Serikali yetu inayoongozwa na mh Rais wetu mpendwa mama Samia IPO kazini muda wote na kwa kila kitu kinachoendelea hapa nchini inakuwa inakitambua na kukifanyia kazi na mikakatika mbalimbali kuweza kutatua kero hiyo, Urais Ni Taasisi inayofanya kazi hata Rais wetu akiwa nje ya mipaka ya Taifa letu anakuwa anapokea Taarifa muda na Wakati wote na kutoa maelekezo muda wote juu ya Nini kifanyike
Lakini pia watanzania Tuendelee kumwomba mwenyezi Mungu atusaidie mvua ziweze kunyesha ili ukame huu uweze kuondoka, lakini pia watanzania tuanze kujenga urafiki na mazingira yetu kwa kuhakikisha kuwa tunapanda Miti, Hatulimi katika vyanzo vya maji, tujiepushe kuchoma misitu yetu kwa shughuli za kilimo au uwindaji au sababu ya aina yoyote Ile inayo haribu mazingira yetu, mwisho Tuendelee kuelimishana wenyewe kwa wenyewe juu ya utunzaji wa mazingira yetu