unaonekana umekosa vyote.
Nikosoe kwa hoja na ujumbe niliyoandika na siyo ukabila,maana hapa siandiki kwa niaba ya kabila au ukoo. Na wala situmwi na kabila au ukoo kuja kuandika hapa. Pia acha mawazo ya kikabila yatakayokupofusha akili yako.Tazama mambo kwa uhalisia na siyo kwa jicho la ukabila.
 
Back
Top Bottom