Rais Samia, unda tume huru kuchunguza mauaji ya Hamza

Wauaji wamekuwepo nyakati zote, lakini je, kila anayeua ni gaidi?

Kuna swali muhimu kuliko yote ambalo ni kwa nini Hamza alifanya mauaji yale tena ambayo yalilenga polisi tu?
Uchunguzi huru ni muhimu sana kwa sababu ni kwanini Hamza aliwalenga polisi wetu na kwanini alienda pale selanda badala ya msimbazi ambapo ni karibu na kwao? Je Kamanda Abdallah Zombe na wale wauza madini wa Morogoro ilikuwaje baada ya uchunguzi huru? Pia tujiulize wale polisi wanaouwana kwenye malindo huwa sisikii nao wanaitwa magaidi ila "sababu ya wivu wa kimapenzi!!" kwanini iko hivyo?
Nadhani hii taasisi imepoteza nidhamu kwa mambo binafsi na siasa inapaswa kujirekebisha badala ya kulindana kwenye mambo ya kijinga ambayo yanaligharimu taifa.
 
Back
Top Bottom