Rais Samia usiende China ukaacha nchi haina maji wala umeme

Rais Samia usiende China ukaacha nchi haina maji wala umeme

Sifi Leo

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
6,354
Reaction score
11,976
Kinachoendelea Tanzania ni Uhaini unaofanywa na baadhi ya Mawaziri wa serikali ya awamu ya sita, haiwezekani mgao wa maji ufike mpaka Vijijini hivi ninavyoandika nipo Marangu mtoni maji yanatoka kwa Don mmoja aliyechimba maji chini.

Kama hiyo haitoshi leo ni siku tatu umeme unakatika saa kumi na mbili unarudi muda usio julikana.

Mh Rais tumesikia umealikwa kwenda China tafadhali tunakuomba usiende ukatuacha kwenye Giza na ukosefu wa maji hii ni hatari Kwa Taifa kiusalama.

Mwisho Rais Nina swali kwako na Kwa watawala wenzako hivi Rais Magufuli aliwezaje kuondoka upuuuzi huu UKIWA Makamu ila Leo hii UKIWA Rais unashindwa kumuiga?

Mh Rais usiliache Taifa katika Giza tafadhali!
 
Sijui kama unauona ukame uliopo hivi sasa katika ukanda huu wa afrika ya mashariki au ndio utaratibu ule ule wa kulalamika bila sababu.

Unajuaje kama huko China hakuna suluhisho la matatizo ya maji tuliyonayo kwa sasa?. Uchungu ulionao wewe wa TZ hao wanasiasa wenye majukumu ya kuongoza nchi wanao pia.

JPM msipambe sana mpaka watu wakafikia hatua ya kumkosea adabu, alikuwa binadamu tu kama mimi na wewe.
 
Kinachoendelea Tanzania ni Uhaini unao fanywa na baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu ya sita, haiwezekani mgao wa maji ufike mpaka Vijijini hivi ninavyoandika nipo Marangu mtoni maji yanatoka kwa Don mmoja aliyechimba maji chini.

Kama hiyo haitoshi Leo ni siku tatu umeme unakatika saa kumi na mbili unarudi muda usio julikana.

Mh Raisi tumesikia umealikwa kwenda China tafadhali tunakuomba usiende ukatuacha kwenye Giza na ukosefu wa maji hii ni hatari Kwa Taifa kiusalama.

Mwisho Rais Nina swali kwako na Kwa watawala wenzako hivi Raia Magufuli aliwezaje kuondoka upuuuzi huu UKIWA Makamu ila Leo hii UKIWA Rais unashindwa kumuiga?

Mh Rais usiliache Taifa katika Giza tafadhali

Bukoba tuna maji hadi wanachezea ng’ombe na Umeme tumefunga kwenye Mabanda ya kuku. Hii shida si ya watanzania wote.
 
Hotuba yake ya mwisho kabla hajatangazwa kuwa rais na alishajua atakuwa rais akiwa Tanga alitangaza mwisho wa kukatika umeme lakini matokeo yamekuwa tofauti
 
Back
Top Bottom